Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,802
- 71,229
Kitendo hiki ni cha aibu sana na kinashusha heshima ya Ikulu yetu. Nina uhakika Mheshimiwa Rais hakufahamu njia zilizotumika na ratiba ya mambo ilivyo pangwa.
Juzi kulikuwa na hafla ya kutia Saini mkataba wa Bandari.
Baadhi ya watu mashuhuri na wengine kutokea TEC akiwamo Fr. Kitima walialikwa lakini bila kutaja wamealikwa kwenye nini Ikulu kama kadi zilivyoonyesha.
Mwaliko ulionyesha Rais (tena kwa kitisho cha Amiri jeshi mkuu) anakualika na hivyo sio rahisi kukwepa. Sasa mbaya ni kuwatumia wasanii kama Mrisho Mpoto kuwasemanga mle ndani eti hata wale waliopinga wapo humu!
Sio uungwana hata kidogo taasisi yenye heshima kama ikulu kufanya mambo ya kwenye vigodoro au kitchen party. Kwani wange Saini na kutoa hotuba zao bila kuwasemanga waliokuwa wanapingankwa maslahi ya nchi kulikuwa na ubaya gani?
Hili hata watu kama Pascal Mayalla wanaotetea mambo ya ikulu kwa kila kitu wataona sio right!