Ikulu mpya na maswali

Hawa watu sijui wanawaza nini, kama kuna pesa hazina kazi mbona watumishi wana madai yao hayalipwi?
 
Kwa kuwa uamuzi uliishafikiwa na Ikulu imeishajengwa tena moja kati ya Ikulu yenye eneo kubwa Duniani, nashauri inunuliwe helicopter moja au hata mbili kwa ajili ya usafiri wa Rais. Itapunguza msafara wa Rais na kusababisha foleni barabarani. 🤔
 
Mshamba ni wewe usiyejua kwamba bajeti lazima izingatie mahitaji ya msingi na vipaumbele. Usisahau kwamba deni la taifa sasa linakimbilia trilioni 80! Amka wewe!
Nafikiri huyu jamaa hajui au ndio wale chawa? Ukute na yeye ni mmoja wa wanufaika na ujenzi huo.. Kaja kutetea maslahi... Hivi hata mtoto wa shule ukiuliza atakwambia kipaumbele ni elimu... Wanajenga hayo ma vitu ila kuongeza maslahi na vitendea kazi kwa mwalimu anaejenga maendeleo kwa kuongeza maarifa wananchi wanamnyonya, wao watoto anasomesha nje ili kesho waje na elimu bora aseme ndio anastahili kuongoza.. Sie wetu wabaki kukaa masjala na vijinafasi wasivyoweza fanya maamuzi ili wao na vizazi vyao wawe watawala... Ole wenu... Siku sitakuja vizazi vyao vyote vitashushwa chini...!
 

Hivyo vyote hata wewe unaweza kujenga, au ulikatazwa?
wananchi wa kawaida anaweza Je kujenga? Hapa hoja ni kwamba hela inayotumika ni ya kodi zetu, tunahaki ya msingi kuhoji.. Kama ingekua hela inayotumika ni yake, isingekuwa issue... Tunaumia kuona serikali inaacha mambo ya msingi na kufanya yasio ya msingi.... Hatupingi uongozi wa mwanamke... Bali maamuzi hayana tija Sana!
 
Wewe ndiyo mfalme wa wajinga bendera fwata upepo wazee wa ndiyoo bungeni
 
Kuna mwananchi gani anakatazwa kujenga shule?

Au hujaona nilivyovijibu umekurupuka tu?

Nakushauri rudi nyuma ukakisome nilichokijibu. Unaonesha umedandia gari kwa mbele.
 
Pumba halikuna lamaana uliloandika
 
Maana nimeuliza maswali ya msingi th, kuwa kuna sababu gani ya kuweka hayo yote?
Magufuli aliwaza ikulu itakayofaa miaka 500 ijayo kama ilivyo ma castle ya waingereza. Kwa hiyo kuwa na hayo mambo yote ni sawa tu
 
Pia sikuona sababu ya Ikulu kuwa na eneo kubwa vile, operations costs ni kubwa sana
Tanzania ardhi ni kubwa sana. Ikulu kuwa na eneo kubwa kuna umuhimu vile vile. Itapunguza msongamano miaka ijayo watu wakishaanza kujenge kuzunguka.

Hii ardhi ya Tanzania haitajaa hata miaka 100 ijayo.
 
Dunia nzima ni masikini.

Hata huko ulaya masikini wapo.

Hata serikali iseme bajeti yote ipelekwe kuondoa umasikini haitatosha hata miaka 100 ijayo.

Wacha vingine vifanyike.
 
Sasa Mbona Umekasilika Kuna Sehem unakula Unapitisha Mrija Wako Wakufyonza Maziwa na Asali Sio bure
 
ukifanya research utagundua Wafanya Kazi Wengi Selikalini Walimchukia Magufuli Kwa Mengi Maana Kuna Uozo Mwingi Mzee Aliukata Upigaji Wa wazi ,Upigaji Wa Ndani bila Wananchi Kujua ,Kuna Mengi Yeye Alianika Wazi Binadamu wakajua Kumbe Kuna ABC Sasa hivi imerudi Enzi Ya Utawala wa Kusifia Ili Uendlee Kula Ufanye Yako
 
Kuna mwananchi gani anakatazwa kujenga shule?

Au hujaona nilivyovijibu umekurupuka tu?

Nakushauri rudi nyuma ukakisone nilichokijibu. Unaonesha umedandia gari kwa mbele.
Ukiona mtu anasema kodi zetu basi ujue huyo kachangia harusi tu hajawahi kulipa kodi hata siku moja.
 
Sasa Mbona Umekasilika Kuna Sehem unakula Unapitisha Mrija Wako Wakufyonza Maziwa na Asali Sio bure
Ni kweli tunahitaji shule sio UMEKASILIA ni UMEKASIRIKA mimi nikiona mtu anachanganya "L" na "R" basi nguvu zinaisha..
 
Nyie endeleeni kula kwa urefu wa kamba zenu...point ya jamaa iko clear, hii nchi wananchi wanashida chungu nzima tena basics...tunapaswa tuwekeze sana kwenye maendeleo ya watu...kila kitu tufanye kwa kiasi na kwa akili..la sivyo kuna kakikundi ka watu chini ya asilimia 10...wataendekea kula mema ya nchi..wengine choka mbaya.Hekima inahitajika kwenye haya,sio ubinafsi na justifiction zisizo na kichwa wala miguu
 
Utasikia Hilo nalo nimelichukua tutalifanyia kazi.
 
Sasa nikuulize je kuna miradi yoyote ya maji aus shule imesimama? pesa za Corona zote zilienda kujenga mashule basi hatuna cha kufanya nikujenga mashule tu au? kuna pesa zimeombwa kujenga flyover Dar kwa hiyo mimi wa Tanga au Moshi niseme tunachezea pesa flyover za nini wakati sisi hatuna maji? kuna vipaumbele vya mtu binafsi na vipaumbele kama nchi kwa ujumla, hii nchi ina wizara zaidi ya 20 na kila wizara ina vipaumbele vyake na wanaomba pesa bungeni ili kazi zifanyike sasa ukianza kusema hiki sio kipaumbele hiki sio hivi au ndege sio muhimu lakini kuna watu wanafaidikia na safari za ndege haya yote yanafanyiwa kazi kwenye mikutano ya budget na mambo mengine sio ya serikali kuu kuyafanya ni huko mikoani au wilayani wana vipaumbele vyao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…