Ikulu mpya na maswali

Mawazo ya kimasikini hayo.
 
Wajenge viwanda, Hospitali n, shule na masoko hapo ikulu.
 
Jana Samia kaongea kuwa Ikulu bado kuna mambo yanafanyika ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia ya kurukia Ndege

Ndege zenyewe zipi? Uwanja complicated wa msalato nao unasubiri, ni hizihizi kodi zetu au?

Well
Vipaumbele vya nchi yetu miaka ya karibuni ni vipi? Elimu ujinga na maradhi vimeisha?

Maana enzi za Mzee Mkapa kila mwisho wa mwezi tulikua tunakumbushwa na kupewa updates where are we heading to…
 
Wajenge viwanda, Hospitali n, shule na masoko hapo ikulu.
Matumizi mabaya ya ardhi na kodi yetu.
Ipo siku atajitokeza mtu atapunguza eneo na kujiuzia
 
Hii nchi haina viapumbele
 
Uwivu huoo hamtaki na sisi viongozi wenu tuanze kujifunza na kucheza golf ikulu..
Mibongo inawivu sana na roho ya kimasikini
 
Usiposema samia complex utahalishaje upigaji wa fedha? Yaani hapo upigaji umehalishwa. Ni mwendo wa kula tu.

Huyu mama kwakweli anawaangusha sana wanawake wenzie kiuongozi.
CCM wenzio hao
 
Kila mtu anataka jina lake liwepo hapo tena kwa kujipigia chepuo mwenyewe mara Zanzibar mara Nungwi golf courts.

Hivi mfano Nyerere aliacha vitu gani vikiitwa kwa jina lake alipokuwa madarakani? Barabara?

Vingi vimepewa jina lake na watu Baki akiwa mstaafu au marehemu.

JNIA yenyewe aliiacha ikiitwa DIA hadi 2005.

BTW:Eneo lenyewe wamehodhi kubwa mno ekari 8,473 zote za nini si heri wangewapa vijana wa maigizo ya kilimo ya BBT ya Bashe.
 

Ikulu = hazina ya nchi?
Wenzetu hua mnatumia ubongo upi kutoa arguments kama hizi? Muulize Mzee Kagame Ikulu iko wapi? Unadhani hawezi kujenga ikulu ya maonyesho?
 
Uliambiwa kuna uhaba wa maeneo ya kulima?
 
Kwa nini iitwe majina yao kwanza huu ujinga wa kuita majina yao kila sehemu nao uangaliwe..na waite hata Tanzania complex au kodi zetu complex
 
Kuna Ikulu duniani yenye uwanja wa ndege au wana taka wawe wa kwanza
 
Kifurushi cha bima ya watoto yenyewe wameshindwa. Kisha mmama mtu mzima wanayemuita rais anashangilia kujengwa kiwanja kwa golf sababu anajua wajukuu zake watatibiwa ulaya.

Na westerners hua wanafurahi sana wakizikopa nchi za africa alafu wakaona zinafanya mambo kama haya hua wanaongeza na rate za mikopo kabisa ili tukope kwa wingi wazidi kumiliki nchi.
 
Watz mnalawama,Sasa bila Barbara ya kutua ndege,ndege ya rais itue vichakani?
 
Ikulu = hazina ya nchi?
Wenzetu hua mnatumia ubongo upi kutoa arguments kama hizi? Muulize Mzee Kagame Ikulu iko wapi? Unadhani hawezi kujenga ikulu ya maonyesho?
Sasa wewe na akili zako zote unatufananisha na kile ki mkoa Rwanda? kweli tunawatu akili zao zina changamoto, leo hii sisi wakutuweka kundi moja na Rwanda ya Kagame kwa lipi haswa? Hii Tanzania na EA mtu wa kushindina naye ni Kenya. Halafu toka lini nchi tukaweka vipaumbele vyetu kwa kuangalia Kagame anafanya nini. Usitukoshee heshima kama nchi kutufananisha na nchi kama wilaya yetu. Hata kama unachuki zako na Mama Samia uko umeenda mbali. Nchi yoyote ni lazima uwe na airport nzuri, Immigration nzuri, ofisi za serikali nzuri na ikulu nzuri ndio sura ya nchi mengine yatakuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…