RIWAYA: Mkakati wa kuelekea Ikulu

RIWAYA: Mkakati wa kuelekea Ikulu

Willy Gamba 1

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2015
Posts
352
Reaction score
377
RIWAYA ;MKAKATI WA KUELEKEA IKULU
MTUNZI: HUSSEIN WAMAYYA

SEHEMU YA KWANZA.

Utangulizi
Wakati Baba wa Taifa anamlea Masurufu Hussein
Masurufu hakuwa anajua kuwa analea mtu ambaye
alikuwa amechoshwa na udhalili wanaoishi
wapigania uhuru.
Hakujua pia kuwa mzazi mwingine wa Masurufu
alikuwa mstaafu wa uliokuwa Muungano wa Afrika
Mashariki na ambaye licha ya kuutumikia
Muungano huo kwa nguvu na uwezo wake wote,
bado ameishia kudhalilika wakati akidai mafao
yake kiasi cha kufikia kuvua nguo hadharani.
Hakujua pia kuwa hizo ni sababu chache miongoni
mwa nyingi zilizomfanya Masurufu huyu aanze
kuhubiri utakatifu huku akifanya uhalifu baada ya
kupata nafasi na kuzitumia vyema fursa za Vita
vya Kagera, Uhujumu uchumi, Ubunge, Uwaziri na
baadae ubalozi wa Tanzania nje ya nchi.
Na sasa akishirikiana na Christopher MacDonald
Beberu wa G-8 Original, Masurufu anajiandaa
vyema kwenda Ikulu kwa lengo moja tu,
kuzinyonya rasilimali za Tanzania mpaka tone la
mwisho…!
Ikoje hiyo safari yake?

SURA YA KWANZA
UHOLANZI - JANUARI 2005


Zilishapita siku za kutosha toka Dr. Masurufu na
watumushi wenzie katika Ubalozi wao kule
Uholanzi wafanye mkutano. Na ilishapita miaka
tisa toka Dr. Masurufu alipoteuliwa kuwa Balozi wa
Tanzania katika nchi hiyo. Asubuhi hii akiwa ndiyo
kwanza ametoka kuoga, mkewe akaingia ndani na
kumuuliza.
“Habari za Asubuhi Baba Rose!”
“Nzuri tu, sijui za kwako” Anajibu hali akijifuta maji
kwa taulo. Mkewe anafungua kabati na kumtolea
suti safi.
“Zangu pia njema!”
“Ulikuwa wapi?”
“Nilikuwa namuhimiza Rose awahi shule. Mwenzie
Dan keshaondoka saa nyingi!”
“Oh!Vizuri!” Masurufu akaanza kuvaa nguo.
“Una habari mume wangu?”
“Habari gani?”
“Rais wa nchi yetu ya Tanzania anamaliza muda
wake mwaka huu. Nasikia chama tawala kitaanza
kugawa fomu mwezi ujao!”
“Sema haki ya Mungu!”
“Haki ya nani tena!”
“We habari hizi umezipata wapi?” Sasa Dr.
Masurufu alikuwa akivaa viatu.
“Redioni. Idhaa ya kiswahili ya BBC.
Zimetangazwa asubuhi wakati ulipokwenda kuoga!”
“Enhe!” Dr. Masurufu akaacha kufunga kamba za
viatu na kumtazama mkewe kwa mshangao.
“Wamesemaje?”
“Katibu Mkuu amesema fomu zitaanza kutolewa
mwezi ujao kwa watanzania wenye sifa. Gharama
yake itakuwa shilingi milioni mbili kwa kila fomu.
Kutoka hapo itakubidi uzunguke nchi nzima
kutafuta wadhamini kabla ya kurudisha fomu
mwezi unaofuata ambapo chama kitayapitia
majina ya wagombea safi na kuyapeleka kwa
wajumbe wa Kamati kuu kwa uamuzi wa mwisho!”
Masurufu akamaliza kuvaa viatu, mkewe
akamuongoza mpaka eneo la kupatia chakula
ambako kulikuwa na chai ya nguvu. Akasema.
“Kikao kilichopita nilitoa onyo kali kwa wale
watumishi wenzangu ambao walidhani wanaweza
kuniendesha kama yule Balozi aliyepelekwa
Singapore. Hiki ni chuma cha pua bwana
hawataniweza katu ha…ha….haaah!” Akacheka.
Mkewe akatabasamu tu. Dakika chache baadae
tabasamu lilizimika akarudi ndani ya tafakuri tena.
“Mpenzi mke wangu!” Dr. Masurufu akamwita
“Kwa nini una majonzi mpenzi? Huonekani kuwa
mke wangu niliyekuzoea. Kulikoni?”
“Huu Uchaguzi laaziz!”
“Uchaguzi?!”
“Ndiyo!”
“Una nini ?”
“Huujali kabisa!”
“Siujali ndiyo!”
“Kwa nini huujali?”
“Unatuhusu nini? Ingawa sisi ni watanzania, tuko
maili nyingi nje ya Tanzania. Sidhani kama una
athari kwetu!”
Kicheko cha uchungu kikamponyoka Glady mkewe!
Akamwambia “Kwa taarifa yako, uchaguzi huu
unatuhusu sisi zaidi, kuliko unavyowahusu
watanzania wengine!”
“Kwa namna gani dia?”
“Swali zuri, sisi tunaitegemea Serikali iliyopo
madarakani kutuweka huku Ubalozini. Ikimaliza
muda wake na kuondoka hatutaipata tena fursa ya
kuishi kivulini hapa Uholanzi. Hatutaipata nafasi ya
kuishi katika kasri hili wala hatutapata wasaa wa
kutembelea magari haya ya kifahari. Hii ni pamoja
na watoto wetu kuacha kusoma shule za kimataifa
na kwenda kubanana na akina kajamba nani huko
uswahilini. Bado tu hujali?”
Yakamuingia Dr. Masurufu. Akavua miwani na
kuisafisha “Unajua kwa nini sijali?” Akairudisha
miwani usoni.
“Sijui!”
“Yupo mtu anayenifanya nisijali. Mtu ambaye
amechangia kwa asilimia kubwa mimi kuwa Balozi
wa Tanzania nchini Uholanzi. Mtu huyu ni Profesa
Zonga!”
“We’ ndiyo uko nyuma kweli kweli. Huyo Profesa
Zonga ndio atasababisha uteuliwe tena?”
“Ndiyo! Hata akiingia nani pale Ikulu, sisi
tutaendelea kuula tu. Watake tutaula, wasitake
tutaula!”
“Yaelekea unajiamini kupita kiasi baba Rose?!”
“Kwa nini nisijiamini mama watoto?! Dawa zake
ninatumia vizuri, masharti yake ninatimiza. Gari
nimemuachia. Nyumba nimemjengea. Kwa nini
nisijiamini?! Kwa nini?”
Mkewe akashusha pumzi za kukata tamaa.
“Lakini mume wangu, utakuwa Balozi mpaka lini?
Lini na sisi tutakuwa viongozi wa juu kabisa wa
Taifa letu la Tanzania, tukiandikwa na vyombo vya
habari kila tunapokohoa, tukilindwa kama miungu
wadogo, tukimiliki uchumi wote wa nchi?
Saini yako ikiamua juu ya kuishi au kufa kwa mtu
yeyote. Ukiwa Amiri Jeshi Mkuu unayeheshimika,
zulia jekundu likikulaki kila unapokuwa ziarani!
Kwa nini hutaki neema hii mume wangu?”
Dr. Masurufu akavuta tafakuri kwa muda.
Akasema, “Tatizo ni watu laaziz, watanikubali
kweli? Watu watanipa nafasi?!”
“Watu ndio kitu gani?”
“Una maana gani?”
“Labda ungezungumzia fedha. Kama huna fedha
kabisa, labda hicho kinaweza kuwa kikwazo. Lakini
watu?! Mbona ukiwa na fedha ni rahisi kupata
chochote unachotaka. Seuze watu! Na wewe fedha
unazo!”
“Lakini hazitoshi kufanya kampeni katika chama na
nchi nzima.”
“Zinatosha mume wangu. Zinatosha kabisa Dr.
Masurufu! Jiulize una rasilimali kiasi gani, una
marafiki wangapi wanaokuunga mkono ndani na
nje ya nchi. Hapa hapa Uholanzi wapo zaidi ya
kumi. Hao ni wale uliopata kunitambulisha na
kuwaleta nyumbani ambao kwa kinywa chako
umekiri kwamba ni wafanyabiashara wakubwa
ambao hawazungumzii milioni bali bilioni!”
“Hilo ni kweli!” Masurufu akaafiki.
“Bado hujanitambulisha wa nje ya hapo. Ambao
sina shaka unao wa kutosha!”
“Ni kweli ninao wa kutosha!”
“Unataka kuniambia wote hawa ukiwaendea
kuwaomba msaada na sio msaada hasa bali
wakuazime na ukishaukwaa urais tu
utawarudishia. Unataka kuniambia watakataa
wote?”
“Glady, unafahamu vizuri sana kama kitu hicho
hakiwezekani!”
“Kumbe kinachokufanya uhofie ni nini?”
“Hofu yangu iko kwenye kuanguka. Watu
wanaweza kula fedha zako halafu wakakunyima
kura!”
“Mawazo kama hayo mtafutaji hatakiwi kuwa nayo,
lakini pia huwajui watanzania vizuri. Watanzania
wana ukarimu uliopatiliza. Wanakumbuka hisani
kama sio fadhila hata katika hali inayokatisha
tamaa kabisa. Wakishakula fedha zako
hawatakuwa na zaidi ila kukupigia kura wakifika
katika sanduku la kura.
Kwa sasa ukiwazungukia marafiki zako wa ndani
na nje wakatupa walau bilioni mbili tu, hesabu
utakuwa umeshinda tayari. Niulize kwa nini!”
“Kwa nini?”
“Ukiwa na fedha hizo, ukaongezea na zako
haidhuru hata zikafikia bilioni nne au tano.
Unaweza kuanzisha gazeti lako ambalo si tu
litakuwa likikupigia debe kama mgombea safi,
mgombea chaguo, mgombea unayefaa na
kupendwa na wengi, usiye na kashfa na kadhalika
na kadhalika. Lakini pia, gazeti lako hilo litashiriki
kwa siri kuwachafua na kuwapaka matope
wagombea wengine kwa hila , wagombea ambao
watakuwa tishio kwako!”
“Enhe, nikingali nakusikiliza!” Dr. Masurufu alianza
kusisimkwa.
“Huo hautakuwa mwisho, utawanunua wahariri na
wamiliki wa vyombo vingine vya habari pamwe na
waandishi wao, ambao kazi yao itakuwa ni
kukufagilia mpaka chama kitakapokupitisha
ambapo hutalazimika kutumia nguvu katika
Uchaguzi Mkuu kwa vile chama na Serikali yake
vitakusaidia kwa nguvu zote, mpaka unaingia
Ikulu!” Masurufu akakenua
“Je,” Mkewe akahitimisha kwa swali akitabasamu
“Bado tu una hofu?”
“Hapana, sina hofu kabisa!” Alijibu Masurufu kwa
moyo mweupe kabisa.
“Kwa hiyo tunakwenda kupigana siyo? Kupigana
kwa ajili ya maslahi yetu, kupigana kwa ajili ya
urais wetu, kwa ajili ya kuiweka Tanzania ya sasa
na ijayo mikononi mwetu siyo!”
“Ndiyo mke wangu!”
“Ahadi?!”
“Ahadi!”
“Good!” Glady akafurahi akitabasamu. Alikuwa
amefaulu kumfanya mumewe arudi katika reli.
Arudi kuyatazama maisha katka mwanga bora.
Mwanga ambao kama utawamulika vizuri
utawafanya waingie katika historia ya nchi na
kuishi kama sio kukumbukwa milele. Heshima iliyo

SURA YA PILI
KIGOMA - 1952

Wakati Tanganyika inapata uhuru mwaka 1961,
Masurufu Hussein Masurufu alikuwa na umri wa
miaka kumi na miwili akiwa darasa la pili katika
shule ya Mkoloni. Alikuwa kijana shababi na
umbile lake liliashiria kuwa atakuja kuwa jitu la
miraba mine baadae. Alijaaliwa sura jamali
iliyowavutia wengi ingawa mwenyewe hakulijua hilo
kwa wakati huo.
Baba yake Kepteni Hussein Masurufu alikuwa
katibu Mkuu wa TANU kanda ya magharibi kanda
iliyojumuisha mikoa ya Kigoma, Tabora na Rukwa.
Yeye akiishi Kigoma Mjini.
Akiwa miongoni mwa wazee wa awali wa
Tanganyika walioianzisha TAA na baadae
kumkaribisha Nyerere kabla hawajamchagua kuwa
Mwenyekiti wake, Hussein alikuwa ameshiriki kwa
kina katika harakati za kuisambaza TAA na baadae
TANU, na kupigania Uhuru mpaka hapo
ulipopatikana
Kuipenda kwake TAA hakukuja bure, alijikuta
akiipenda TAA kupita kiasi baada ya kuchoshwa na
utawala wa kibabe na wa kidhalimu wa wakoloni
wa Ujerumani na baadae Waingereza.
Awali alikuwa chini ya wajerumani Kapteni wa
meli, akiendesha meli za MV Lyemba na MV
Mwongozo zilizokuwa zikitoa huduma katika ziwa
Tanganyika kwenda katika nchi za Zambia, Burundi
na Zaire (sasa Congo), kupitia katika vijiji vilivyopo
katika mwambao wa Ziwa hilo lenye kina kirefu
kuliko yote Afrika. Katika Dunia likishika nafasi ya
pili baada ya lile la Bekari lililopo Urusi.
Alikuwa akilipwa mshahara mzuri wa wastani
uliomfanya awe na maisha mazuri tofauti na
wananchi wengi ambao walikuwa hawaishi
kuwatupia lawama wakoloni kuwa hawafai
hawafai.
Yeye akiwa na kisomo cha darasa la nane,
kilichomuwezesha kuzijua lugha za kingereza,
kijerumani, kigiriki na kiitaliano sawasawa, mke
mzuri, nyumba bora, mshahara wa kutakata na
mengine mengi, kamwe hakuona ubaya wa
wakoloni mpaka ilipofika siku ile.
Siku ambayo alikuwa anakabiliwa na safari ya
kwenda Zambia na baadae Zaire. Kama kawaida
alijilawa asubuhi na mapema na kuelekea bafuni.
Aliporudi mswaki ukingali mdomoni na taulo likiwa
mkononi ndipo mambo yalipoanza kuwa mambo.
Mkewe ambaye alikuwa mjamzito mwenye mimba
ya miezi nane na ushei alikuwa akigaa gaa huku
na huko kitandani mdomoni akiachia mayowe
yaliyoashiria kuwa alikuwa ndani ya Uchungu
uliopatiliza
Taulo likatupwa kushoto mswaki ukindondoka
mdomoni bila yeye kuwa na habari akakimbia
kimbia hovyo mle ndani akishika hiki na kile bila
uelekeo maalumu baadae akili zikamrejea,
akamjongelea mkewe na kumuuliza
“Fatuma…. Fatuma, vipi mpenzi?!”
“Na… na…. nahisi siku zimefika!” Akasema kwa
taabu akishusha pumzi kwa nguvu. Maumivu
yakamzidi katika nyonga.
“Kwani hujaenda kliniki tena?”
“Nilienda! Niitie gari Hussein”
“Madaktari walisemaje?”
“Gari Pliz, gari tafadhali”
“Bila kujua tatizo ita…!
“Hussein!” Fatuma akabweka kwa nguvu machozi
yakimtoka kwa wingi. Hussein Masurufu
akashtuka, “Naam!” Akaitika kwa woga!
“Unataka nife?”
“Oooh! No hapana…. Hapana mahabuba wangu
nakupenda sana!”
“Basi ita gari Upesi!”
Wakati anainuka akayaona majimaji mazito
yakichuruzika katika miguu ya mkewe. Akaogopa
zaidi umakini ukimpotea akaondoka upesi
akielekea sebuleni akajigonga katika mlango na
kuanguka chini.
“Shit!” Akaguta akiinuka na kuingia sebuleni.
Akaifikia simu ya mezani na kupiga hospitali
kuomba aletewe gari la wagonjwa. Baada ya
kuelekeza vya kutosha, alirudi tena sebuleni kwa
mkewe, akawa akiugulia pamoja nae. Ingawa huu
ulikuwa uzazi wake wa kwanza, na uchungu
ulikuwa ukimsumbua bado, lakini mafundisho
aliyoyapata kabla hajaolewa na Hussein Masurufu
yalikuwa yakingali mabichi kichwani mwa Fatuma.
Alimuagiza mumewe amuandalie kanga na pamba
za kutosha katika mkoba. Alimwambia pia
amchukulie kadi ya kliniki chupa la chai na vingine
vingi.
Kutahamaki gari lilishafika
Fatuma alichukuliwa mpaka katika hospitali ya
Maweni akapokelewa na kupewa kitanda. Manesi
wakimuakikishia Hussein kwamba mgonjwa wake
angejifungua baada ya muda mfupi.
Dakika kumi baadae akawa ndani ya Teksi no. 7
Peugeot 404 mali ya mzee Shaka wakieleka
Kasingirima Ujiji aliko mama mzazi wa Fatuma
Malilo. Ambako alifika anamzoa na kuja nae
hospitali.
Kichwa chake kikiwa hakitulii, Hussein Masurufu
alirandaranda hospitali nzima bila uelekeo
maalumu mpaka zilipokuja zile taarifa za faraja
masaa sita baadae, kwamba mkewe alikuwa
amejifungua mtoto wa kiume kwa operesheni
ndogo.
Furaha zilizomvaa hazikuwa na mfano, “Nami
nitaitwa baba! Nimemzaa baba yangu! Mzee
Masurufu Laiti angelikuwepo!” Aliendelea kufurahi
nusunusu mpaka waliporuhusiwa kuingia wodini na
yeye kukabidhiwa mtoto ambebe! Akambeba kwa
furaha na bashasha, tabasamu likiupamba uso
wake. Walifanana kama reale kwa ya pili
Waliporuhusiwa na kurejea nyumbani, ndipo akili
zilipomrejea Hussein kwamba alitakuwa kuwa
ndani ya meli ya Liemba muda huu akiwapeleka
abiria Zambia, Zaire na baadae Burundi. Ukweli
huu ukafanya akiliye iingiwe na ganzi.
Aliwafamu waajiri wake vizuri sana kosa dogo tu la
kutosafisha sakafu vizuri lingeweza kukugharimu
kibarua. Au wizi wa mali ya shirika wakati chombo
kikiwa safarini, hukumu yake ilikuwa kutoswa
baharini na kupoteza maisha yako.
Akajifikiria yeye!
Meli ilitakiwa kuondoa saa mbili kamili asubuhi.
Inapeleka abiria. Abiria waliolipa pesa zao, pesa
ambazo zinampa yeye mshahara. Mpaka muda
huu saa nane mchana yeye alikuwa hajatokea
bandarini
Masaa sita mbele!
Akajipeleka ofisini kama ambavyo mbwa hujipeleka
mbele ya chatu tayari kuliwa! Yeye akiamini
kwamba alikuwa na sababu ya msingi. Sababu ya
kuokoa maisha ya mkewe na maisha ya mwanae.
* * *
 
SEHEMU YA PILI.
waajiri wake vizuri sana kosa dogo tu la
kutosafisha sakafu vizuri lingeweza kukugharimu
kibarua. Au wizi wa mali ya shirika wakati chombo
kikiwa safarini, hukumu yake ilikuwa kutoswa
baharini na kupoteza maisha yako.
Akajifikiria yeye!
Meli ilitakiwa kuondoa saa mbili kamili asubuhi.
Inapeleka abiria. Abiria waliolipa pesa zao, pesa
ambazo zinampa yeye mshahara. Mpaka muda
huu saa nane mchana yeye alikuwa hajatokea
bandarini
Masaa sita mbele!
Akajipeleka ofisini kama ambavyo mbwa hujipeleka
mbele ya chatu tayari kuliwa! Yeye akiamini
kwamba alikuwa na sababu ya msingi. Sababu ya
kuokoa maisha ya mkewe na maisha ya mwanae.
* * ********

Hussein hatakaa aisahau siku ile. Maana alimkuta
mwenyeji wake Meneja uajiri akiwa mwekundu
amefura kwa hasira. Hakupewa hata nafasi ya
kusikilizwa, alitupiwa barua ya kufukuzwa kazi
akingali mbali wa hatua tano hivi toka ilipo ofisi ya
Meneja.
Maneno ya kashfa kejeli na dharau yakimfuta huku
akimtimua na kumfukuza ki-mbwa kinguruwe!
Katika mambo yote hili Hussein hakulitarajia.
Kufukuzwa kazi?! Kwa staili hii? Hata kama
alikuwa na makosa bado alikuwa na haki ya
kusikilizwa, haki ya kuachishwa kistaarabu na
mengine mengi. Ni hili lililomfanya asiondoke licha
ya matusi na kashfa alizopewa.
“Tokah!” Von Duzy Meneja uajiri akaunguruma
“Toka unasuburi nini? Sitaki uingie ofisini kwangu
wala sitaki kukuona hapa teena. Tokah!”
“Ungenisikiliza kwanza lakini!”
“Eti nini?” Kicheko cha Uchungu kikamtoka Von.
“Sikiliza wewe Sokwe mweusi usiye na mkia.
Baada ya hasara yote uliyotutia bado unataka
tukusikilize? Umefanya tuingie gharama ya
kumkodia mtu ndege kutoka Zambia aje apeleke
meli? Tumekupigia simu hupatikani tumekuja
nyumbani kwako haupo, la hapana wako wengine
wa kuvumilia sio sisi. Tokaah!”
“Ndio, ungenisikiliza sasa!”
“Sitaki, tokaah!”
“Nilikuwa na matatizo…!”
“Tokaah!”
“Mke wangu ame…!”
“Tokaah!”
“Lakini…!”
“Tokaah!”
Hasira zikaanza kumpanda Hussein. Mikono
ikanza kumchezacheza hali akili yake akishindwa
kuidhibiti sawaswa. Naye akabweka!
“Sitoki! Sitoki sasa!”
Von akageuka na kumtazama vizuri, zaidi
akimshangaa. Hussein akaendelea
“Kama mnadhani kunifukuza ndio tumemalizana
mnakosea. Nimekuwa mfanyakazi wenu kwa
karibuni miaka 10 sasa. Bado nina wadai haki
zangu nyingi tu, tena za msingi kabisa.”
“ Haki?” Von akauliza kama ambaye hakulisikia
vizuri neno lile.
“Ndiyo haki!” Hussein akaunguruma tena.
“Haki gani?”
“Kwanza mafao, nataka nipewe pesa zangu za
kiinua mgongo!”
“Oooh!” Alikuwa Von kwa dharau, kumbe unataka
haki; ngoja nikuletee. Von akavuta hatua ndefu
ndefu mpaka pale aliposimama Hussein.
Alimpofikia tu bila kuchelewa akaupeleka mkono
wake kushoto na kuurudisha kwa nguvu, ukatua
vizuri sana katika shavu la kulia la Hussein na
kulia Paah! “Ukiambiwa uwe unaelewa kenge we!”
Ikawa kauli iliyosindikiza kofi.
Kofi kali la Kelbu.
Hussein akayumba mara mbili kwa nguvu na
kwenda chini sikio lake la kulia likipiga mbinja ya
kukata na shoka. Alikuwa amepigwa na kitu kama
ubao vile. Shavu lote lilikuwa linawaka moto
vibaya sana.
Kupigwa?! Hussein akashangaa zaidi ya alivoumia.
Hakuwa na kumbukumbu kama aliwahi kupigwa
toka kule shule ya msingi ambapo alichapwa fimbo
mbili tu kutokana na mwenendo wake mzuri.
Hasira sasa zikauvaa mwili katika namna ambayo
hakuweza kuihimili. Akaimuka kama zombie,
akamkamata Von na kumkunja kunja huku
akimsuka suka kwa nguvu kabla hajampigiza chini
mara mbili.
Pamoja na Von kujitahidi kupambana na Hussein
bado alijikuta chini mara kadhaa mpaka nguvu
zilipomuishia ambapo aliamua kupiga filimbi ya
hatari iliyofika inatuama kunako masikio ya walinzi
wake vibaraka.Wakaja mbio na kumdhibiti Hussein.
Hapo ndipo Von aliposimama akaanza kumtandika
Hussein makonde mazito mazito katika katika
tumbo, mbavuni, usoni na pengine popote
alipoweza kupiga. Alimtandika hasa, alimtandika
kweli kweli. Kutoka hapo mashataka yakaandaliwa
ombi likapelekwa kwa DC na baadae mahakamani.
Kesi ikapelekwa haraka haraka, hatimaye Hussein
akafungwa jela miezi tisa na kazi ngumu.
Hakuna cha mafao, hakuna haki, hakuna
kusikilizwa, hakuna kila kitu na kifungo juu.
Alipotoka kifungoni, kila kitu kilikuwa kimebadilika!
Kila kitu. Alikuwa amepoteza kazi, wamefukuzwa
katika nyumba ya Shirika mwanae alikuwa na afya
mbaya huku akiwa hana uhakikia wa chakula; Hali
wajerumani wakiwa wameondoka tayari na nafasi
yao kuchukuliwa na Waingereza. Ni hili lililomfanya
awachukie wakoloni.
Akaapa kupambana nao.
Kupambana kwa hali na mali. “Ni aibu
kutawaliwa!” Aliropoka mara kwa mara
akiwahamasisha wenzake kuungana pamoja ili
kumtia adabu Mjerumani, “Umoja ndiyo nguvu
yetu. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu!”
Aliendelea kuhamasisha. Watu wakaendelea
kumuunga mkono.
Halafu akasikia kitu
Kwamba akina Abdulwahid Sykes, Dossa Aziz
Dossa na Tewa Said Tewa walikuwa wameanzisha
chama, Tanganyika African Association TAA.
Chama cha kudai na kupigania uhuru. Zilikuwa
zaidi ya habari njema. Haraka akaruka hadi Pwani
akaeleza dhamira yake na kupokelewa kwa mikono
miwili akapewa kanda nzima ya magharibi
ahangaike nayo.
Akarejea nyumbani na kuhangaika nayo.
Hata Nyerere alipojiunga na TAA baada ya juhudi
zake na wenzake za kuanzisha chama cha
kupigania Uhuru wa Tanganyika yeye na wenzake
kule Makerere kukwama, alikuta wakina Hussein
wameshafanya kazi kubwa hasa. Kazi ya kutosha
kama sio kujivunia.
Kwa sababu ya usomi na uwezo wake wa kujenga
hoja, kushawishi wachilia mbali Busara na hekima
alizokuwa nazo, Nyerere akapewa Uongozi mara
moja katika mkutano uliofanyika Tarehe 17 April
1953 katika ukumbi wa Arnatouglo; huku
waanzilishi wakikaa pembeni kwa hiyari yao.
Wakibakia kuwa washauri. Na hatimaye ikaundwa
TANU badala ya TAA chini ya Nyerere.
Na matunda yakaonekana. Ghafla TANU ilivuma na
kupaa kama dege la kivita. Kila mmoja aliisikia.
Kila mmoja akaipenda kuitamani, kuikubali na
kuihubiri. Nchi ikawa haitawaliki kwa raha. Kila
mara, kila mahali ikawa ni kelele za Tunataka
Uhuru! Tumechoka kutawaliwa!
Wakati huu akiwa anatawala Muingereza hali
ilikuwa mbaya zaidi, watu walipigwa na wengine
kuuawa wakidai na kuulilia Uhuru, wakiupigania
ujamaa na kujitegemea wakiuhami umoja na
mshikamano hadi ilipofika ile siku.
Siku ambayo Nyerere alisimamama katika baraza
la Udhamini la la Umoja wa Mataifa pale New York
Marekani na kuuhutubia Ulimwengu. Akawaambia
Waingereza sasa inatosha! Mmeshatutawala kiasi
cha kutosha, Tunataka nchi yetu, Tunataka Uhuru!
Kama mnadhani kwamba hatuna uwezo wa
kujitawala mmekosea sana. Tupeni nchi yetu kisha
mje kuitazama tena baada ya miaka kumi tu.
Mtaona jinsi tutakavyokuwa tumeboresha huduma,
mtaona tutakavyokuwa tunaishi kwa upendo,
amani na mshikamano, mtayaona matunda
matunda ya uhuru wetu, mtaona… mtaona!
Nyerere akasema mengi na vingi. Hotuba yake
ikamvutia na kumsisimua kila mmoja. Mmoja wapo
akiwa Malkia wa Uingereza. Huyu aliamua
kumtembelea Nyerere jioni yake Akamsaili hili na
kumuuliza lile. Akapokea maelezo timilifu
yaliyomtosheleza. Mpaka anaondoka, moyo wake
ulikuwa safi na usio na chembe cha shaka juu ya
Tanganyika.
Hatima ya mkutano huo ikawa ni Nyerere kurejea
tena Uingereza kwa mara kadhaa na aliporudi kwa
mara mwisho, Uhuru wa Tanganyika ukawa
umepatikana.
Kila mmoja hakuamini. Kila mmoja alifurahi kupita
kiasi. “Hatimaye!” watu walinong’ona baada ya
kuona bendera ya Mwingereza ikishushwa na
kupandishwa ya Tanganyika “Mwingereza
amesalimu amri! Shenzi taip!” walihitimisha.
Miongoni mwa watu ambao hawakujiweza kwa
furaha alikuwa Kepteni Hussein Masurufu. Yeye
alicheka mpaka nguvu zikamuishia. Akacheka
mpaka machozi yakamtoka.
Aliitamani alie, apae juu hadi juu ya kilele cha
Mlima Kilimanjaro akaitangazie dunia kuwa
wamefaulu kuirudisha nchi mikononi mwa
watanganyika, akatamani laiti angeweza kufyatuka
atoke mbio aende mpaka kule bandarini ili
akampashe yule -----, gabachori wa kijerumani
Von. Kwamba nchi imerudi mikononi mwa wenye
nayo, wananchi! Na kwamba afungashe kila kilicho
chake arudi kwako.
Hakuweza kufanya lolote kati ya hayo, na hii
ilikuwa ni baada ya kujikumbusha kuwa
Wajerumani walishaondoka kitambo. Akaishia
kucheka tu. Alicheka na kucheka na kucheka. Watu
walipomuulizia jibu lake lilikuwa moja tu “Yako
wapi?
Wangemuulizia zaidi angeanza kuimba ule wimbo
maarufu wa uhamasishaji “Wako wapi
waliowakijigamba sasa twawataka! Tumekwisha
kuwakanyagaa..!”
“Huu Uhuru unatufanya tuwehuke sasa!” Mmoja
alihitimisha wakiondoka.
* * ******** * *******

Akiwa amekwishakuwa mwanasiasa mzoefu,
Kepteni Hussein Masurufu alikataa tena kurudi
kuendesha meli, kazi aliyokuwa akiifanya awali.
Hili lilijiri wakati kamati kuu ya TANU, ilipoketi
chini ya Uenyekiti wa Rais Nyerere na kuamua kipi
kiende wapi baada ya Uhuru.
Kwa kuzingatia historia yake na mchango wake
katika chama, Hussein alikuwa amepewa
kuisimamia Bandari ya ziwa Tanganyika.
Akawashangaza watu pale alipokataa jukumu hilo.
Alipotakiwa kutoa sababu zilikuwa tele, kwamba
ameshazoea harakati, kwamba umri ulikuwa
unaanza kumtupa mkono na hadhani kama
angeweza kuhimili mikikimikiki ya Bandari. Akataka
aendelee kuwa Mwanasiasa.
Ni hapo alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa TANU
kanda ya magharibi ili aendelee na siasa. Aendelee
kufanya ile kitu roho yake inapenda. Aliifanya kazi
hiyo kwa miaka michache kabla hajateuliwa kuwa
Katibu Tawala wa kanda ya magharibi, wadhifa
aliondelea nao hadi alipostaafu miaka mingi
baadae.
Masurufu angali anakumbuka vizuri sana.
Kwamba kitendo cha baba yake kustaafu kilikuwa
kama kukata mzizi wa mwisho wa mawasiliano
baina yake na TANU na viongozi wa Serikali.
Vile alikuwa kiongozi bora na siyo mtawala, vile
alikuwa mkweli wa maneno na vitendo, vile
ambavyo alichukia ubepari na kukataa
kujilimbikizia mali kama walivyo Nyerere, Kawawa
na wengineo, Kapteni Hussein Masurufu alijikuta
hana pa kushika.
Hakuwa amejilimbikizia mali, rasilimali pekee
aliyokuwa nayo lilikuwa shamba la michikichi la
ekari tano ambalo ndani yake kulikuwa na kibanda
cha kuishi kilichokandikwa tope na kuezekwa Bati
huko katika mashamba ya Ruwanda kando kando
ya mto Luiche.
Baada ya kustaafu na kutoka katika nyumba za
shirika la nyumba la Taifa pale Mwembetogwaalik
okuwa amepangiwa, Hussein Masurufu alikwenda
kuishi katika kibanda hicho yeye na familia yake.
Wakati huu mwanae Masurufu alishakuwa mkubwa
akielekea kunako balehe, sasa akiwa anasoma
middle school.
Maisha mapya baada ya kustaafu katika viunga
hivi vya mto Luiche yalikuwa mabaya na
yaliyoumiza sana waliishi kwa kutegemea kilimo
ambacho nacho hakikuwa msaada wa kujivunia.
Hali ikiwa hivi kwa upande mmoja upande, upande
wa pili mafuriko hayakuwaonea huruma hata
kidogo, yaliwajia mara kwa mara na kusomba
mazao kama sio mifugo yao. Yalisomba hata akiba
ya chakula walikuwa wamehifadhi ghalani kwa ajili
ya baadae.
Nguvu zikiwa zimeanza kumtupa mkono, Hussein
kwa msaada wa mwanae Masurufu alifanya kila
alichoweza kutaka kuonana na viongozi wa TANU
ili wafikishe kilio chake makao makuu ambako
wangeweza kumsaidia.
Jibu alilopewa mara zote lilimtia matumaini
“Suala lako linajulikana na linashughulikiwa njoo
mwezi ujao, kila kitu kitakuwa sawa!” Sekretari
angemjibu lakini angekuja tena huo mwezi ujao jibu
hili hili lingekuwa linamsubiri tena. Mara hii
alipojibiwa tena hivi mwanae Masurufu hakukubali
“Lakini mwezi uliopita ulituambia hivyo hivyo”
akakumbusha kwa hasira.
“Mimi nakueleza nilichoambiwa!” Alikuwa Sekretari
wa Mwenyekiti kijeuri kabisa.
“Ndio maana nimekwambia leo tunahitaji
kumuona. Vyovyote iwavyo lazima tumuone.
Hatutaondoka hapa hadi tumemuona!”
“We bwana ni kiziwi, hayawani au kitu gani?”
Sekretari akauliza kwa karaha akiacha kujipodoa
kwa muda na kumtazama Masurufu kwa jicho kali.
Akaendelea, “Nimekwambia Mwenyekiti hayupo
mwezi wa pili huu. Anahudhuria semina za
Utawala bora kule Ngurdolo! Semina zitachukua
mwezi mzima!”
“Basi tumuone Katibu mkuu!”
“Hayupo pia! Wameondoka pamoja!”
Kitu fulani kikamfanya Masurufu ashindwe
kuondoka hapo, akimtazama baba yake, akifikiria
shida walizonazo kule shamba na yale mafuriko ya
wiki iliyopita ambayo yaliwachukulia akiba yote na
kuwaachia roho zao katika tundu la sindano baada
ya wao kuparamia paa la nyumba, akaona leo
hawezi kuondoka mpaka kimeeleweka.
“Kwa hiyo?” Akauliza tena. “Shughuli za hapa kwa
wakati huu anazifanya nani? Au wameondoka na
ofisi yao?”
Jicho alilotazamwa lilitosha kuwa jibu.
“Si nimekuuliza dada yangu!”Akakazania.
“Anakaimu Mapunda! Program 0fficer!”
“Tunaomba tumuone huyo huyo, pengine hujui tu.
Lakini wenzio tuna tatizo na kuendelea kwenu
kutupiga kalenda kunatuumiza zaidi.”
“Naye hayupo! Msubiri pale katika benchi la ofisi
yake.”
Alipomaliza kuwaambia hivyo akageukia kioo
chake na kuendelea kujipodoa! Hussein na mwanae
wakaenda na kuketi.
Mapunda aliingia ofisini saa tisa mchana. Alikuwa
na haraka mno. Akawasikiliza kidogo na
kuwaambia, “Suala lenu linashughulikiwa! Njooni
wiki ijayo!”
Hussein ambaye wakati huu hakuwa muongeaji
sana alimtuliza mwanae na wakaondoka na kurejea
shambani kwao. Njiani alisononeka sana
kutosikilizwa, thamani yake kutoonekana na vibinti
vidogo vidogo kutomtambua na kumdharau kana
kwamba alikuwa si lolote si chochote.
Masononeko hayo na hali halisi ya maisha
waliyoishi vilimchosha, kumuudhi na kumuumiza
sana mwanae Masurufu. Akajikuta anaanza
kukichukia chama, Serikali na viongozi wake.
Binafsi hakuona ni vipi chama kilishindwa
kutengeneza mifumo ya kuwasaidia watu
waliojitolea jasho na damu katika kupigania
kufikisha chama hapo kilipofika. Hakuona ni vipi
walishindwa kumjengea mzee wake nyumba ya
kisasa, kumpa gari ya kutembelea na nyenzo
zingine za kuboreshea maisha katika wakati huu
ambapo nguvu zilikuwa zimemtupa ukweli wa
kumtupa.
“Bahati yake!” Hussein alimsikia mwanae
akiropoka kwa bahati mbaya, mara tu
walipomaliza kujenga zizi jingine. Akamsaili kwa
macho na kugundua kwamba ingawa Masurufu
alikuwa jirani yake pale alipoketi juu ya mtumbwi;
lakini alikuwa maili nyingi nje ya pale kifikra.
Ilikuwa ni katika wakati huu Hussein alipopata
fursa nyingine ya kumwangalia mwanae vizuri.
Alikuwa kijana barobaro hasa, videvu vikianza
kuchomoza kidevuni misuli iliyokaidi kukaa vizuri
katika mikono yake ilikuwa imevimba na kutokeza
hapa na pale katika mikono yake na kuashiria kitu
kimoja tu, kuwa itakuwa mikono yenye nguvu.
Ile sura ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa
imeanza kuachana na ujamali, sasa ilikuwa
imerandana na ya kwake ikiashiria upole na utulivu
siku zote. Kifua kipana na mwili wa wastani, upole,
utaratibu, busara na hekima vilimfanya Hussein
atabasamu tena. Alikuwa amejizaa “Bila shaka
litakuwa jitu la miraba minne”

ITAENDELEA
 

SEHEMU YA TATU

ni katika wakati huu Hussein alipopata fursa
nyingine ya kumwangalia mwanae vizuri. Alikuwa
kijana barobaro hasa, videvu vikianza kuchomoza
kidevuni misuli iliyokaidi kukaa vizuri katika mikono
yake ilikuwa imevimba na kutokeza hapa na pale
katika mikono yake na kuashiria kitu kimoja tu,
kuwa itakuwa mikono yenye nguvu.Ile sura ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa
imeanza kuachana na ujamali, sasa ilikuwa
imerandana na ya kwake ikiashiria upole na utulivu
siku zote. Kifua kipana na mwili wa wastani, upole,
utaratibu, busara na hekima vilimfanya Hussein
atabasamu tena. Alikuwa amejizaa “Bila shaka
litakuwa jitu la miraba minne”
Akanong’ona, akiendelea kumuangalia mithili ya
msanii anayeangaliwa kazi bora kabisa aliyoifanya
kwa mikono yake.
Halafu wazo likampata. Itakuwaje mwanae akiwa
mwanasiasa, kama yeye? “Bila shaka na yeye
ataishia katika maisha haya!” Akawaza kwa uoga
akijitahidi kuyafukuza mawazo haya.Lakini ikamshangaza mawazo haya yalipoonyesha
ukaidi, yakarudi kumtembelea tena tena. Katika mawazo haya alimuona mwanae katika picha na vyeo vya kisiasa. Ubunge, Uwaziri na kadhalika,
akipitia huku na huko akifanya mambo makubwa
kama akina Nyeree, Kawawa, Sokoine, Karume na
wengine.Vyombo vya habari vikimsimulia kama kiongozi wa
mfano, mtu wa watu kama baba yake, akialikwa
huku na huko kufanya shughuli za kijamii zenye
tija. Akiwa havumilii uozo wa aina yoyote, hana
tamaa ya utajiri, muadilifu, mwenye kukubali
matakwa ya jamii, mtu wa watu n.k.Huku yeye Kapteni Masurufu wakati huo licha
pengine ya umri wake kuwa umeenda sana
akisimama kidete kumshauri kufanya haya na yale,
historia yake ikiendelea kudumu masikioni mwa
watu kupitia kwa mwanae Neema iliyoje! Fahari
iliyoje? Akawaza tena tabasamu lake likikomaa
zaidi.Bila shaka, akaendelea kuwaza kwa furaha hali tabasamu likiwa bado limeupamba uso wake. Nchi itakimbia vibaya sana. Utendaji wake utawaambukiza vijana wengi kama sisi tulivyoambukizwa uadilifu na Nyerere, na hapo
Tanzania itaelekea moja kwa moja katika nchi ya
maziwa na asali bila wasiwasi wowote tena…
“Bahati yake!” Sauti ya mwanae ikatoka tena kwa
ukali ikayakata mawazo yake. Akaacha kuwaza na
kumtazama Masurufu kwa mara nyingine tena.
Bado Masurufu alikuwa mbali kifikra. Akamsogelea
taratibu na kuketi jirani yake. Akamtikisa mwanae
taratibu, akimuuliza.
“Bahati yake nani?”
Mwanae akashtuka na kutaharuki “Hapana!”
Akasema kwa hofu na kuongeza “Hakuna kitu!”.
Hussein akamkazia macho na kumsaili tena
“Kwani nani amesema kuna kitu?”Masurufu akababaika asijue mzee wake amekusudia nini hasa Akajikusuru “Si wewe umeniuliza?”
“Ndiyo nimekuuliza, Bahati yake nani? Sijakuuliza
kama kuna kitu!”
Masurufu akashindwa kujibu. Mzee Hussein akaendelea “Mara mbili nimekusikia ukitamka kwa dhati bahati yake! Tena ukiwa hatua nyingi nje ya hapa kifikra. Ndio maana nikaona nikurudishe
tusadiane kufikiri usiumize kichwa peka yako mwanangu!”
Masurufu akatahayari.
Akashangaa jinsi alivyokosa umakini hata akaruhusu maneno kutoka nje ya kinywa pasipo ridhaa yake. Hakujua ametamka mangapi akiwa
katika hali hiyo. Hata hivyo akajikakamua na
kusema “Leave it baba, yaache tu. Hayawezi kukusaidia!”
“Kwa nini?”
Akashusha pumzi. “Nahisi kama ni ya kijinga. No!
yaache kama yalivyo baba!”
“Masurufu!” Hussein akaita kwa upendo. Mwanae akaitika “Naam!”
“Umeanza lini tabia hii?”
Masurufu akatatanishwa, akainua uso na kumtazama baba yake. Akajikuta akitazamwa mfano wa fundi aingaliavyo saa ya thamani kutafuta tatizo liisumbuavyo. Akashindwa kuyakabili macho ya baba yake na kuangalia chini haraka.
“Tabia gani?” Akauliza kwa sauti isiyo yake!
“Ya kunificha mambo yako?”
“Kukuficha mambo yangu? Mambo gani baba?”
“Mambo yako ndiyo!! Mara hii umesahau kwamba
mimi ndimi baba yako, rafiki yako mpendwa na
mwandani wako pekee. Ambaye daima
nimeondokea kuwa mshauri, kiongozi na msiri
wako mkuu. Ulidiriki kuniambia hata habari za Glady msichana ambaye ungependa awe mkeo
baadae! Mbona hayo hukutaka niyaache yalivyo?!
Halafu ujinga unaoweza kukutoa mbele yangu na
kukupeleka maili nyingi nje ya hapa, ni ujinga ambao kila mzazi mwenye mwanae angependa kuusikiliza. Au ndio umekuwa sana siku hizi?”
Masurufu akajiona mwenye hatia.
“Mimi najua!”Aliendela kushutumu mzee Hussein
“Najua lipo jambo. Tena jambo kubwa, jambo linaloitafuna akili yako kiasi hata cha kuondoa kama sio kuathiri umakini wako. Na kwa taarifa yako mimi ninamjua sana Mwanangu Masurufu.
Huwa hapotezi umakini kizembe.Toka ulivyomaliza kazi niliyokutuma na wewe
kuketi juu ya mtumbwi huo, nimekuwa jirani yako
nikikuangalia na kufuatisha kila akitendo chako,ambapo nimegundua mengi tu! Ndio maana nakuuliza umeanza lini tabia hiyo?” Akahitimisha Hussein.Hatia zikamuelemea Masurufu, machozi yakamtoka. Akainuka na kwenda kupiga magotimbele ya baba yake. Huku machozi yakiendelea
kumtoka akamwambia kwa majuto.
“Samahani baba, nimekosa!”
Baba yake akamuinua pale chini na kumketisha
jirani yake kwa upendo uliotukuka. akamfuta
machozi huku akinong’ona “Haina haja ya kulia!
Usilie kijana wangu. Kulia ni tukio la mwisho unaloweza kufanya baada ya kutokea kitu ambacho hukipendi na jitihada zako zote zimeshindwa kukizuia.Mimi na wewe hatujafika huko bado tukingali tuna nguvu nyingi uwezo mzuri wa kufikiri na njia nyingine mbadala. Tafadhali yahifadhi machozi yako leo, ili siku utakapoyahitaji uweze kuyatumia kikamilifu sawa?” Akatua na kumeza mate
Masurufu akaafiki kwa kutikisa kichwa
“Good!” Baba yake akasema kwa furaha “Sasa
niambie huyo unayemwambia bahati yake ni nani?”
“Nyerere!” Masurufu akajibu pasipo kutafuna maneno
Ilikuwa sawa na nyundo iliyogongwa katika kichwa
cha Kapteni kwa nguvu, Akahisi akipepesuka mithili
ya bondia aliyepigwa konde la maana jukwaani.
Akauliza kwa mshtuko.
“Umesema nani?”
“Nyerere! Julius Kambarage. Baba wa Taifa la Tanzania!” Masurufu alirejea jibule kwa sauti thabiti. Safari hii akimtazama baba yake usoni,kuashiria kwamba alikuwa na uhakika na anachokinena.
“Kwa nini?” Mzee Hussein akasaili kwa macho.
Jibu la Masurufu kwa baba yake likawa kuyasaili
mazingira wanayoishi kwa macho. Ile nyumba ya
tope ya vyumba vinne na sebule mbili ambayo
iliezekwa bati ndiyo kilikuwa kitu pekee cha thamani.
Vingine viivyofuatia vilichusha na kuudhi. Zizi bovu
la ngo’mbe na mbuzi ambalo halikuwa na mifugo
ya kujivunia, mabanda ya kuku ambayo nayo yalikuwa matupu baada ya mafuriko kuwachukua.
Ghala lisilo na kitu, Mashine ya kukamulia mafuta,
michikichi michache isiyo na afya na pengine siha
ya kuridhisha pamoja na kutokuwa na uhakika
vilikwisha baadhi ya vitu vilivyoyafanya mazingira
yao kuwa duni hasa, duni kwa maana halisi.Kamwe maisha haya hayakumstahili mtu
aliyepigania uhuru kwa jasho na damu yake.Hayakumfaa hata kidogo mtu aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama na katibu Tawala wa Kanda ya
magharibi katika Serikali ya wamu ya kwanza.
Hayakumstahili hata kidogo.
Ilikuwa ni baadae sana Masurufu alipoanza kueleza
“Chama kimekutelekeza baba, Serikali hali kadhalika. Jinsi ulivyokitumikia na kukitendea sivyo kinavyokutendea wewe. Nimefikiria sana baba,
halafu nikajaribu kubashiri mwisho wa maisha yetu
nikagundua utakuwa mbaya na unaodhalilisha
kama sio wa kuabisha.
Ni haya yanayoyonifanya nikione chama na Serikali
katika jicho hasi, ambalo daima dawamu huwa halivutii hata kidogo. Na bahati yake alivyoufuta upinzani na vyama vyake. La sivyo mimi ningejiunga na upinzani, nikashirikiana na akina Kasangatumbo, Kasela Bantu, Kambona na wenzao
kuwaeleza wanachi ukweli hata wakauona ubaya
wa chama na Serikali yake. Ningekuwa na mifano
hai Mingi wewe ukiwa mmoja wao!”
Hussein akatabasamu
Mwanae alikuwa anaanza kuiva kisiasa. Uwezo wa
kuunganisha mambo na mazingira, na kisha
kuufanyia uchambuzi mzito, ulikuwa unalithibitisha
hilo vizuri kabisa. Kwa upande mmoja akauhusudu
upande huu, lakini kwa upande mwingine hakuvutiwa na njia aliyotaka kupita mwanae. Njia
ya chuki dhidi ya Nyerere na Serikali yake. Chuki
dhidi ya chama tawala.
Hapana ninahitaji kufanya kitu. Akajiambia akimwambia mwanae.
“Penginse uko sahihi mwanangu, pengine hauko
sahihi. Ninachotaka kukwambia ni hiki, humjui
Nyerere mwanangu. Humjui baba wa Taifa na katika hili kumlaumu au kumchukia ni kumuonea bure. Mimi nimefanya kazi na Yule mtu. Ni mtu muadilifu mfano hakuna, msikivu, mtulivu na mwaminifu hujapata kuona. Mtu anayewatazama wenzake
kwanza. Anayeitazama nchi yake kwanza! Sisi ametulea hivyo na ndio maana unaona hatukujilimbikizia mali japo uwezo huo tulikuwa nao.Mali hizo tuliwawekea ninyi, nanyi mnatakiwa kuzitunza kwa manufaa ya vizazi vyenu.
Unachosahau ni kwamba, Nyerere sasa ni kiongozi
wa juu kabisa nchini. Ana watu na matatizo mengine mengi ya msingi. Na tena usisahau kuwa
mimi ni mwakilishi wa kanda moja tu ya magharibi.
Wapo wa kanda ya mashariki, kanda ya kati,kanda ya Nyanda za juu kusini, kanda ya Kaskazini na kanda ya pwani. Na kote kuna watu zaidi ya
mmoja, ukisema aboreshe mazingira ataboresha
mazingira ya wangapi? Na rasilimali za kufanya
hivyo ziko wapi hali unajua kuwa nchi yetu ni miongoni mwa nchi masikini kabisa duniani?Mbona mie tayari nimepewa kiinua mgongo? Nimejenga na kufuga ingawa Mungu hakupenda.Nadhani kutokuwa na uhakika wa maisha ya kesho kunatokana na sisi kutokuwa na kazi. Unaonaje nikikutafutia kazi mwanangu?” Akahitimsha.
“Hakuna taabu!” Masurufu akakubali akitafakari
maelezo ya baba yake. Alikuwa na hoja, ingawa haikuwa na nguvu kiasi kile. Kama Serikali inaweza kuwahudumia makatibu Kata, Tarafa, Wakuu wa wilaya, Mikoa, Wabunge, Mawaziri, Waalimu,
Wanajeshi na wengineo, inashindwaje kuwaangalia
hawa wapigania Uhuru? Ambao idadi yao haifiki hata mia mbili?
Eti kiinua mgongo! Akawaza kwa hasira. Kiinua mgongo gani ambacho kimeshindwa hata kuigharamia elimu yangu hapa hapa nchini? Hivi
wabunge na mawaziri nao wanalipwa kiinua mgongo kama hiki. Kama sio ugawaji wa rasilimali za taifa usiozingatia jinsia ni nini? Katika hali hii unawezaje kukiita kiinua mgongo?! Hapana hiki ni kiua mgongo kabisa.Na je, hivi yeye Nyerere anaishi maisha kama haya
ya Hussein Masurufu kule Ikulu? Mjadala ulikuwa
mkali sana kichwani mwake. Na aliufanyika kichwani mwake kwa vile alimjua vizuri baba yake,kwamba Demokrasia ilikuwa imemuingia hadi
katika mishipa ya damu yake na kuweka hifadhi ya
kudumu ndani ya mifupa na chini kabisa ya moyo
wake.Kubishana na huyu ni kujisumbua. Akaamua
kukubaliana nae kwa nje huku ndani akimpinga
vibaya sana. Bahati yake hakuna upinzani!
Masurufu akarudia kuwaza tena, baada ya kukubaliana na mzee wake, na mzee huyo kuondoka. Kungekuwa na upinzani imara ningejiunga na kumuondolea mbali! Akahitimisha.
* * ******&******&******

Wiki iliyofuata walirudi tena ofisi za chama pale
mkoani Mapunda akawapokea na kuipeleka shida
yao kwa Mwenyekiti. Mwenyekiti naye
akuwazungusha kwa siku kadhaa mpaka Masurufu
alipomlilia machozi ofisini. Ambapo alisutwa na
dhamira akajikuta akimshughlikia kikamilifu,
wakapata fedha za kutosha kiasi.Pesa ambazo, Hussein alizitumia pia kama nauli
kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kwenda
kuonana na Nyerere!
Walipokelewa vizuri sana, na kupelekwa nyumbani
ambako waliandaliwa chakula cha maana. Chakula
maalumu wakala na kusaza kama vile haitoshi
wakaletewa hiki na kile na mradi tu wajisikie wako
nyumbani.
Jioni Nyerere alirudi, akaketi na kuzungumza pamoja nao. Kapteni Hussein alimueleza maisha anayoishi sasa na jinsi alivyo na taabu. Machozivya uchungu yakamtoka Nyerere.
“Pole sana!” Akamwambia kwa upendo
“Kwanini hukwenda pale makao Makuu na ukawaeleza shida yako?”
“Nilikwenda lakini sikupolewa vizuri.Nimezungushwa karibuni miezi sita!”
“Kitu gani?” Nyerere akaghadhibika
Hussein Masurufu akamueleza kila kitu tokea walivyoanza kufuatilia, dharau walizoonyeshwa,ahadi za njoo kesho na mengine kadha wa kadha hadi pale walipompigia magoti na kumliliavMwenyekiti ofisini kwake ambapo aliidhinisha pesa kidogo walizopewa.
Kilichofuatia hakuna aliyekitarajia.Kwa kutumia simu,Nyerere alimuauru Katibu Mkuu wa TANU Taifa kuushughulikia Uongozi wa mkoa Kigoma kwa vitendo walivyomfanyika Kapteni
Hussein na familia yake, akaomba kupewa taarifa
zake ndani ya wiki moja
“Mie sitapenda uwafukuze kazi?” Hussein alimwambia baadae Hasira zilipotulia. Nyerere akamtazama kwa mshangano, kabla hajamuuliza
baadae.
“Kwa nini?”
“Ningependa waonywe tu, ili kama watarudia tena,
ndippo hatua hizo zichukuliwe maana wana familia
zinazowategemea! Kuwaondoa pale itawafanya
wao na hasa familia zao kuishi katika wakati
mgumu na m’baya zaidi!”
Nyerere akatafakari tena akishangazwa na moyo
wa mtu huyu.
Hata hivyo alitabasamu alipoona kuwa falsafa yake
ya Ujamaa na lile azimio la Arusha vilikuwa vimewakaa watu wake katika namna iliyomfanya hata wakati mwingine awaogope. Walikuwa na huruma mno! Wakawa na upendo uliopitiliza huku
wakiiweka nchi na raia wao mbele. Pamoja na ukweli kwamba wao walikuwa washika wadau wakuu, walihakikisha washikiwa dau
wengine hasa jamii wamenufaika vya kutosha
ndipo na wao walipofikiria kunufaika. Bahati mbaya
washikiwa dau hao walikuwa wengi mno, wengi
hasa! Kuwanufaisha wote ingekuwa shughuli pevu
kweli kweli, pevu haswa! Kwa maana hiyo wao
waliendelea kusubiri mpaka mdau wa mwisho
afikiwe…, ndipo wajifikirie na wao!
“Any way!” Akasema baadae. “Tuache hayo,
tuzungumze yetu, nimemleta kijana! Nataka
umsaidie kupata kazi ili naye anisaidie kuishi.
Pamoja na kazi nataka pia umfundishe siasa!”
Nyerere akamtazama Masurufu kwa muda na kutikisa kichwa. Alikuwa kama anayemuangualia Kapteni Hussein enzi za ujana wake. Akaulizia elimu yake na kuambia darasa la sita.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA NNE
Nyerere akamtazama Masurufu kwa muda na
kutikisa kichwa. Alikuwa kama anayemuangualia
Kapteni Hussein enzi za ujana wake. Akaulizia
elimu yake na kuambia darasa la sita.
Alipouliza sababu ya kutohitimu, jibu lilikuwa lile
lile, umaskini ulioikumba ghafla baada ya yale
mafuriko. Nyerere akasikitika tena.
“Itabidi asome kwanza!”
“Hilo silikatai, lakini kwa sasa huyu ndio mboni
yangu. Namtegemea kwa kila kitu. Nilitegema
mshahara atakaopewa…!”
“Usijali!” Akamkata kalima na kuendelea
“Tutafanya utaratibu uwe unapata senti za
kujikimu, huyu mwache asome. Akifanya siasa
huku ana kisomo atakuwa msaada mkubwa kwa
taifa sawa?
“Sawa” Alikuwa Kapteni kwa shingo upande.
Hakutaka kuendelea kuwa tegemezi kwa chama na
Serikali lakini alipojitahidi alisemee hili, akawa
anazidiwa hoja.
Ndivyo ilivyokuwa.
Masurufu akarudi shule, akawa pia miongozi mwa
watoto kadhaa waliokuwa wakilelewa na mwalimu.
Kapteni Hussein alikaa pale kwa wiki chache kabla
hajaomba ruhusa na kurejea nyumbani kwa
mkewe. Juhudi za kumtaka abakie hapo ikibidi
ailete familia yake zikashindikana.
Kitu kimoja kilikuwa dhahiri kwa Masurufu.
Kwamba mafahali wa uadilifu walikuwa
wamekutana! Mazungumzo yao na mapendekezo
yao kuhusu maisha na familia zao yakawa
yamemfanya ajifunze kitu kikubwa maishani.
Kwamba ni muhimu kuishi kwa ajili ya watu, kwa
ajili ya makundi yaliyo pembezoni. Ili
utakapoondoka duniani uwe umetimiza wajibu
wako wa kuletwa hapa duniani. Jamii ikukumbuke
na uendelee kuishi milele.
Pia akagungua kuwa kumbe Nyerere hakuwa mtu
mbaya. Alikuwa mtu mzuri kwa maneno na
vitendo, akifurahia kuona mabadiliko na maendelo
ya kweli ya watu wake. Lakin ah! Laiti angeliweka
utaratibu wa kuonana na watu wake mara kwa
mara na kusikiliza shida zao…
Akaendelea kusoma akiongeza bidii na juhudi
katika masomo.
* * ********

Ki’ uhakika kabisa, Masurufu aliacha kabisa
kumchukia Nyerere na CCM. Badala yake
akampenda na kumthamini. Akawa jirani nae
akimuomba ushauri huu na ule pamoja na
kumsaidia kazi hizi na zile. Ni katika wakati huu
Nyerere alipogundua akili na Busara za kijana
huyu. Naye akajikuta akimpenda na kumuamini.
Shule alihitimu vizuri akajiunga jeshi la kujenga
Taifa baadae akaenda Chuo kikuu kuchukua Digrii
ya Sayansi na utawala wa jamii miaka mitatu
baadae akarudi na kuwekwa Makao Makuu ya
chama ofisi ndogo pale Lumumba, akisaidia hiki na
kile pamoja na kuisaidia ofisi ya umoja wa vijana.
Hakudumu sana, akapelekwa Kigamboni kuongeza
ujuzi wa kisiasa na kupelekwa nje ya nchi mara
kadhaa. Aliporejea akapewa kazi ya kuwaandaa
vijana kuwa wanasiasa bora, kupenda siasa ya
nchi yao na kupenda kujitolea kwa ajili ya nchi
yao.
Kazi alizozifanya kwa moyo mmoja.
Matokeo yake yalishangaza kama sio
kustaajabisha. Vijana wakatokea kuwa wazalendo
wa kweli , wakiijenga nchi yao kwa kasi ya aina
yake.
Hali ikiwa hivi, akili ya Masurufu ilikuwa haitulii
kila kukicha yeye alikuwa akitafuta mwanya wa
kujilimbikizia mali, kuchuma zaidi. Hakutaka kuja
kuishi kama babaye yake.
Katika Upenzi huo baina yake na Nyerere, alikuwa
amefaulu kutembelea mikoa mingi na akawa
amejionea kwa macho yake namna wastaafu wengi
wakiwemo mawaziri jinsi wanavyoishi maisha duni
kwa kutegemea kilimo na mifugo, huku jamii
ikiwacheka na kuwaona mabwege. Wakitolewa
mfano usiofaa na kususuikwa hata na watoto
wadogo.
Hapana! Haya siyo maisha!! Masurufu akaamua
kwa dhati. Leo Nyerere yupo, kesho atakuwa
hayupo. Nisipogangamala na kuuanika katika kijua
hiki, ntautwanga mbichi.
Kweli akagangamala
Alihubiri na kufundisha uadilifu huku yeye akifanya
uhalifu. Kila ulipotokea mwanya aliutumia
kikamilifu kwa maslahi yake binafsi kwa manufaa
ya baadae. Kila alipotumwa mahala, hakusita
kujipa majukumu ya ziada.
Majukumu ambayo yalimkutanisha na
wafanyabiashara wa magendo, wakwepa kodi,
majambazi wa kalamu na wengineo. Ambapo
aliwatisha na kuwaambia ametumwa na Nyerere
awashughulikie. Kitambulisho chake halisi na kile
cha bandia vikimtisha yeyote aliyeonyesha ukaidi.
Naam! Alifanikiwa, akaunti na miradi yake
ambavyo alivifungua kwa majina bandia na mikoa
tofauti zikinenepa taratibu. Alipohisi uwepo wa
msako wa wahujumu uchumi waliopenya kwenye
chujio la azimio la Arusha, Upesi akazihamisha
pesa zake nchini na kuzifungulia akaunti nje ya
nchi.
Bahati ikawa yake, yeye akapewa ukuu wa
kuendesha msako huo. Ilikuwa neema nyingine.
Waliokamatwa na kufikishwa mbele ya sheria ni
wale tu ambao yeye hakuafikiana nao, au walileta
ujuaji na kujifanya wajuzi.
Nduli alipotuchokoza na mwalimu kutangaza vita,
baada ya TANU kuungana na Afro-Shiraz Party na
kuzaa CCM; Masurufu naye hakuwa nyuma.
Alishirikiana vilivyo kumchapa nduli Amin ambaye
alikimbia na kuacha vitu vingi vya thamani katika
Ikulu yake.
Yeye akiwa miongoni mwa askari wachache
waliongia katika Ikulu ya Uganda na kukuta amana
hizo madini yakiwemo, akajikuta akipagawa huku
akiomba kimoyomoyo wagawane. Hawakugawana!
Badala yake vito hivyo walimpa Masurufu avifikishe
kwa Nyerere kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.
Hakufikisha.
Waliporejea kutoka Uganda na yeye kuzifanyia
utaratibu wa kuzificha na kuziingiza mali
alizochuma katika mkondo halali; akawa
amemkabili Nyerere na kumuomba ruhusa aende
kwao akagombee Ubunge. Nyerere akamshangaa
kwa uamuzi huu, akamuuliza.
“Kwanini umefikiria uamuzi huu Dokta?”
Aseme nini? Akawaza kwa haraka. Ndiyo kwanza
akagundua kuwa hakuwa amejipanga kama
angeulizwa hivi. Sababu ya kutaka kupata
mshahara mnono, saluti, gari la mamilioni, posho
hata ukisinzia, lita elfu moja za mafuta kila mwezi,
na marupurupu mengine, hazikuwa sababu ambazo
zingemvutia Nyerere.
“Nataka kuwa karibu na baba yangu!” Akatamka
baada ya kufikiri kwa muda “Nataka kuwa jirani
nae. Nataka kuwapigania watu wa jimbo langu,
kusaidiana nao kuboresha maisha na miundombinu
yetu! Nataka… Nataka..”
Alisema vingi na mengi! Nyerere alimsaili zaidi na
zaidi kabla ya kuridhika na kumpa ridhaa.
Akamuuliza tena, “Vipi vijana wako pale Umoja wa
vijana?”
“Hakutaribika kitu!” Akamjibu kwa unyenyekevu.
“Nimeacha kila kitu katika mstari. Boniface
ataendelea pale nilipoishia. Ni mmoja kati vijana
wangu ninaowaamini. Na Kigoma sio kuzimu
mwalimu nitakuwa nikirudi mara kwa mara
kuangalia maendelo ya pale nilipoishia. Isitoshe
kuna simu, naweza kupigiwa na kuambiwa hivi au
vile nami nikatoa ushirikiano wangu!” Akamalizia.
Ilitosha.
Mwalimu akainama kutafakari. Masurufu ambaye
sasa alikuwa Daktari wa filosofia alikuwa na
sababu za msingi. Vile alikuwa kijana mwenye
busara na hekima huku akifanya kazi kwa nguvu
zake zote, Nyerere akajaribu kuuhisi upweke
ambao ungemtawala baada ya Masurufu
kuondoka.
Hata hivyo akajirudi pale alipogundua kuwa Dokta
Masurufu sasa sio mtoto tena ingawa angali
alikuwa akihitaji ushauri wa hapa na pale. Ushauri
utakaomfanya aendelee kuwa Masurufu halisi
liwazo na chaguo la watu.
“Dokta” Nyerere akasema akingali ameinama kwa
tafakari “Sio uamuzi mbaya! Sio uamuzi mbaya
hata kidogo. Bahati mbaya na mimi nang’atuka,
Uchaguzi ujao sitagombea Urais wa nchi hii tena,
miaka ishirini na mitano niliyokaa Ikulu ni mingi
sana, inatosha. Nastaafu! Nawapa nafasi wengine.
“Kitu gani?” Dokta akashtuka. Zilikuwa habari
mpya kwake.
“Umesikia vizuri. Ukigombea Ubunge na kushinda
kisha Rais atakayeteuliwa akakuwekea katika
Baraza la mawaziri, nchini itakimbia vibaya sana.
Ni hili linalonifanya nikuruhusu kwa moyo
mkunjufu. Maana hata nikiendelea kukuzuia bado
unatakiwa uwatumikie watanzania wote ambao ni
muhimu kuliko mimi mmoja, watanzania ambao
kwa hakika wanahitaji mchango wako ili
kufanikiwa. Nenda baba, nenda ukatimize wajibu
wako wa kuletwa hapa duniani! Nenda!”
Nyerere alisema mengi kumuasa Masurufu.
Haikuhitaji digirii kujua kuwa Nyerere alikuwa
anaumizwa na kutengana na kijana huyo. Lakini
angefanya nini? Akamruhusu.
Labda ambacho hakukijua na ambacho kilikuwa
chini kabisa ya moyo wa Dokta Masurufu ni ule
ukweli uliotisha. Kwamba Masurufu huyu, hakuwa
yule Masurufu anayeonekana mitaani kila siku
akihubiri na kutenda upendo, midomo yake imejaa
maadili na macho kubeba utakatifu.
Huyu alikuwa Masurufu mwingine chui katika ngozi
ya kondoo. Masurufu mwenye pipi mdomoni hali
mikono yake ikichuruzika damu. Masurufu mwenye
hofu ya umaskini unaochusha na kuudhi baada ya
kustaafu.
Ilikuwa vigumu kwa Nyerere kujua. Kwani Masurufu
aliyafanya haya kwa hila sana, wakati mwingine
katikakati ya usiku mnene huku akiwa kilometa
nyingi nje ya macho na upeo wa Nyerere. Wakati
huo huo akimpeleka kuzimu yeyote aliyeonyesha
kumjua na kutaka kutia mchanga kitumbua chake.
Akaruhusiwa.
Akijua anakwenda kuingia katika siasa rasmi, sasa
Masurufu aliweza kuandaa washenga waliopeleka
posa kwa mpenzi wake Glady. Majibu yalipokuja
mazuri na taratibu zingine kufanyika, ndipo
Masurufu Hussein Masurufu alipofunga pingu za
maisha na Glady Stevenson Ombwe. Ndoa yao
ilifanyikia bomani kwa Mkuu wa wilaya.

****Mnh! Haya...
 
SEHEMU YA TANO
Akijua anakwenda kuingia katika siasa rasmi, sasa
Masurufu aliweza kuandaa washenga waliopeleka
posa kwa mpenzi wake Glady. Majibu yalipokuja
mazuri na taratibu zingine kufanyika, ndipo
Masurufu Hussein Masurufu alipofunga pingu za
maisha na Glady Stevenson Ombwe. Ndoa yao
ilifanyikia bomani kwa Mkuu wa wilaya.
* * *&&&&***

Kigoma alipokelewa kwa mbwembwe kama shujaa.
Dhamira yake ikajulikana mitandao ikaundwa naye
akagombea Ubunge wa Kigoma mjini. Ushindani
ulikuwa mkali, alitumia mbinu huku akipewa
ushauri huu na ule na wazee wa chama Nyerere
akiwemo.
Lakini wananchi wakamkataa, kura zikagoma
kutosha.
Pengine walimwona mdogo kiumri, pengine
walikuwa hawajamzoea na mengine mengi.
Sanduku lilipofunguliwa mpinzani wake alikuwa
amemshinda kwa kura chache. Akiwa
hakutegemea, Masurufu alitaharuki. Akawachukia
wananchi vibaya sana. Akapanga kuwafanyika
mambo ya ajabu ajabu. Lakin mzee wake Kapten
Hussein alikuwa jirani yake siku zote akimfariji kwa
maneno mazuri, maneno yatiayo faraja na nguvu.
“Huna haja ya kukata tamaa kiasi hicho. Umri
wako bado unaruhusu, damu inachemka. Ni wakati
wako sasa wa kufanya maandalizi ili awamu ijayo
usifeli tena. Mwenzio imemchukua miaka kumi
kujiandaa wewe usingweza kumshinda kwa
maandalizi ya miezi sita. Kuchukulie kuondoka
kwake kama fursa ya wewe kujijenga zaidi sawa?”
“Sawa!”
Kweli alijijenga. Akaingia mzima katika shughuli za
uhamasishaji wa chama akipita hapa na kusema
hiki kabla hajashauri kile kule. Upande wa pili
akajizatiti na kupanua wigo wa biashara zake
alizozifungua kwa majina bandia katika maeneo
mbalimbali.
Miaka mitano ilipokatika, Masurufu alikuwa sawa
na mti wa mbuyu kwa ukubwa, Kisiasa alifahamika
na kukubalika sana. Kijamii alikuwa kipenzi cha
watu, katika chama alikuwa kipenzi cha kila
mmoja, hali kitajiri akiwa na uchumi imara kabisa!
Naam, mtu anayejiweza kwa maana halisi!
Safari hii akaongeza na kitu kimoja zaidi.
Akamtafuta Profesa Zonga aliyemsaidia katika
ushirikina. Uchaguzi ulipofika aliingia Bungeni
kama anamsukuma mlevi vile vile. Nyerere alikuwa
angali mshauri mkuu wa Serikali, na kiongozi
anayekubalika sana kwa watu. Dokta Masurufu
hakushangaa pale alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri
wa viwanda na Biashara, Akapelekwa Nishati na
Madini kabla hajateuliwa kuwa Waziri wa Fedha.
Mambo yalikimbia haraka sana, huku mtalamu
wake Profesa Zonga akimpa ushauri huu na ule, na
kumtaka atimize masharti haya na yale. Vitu
ambavyo Dokta Masurufu alivifanya kwa umakini
wa hali ya juu.
Huu ulikuwa wakati mwingie ambao kila
alichogusa kiligeuka dhahabu na kila alichokanyaga
kikawa petroli. Jina lake likaimbwa kila mahala,
wazazi wakawapa watoto jina lake. Akawa kiogozi
wa kutolewa mfano.
Ambacho wananchi hawakukijua ni kwamba
wadhifa huu mpya ulimfanya akutane na watu
wenye kiu kali ya utajiri. Kiu ya kupora na kumiliki
mali ya umma. Watu hawa wakageuka kuwa
marafiki zake na kwa pamoja wakajitengenezea
mtandao wao wa kufisadi mali za umma uliokuwa
na maafisa wa jeshi, mapolisi, wabunge, mawaziri
n.k. kwa lengo la kujinufaisha kwanza wao,
mengine baadae.
* * ********&&&&&&&*******

Halafu ikaja ile ishu ambayo ilimgharimu hasa.
Dokta Masurufu angali anakumbuka vizuri jinsi
ilivyotukia kwa bahati mbaya kama mtoto mwenye
jnsia mbili. Ilikuwa ishu ya msamaha wa kodi kwa
wafanyabiashara wa vifaa vya pikipiki za kichina,
wenye asili ya kiasia. Likiwa dili ambalo
ameunganishwa na rafikie mpendwa Akimu Yusuph
ambaye alimuamini.
Dokta Masurufu akawa amesahau kuchukua
tahadhari zake za kawaida, akafanya majadiliano
na wafanyabiashara hao katika hoteli ya kawaida
ambayo pia kulikuwa na waandishi wa habari.
Waasia hao wakamuahidi kumpa mshiko wa
kutakata kama angeweza kuwaondolea kodi hiyo.
Akiwa Waziri wa fedha, hii ilikuwa shughuli ndogo
sana kwake. Barua moja kwa Mkuu wa Bandari na
TRA, vimemo kadhaa kwa watumishi wa bandari
na kadhalika na kadhalika vingeweza kumfanya
aifanye kazi hiyo kwa wepesi tu. Akaahidi
kuwasaidia
Waandishi wakazinasa habari hizo na kuanza
uchunguzi siku chache baadae shehena ya mzigo
wa spea za pikipiki ukaingia nchini.
Siku hiyo hiyo, Waziri Masurufu akapokea
waandishi ofisini kwake ambao walimuuliza
maswali kadhaa kuhusu spea hizo na tetesi
walizonazo za Spea hizo kutolipiwa kodi.
Akawajibu waandishi wale kijeuri na kuwatimua.
Waandishi wakaondoka na kwenda kuandika hali
halisi.
Habari zilipotoka, Dokta Masurufu alijikuta akiujutia
uamuzi wake. Jamii ilizipokea katika namna
ambayo hakuitarajia. Vyama vya upinzani vikailaki
kama mpira wa kona na kuigeuza ajenda ambapo
viliipigia debe huko na huko, hali mashirika yasiyo
ya kiserikali yakiandaa matamko, makongamano
na maandamano kuipinga na kumtaka Rais
amuwajibishe Masurufu
Katika hali hii masurufu alifanya kila alivyoweza
kukutana tena na wale waandishi, safari hii na
wahariri wake ili kuibalansi habari iliyotoka, jibu
alilopewa lilimkatisha tama
“Tungeweza kuibalansi vizuri kabla haijatoka”
Alijibu mwandishi mmoja na kuongeza “Lakini sasa
haitawezekana, na hili limetokana na wewe kujibu
jeuri na kuwafukuza waandishi. Isitoshe
walioipokea habari hii tayari wamefanya mengi,
tayari wana ushahidi wa kutosha hata sie tukikana
haitasaidia!”
“Je” Dokta Masurufu akauliza kwa sauti iliyokata
tamaa “…Huwezi kufanya namna yote nikaokoka
na hii adha? Kila mahala sasa ni msamaha wa
kodi… Msamaha wa kodi!”
“Tunaweza kufanya namna mkuu!” Akasema
Mhariri mmoja na kuongeza “Zipo njia za kuifanya
habari hii isiendelee”
“Njia zipi na kwa nini zisitumike?”
“Zipo njia mbili ya kwanza ni kuzusha jambo
lingine kubwa kuliko hili, na wakati huo huo kuanza
kuandika makala za kukupamba na
kuwasahaulisha watu kilichotokea! Ila itachukua
muda kidogo na itahitaji pesa! Mbinu ya pili ni…”
“Subiri kwanza!” Masurufu akamkata kauli akiwa
na wahka. Akaendelea “Niambie!
Itahitaji pesa gani?”
“Kitu kama million tano hivi!”
“Basi andaeni. Pitieni kwa Sekretari wangu
atawaandalia cheki hiyo. Nisaidieni leo
nitawasaidia kesho!” Aliomboleza Masurufu,
hakuiona hata haja ya kusikiliza njia ya pili.
Waandishi wakakubali na kuanza juhudi za
kumsaidia. Juhudi ambazo zilikuwa sawa na
kubwa mithili ya mbegu ya haradali. Hazikusaidia
kitu.
Kuona hivi, Dokta Masurufu akakimbilia kwa
mtaalamu wake Profesa Zonga wa Zonga. Huyu
alikuwa Mtabiri na Mnajimu maarufu wa ndoto.
Kiuhalisia hakuwa mganga hasa ila mtundu fulani
ambaye aliweza kucheza vizuri na namba pamoja
na akili za watu Masurufu akiwemo, kiasi cha
kuwafanya watu hao wafanye mambo ambayo wao
wenyewe wasingeweza kuyafanya kama Profesa
Zonga asingekuwa nyuma yao.
Zonga alimpokea vizuri, akamsaili na kumsikiliza.
Akajua Masurufu ana hofu, wasiwasi na
ameshakata tamaa. Na dawa ya kukata tamaa
aliijua, si zaidi ya matumaini. Akampa moyo, dawa
na masharti. Mpaka Dokta Masurufu anaondoka
kwa Profesa Zonga, alikuwa na uhakika wa
kutosha wa kuendelea kutesa.
Kesho yake akiwa katika kufuata ushauri wa Zonga
na kutekeleza masharti yake, Dokta Masurufu
alikwenda kumuona Rais kumueleza kilichotokea.
“Masurufu!” Rais alisema akizipanga karatasi zake
vizuri pale mezani baada ya kunakili mambo
muhimu kutoka katika maelezo ya Dokta Masufuru.
Akaendelea “Umefanya vizuri sana kuja na
kunieleza yaliyotokea.
Ungechelewa zaidi ungekutana na rungu langu
kwani nisingevumilia upuuzi wa Serikali yangu
kuchafuliwa. Niliunda Tume na imenipa ukweli
wote, toka ulivyofanya mpaka mtazamo wa jamii
juu ya Serikali yangu. Kwa sasa hali ni mbaya
sana, una njia moja tu ya kujinusuru na kadhia na
kuendeleza heshima yako ambayo ulikuwa
umeanza kujikusanyia! Nayo ni kujiuzulu!”
Moyo wa Dokta Masurufu ukafanya Puuh!
“Kujiuzulu!!” Akashangaa zaidi ya kuelewa Heshima
yote, fedha zote, kiinua mgongo chake! Vyote
viende na maji? Impossible. Akawaza kwa hasira
“Mheshimiwa…” Masurufu akaita kwa sauti
iliyopwaya. Ni dhahiri alikuwa amevunjika moyo
vibaya sana “Nitaishi vipi baada ya hapa?! Ndio
kwanza nina miaka miwili katika Ubunge na mmoja
katika Uwaziri? Ina maana huu ndio mwisho
wangu?”


****Sasa we' ulitaka uwe mwisho wa nani
Masurufu? Jiuzulu huko!
 
SEHEMU YA SITA
Moyo wa Dokta Masurufu ukafanya Puuh!
“Kujiuzulu!!” Akashangaa zaidi ya kuelewa Heshima
yote, fedha zote, kiinua mgongo chake! Vyote
viende na maji? Impossible. Akawaza kwa hasira
“Mheshimiwa…” Masurufu akaita kwa sauti
iliyopwaya. Ni dhahiri alikuwa amevunjika moyo
vibaya sana “Nitaishi vipi baada ya hapa?! Ndio
kwanza nina miaka miwili katika Ubunge na mmoja
katika Uwaziri? Ina maana huu ndio mwisho
wangu?”
“Sikiliza Masurufu! Kujiuzulu siyo mwisho wa
maisha, wakati mwingine tunalazimika kutoana
kafara ili tuweze kutimiza lengo. Jiuzulu, tusafishe
hali ya hewa halafu tutakutana kuona tunafanyaje!”
Rais akahitimisha na kuinuka.
Masurufu naye akainuka akiwa na moyo mzito.
Safari yake iliishia kwa Profesa Zongo ambaye
alimuhakikishia ajiuzulu hakuna shida. Kwamba
kila kitu kitakuwa sawa sawa. Nyumbani mkewe
naye pia alimshauri kufuata ushauri wa Rais.
Siku iliyofuata akawaita waandishi akawasomea
hotuba nzuri aliyoandaliwana mtaalamu wake wa
siasa na mwisho hotuba atakangaza kujiuzulu.
Kilichofuata kilikuwa ajabu na kweli.
Mara moja aligeuka shujaa. Mtu wa mfano,
kiongozi bora na muwajibikaji. Ikatolewa orodha ya
viongozi wenzie ambao wanatuhuma na kashfa
nyingi ambao wamegoma kujiuzulu, yeye
akatofautishwa nao.
Hakuna aliyekumbuka kuulizia hatima ya zile spea
ambazo wakati huu zilikuwa madukani zikiuzwa.
Hakuna aliyetoa walau ushauri wa kuchukua kitu
kidogo alichopewa ili kitumike katika shughuli za
maendeleo ya jamii. Kila moja aliimba Masurufu
Shujaa, Masurufu Shujaa.
Aliporudi kwa Profesa Zonga safari hii hakurudi
mikono mitupu alikuwa na Bonge la gari, jipya
kabisa la kifahari aina ya Landcruiser Wizard.
Akamwambia mara aliposhuka.
“Nashukuru mzee, nimeona nguvu zako! Kila
mmoja anaimba jina langu! Hii ni zawadi yako”
Akahitimisha akimpa fungo na kadi ya gari.
“Tawire” Profesa Zonga akashtuka akimtengea
kapu la madawa aweke vitu hivyo. Nusu haamini
kama kweli ameletewa gari hilo la kifahari.
“Nilikwambia, we jiuzulu tu. Si umeona sasa? Na
bado itakuwa zaidi ya hapo we subiri tu!”
“Nashukuru!” Alikuwa Masurufu. “Na je kuhusu
wadhifa, ntapata mwingine kweli?”
“Kwa nini usipate? Nyota yako sio chafu tena.
Nilishaitengeneza kitambo na sasa inang’ara kweli
kweli. Inang’ara mithili ya maua katika jua la
asubuhi! Kamwe usiwe na shaka. Midhali Profesa
Zonga yungalipo Dokta Masurufu yuko salama siku
zote!”
“Nitashukuru Profesa. Nikirejea tena kazini
nitakujengea jumba la maana ili iwe kumbukumbu
yangu kwako. Najua maadui ni wengi lakini nikiwa
na wewe hawatoniweza!”
Dokta aliendelea kushukuru, kabla hajapewa dawa
zingine tena na masharti. Waliaagana kila mmoja
akichekelea tumboni Zonga akichekelea gari jipya
la thamani la chee alilolipata bila jasho, Masurufu
akichekelea namna alivyowapatia watanzania na
matarajio yake ya kushika wadhifa mkubwa nchini.
Ndiyo ilivyokuwa.
Alipokutana na Rais, Rais alimwambia asiwe na
papara. Atulie ayasome mazingira na kufanya kazi
yake ya ubunge vizuri. Akatulia na kusoma
mazingira akiendelea kuutumikia ubunge na
kufanya biashara zake kwa siri.
Muda wa Ubunge ulipokwisha, Rais akamshauri
asigombee na uchaguzi ulipokwisha akawa
ameteuliwa na Rais kuwa Balozi wa Tanzania kule
Uholanzi. Uteuzi huu ulikaribia kumfanya awe chizi
kwa furaha. Ukweli huu ulijidhihitisha pale alipojua
kuwa atakuwa mbali na vyombo vya habari na
macho ya wanoko wengine na hivyo kupata fursa
ya kutusua mali za wabongo bila woga.
Ni hapo alipokwenda tena kwa Dokta Masurufu na
kuitimiza ahadi yake ya kumjengea nyumba.
Akamjengea Bangaluu hasa, kabla hajamleta
Uholanzi aizindike nyumba na kumuombea dua
njema.
Kuondoka kwa Profesa Zonga, kulimfanya afanye
kazi kwa moyo wote akiiendeleza mipango yake
kwa nguvu zake zote. Haikuchukua muda sana lile
alilolihofia likatimia. Mlezi wake Mwalimu alifariki
dunia. Dunia nzima ilatikisika na kuomboleza.
Masurufu akalia na kulia na kulia. Akaruka yeye na
familia yake mpaka Dar es salaam,Tanzania na
baadae Butiama ambako alishiriki kikamilifu katika
Msiba wa Baba wa Taifa.
Msiba uliisha, siku za majonzi na maombolezo
zikaisha pia hatimaye akarejea Uholanzi.
Kutoka hapo ameishi vizuri katika nchi hiyo ya
maziwa na asali hadi ilipofika ile siku ambayo
alikuwa ametoka bafuni ambapo alikutana na
mkewe Glady aliyempa habari za kusisimua. Habari
za Tanzania kuingia katika awamu nyingine ya
kinyang’anyiro cha Urais.
Awamu ambayo nae aliamua kwa dhati kuiingia
baada ya majadiliano ya kina na mke wake
mpendwa. Naam! Dokta Masurufu aliwaza kwa
furaha wakati akitoka nyumbani kwake. Naitaka
nchi yangu, naitaka Tanzania! Lazima nikae Ikulu
na hakuna wa kunizuia!
Akahitimisha akiitekenya stata ya gari yake na
kuondoka hali tabasamu lingali limeupamba uso
wake.

CHRISTOPHER MACDONALD
Safari yake iliishia ofisini kwake ambapo alijikuta
akiwa na mambo mengi ya kufanya hali muda
ukimfanyia hiyana alipiga simu nyumbani Tanzania
kuulizia hili na lile ukiwemo upepo wa kisiasa n.k.
majibu aliyopata yakampa moyo na kumfurahisha.
Akatengeneza orodha ya mahitaji kabla hajaanza
kujipangia mkakati wake wa kuelekea Ikulu.
Ulikuwa mkakati mzuri ambao ulimchukulia muda
kiasi.
Alipomuonyesha mkewe ambaye alikuwa hodari wa
kusoma, akauafiki hadi akatikisa kichwa kwa
namna ya kushangaza. Mkakati ulikuwa
umemridhirisha katika namna iliyomfurahisha.
“Mkakati safi sana huu. Unahitaji maboresho
machache sana kuwa mpango mkakati imara
utakaofanikisha kuitwaa Tanzania. Nani
amekuandalia?”
“Sionekani kuuandaa mimi?” Alijibu kwa swali
masurufu na kuongeza. “Mara hii umesahau kuwa
mimi ni bingwa wa kuandaa michanganuo ya
miradi ya kijamii na ile ya kibiashara? Kwa kujibu
swali lako nimeuandaa mwenyewe. Umenigharimu
siku mbili tu kuutengeneza!
“Hongera!’
“Asante!”
Ukimya mfupi ukapita, Glady mkewe akiurejea
mkakati kutafuta maeneo ambako alikuwa
ameweka alama.
“Glady mpenzi!” Dokta Masurufu akasema akivunja
ukimya. Mkewe akaitika “Beeh laaziz!”
“Je” Akauliza “Utafaa?”
“Kwanini usifae! Nimekwambia mkakati safi sana
huu. Ungali unahitaji marekebisho machache kuwa
mpango bora kabisa. Utafaa mume wangu. Ila
lazima ufanye kitu kimoja!”
“kitu gani?”
“Utalazimika kuupeleka kwa watu wengine kadhaa
unaowaamini ili na wao wakupe maoni na mawazo
yao! Naamini ukipita mikononi mwa watu kadhaa
utakuwa mkakati usio na shaka ndani yake!”
“Hilo nalifahamu fika mke wangu. Katu sitaweza
kuuacha kama ulivyo! Lazima upite kwa wajuzi
kwanza!”
Naam mkakati ulipitishwa kwa watu kadhaa baada
ya mkewe nae kuongeza mawazo yake. Mpaka
unatoka kwa mtu wa mwisho ulikuwa safi na tayari
kwa utekelezaji. Kukamilika kwa hatua hii
kulifuatiwa na ile hatua muhimu ya kuongeza
nguvu za kiuchumi. Alianza kuangalia katika
marafiki zake ni nani na nani wanaoweza kumpa
kama sio kumkopesha au kumfadhili ili aingie
katika kinyang’anyiro cha urais kama mshindani
aliyepania kushinda na kwenda Ikulu na sio
mshindani anayetarajia kuwa msindikizaji.
Masurufu hakuwa mjinga. Alifahamu fika kuwa
wako wengi ambao wangependa kushiriki katika
mbio hizi za Ikulu, ambao wangetamani kujimwaga
katika hekaheka za uchaguzi, hekaheka ambazo
zingewasafishia njia katika safari ya kuelekea
Ikulu!
Aliamini wote wana nia na mbinu. Baadhi
wanakubalika na baadhi hawakubaliki. Lakini yeye
mbali ya kujivunia sifa zake, sifa ya na kiongozi
anayeheshimika zaidi nchini. Wachilia kuwa kwake
kiongozi wa mfano kwa kujiuzulu alipotuhumiwa
kusamehe kodi, alijua lazima atahitaji fedha. Fedha
za kutosha.
Fedha ambazo zitamtangulia mbele na kutatua
vikwazo vyote ambavyo vitakuwa vimeshindwa
kutatuliwa na sifa zake. Ni kwa mantiki hii ndiyo
maana leo asubuhi alikuwa amefika ofisini
mapema na kuwatambua marafiki zake muhimu
akawapata wa kuridhisha.
Hatua iliyofuata ilikuwa kuwapigia simu na kuomba
miadi nao, baadae akawatembelea na kufanya nao
mazungumzo ya kina mmoja baada ya mwingine.
Baadhi walimwelewa kwa urahisi, wengine
walimwona kama mwendawazimu na wengine
walimsikiliza kwa makini zaidi na kuupitia mkakati
wake na kumpa ushauri huu na Yule, huku
wakimpa matumaini na kumtia moyo.
Waliomwelewa wakaanza kumpa michango, dola
laki moja, dola elfu hamsini, thelathini mpaka kumi
zikaingizwa katika akaunti yake, akaunti
aliyoifungua maalum kwa ajili ya kurahisisha safari
yake ya Ikulu.
Fedha hizi zilipochanganyika na zile za kwake
ambazo alikuwa amezificha huku na huko,
matumaini yake ya kushiriki vyema katika
kinyang’anyiro cha kuteuliwa na chama, kupitishwa
na mwishowe kutwaa urais; yakaongezeka!.
* * ************

Miongoni mwa waliomsikiliza vizuri na kumpa
moyo Masurufu alikuwa Dr Christopher McDonald!
Huyu alikuwa amesisimkwa na kuvutiwa sana na
mpango wa Dk Masurufu Hussein Masurufu hata
akawa amemtembelea tena siku hii ofisini kwake
kwa siri.
“Umesema unataka kuwa rais wa Tanzania siyo?”
“Ndiyo!”
“Good idea!” MacDonald akashindwa kuizuia
furaha yake “Nimekuhusudu kwa hili!” Akaongeza.
Masurufu akatabasamu tu, halafu akajibu.
“Nami nakushukuru sana kwa mchango wako. Dola
laki moja sio fedha ndogo hata kidogo hasa
ukizingatia thamani ya fedha ya kwenu ilivyo juu!”
“Usijali!” McDonald akasema kama asiyejali sifa
hizo, “Kilichonileta hapa ni kufanya mazungumzo
mengine ya kina na wewe, mazungumzo ambayo
sina shaka yataweka lami katika safari yako ya
Ikulu!” Akatua na kujiwashia sigara. Akavuta na
kupuliza moshi mwingi hewani. Akasema
“Ninachokitaka kujua ni kama umedhamiria kweli
kweli kuwa rais wa nchi yako. Rais wa Tanzania?”
Dokta Masurufu akamtazama vizuri mgeni huyu
hali hasira zikianza kumpanda. Hakujua ni dhamira
gani izungumzwayo, wakati tayari alikuwa
ameandaa mkakati wake maridhawa na tayari
alikuwa ameanza kuchangisha na kukopa na
akingali anaendelea na zoezi hilo hadi leo. Hata
hivyo akazimeza hasira zake na kumuuliza mgeni
wake taratibu.
“Nadhani sijakuelewa McDonald.”
“Nataka kujua msimamo wako katika hili. Je uko
thabiti au unatingisha kiberiti?”
“Kutingisha kiberiti?” Masurufu akafoka. “Wakati
nimeandaa mkakati wangu, wakati hata wewe
umeuafiki na kuchangia? Wakati kila mmoja
amenipa moyo! Wakati...!”
“Sikuja kwa shari Masurufu!” McDonald akamkata
kaIima. “Nimekuja kukusaidia, nimekuja kuongeza
nguvu katika mipango yako. Nichukulie kama rafiki
na mtu niliye upande wako ili tuweze kwenda
vizuri!”
“Kumradhi Chris!” Masurufu akapoa. “Nilidhani
umekuja kunidhihaki. Ni kweli nimedhamiria kwa
dhati na ninahitaji msaada wako wa hali na mali
katika kutimiza hili. Na ninaapa lazima nikumbuke
fadhila. Sisaidiwi bure, nakopa na nitarejesha!”

***Wacha we! Masurufu huyo! Tunao wangapi
Tanzania hawa? Mi sijui!
 
SEHEMU YA SABA
“Kumradhi Chris!” Masurufu akapoa. “Nilidhani
umekuja kunidhihaki. Ni kweli nimedhamiria kwa
dhati na ninahitaji msaada wako wa hali na mali
katika kutimiza hili. Na ninaapa lazima nikumbuke
fadhila. Sisaidiwi bure, nakopa na nitarejesha!”
Akatua kumeza mate. McDonald akatabasamu.
Lilikuwa tabasamu la dhati kwa kuwa Masurufu
alikuwa amegusa pale alipotakiwa aguse ...lazima
nikumbuke fadhila! mvumo wa sauti ya masurufu
ukavuma tena akilini mwake na kubakia ukirejea
kama mwangwi ...sisaidiwi bure, nakopa,
nitarejesha!
Ni hili alilotaka kulisikia. Ni hili ambalo alikuwa
amepanga kutumia hila kulipenyeza, hadi hapo
Masurufu atakapolikubali ili aweze kumsaidia
kinaganaga, kumsaidia kichwa na miguu. Hata
hivyo alijirudi pale alipogundua amefurahi kiasi cha
kujisahau na kukaribia kuweka siri yake peupe.
Akasema
“Sikiza masurufu! Tanzania ni nchi yenye kila kitu,
amani, upendo , demokrasia na zaidi utajiri wa
mali asili. Ni moja kati ya nchi kubwa zenye
heshima ya aina yake ulimwenguni, ambazo zingali
masikini hadi leo hii. Bila kupatikana kiongozi
makini kama wewe, aliye na dhamira na nia ya
dhati ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi,
haitajikwamua maisha.
Ukiacha hilo, kwa upande mwingine Urais ni taasisi
kubwa ambayo kila aliyetimamu anatamani
kuimiliki walau kwa miaka mitano tu. Ili awe na
kauli ya mwisho kuhusu matumizi ya mali na
rasilimali za nchi.
Kwa maana hii kuingia kwenye kinyang’anyiro
kikubwa kama hiki na kushinda sio shughuli ndogo.
Ni lazima nguvu nyingi zitumike na jasho jingi
limwagike ili dhamira yako iweze kufanikiwa! Tuko
pamoja?”
Masurufu akakubali kwa kutikisa kichwa. Wakati
huo mlango ukafunguliwa na mhudumu wa Dk
Masurufu, akaingia na kuwatengea chai.
“Ndiyo maana!”Akaanza tena McDonald huku
akijiwekea sukari katika kikombe cha maziwa
“Nikakuuliza. Ni kweli umedhamiria? Maana
dhamira ni kitu kingine na ukipanga ni lazima
utimize. Liwake jua, inyeshe mvua lazima mkakati
ufanikiwe.
Maana mwenye dhamira ya kweli huwa haoni
taabu kuipinda na kuipindua mikakati yake ili tu
lengo lake kuu, lengo lake la mwisho litimie.
Nikirejea kwako sina shaka lengo lako kuu ni
kwenda Ikulu siyo! Na uko tayari kufanya lolote
kutimiza dhamira hiyo siyo?”
“Ndiyo!” Masurufu akajibu kwa moyo mzito. Sasa
akiwa ameanza kukerwa na mtu huyu ambae
alimuona kama anazunguka zunguka tu pasipo
kusema wazi anataka nini. McDonald akaendelea
“Na sina shaka kuwa dhamira yako ni ya ukweli na
ya dhati, si ndivyo?”
“Kabisa Chris!”
“Good! Very good!” McDonald akasema akisimama
bila hata kumalizia kikombe cha maziwa ambacho
alikuwa amekionja tu. Akaongeza akingali
amesimama.
“Nimefurahi kusikia hivyo Dokta! Ni hilo lililonileta
kwako, nadhani utafanikiwa katika mkakati wako.
Kwa heri ya kuonana na kila la kheri ndugu yangu!”
“Mara hii!” Masurufu aliwaza nae akisimama kwa
lengo la kumzuia McDonald, ambaye wakati huu
alikuwa anafungua mlango wa ofisi tayari kwa
kuondoka.
“Hapana!” Hatimaye Masurufu alisema kwa taabu
akianza kuvuta hatua kumfuata mgeni wake huyu.
“Hauwezi kuondoka kwa haraka hivi. Bado nina kiu
ya kuongea na wewe!”
Akatua akihema. Sasa walikuwa mlangoni,
“Bado hujanieleza kwa nini umeamua kuja ofisini
kwangu kwa siri namna hii, kwa nini umekazania
kujua nia yangu na kama nina dhamiri ya dhati!
Lazima kuna jambo na huwezi kuondoka bila
kuniambia, tafadhali Chris!”
Christopher McDonald akasimama mlangoni na
kumtazama Dokta Masurufu. Ni kweli alikuwa na
kiu ya kujua. Akaachia tabasamu la haja kumpoza.
Akamwambia
“Usijali Dokta, usijali! Tuliloliongea leo ni la
muhimu kuliko yote unayotaka kuyajua. Na muda
bado upo. Ingawa uchaguzi ni mwaka huu, lakini
ndio kwanza huu ni mwezi wa kwanza. Bado kuna
miezi tisa mbele.
Usiwe na haraka. Naenda kuwaona marafiki zangu
ambao niliwataka wakuongezee fedha za kutosha
ili uweze kutimiza dhamira yako . Na nisingeweza
kuwaona bila kujua kama una nia ya dhati au lah!”
“Hao marafiki zako ni akina nani?” Ushawishi
ukamzidi Masurufu. Tabasamu la McDonald
likakomaa, akacheka!
“Haraka ya nini Dokta?” Akasema katikati ya
kicheko. “Ndio kwanza nawapelekea wazo baada
ya mimi kuuona mkakati wako na kuukubali.
Baada ya kukukabili na kugundua ukweli wa
dhamira ya dhati uliyonayo na sio ubabaishaji.
Nipe muda. Ikibidi kuwajua utawajua. Wacha
niwape wazo lako. Pengine watakubali, pengine
wasikubali. Ila kama watakubali na kukupa fedha
lazima uwe tayari kufanya kitu kimoja muhimu!”
“Kitu gani!”
“ Kuupitia upya mkakati wako pamoja nao, ili
kuona kama utakidhi vigezo. Na katika hili inabidi
uwe tayari kuubadili na kuupanga kisomi zaidi
pasipo kuathiri lengo lako kuu. Lengo la wewe
kuwa rais wa Tanzania!”
Zilikuwa habari njema kwa Dokta Masurufu.
Akauliza,
“Kwanini tuufumue mkakati wangu uliogharimu
muda, fedha na akili kuutengeneza”
“Swali zuri” Alikuwa McDonald akirudi na kuketi
katika sofa.
“Swali zuri sana!” Akaingiza mkono katika koti,
akatoa pakiti ya sigara na kujiwashia sigara
nyingine kama kawaida akaivuta na kupuliza moshi
mwingi.
Akasema “Rafiki zangu ni wafanyabiashara Dokta.
Ni watu Smart na makini wakati wote.
Wanapoweka mkono wao mahala ni lazima waone
mafanikio ya uwepo wao huko. Umeelewa?”
“Nimeelewa!” Masurufu akasema kwa mshangao.
“Je”, akauliza “Wao wanatarajia kunufaika katika
hili?”
“Mara hii umesahau umeniambia unataka kukopa?
Kwamba ukishakuwa rais pale Ikulu utarejesha
kufumba na kufumbua?!”
Dokta Masurufu akatahayari. “Kumradhi Chriss!”
Akaomba.
“Samahani ya nini Dokta?! Huhitaji kuomba
samahani hata kidogo, pengine ninayestahili
kuomba samahani ni mimi!” Akatua na kupiga
mkupuo mwingine mrefu wa sigara. Akaacha
moshi wa sigara uingie mapafuni kwa wingi na
huku akiruhusu kutoka nje kidogo kidogo. Bado
Masurufu alikuwa amemtumbulia macho.
MacDonard akaendelea.
“Mimi ambaye nimekuja na kuingia ofisini kwako
bila ruhusa yako, bila miadi na zaidi bila mwaliko.
Na kama hiyo haitoshi nikaanza kukuuliza maswali
yasio na kichwa wala miguu. La! kumradhi bwana
Masurufu!”
“Usijali Criss,” Akasema Masurufu kwa bashasha
“Nitapenda kusikia kutoka kwa marafiki zako!”
Akaongeza.
“Tuombe Mungu!”
“Inshallah!”
MacDonald akainuka, Akaagana na Masurufu
akafungua mlango na kutoka. Kabla hajafika mbali
akaitwa tena, akageuka na kumtazama Masurufu
kwa Mshangao.
“Samahani, nakutegemea!”
“Unanitegemea?”
“Yeah! Hakikisha umewashawishi rafiki zako,
mpaka wakubaliane na matakwa yangu. Wakikubali
hata wewe utakuwa na fungu nikifanikiwa!”
“Kweli?!”
“Haki ya Mungu tena!”
“Nitajitahidi!” Likawa jibu la mwisho. MacDonald
akaondoka zake. Waliachana kila mmoja roho yake
ikiwa kwaatu kabisa, kila mmoja akiona
amempatia mwenzake.
* * *£££££******

Christopher MacDonald alikuwa mmoja kati ya
wageni wengi walioihusudu Tanzania kupita kiasi
hata wakijikuta akiomba uraia wa nchi hiyo kwa
siri. Kuihusudu huku kulikuwa kumekuja kama
nasibu tu, wakati ule Benjamini Mkapa
alipolihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa na
kupaza sauti kuwa tayari amefungua milango kwa
wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania.
Kwamba tayari ametengeneza mazingira mazuri
ambayo siyo tu yatavutia wawekezaji pekee, bali
yatawafanya wajisikie wako nyumbani hasa.
Akiwa mfanyabiashara wa kimataifa, aliyewekeza
vitega uchumi vya haja katika nchi za Angola,
Botswana, Zambia, Congo na Afrika ya kati;
Christopher hakuona kama kuna ubaya wa kwenda
Tanzania kujionea ukweli wa hali halisi na kile
alichokisema Mkapa kule UNO.
Akaja!
Alianza kuyakubali maneno haya mara tu
aliposhuka katika Uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Mwalimu Julius K. Nyerere pale Kipawa Dar es
salaam, akitumia ndege ya kukodi akitokea Congo
ambako pia alikuwa mwekezaji katika sekta ya
madini.
Hali ya hewa ilikuwa nzuri na ya kuvutia sana, jua
likiwaka mchana na giza kuingia usiku tofauti na
kwao. Ardhi ikiwa ya kijani iliyobeba majani na
mimea ya kijani haswaa. Kabla hili halijamkifu
akashangazwa na ukarimu na upendo waliokuwa
nao watu wake. Wachilia mbali umoja na
mshikamano. Ikamshangaza zaidi kuona mtu
anaingia dukani kununua bidhaa akiwa na hela
mkononi na kuomba auziwe! Badala ya kuamuru
apewe.
Na hata baada ya kuhudumiwa na kulipia bado
alisema ahsante kabla ya kuondoka. Ukarimu huu!
Christopher alishangaa kwa dhati Ustaarabu
ulioje?
“Naam!” Akakubali “Nyerere alifanya kazi kweli
kweli!”
Siku kadhaa zikakatika akisoma hiki na kujifunza
kile. Kutoka hapo akaenda kupanda mlima
Kilimanjaro. Mlima mrefu kuliko yote Afrika,
akajionea vilele viwili maridhawa vya Kibo na
Mawenzi.
Akajionea pia chemchem ya maji safi ambayo kwa
macho yake aliona kuwa yalikuwa bora kabisa.
Safari yake haikuishia hapo alikwenda Selui,
Mikumi, Tarangire, Manyara, Mahale na kwingineko
ambako alijionea utajiri wa wanyama wakiwemo
sokwe mtu ambao kwa Afrika walipatikana
Tanzania na Congo pekee.
Yale Maziwa yenye maji baridi yaliyoizunguka
Tanzania nzima, samaki wa migebuka wakubwa,
watamu na watamu waliomo katika ziwa
Tanganyika na lile la Viktoria vilikuwa vitu vingine
vilivyomfanya ailaani bahati yake kwa nini
hakuzaliwa Tanzania.
Alipokuja kuyatembelea machimbo ya Dhahabu
yaliotapaa karibu mikoa yote, Machimbo ya Almasi
kule Mwadui na Tanzanite pale Arusha, Christopher
alijikuta akiachama kwa mshangao na kusema.
“Masalaleeh! Kweli kwenye miti hakuna wajenzi!”
Wiki moja baadae alikuwa ofisini kwa Mkuu mmoja
wa Serikali kuulizia taratibu za uwekezaji, ambako
mshangao mwingine ulikuwa ukimsubiri.

****Mnh! Mshangao gani tena jamani???
 
SEHEMU YA NANE
Alipokuja kuyatembelea machimbo ya Dhahabu
yaliotapaa karibu mikoa yote, Machimbo ya Almasi
kule Mwadui na Tanzanite pale Arusha, Christopher
alijikuta akiachama kwa mshangao na kusema.
“Masalaleeh! Kweli kwenye miti hakuna wajenzi!”
Wiki moja baadae alikuwa ofisini kwa Mkuu mmoja
wa Serikali kuulizia taratibu za uwekezaji, ambako
mshangao mwingine ulikuwa ukimsubiri.
Ahadi ya kupewa msamaha wa kodi kwa miaka
mitano endapo angewekeza nchini, pamoja na
kuipa serikali mrabaha sijui mrahaba wa asilimia
tatu tu za faida kati ya silimia mia moja kwenye
sekta ya madini na yenyewe pia ilikuwa ni ahadi
iliyomfanya asahau hata kumuaga mwenyeji wake
na kurudi kwao Uingereza na Marekani.
Huko alikutana na wenzake watatu ambao
walikuwa na mtandao wao. Mtandao ambao kazi
yake ilikuwa moja tu. Kupora utajiri wa Afrika na
kuurudisha Ulaya, huku wakiziachia nchi za Afrika
uhuru wa bendera chini ya sera yao ya ukoloni
mamboleo.
Mtandao huu ulikuwa umeanza kama utani tu
baada ya wahusika wake ambao walikuwa
wanachama katika Mashirika ya CIA, BOSS,
MOUSAD. IMF na Benki ya Dunia; kuamua kujitoa
na kutengeneza chombo kingine ambacho
kingeweza kuyatekekeleza malengo yao kwa ufanisi
na haraka zaidi ukilinganisha na huko walikotoka.
Ni katika hili walipojibatiza uwekezaji ambapo kazi
yao kubwa ilikuwa kuandaa mipango ya kiutendaji
(Business Plan) yenye majina ya kuvutia kama
NEPAD, Structure Adjustment Programme,
Utandawazi, Mkakati wa kupunguza Umasikini,
Malengo ya Milenia, Maono 2015 n.k na kuwauzia
marais wa nchi za Afrika ambao walilazimishwa
kuwasikiliza na G8 ambayo ilikuwa moja kati ya
mitandao yao.
Na matokeo ya Business Plan hizo, yakawa ni
marais wa kiafrika kuwakaribisha nchini mwao na
kuwapa makampuni ambayo yalikuwa
yakiendeshwa na wazawa ili wao wayainue yawe
na tija na kuongeza ushindani.
Wakapewa kila kitu! Heshima, makazi, mikopo ya
mitaji na uhuru wa kutosha. Matokeo yake badala
ya kuyafufua mashirika hayo, wao wakayaua huku
wakipora kila rasilimali waliyopewa na wenyeji wao
na kwenda kuujenga Mtanadao wao.
Kutahamaki mashirika yakafa. Mtandao wao
ukakaua. Wakayaacha mashirika hayo yakiwa hoi
mikononi mwa Serikali yakihangaika japo kurudisha
utendaji wao wa zamani.
Wakati nchi nyingi za kiafrika zikianza kulalamikia
hali hii katika Umoja wa Mataifa kama ilivyo
kawaida, Mtandao wa akina Christopher ulikuwa
umekua tayari na kuanza kuwekeza katika nchi za
kiafrika na kuuchuma utajiri wa nchi hizo taratibu
na kuurudisha kwao.
Kama vile haitoshi, Mtandao ulijihusisha na kwa
siri sana kufanya ujangili katika maeneo yenye
malighafi nono, yakapenyeza silaha kwa waasi
mbalimbali na kuchochea vita vya wenyewe kwa
wenyewe katika nchi za ukanda wa Maziwa
makuu, huku wao wakijichotea rasilimali zao
kiulaini kabisa.
Agenda yao ilikuwa ile ile, kunyakua kila
kilichowezekana madini, malighafi na vinginevyo na
kukimbiza Ulaya na Amerika. Naam, hawakuwa na
rafiki wala adui wa kudumu. Wao walikuwa na
maslahi ya kudumu tu.
Hatimaye walichokitaka kilitimia. Utajiri waliokuwa
nao ulizidi kuwatetetemesha vigogo wengine wote
katika Bara la Amerika na Ulaya. Wengi walihitaji
kujiunga na kushirikiana nao katika hujuma
mbalimbali.
Kutahamaki wakawa wameziweka chini ya himaya
yao Taasisi kubwa kubwa kama zile za Shirika la
Biashara Ulimwenguni WTO, Shirika la fedha
ulimwenguni IMF, Benki ya Dunia WB na jamaa zao
wa nchi tajiri kabisa ulimwenguni G8. Na kwa
makusudi kabisa wakawa wameamua kujiita G-8
Original. Naam, kila mmoja aliwanyenyekea!
* * *$$$$$*****

Wenzake walizipokea taarifa za uwepo wa neema
katika Tanzania mithili ya wachezaji wa mpira wa
miguu wanavyoupokea mpira wa kona tayari kwa
kufunga goli na pengine kuokoa. Wiki ya kwanza
wakawa Tanzania ambapo walizunguka tena na
MacDonald na kuangalia hiki na kile kwa pamoja.
Wiki ya pili wakawa Uingereza tena, wakajipanga
na kuchukua kila kilichohitajika. Waliporejea tena
Tanzania na kuomba kuonana na Waziri wa nchi
pale Ofisi ya Rais Mipango na ubinafsishaji,
walipokelewa kama wafalme na kunyenyekewa
zaidi ya malkia Elizabeth.
Wakapewa maeneo waliyohitaji, ulinzi na msamaha
wa kodi wa miaka mitano! Wakachuma na
kuchuma. Miaka mitano ilipoisha walibadili majina
ya kampuni kwa hila ya kuleta jamaa zao wengine
ambao nao walipata msamaha wa kodi wa miaka
mitano tena.
Wakaendelea kuchuma, rasilimali zilipopungua
sehemu moja, walihamia sehemu nyingine bora
yenye rasilimali nzuri zaidi. Ni katika kipindi hiki
Christopher alipoomba uraia wa nchi hii ambayo
ukweli alitokea kuipenda sana.
Ndio! Nchi gani kila mmea unaoupanda unaota na
kustawi kana kwamba ardhi hiyo imetengenezwa
kwa ajili yake?
Halafu malalamiko ya wananchi yakaanza. Nchi
ikabadili muundo wa kuingia katika mfumo wa
vyama vingi. Wapinzani nao wakazaliwa na kuanza
kubweka huku na huko.
Laiti wasingaliuogopa Uchaguzi mkuu wa kwanza
wa vyama vingi na kusitisha mikataba yao kabla
ya kuondoka nchini kabisa kwa hofu kwamba
uchaguzi ungeambatana na umwagaji damu;
Pengine wangekuwa wanatawala hadi leo hii.
Uchaguzi ule uliopita salama na Benjamini Mkapa
akawa Rais na kuingia Ikilu huku akifuatisha
falsafa ya ukweli na uwazi kwa kutumia miiko ya
uongozi. Kidogo mambo yalibadilika, hivyo
Christopher MacDonald na wenzie akina Bob
Roberts Marshal, Alfred Winer na Anton Baker
Senior wakashindwa kuingia kwa urahisi.
Hili likawashangaza sana.
Hata walipofuatilia kwa Rais bado
hawakukubaliwa, sababu zilikuwa nyingi, lakini
kubwa ikawa ni kwenda kinyume na makubaliano
na kupora rasilimali za Taifa. Wakaghadhabika na
kuondoka kwa hasira.
Siku chache baadae wakawa wakiongea na
viongozi wa kisiasa.
Walianza na Augustine Lyatonga Mrema wa
Tanzania Labour Party, wakafuata na Dokta
Ibrahimu Haruna Lipumba wa chama cha Civic
United Front na baadae na John Momose Cheyo
wa United Democratic Party. Kama vile haitoshi
walionana tena na Bob Makani na Freeman Mbowe
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na
kuhitimisha na Chrisopher Mtikila wa Democratic
Party.
Mazungumzo na viongozi hao wa upinzani yalianza
na kwisha vibaya kwani viongozi wote walikataa
kuiingiza nchi katika machafuko kwa kuipindua
serikali ya CCM.
Pamoja na kwamba akina Christopher MacDonald
walikuwa tayari kutoa pesa za kutosha kwa
vyama, pesa za maandalizi, silaha na utaalamu na
kusaidia uratibu hadi pale Rais atakapoondoka
madarakani; bado viongozi hao hawakuwa tayari
asilani.
Wakaishia kuwalaani kuwa walikuwa na uoga wa
kipumbavu na kwamba kamwe asilani hawataweza
kufanikiwa kuitia nchi mikononi mwao kama
wataendelea kuwa waoga kiasi hicho. Kila mahala
pakaondokea kuwa pagumu. Wakawa hawana jinsi
ila kurudi kwao kutafuta namna mpya. Namna ya
kumuweka mtu wao pale Ikulu! Mtu ambaye
ataiongoza nchi kama kivuli huku akitamka na
kutenda kila watakalomwambia!
Wote walikuwa wamekubaliana kuionyesha serikali
ya CCM kile kilichomnyoa kanga manyoya. Na hili
lilitakiwa kutimia kwa kila hali. Bahati haikuwa yao
kwa vile kila waliyejaribu kumuuzia wazo hilo,
aliwaona kama wendawazimu. Miaka mitano ya
Mkapa ikaisha, akaongezewa mitano mingine.
Christopher na wenzie wakaendelea kutafuta
namna, muda ukiendelea kupita.

ITAENDELEA...
 
SEHEMU YA KUMI
Hili lilipata nguvu pale alipofanya mikutano
michache na MacDonald ambayo ilikuwa ikimaliza
kwa Masurufu kupewa ‘posho’ ya maelfu kwa
maelfu ya dola. Hatua hii ikamfanya Masurufu
amgeuze Christopher MacDonald kuwa baba na
mama akimtaka ushauri wa hili na lile.
Hali hii iliendelea mpaka pale alipomuita katika
kikao cha mwisho ambacho alimwambia kile
ambacho Masurfu alikuwa akihangaika kukijua.
Kwa nini akina MacDonald wamsaidie? Maana hata
kama angekuwa Rais, madeni yale yangeweza
kuchukua miaka kuyalipa. Ndiyo! yalikaribia
kufanana na yale ya Tanzania inayodaiwa na IMF,
WTO, World Bank n.k
MacDonald alimueleza kwamba wameamua
kumsaidia kwa kuwa wanatarajia kulipwa fadhila
kutoka kwake yeye ambaye uchunguzi wao
ulithibitisha kuwa ana nafasi kubwa ya kuwa Rais
katika uchaguzi huu.
Fadhila walizotarajia ni kuwa washauri wakuu wa
Rais katika sekta ya uchumi. Kwamba akiwa Rais
asingeruhusu watu kuwekeza Tanzania pasipo
ushauri wao, lakini pia kampuni kutoka nchi zao
zipewe kipaumbele katika uendeshaji wa sekta za
madini, utalii, misitu na uvuvi.
Ambapo wao watahakikisha kampuni hizo zinaajiri
wazawa na baadae kulipa kodi baada ya mitaji yao
kukomaa na wao kujijenga. Tena walimwambia
hawatokula peke yao, Rais pia atakuwa na hisa
kwa kila kitakachofanyika. Na fungu la Rais
linaeleweka. Sio dogo hata kidogo.
Na kama atauafiki mpango wao huo, msaada wa
fedha zote za kampeni na mwingine wa ziada
ataupata bila masharti ukiwa na ziada ya ulinzi,
mipango na hata utekelezaji wa baadhi ya mambo
akihitaji.
Akiwa na akili timamu na uwezo mzuri wa kufikiri,
mahitaji haya yaliingia na kutuama chini kabisa za
fahamu zake. Akachukua muda kuyatafakari kabla
hajamuuliza MacDonald maswali haya na yale.
Maswali ambayo yalikuwa na majibu muafaka.
Kwamba hawatamuingilia katika maamuzi ya
kuongoza nchi. Atapewa kila anachohitaji na
kwamba ubia huu utamfanya nae awe miongoni
mwa wale mabilionea wanne wanaounda G8
Original.
Jioni alichukua muda wa kutosha kujadiliana na
mkewe ambaye alimtaka kuondoa hofu na
kuchangamkia tenda.
“Kwa sasa wewe ni sawa na mtaka cha uvunguni!”
Glady alimwambia akimkumbatia. “Huna budi
kuinama!” Akambusu.
“Lakini kuinama huku…!” Glady aliendelea,
“Kutakuwa kwa muda mfupi tu. Itachukua pigo
moja tu la Almasi pale Mwadui au mawili ya
Tanzanite pale Mererani kurejesha deni lao lote!
Kubali mume wangu, kubali baba Rose. Woga
wako ndio umasikini wako!” Akambembeleza.
Ilitosha kuulegeza moyo wake. Penzi la haja
alilopewa usiku likawa limemmaliza kabisa.
Masikini laiti angejua kwamba mkewe nae alipewa
donge nono ili amshawishi?!
Alipokutana na MacDonald na kumwambia kuwa
amekubali, hapo ndipo aliposhuhudia tabasamu la
furaha ya dhati likichanua katika uso wa Criss na
kung`ara mithili ya maua katika jua la asubuhi.
Tabasamu hili lilifuatiwa na Masurufu kukatazwa
kuombaomba tena michango hovyo, na kufuatiwa
na ile safari ya Uingereza ambapo alikutana kwa
mara nyingine na ile timu ya wafanyabiashara wa
kimataifa wanne wanaojiita G8 Original na kufanya
mazungumzo yale yenye mafanikio.
Masurufu aliporejea nyumbani kwake, bado
tabasamu lilikuwa limeupamba moyo wake.
* * *
Nchini Tanzania vuguvugu la uchaguzi lilikuwa
limeanza mapema kuliko ilivyofikiriwa. Mheshimiwa
Frederik Tluway Sumaye Waziri Mkuu wa Tanzania
alikuwa wa kwanza kutangaza azma yake ya
kugombea uraisi kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi akitumia mahojianao maalum
aliyoyafanya na gazeti la Tanzania Daima.
Tangazo hili lilifuatiwa na lile lililotolewa na
Mheshimiwa John Samweli Malechela. Kabla
hawajafuata wakina Salim Ahmed Salim, Balozi
Patrick Chokala, Balozi Ali Karume na Profesa Mark
Mwandosya.
Kama vile haitoshi siku kadhaa mbele walijitokeza
akina John Magale Shibuda, Abdalah Kigoda na
Dokta Wiliam Shija. Wakati siku zikielekea ukingoni
wakawa wamejitokeza tena akina Iddi Simba,
Jakaya Mrisho Kikwete na John Charles
Tengeneza, huku wengine wengi zaidi wakitarajiwa
wajitokeze katika siku za baadae.
Huu ukiwa upande wa CCM, kambi ya upinzani
nako mambo yalikuwa yamepamba moto. Mbali ya
Mrema na Lipumba ambao waliwaambia wapenzi
wao kuwa wao wataendeleza libeneke la kugombea
urais;
Walijitokeza vijana wengine machachari kama
akina Freeman Mbowe aliyetangaza kuing’oa CCM
kupitia Chadema, akiahidi kutumia Helkopta.
Mgombea pekee wa kike Mama Anna Senkoro
aliyepitia PPT – Maendeleo, Christopher Mtikila na
chama chake cha DP na wengine wengi.
Tofauti na matarajio ya wengi, safari hii mgombea
kipenzi cha wasukuma na ambaye ni nadra
umsikilize bila kucheka kutokana na utani
anaoiingiza katika hotuba zake, Bwana John
Momose Cheyo wa UDP yeye kwa makusudi kabisa
alitangaza kuachana na Urais na kwenda
kugombea Ubunge nyumbani kwao Bariadi
Shinyanga.
Hekaheka hizi, kufumka na kuibuka kwa utitiri wa
vyombo vya habari hasa magazeti ambayo sio siri
mengi yalidaiwa kumilikiwa na wagombea Urais na
ubunge kwa ajili ya kupata urahisi wa kupeleka
habari zao na kujinadi kwa wananchi; pamoja na
kule kutazamwa na macho yote ya ulimwengu, kwa
pamoja vilimfanya Kamishna Msaidizi wa Jeshi la
polisi Inspekta Kimaro kuwa hoi kimawazo na
taabani kifikra.
Tayari alikuwa amechukua kila tahadhari aliyoiona
inafaa ili kuhakikisha imani inaendelea kuwepo ili
kulinda heshima ya Tanzania usoni mwa
ulimwengu.
Kila kitu kilikuwa sawa, kila hatari ilikuwa
imeondoshwa hata kabla haijatukia. Na machoni
pa wengi hali iliendelea kuwa shwari, lakini kwa
Inspekta Kimaro bado alikuwa na wasiwasi, bado
alikuwa na hofu.
Hakujua ni vipi anaweza kuimaliza hofu hii. Vijana
wake makini aliowapachika kila kona, kila mahala
ambako aliamini kungeweza kutokea lolote hasa
katika vyama vya siasa, walikuwa wakichpa kazi
barabara chini ya maelekezo yake na kumpa
taarifa zote. Yeye Akiwapa amri hii na ile.
Pengine ni hili lililomfanya leo amwite Samson
Kidude, yule mpelelezi wa kujitegemea ambaye
awali alikuwa mwajiriwa wa jeshi la polisi, lakini
akawa ameacha kazi katika mazingira ya
kutatanisha, na akaanza kujadiliana nae.
Majadiliano ambayo yaliisha bila tija kwani
Samson nae hakuwa na lolote la maana zaidi ya
kuendelea kumsisitizia kuwa hali ilikuwa shwari.
“Kwanini unaamini hivyo?” Kimaro akauliza kwa
karaha.
“Nina sababu za Msingi Kamishna!” Akajisogeza
vizuri kitini na kuendelea “Nimechunguza kila
mahala, kila nilipopatilia shaka. Bahati mbaya
nimekutana na madai ya kipumbavu tu! Madai
ambayo yeyote aliyeyazusha ama alikuwa na
ajenda zake, ama hakuwa timamu kichwani!”
“Madai gani?” “Kuna vile visu vya rangi ya Bluu,
Nyeupe na kijani. Ambavyo ilizushwa vimeletwa na
chama cha wananchi CUF ili wakishindwa
waanzishe vita na kumwaga damu!”
“Kweli hilo ni dai la kipumbavu sie pia lilifika
kwetu. Mwenzetu mmoja akalikurupukia, lakini
uchunguzi tulioufanya ulidhihirisha kuwa CUF
hawakuwa wanahusika. Enhe dai lingine?”
“Ilisemwa pia CCM imemnunua Bi Naila Jidawi ili
apambane na Maalimu Seif ili kupunguza kura
zake za urais na kumpa ushindi mgombea wa CCM
madai haya yalifanya Maalim aje juu, kitu ambacho
kilipofuatiliwa kikaonekana hakina ukweli na suala
hilo likamalizwa kwa njia za kidiplomasia.
Kamishna akatikisa kichwa kuafiki. Mengi ya madai
yaliyotolewa na Samson yeye pia alikuwa na habari
nayo kwa kuwa vijana wake walimpa mengi na
vingi. Kumwita kwake Samsoni ilikuwa ni kutaka
kujua kama Samson ambaye ni hodari wa kunusa
kama bado hajaambua lolote. Ikamshangaza kuona
Samson aking’ang’ania tu kuwa hali ni shwari!
“Lakini hii haimaanishi hali ni shwari Samson!”
“Kwa nini Kamishna?”
“Ule uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, hali
ilikuwa shwari hivi hivi, lakini kilichokuja kutokea
kwa King Halfan King na yule beberu Adrian sote
tunakifanamu. Laiti Adrian asingegongwa na gari,
bila shaka muda huu tungekuwa tunaongea
mengine!”
“Ni kweli lakini uchaguzi huu ni toauti na ule?”
“Ki vipi?”
“Huu hauna mdahalo!”
“Lakini muda bado, lolote linaweza kutokea!”
“Ndio lolote linaweza kutokea lakini sio la
mdahalo. Tayari Augustine Mrema ambaye wakati
huu atagombea tena kwa tiketi ya Tanzania
Labour Party amesema hatoshiriki. Yeye anaamini
alihujumiwa kwenye midahalo alipogombea mara
ya kwanza kwa tiketi ya chama cha NCCR
Mageuzi, na kwamba mdahalo ule alichangia
kumpora kura zake za urais.
Wakati Mrema ametangaza na kusema hatoshiriki
katika midahalo, ipo minong’ono kuwa wagombea
wanaotajwa kugombea kupitia upinzani na hata
chama tawala nao watakataa kata kata kushiriki
katika mdahalo!”
“Kwanini wakatae?” Inspekta Kimaro akasaili.
“Sasa mi’ nitajuaje mkuu hali mimi sio
mwanasiasa? Sio mgombea urais? Waulize
wenyewe wanasiasa waliotangaza kugombea.
Pengine wana udhaifu wa kujenga hoja, pengine
sio mahiri wa kujieleza mbele ya wagombea
wenzao, waandishi wa habari na wananchi kwa
ujumla. Pengine wanaogopa maswali ya moja kwa
moja toka kwa jamii na pengine wanaogopa
kulogwa!” Akatua. Hili la mwisho likamfanya
Inspekta Kimaro acheke. Akacheka sana. Samson
pia akacheka na kumwambia bosi wake
“Huonekani kuamini uchawi Inspekta!”
“Nitaamini vipi vitu visivyo na uthibitisho. Pengine
upo, pengine haupo!” Akajibu akiendelea kucheka.
“Uchawi upo mkuu!” Samson akasisitiza.
“Kama upi?”
“Kuna kesi ya Rama yule aliyekutwa akila kichwa
cha mtoto kule muhimbili, kuna yule aliyeua mtu
chumbani kwake kule Kibaha na kisha kulichukua
fuvu lake kuliweka chini ya uvungu ndani ya ndoo
ya plastiki iliyojaa mafuta, kuna mauaji ya
vikongwe wenye macho mekundu kule Shinyanga.
Kuna mauaji na uchunaji wa ngozi ulioshamiri
miaka ya nyuma kule Mbeya. Vyote hivi ni Baadhi
tu ya uthibitisho wa kuamini kwa watu juu ya
uwepo wa nguvu za giza!”
Inspekta akachoka.
Aliyoambiwa na Samson yalikuwa ya ukweli na
baadhi ya operesheni kesi hizo ameziongoza yeye
na kuwatia ndani watuhumiwa. “Hata hivyo!”
akasema baadae na kuendelea
“Hatupaswi kupuuza kitu! Hali bado ni tete na tuna
wajibu wa kuwa macho zaidi!”
“Haina neno Kamishna. Samson Kidude unamjua
fika, akipata lolote atakujuza tu!” Baadae
waliagana. Samson akaondoka akimuacha Kimaro
akiendelea kutaabika kama sio kukonda kwa
mawazo.
* * *

ITAENDELEA
 
[SEHEMU YA KUMI NA MOJA
“Haina neno Kamishna. Samson Kidude unamjua
fika, akipata lolote atakujuza tu!” Baadae
waliagana. Samson akaondoka akimuacha Kimaro
akiendelea kutaabika kama sio kukonda kwa
mawazo.
* * *

Mkutano wa pili bainaakinaMacDonald MacDonald ulikuwa mfupi na mzuri kuliko mingine
mingi iliyotanguliwa. Safari hii ulifanyikia Born
Ujerumani katika mazingira yale yale ya usiri.
Mkakati wake ulikuja ukiwa umepangwa kisomi na
vizuri zaidi. Ulimvutia kupita kiasi. Maeneo kadhaa
yaliokuwa na utata yalikuwa na maelezo ya kina
yaliyoiondoa shaka yake yote.
Labda kilichomfurahisha ni kule kukuta maelezo
yalioandikwa kwa wino mzito mweusi na kupigwa
mstari. Kwamba lazima mkakati huu ufanikiwe kwa
bei yoyote ile, hata kama ni kwa mtutu wa bunduki
baada ya njia ya kidiplomasia kushindikana. Ni hili
alilotaka kusikia, ni hiki alichotaka kukiona.
Baada ya kumaliza kusoma mkakati wa kuelekea
Ikulu, mkataba wa makubaliano yao nao ulikuwa
mezani ukimsubiri. Aliusoma neno kwa neno.
Baadhi ya mambo yalimsisimua na mengine
kumugofya. Kilichomfurahisha ni kule kukuta
kipengele kinachomuingiza katika lile kundi la
mabilionea wanne baada ya yeye kusaini.
Kuingia huku kutamfanya apewe mtaji wa dola
bilioni 40 ili anunue hisa na kuwa mmoja wao,
Mwanachama wa G-8 Original! Ilikuwa ajabu na
kweli! Machozi ya furaha yakamlengalenga huku
moyoni akifoka taratibu. “Nimeukata… nimeukata…
nimeukata!”
Aliendelea kuusoma kwa makini mpaka alipofika
mwisho ambapo alikuwa akitetema. Akautua ule
mkataba chini na kumtazama MacDonald.
Akamuuliza.
“Kwenda kinyume na makubaliano haya, adhabu
yake ni kifo?!!!”
“Ndiyo!”Akasisitiza akimtazama usoni moja kwa
moja.
Masurufu akaogopa. Kwa mikono inayotetemeka
akauinua tena ule mkataba na kuisoma tena
sehemu ile. Maandishi yaliendelea kuwa vile vile
kama yanayomdhihaki. Akauliza kwa pupa
“Kwa nini kifo? Mnataka kuniua?!”
“Hatutazamii kuuana katika hili, ni endapo tu
makubaliano yataenda kinyume kwa makusudi!”
“Ikitokea ninyi ndio mmekwenda kinyume?”
Ikawa zamu ya MacDonald kumtazama Masurufu
vizuri. Halafu akaangua kicheko cha haja huku
akitikisa kichwa kushoto na kulia. “Kitu kama hicho
kwetu, kamwe hakitawezekana. Ujue sie ni watu
ambao daima damu huwa hatuyakani maamuzi
yetu.
Mwenyewe umeliona hilo, nilipokuahidi mchango
nilikupa bila usumbufu na ningali ninakupa fedha
zingine hadi leo, fedha ambazo zipo nje ya
makubaliano. Na kabla ya kukaa na wewe, tulikaa
na wenzangu na tukakubaliana kufanya
tulichokifanya. Sioni kwa nini tugeuke! Naam
hatutageuka!” MacDonald akatua, akavuta sigara
na kutoa moshi mwingi hewani, akaongeza.
“Halafu makubaliano kama haya mkigeukana na
kupelekana mahakamani ninyi ndio mtakaofungwa.
Ni ya kihaini!”
Maswali mawili matatu yaliyofuata kutoka kwa
Masurufu yanajibiwa vizuri na washirika wa
MacDonald. Hofu inamuondoka Masurufu. Anavuta
peni na kuweka saini yake katika mkataba ule.
Nakala moja ngumu ya mkataba akapewa
Masurufu na kuiweka katika mkoba wake na ile
laini akaiweka katika Laptop na flash yake. Nakala
nyingine akazichukua MacDonald.
“Hizi ni fedha za awali!” MacDonald akampatia
Masurufu mfano wa kadi ya ATM ya rangi ya
hudhurungi. Masurufu akaipokea. “Nenda katika
ATM yeyote, ila ya benki yako ni zuri zaidi!”
Akaendelea MacDonald. “Ita nambari za akaunti
yako na uingize kadi hii. Baada ya muda utapokea
ujumbe wa salio la akaunti yako na unaweza
kuanza kazi!”
“Ahsante!” Akashukuru Masurufu.
“Kumbuka kuanzia sasa sisi ndio washauri wako
wakuu. Hupaswi kufanya chochote bila kutuambia.
Na ukifanya tutajua mara moja ingawa sisi
hatutokuja Tanzania! Na tukijua itakuwa hasara
kwako!”
“Msijali! Tuko pamoja”
“Unaweza kwenda!”
Masurufu akasimama na kuondoka.
“Masurufu!” MacDonald akamwita tena alipofika
mlangoni. Dokta Masurufu akageuka.
“Nakuonya tena, huwa hatugeukwi ndugu yangu
pesa hizo!”
Kiasi Masurufu alianza kukereka. Ananitisha?
akajiuliza. Nusura arudi na kumrushia ile kadi yake
alipojirudi …Kumbuka wewe ni mtaka cha
uvunguni… Mvumo wa sauti ya mkewe ukamrejea
na kumpa nguvu. Akaachia tabasamu la haja,
halafu akasema.
“Huna haja ya kuwa na hofu Chris, Ninajua
ninachokifanya. Usihofu kabisa!”
“Kweli?”
“Kweli tupu!”
“Poa kila kheri!”
“Kwako pia!”
Masurufu akatoka.
Safari yake iliishia benki alikofika anafanya
aliyoelekezwa na MacDonald. Alipouliza salio
alikaribia kuzimia kwa mshtuko. Dola Milioni Mia
mbili na hamsini zilikuwa zimetulia tuli katika
akaunti yake! Ikiwa ni kinyume na dola milioni
hamsini alizoomba katika mchango wake!
Hakuamini akaingia ndani kwa keshia na kuuliza
salio tena.
Jibu lililokuja lilikuwa lilelile. Kwamba ana dola
hizo. Kwamba ameingia miongoni mwa mabilionea
wachache waliopo. Furaha asiyomithilika ikamvaa
na kumchukua hata kumtoa machozi.
Alipomueleza mkewe kuhusu hili, Glady alishindwa
kujizuia na kuangua kilio cha furaha. Walikuwa
wameukata kwa kila hali. Sasa safari ilikuwa yao.
Njia ilikuwa nyeupe kuelekea Ikulu. Kikwazo pekee
ambacho waliamini kingekuwa kikwazo, tayari
kilikuwa kimeondolewa na G-8 Original.
Siku chache baadae kwa kuitumia familia na
marafiki zake walio Tanzania. Masurufu alipokuwa
amepata timu ya watu kadhaa ambao
walikubaliana kushikamana kwa namna na kwa
kadiri ya uwezo wao hadi pale Masurufu
atakapoingia Ikulu. Mmoja wa watu hawa alikuwa
Frank John Mariki.
* * *€€*******

“Faili lako hili hapa bosi!” Sekretari alimwambia
Christopher mara tu alipoingia katika ofisi yake na
kulitua faili juu ya meza. MacDonald aliinua macho
kutoka katika Laptop aliyokuwa ameiinamia muda
wote na kumwambia.
“Ahsante Suzane, unaweza kuendelea na shughuli
zako!”.
Suzane alisimama kwa heshima, akageuka na
kuondoka. Alipogusa kitasa cha mlango tu,
MacDonald alimwita tena.
“Beeh!”Akarejea na kusimama tena kwa heshima
mbele ya bosi wake. “Suzane?” MacDonald aliita
akingali ammeiinamia kompyuta.
“Mie hapa bwana wangu!”
“Ule mpango ulimaliza kuuchapa?”
“Ndio bwana, tena niliutuma kwa barua pepe kwa
wana G-8 kama ulivyoamuru. Baadhi wameleta
maoni na baadhi wameusifu. Nilikuwa sijafanya
hitimisho pale utakapouona na kutoa maoni yako
ya mwisho!” “Vizuri!” MacDonald akaendelea
kuchapa. “Vizuri sana. Ndio maana nakupenda
sana sekretari wangu. Naomba uziprint hizo
coments zao na niletee haraka!”
“Nitafanya hivyo!”
“Tena wapigie simu G-8 wote, waambie tuonane
mahala palepale pa siku zote haraka
iwezekanavyo. Sawa?”
“Sawa bosi!”
Suzane alipoondoka, MacDonald aliinua faili
alilolileta Suzane na kuanza kulipekua. Alilipekua
kwa haraka huku akinakili baadhi ya vitu kadhaa
pembeni kwa kalamu.
Alifanya hivi mpaka alipofika kwenye ukurasa fulani
ambao aliutazama kwa makini kabla hajaachia
tabasamu la haja lililofanya sura yake iwe na
mng’ao wa aina yake. Tabasamu hili liliendelea
kwa muda kadiri alivyozama katika kuusoma
ukurasa wa faili lile. Mara kadhaa, tabasamu
lilikomaa sana hata akakaribia kucheka kabisa,
lakini hakucheka. Kutoka hapo aligeukia Laptop
akataipu kidogo kabla ya kile alichokitaka
kufunguka. Ilikuwa ni tovuti mpya. Tovuti ya
Steven Lawrence Marvin.
Ni wakati anasoma taarifa za Steven katika tovuti
hii ndipo alipogundua mtu huyu alikuwa muhimu
kwao kwa kiasi gani. Alikuwa na habari nzuri hasa,
nzuri alizozihitaji MacDonald.
Suzane aliingia tena kuleta alichotumwa na bosi
wake pamwe na kutoa taarifa kwamba akina G-8
walikuwa njiani. MacDonald akamshukuru, Suzie
akaondoka.
Alipomaliza, akageukia maoni ya wenzake ambayo
yalikuwa na uzuri usiochusha, wenzake walipofika
walimkuta amekwishamaliza kuyapanga maoni
yake vizuri. Na sasa alimwita Suzie kwa ajili ya
kufanya hitimisho.
Kwa takribani saa moja na nusu, MacDonald na
wenzake walikuwa wakiwajadili vijana watatu
wenye sura, rangi na mionekano tofauti kutoka
mabara kama sio mataifa mbalimbali ya Ulaya.
Kila mmoja alikuwa amechukuliwa kwa namna
yake, maelezo yake yakachujwa na kuhifadhiwa
katika faili la siri la Christopher. Huu ukiwa
mwanzo, MacDonald alihakikisha anakutana na kila
mmoja, akazungumza nae na kupima uelewa wake,
halafu akampa jaribio na matokeo ya majaribio
haya, ikawa ni makubaliano ya kuingia mikataba
na watu hawa kwa matarajio ya kuwatumia
baadae.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Kwa takribani saa moja na nusu, MacDonald na
wenzake walikuwa wakiwajadili vijana watatu
wenye sura, rangi na mionekano tofauti kutoka
mabara kama sio mataifa mbalimbali ya Ulaya.
Kila mmoja alikuwa amechukuliwa kwa namna
yake, maelezo yake yakachujwa na kuhifadhiwa
katika faili la siri la Christopher. Huu ukiwa
mwanzo, MacDonald alihakikisha anakutana na kila
mmoja, akazungumza nae na kupima uelewa wake,
halafu akampa jaribio na matokeo ya majaribio
haya, ikawa ni makubaliano ya kuingia mikataba
na watu hawa kwa matarajio ya kuwatumia
baadae.
Katika vijana hao wanne alikuwemo Wallace
George. Huyu alikuwa raia wa New Zealand. Mrefu
kiasi, mnene wa kadiri mwenye mwanya mzuri
ambao daima uliwaumiza wanawake kila
alipotabasamu.
Huyu mbali ya ujuzi wake wa karate na kungfu, pia
alikuwa hodari wa kujipenyeza mahala, kutega
bomu na kuondoka pasipo kujulikana. Ingawa
alikuwa mweupe pee, uwezo wake wa kiakili na
kule kule kuweza kwake kujibadili kwa kwa kuvaa
nguo zinazofanana na aendako, kulimfanya apoteze
jina lake la Wallace na Kinyonga kuchukua nafasi
yake.
Ukiacha huyu kulikuwa na William Peter. Miaka
yake arobaini na moja ilikuwa amemtoa kabisa
katika ujana ingawa sura na mwili wake pamoja na
ule mtindo wake wa unyoaji ndevu vilimfanya
aonekane kijana wa miaka kati ya ishirini na sita
na thelathini na nne. Mama yake alikuwa na asili
ya Japani wakati baba alikuwa mzungu wa
Uingereza.
Huyu alikuwa mkali wa judo na kumchezea shere
adui yake hata akachoka kabla hajatimiza lengo.
Mara nyingi alikuwa akiwafanyia hili maadui zake,
akawachosha kwa hila, na walipochoka na
kumpuuza ndipo nae alipofanya vitu vyake! Ilikuwa
aghalabu sana kwa willy kushindwa kutekeleza
mipango aliyotumwa kufanya. Ni rekodi hii
iliyomfanya atumwe na Mataifa mbalimbali katika
kutekeleza mipango ya siri.
Halafu alikuwepo Steven Lawrance! Huyu alikuwa
mbantu haswaa kwa kuwa wazazi wake wote
wawili walikuwa wamerekani wenye asili ya
kiafrika. Kutokuwa na uhakika wa chakula, ubaguzi
wa rangi na umasikini uliochusha na kuudhi
vilikuwa vimemsukuma katika mkondo hasi wa
maisha. Mkondo uliomfanya akulie katika maisha
duni hujaona, maisha ambayo yaligeuka na kuwa
ya uchokoraa pale wazazi wake walipofariki mmoja
baada ya mwingine wakiwa wameachiana hatua ya
miaka miwili miwili.
Akajikuta akijilea mwenyewe kwa ushauri toka kwa
watoto machokoraa wenzake waliokuwa wakiishi
katika vitongoji mbalimbali katika jiji la New York
walijipatia chochote toka kwa yeyote. Katika
malezi haya alijikuta akithamini vitu viwili tu,
chakula na starehe. Starehe ya wanawake na
pombe.
Haikumchukua muda kugundua kuwa chakula na
starehe ambavyo daima huwa havikopwi
visingeliweza kupatikana bila fedha. Na fedha
hawakuwa nazo wakajingiza katika wizi na
udokozi.
Mara nyingi walifanikiwa. Zile siku kadhaa
walizoangukia katika mikono ya raia wenye hasira
walijikuta wakichezea kipigo cha haja
kilichowafanya waone umuhimu wa kujifunza
sanaa ya mapigano, wakajifunza.
Ni katika wakati huu kipawa cha Steven
kilipoonekana. Alikuwa na upeo wa hali ya juu.
Aliyafuata maelekezo ya walimu wake barabara,
mazoezi ya nadharia yakafanyika katika kule Gym
wakati ya vitendo alifanya katika mitaa mbalimbali
ama katika mikusanyiko ya mapigano.
Matokeo ya mazoezi haya yakawa ni jina lake
kujulikana huku polisi wakimtafuta kwa udi na
uvumba. Staili yake ya kupiga mapigo mazito ya
kushtukia ilimfanya awe anaua kama mchezo.
Halafu akakamatwa na kufungwa katika lile gereza
la Guantanamo.
Gerezani alikutana na mateso ya kila namna.
Mateso ambayo badala ya kumfunza awe raia
mwema, yalimfanya awe katili zaidi huku mikasa
ya aina kwa aina waliyokuwa nayo wafungwa
wenzake ikichangia kumfanya awe zaidi ya nduli.
Adhabu zikamkomaza, mateso yakamjenga. Chuki
yake dhidi ya binadamu na ulimwengu ikashamiri,
haja yake ya kupata fedha ili afanye starehe nayo
ikashika hatamu, huku akipanga kutoroka katika
gereza hilo mara tu upenyo utakapopatikana.
Hakufaulu kutoroka, alitoroshwa!
Genge la MAFIA lililokuwa limesikia sifa zake
lilifanya kila njia hadi kumtorosha. Kazi kadhaa
alizopewa badae ambazo alizifanya bila ufanisi wa
maana ndizo zilizopelekea kiongozi wa Mafia
wakati ule ambaye alifahamika kwa jina moja tu la
Biggie aamue kumuendeleza.
Alimpeleka katika shule za hali ya juu za karate,
kung fu, kick boxing na judo. Alipofuzu
akampelekea katika majeshi yao ya siri ambako
alijifunza ukomandoo ambako pia alifuzu vizuri
sana. Akawa na shabaha hujaona.
Hitimisho ikawa ni kupelekwa mashirika
mbalimbali ya kijasusi ambao kulikuwa na marafiki
zake, huko alijifunza ujasusi wa kiwango
kilichowafanya hata walimu wake wamuhusudu na
kumng’ang’ania. Kutoka hapo akarejea katika
kundi lake la Mafia na kuanza kuihangaisha Serikali
ya Marekani na washirika wake. Wakawa
wakifanya vitu watakavyo kana kwamba walikuwa
wamejitangazia uhuru wa Taifa lao dogo ndani
Marekani.
Uhalifu wao haukuishia ndani ya Marekani pekee,
Walivuka mipaka mpaka Asia, Ulaya na Afrika
ambako MAFIA ilikuwa na maslahi. Chini ya
uratibu wa Steven Lawrence, hakuna mpango
walioupanga ukashindwa.
Hili likamfanya Steve pia kutimiza azma yake ya
kupata fedha na starehe. Alistarehe haswaa huku
utanashati wake wa mavazi ya heshima, suti za
kaunda, suruali za vitambaa na vingine
vikimtofautisha na wenzake wengi.
Ilikuwa ni baada ya Biggie kufariki na Bill Clintoni
kuingia madarakani hali akiwa na ukwasi wa
maana ndipo Steven alipotundika bastola na
kuamua kustaafu! Mara chache alitumiwa na watu
wenye mahitaji kama ya MacDonald kwa malipo
manono kwa kazi maalumu na alipozimaliza kazi
zao alirejea kuwa raia mwema.
Mwisho wa kikao, MacDonald na wenzake
walikubaliana kumtumia Steven Lawrence Marvin
kama mlinzi wa Daktari Masurufu. Hii ilikuwa
baada ya kuzichambua na kuridhika na sifa zake.
Ule ubantu wa Steve ukiwa sababu nyingine.
Siku chache baadae MacDonald alikutana na steve
na kuingia nae mkataba. Kazi za Steve zilikuwa
chache tu kuhakikisha anaumwaga ubongo wa
yeyote anayetishia kutofanikiwa kwa harakati za
Dokta Masurufu. Kumvunja shingo ikibidi na
mgongo yeyote anayejitia kumjua jua sana
Masurufu kwa lengo la kumkwamisha. Jukumu
kubwa zaidi ilikuwa Steve kuwapa taarifa hasa za
hali halisi inavyoendelea.
Akina MacDonald hawakuwa wajinga, walijua
Dokta Masurufu ni Mtanzania, anakwenda kuonana
na watanzania wenzake kwa ajili ya Tanzania yao.
Hujui wataongea nini na ndani hasa ya mioyo yao
kuna nini. Uzalendo unaweza kuwashinda nguvu
nao wakajikuta wakikusaliti ukawa umepoteza
nguvu, fedha na muda!
Hivyo mbali ya kupokea taarifa za maendeleo na
utekelezaji wa mkakati wao toka kwa Masurufu
mwenyewe, pia walitaka wapokee taarifa nyingine
kutoka kwa Steven ili kuona kama Masurufu
hafanyi hila. Na katika hili waliazimia kumuamuru
Steve amuue Dokta Masurufu kama kungelikuwa
na hila yeyote.
Halafu wakampa theluthi ya malipo ya Awali.
Yalikuwa malipo ya kutakakata yaliomfanya Steve
aahidi kufanya kazi hiyo kwa moyo wake wote.
Theluthi mbili akiahidiwa kupewa pengine na zaidi
kama atalisimamia zoezi vizuri.
Kilichofuata baadae ni kumkadidhi Steve kwa Dokta
Masurufu.
“Huyu atakuwa mlinzi wako!” Alimwambia siku
chache kabla ya Masurufu kuondoka.
“Wow!” Masurufu alifurahia akimshika mkono
MacDonald “Nashukuru sana. Umefikiria kitu
muhimu sana. Rais mtarajiwa ana maadui wengi
ati?!” Wakacheka
“Lakini vipi uwezo wake?”
MacDonld akatabasamu. “Hauna shaka. Katika
watu tulionao huyu ni the best, na zaidi ni mbantu
mwenzio tunaamini hatapata shida kujichanganya
na wabantu wenzie. Ukiwa na shida yeyote
mueleze nae atatatua katika namna
itakayokufurahisha. Shida yeyote isipokuwa ya
kifedha sawa?
“Sawa!”
Ikawa hivyo. MacDonald akaondoka. Steve
akaanza kazi hapo hapo. Akamfunga Dokta
Masurufu vifungo vizuri, akakagua na kusafisha
ofisi, akakagua gari yake na vingine vingi. Baadae
akakaa nae na kumuhoji maswali machache
kuhusu mpangilio wa ratiba yake kwa siku,
nyumbani kwake huko Tanzania na mengine mengi.
Masurufu alimueleza yote kwa moyo mkunjufu.
“Vizuri!” Steve alisema baadae kwa kiswahili
akiifunga laptop yake. “Nimeingiza utaratibu huu
katika programu zangu ambazo wakati mwingine
hufanya kazi bila ya mimi kuwepo! Tafadhali
usibadili utaratibu huu bila kunijulisha!”
Masurufu akashangaa “Unajua kiswahili? Tena
kizuri hivi umejifunzia wapi?”
“Niliwahi kufanya kazi Congo enzi zile ikitwa Zaire
chini ya Mobutu Seseseko kuku Ngbedu wa
Zabanga. Kule ndiko nilikopata hamu ya kujua
lugha hii. Hata hivyo nilijifunza China sio siri lugha
yetu ni nzuri sana!”Akahitimisha kwa kusifu.
“Ahsante! Na je, Congo ulikwenda kufanya nini?”
Steve akatabasamu. Akajibu “Kazi ndogo tu ya
kumtoa Mobutu madarakani na kumweka Kabila!”
“Kumbe?” Masurufu akashangaa kiasi akiogopa.
“Ndiyo !” Steve akajibu. Ukapita ukimya wa muda.
Steve akauvunja kwa kumuuliza. “Kwa hiyo
tumeelewana?”
“Kuhusu utaratibu?”
“Ndiyo!”
“Nimekuelewa, ila sidhani kama nikiwa nyumbani
Tanzania nitaweza kuufuata utaratibu kama
nilivyojiwekea. Siunajua wagombea urais taratibu
na ratiba zao hupangwa na wapambe?”
“Najua! Tukifika huko tutapanga zaidi na kujipanga
upya. Muhimu ni taarifa tu baina yangu na wewe!’
“Haina shida!” Masurufu alikubali.
Steve akaondoka.
Akiwa ameyaacha maelezo yale palepale ofisini,
Masurufu alishangaa alipojikuta anapigiwa simu
usiku na Steve na kuambiwa.
“Kuna kitu hakipo sawa bosi!”
“Kitu gani?” Masurufu akauliza kwa mshangao
akijikagua.
“Hujaenda kuudurusu mpango wako na wakati huu
umelala kwenye kochi badala ya kitandani!”
“Ni kweli!” Masurufu akakubali akishangaa Steve
amejuaje hali hawakuwa wanaishi pamoja.
Akaongeza “Nilichoka mno baada ya mizunguko
mingi ya kutwa nzima ya leo!”
“Nilikwambia taarifa ni muhimu bosi!”
“Kumradhi Steve!”
“Usijali. Usiku Mwema!”
“Kwako pia!”
Wakaagana. Masurufu akaingia ndani. Kabla ya
kulala Masurufu alipekuwa kila mahali kuona kama
kulikuwa na kamera mahali au kitu kingine
chochote kinachosafirisha muenendo wake kwa
Steve, hakukiona.
Hii ilijiri kwa kuwa hakuwahi kumleta Steven hapo
nyumbani kwake. Alipochoka alipanda kitandani,
akamkuta mkewe Glady akimsubiri, wakafanya
mapenzi ya kutosha. Walipotosheka, walianza
kumjadili MacDonald, Steve na baadae safari yao
ya Tanzania kabla hawajalala.
Alipofika ofisini kesho yake, alimkuta Steve
ameshafika tayari. Wakasalimiana kwa bashasha
kabla ya Steve hajamuliza Masurufu swali jingine!
“Jana usiku ulikuwa ukitafuta nini?”
Masurufu akatoa macho “What? Unasemaje
Steve?”
“Unaelewa vizuri sana ninachokisema!”
Masurufu akatabasamu na kuangalia chini kwa
aibu. Atakuwa ameona pia nilivyokuwa nikifanya
mapenzi na Glady! Akawaza kwa uoga na hasira.
Sasa ulinzi gani huu unaoninyima hata faragha?
Hata hivyo alijirudi pale alipogundua kuwa yeye ni
mtaka cha uvunguni. Hana budi kuinama. Bila
kujibu chochote akamuacha Steve akitabasamu
kwa ushindi, akaingia ofisini kwake na kuchapa
kazi.

SURA YA TANO
DAR ES SALAAM – FEBRUARY 2005

Ilikuwa asubuhi njema kwa kila hali. Asubuhi yenye
afya kama kawaida ya jiji la Dar es salaamu.
Tayari miale ya jua ambayo awali alikuwa ya
dhahabu, ilikuwa imeanza kuikumbatia ardhi baada
ya hekaheka za kuibusu zilizoanza toka alfajiri
kumalizika.
Haliwi kumbatio la faraja hata kidogo. Lile joto lake
ambalo awali lilikuwa na vuguvugu lililoufariji mwili
hata kuufanya ulitamani milele, sasa lilikuwa kali
lililouchoma sio mwili pekee bali hata ardhi na
vyote na vyote ilivyobeba na kuifanya ardhi ianze
kuzalisha miale ya kujitetea na adha ya makali ya
jua.
Kama ilivyo ada jiji lilikuwa limeanza
kuchangamka. Watu walikuwa katika pilika pilika
za maisha yao ya kila siku pengine kwa ajili
yakujitafutia mkate wao wa kila siku. Harakati hizi
zingeweza kulinganishwa na harakati za siafu
wafanyao kazi kwa bidii kila mmoja kwa namna
yake bila usimamizi maalumu.
Katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere zamani DIA, hali ilikuwa hivi.
Watu walikuwa wengi sana. Sare zao za chama
zilizobeba picha ya Dokta Masurufu Hussein
Masurufu, vibendera vidogo vya mikono na bendera
kubwa kwa pamoja viliufanya uwanja wote kuakisi
rangi mbili maridhawa, kijani na njano.
Vile vikundi vya sanaa ambavyo wakati huu
vilikuwa vikitumbuiza kwa ngoma za asili, vikundi
vya matarumbeta, ngoma za asili, ngongoti na
Brass Band kwa pamoja viliendelea kupafanya
uwanjani hapo kuwa na uhai zaidi kuliko eneo
lolote hapo kipawa.
Ukiacha hawa walikuwepo waandishi wa habari
kutoka karibu vyombo vyote vya habari vikichukua
tukio hili la kihistoria. Redio moja na Televisheni
mbili zikirusha matukio haya moja kwa moja
kutoka hapo uwanjani, Live! Hawa mbali ya kuwa
walikuwa wamewekewa eneo lao maalum ili
waweze kupata kila kitu kwa ubora unaotakiwa,
bado kila wakati waliliacha eneo lao na
kujichanganya na watu, kwa lengo la kupata hili na
lile.
Upande mwingine wa uwanja walikuwepo vigogo
wa chama ambao hawakuwa maarufu na pengine
mashuhuri katika vyombo vya habari. Hawa
walikaa na watu wengine wa nyota tano ambao
walishindwa kulivumilia baridi lililomo katika
vyumba vyao vya VIP pale Air port na kuja
kuangalia shamra shamra hizi za kurejea kwa
Dokta Masurufu.
Kona nyingine walikuwemo mabalozi wa nchi anuai
ambao walikuwa wameombwa kushiriki na
kukubali. Hawa waliketi sambamba na mawaziri
kadhaa ambao kwa makusudi walikuwa
wameondoa nia zao za kushiriki katika
kinyang`anyiro hicho ili wampe nguvu Dokta kwa
matarajio ya kupata vyeo nyeti zaidi wakati
Masurufu atakapokuwa rais wa nchi hii.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU

Upande mwingine wa uwanja walikuwepo vigogo
wa chama ambao hawakuwa maarufu na pengine
mashuhuri katika vyombo vya habari. Hawa
walikaa na watu wengine wa nyota tano ambao
walishindwa kulivumilia baridi lililomo katika
vyumba vyao vya VIP pale Air port na kuja
kuangalia shamra shamra hizi za kurejea kwa
Dokta Masurufu.
Kona nyingine walikuwemo mabalozi wa nchi anuai
ambao walikuwa wameombwa kushiriki na
kukubali. Hawa waliketi sambamba na mawaziri
kadhaa ambao kwa makusudi walikuwa
wameondoa nia zao za kushiriki katika
kinyang`anyiro hicho ili wampe nguvu Dokta kwa
matarajio ya kupata vyeo nyeti zaidi wakati
Masurufu atakapokuwa rais wa nchi hii.
Kona ya mwisho walikuwepo wazee wa chama
waliopigania uhuru. Hawa walikuwa wamemuona
Masurufu kama chaguo pekee kwa kule kuwa
miongoni mwa vijana waliolelewa na Mwalimu.
Miongoni mwa hawa alikuwepo baba yake Kapteni
Husein Masurufu!
Muda si muda mvumo wa ndege ulianza kusikika
hewani na kuwafanya watu wainue nyuso zao na
kuangalia juu. Picha ya ndege ndogo ikawalaki.
Jinsi ilivyokuwa haikuwa rahisi kugundua ni ndege
ya aina gani.
Kadiri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo ndege ile
ilivyozidi kuikaribia ardhi, taaswira yake
ikiongezeka na kuwa kubwa hali iliyowafanya watu
waanze kuitambua. Maandishi madogo Gulf Air
ways SHT-511 yakaonekana ubavuni na kuwavutia
wengi kwa namna yalivyotengenezwa kwa namna
ya kuvutia kabisa.
Dakika chache baadae ndege hiyo ndogo ya kukodi
yenye uwezo wa kuchukua watu thelathini ilikuwa
ikisota na kutafuta parking kandokando ya uwanja,
sio mbali sana na pale walipokuwa wakitumbuiza
Brass Band.
Ndege iliposimama tu, haraka wale waheshimiwa
walisogea na kuweka mstari mmoja mnyofu ambao
vigogo kama sio vingunge aina kwa aina
walijipanga kati yake. Vikundi vya burudani,
ngongoti na vinginevyo vilikaribia kujivunja viuno
kwa kucheza.
Mlango wa ndege ukafunguliwa, watu wakaanza
kutoka mmoja baada ya mwingine. Dokta
Masurufu alikuwa watano kushuka akifuatiwa na
mkewe na Steven.
Mara tu alipochomoza uwanja mzima ukalipuka
kwa vigelegele. Rais…Rais…Rais! Akasimama
mlangoni tabasamu paana likiupamba usowe,
akainua mkono na kuwapungia waliokuja
kumpokea. Shangwe zikazidi, hali wapiga picha
wakipigana vikumbo kutaka kupata picha bora
zaidi.
Sekunde kadhaa zikayoyoma akiwa amesimama
katika lango la ndege, halafu akaanza kushuka
ngazi. Aliposhuka chini vijana wa skauti
wakamfuata na kumvisha skafu na shada la maua,
halafu akaenda katika mstari wa vigogo na kuanza
kuwasalimu mmoja baada ya mwingine.
Wapo waliomkumbatia, waliomuombea dua,
waliompongeza kwa uamuzi wake na kumwambia
tuko nyuma yako. Basi kila mmoja alimwambia
lake. Kutoka hapo aliangalia sanaa kidogo, akajibu
maswali ya wanahabari kwa ufupi sana, kabla
hajajifungia katika chumba cha VIP pale uwanjani
na kuteta na wazee wa chama.
Alipotoka safari iliishia New Afrika hotel ambako
wazee wa mkoa wa Dar es salaam na vitongoji
vyake walikusanyika. Ni hapo alipotangaza nia
yake ya kugombea wadhifa huo mkubwa kabisa
katika nchi na sababu zake, kwamba alikuwa
ameamua kugombea awapeleke watanzania katika
nchi ya maziwa na asali.
Kwamba ilikuwa ni aibu kwa watanzania kuwa
masikini na kutegemea misaada wakati ni
miongoni mwa nchi tajiri kabisa duniani. Yeye
alitaka kutumia utajiri kuongeza pato la wananchi
ili iwe walau dola tano kwa siku tofauti na chini ya
dola moja kwa sasa, pamoja na kukuza uchumi
wanchi na thamani ya shilingi ya Tanzania.
Alisema chini ya utawala wake, wabadhirifu wa
mali wa mali za umma na mafisadi wataadhibiwa
na kufilisiwa, ataboresha huduma ya afya kwa
mama na mtoto ili kupunguza vifo vya uzazi,
ataongeza shule na kuboresha kiwango cha
taaluma ili wahitimu waweze kuingia vizuri katika
soko la ushindani wa ajira.
Vitu kama ajira kwa vijana, miundo mbinu,
mazingira, mifumuko ya bei, kilimo cha kutegemea
mvua, ukosefu wa soko la uhakika wa mazao na
bidhaa za kitanzania, aliwahakikishia kuwa
vinaweza kupatiwa ufumbuzi baada tu ya kuleta
mjadala wa kitaifa, amabao utawashirikisha
watanzania wote na kuwapa fursa ya kushiriki kwa
vitendo katika kugawanya rasilimali za taifa kwa
usawa na kuamua zielekezwe sekta gani kukabili
changamoto za kimaisha.
Alidai muundo wa Bajeti ya serikali yake utaanzia
chini na kupanda juu na angehakikisha kila
mtanzania anashiriki na daima angeheshimu
mawazo hayo kwa kurudisha Bajeti hiyo kama
ilivyo na kamwe asingepokea vipaumbele kutoka
Benki ya Dunia, Shirika la fedha duniani, Shirika la
biashara ulimwenguni pamoja na Umoja wa nchi
nane tajiri zaidi duniani.
Kwa ujumla hotuba yake ya kutangaza nia ilikuwa
nzuri iliyomvuta kila mmoja. MacDonald alikuwa
ameiandaa vizuri sana baada ya kutafiti mahitaji
halisi ya watanzania.
Mwisho wa kikao, kila mzee alipewa posho ya
nauli ya shilingi tano, hali waandishi wa habari
wakipewa shilingi milioni moja kila mmoja.
Wakati huu Masurufu hakusahau kuwaomba
wamuunge mkono na kupigania kwa kila hali nae
atawawezesha kila patakapokuwa na tukio. Wazee
na waandishi kwa pamoja walimuahidi Masurufu
sio tu kumpa zaidi ya ushirikiano pekee, bali na
kumuunga mkono pia.
Kwa kutumia ndege ileile ya kukodi Dokta
Masurufu na timu yake, vingunge adhaa wa chama
pamoja na waandishi wa wahabari walisafiri
pamoja mpaka Dodoma ambako Dokta Masurufu
alichukua fomu ya chama ya kuomba kuteuliwa
kugombea urais kwa Katibu mkuu wa chama na
kulipa shilingi milioni mbili!
* * *
Siku ya pili magazeti yote yalibeba habari za Dokta
Masurufu kwa uzito wa pekee. Baada ya Redio,
Televisheni na mitandao kuzionyesha katika namna
ivutiayo. Ni Masurufu tu nabii anayekubalika kwao!
Lilinadi gazeti moja.
Hatimaye nuru ya mafanikio imeng’aa Tanzania,
Masurufu kuipeleka nchi katika maziwa na asali!
Lilidai gazeti jingine. Mkombozi aja! Hili liliripuka
kwa maandishi mazito meusi na kufuatiwa na
vichwa vingine vidogovidogo. Ni Dokta Masurufu
Hussein aliyezaliwa na mpigania uhuru na kulelewa
na mwalimu. Amewahi kuwa mbunge na waziri.
Ripoti yake ya uadilifu inatisha. Hotuba yake
yawaliza wazee wa Dar es salaam. Hili lilikuwa
gazeti jingine.
Dokta Christopher MacDonald aliendelea
kuzitazama habari hizi kwa furaha na matumaini
makuu.“Umekuwa mwanzo mzuri, mwanzo wa
kuitwaa Tanzania na kuiweka mikononi mwangu!
Hatimaye...” Aliwaza kwa furaha akiipitia tena
ripoti ya awali kutoka kwa Steve. Kila kitu kilikuwa
shwari, mambo yanakwenda kama yalivyopangwa
na kwamba sasa ilikuwa imeanza ile safari muhimu
ya kuwafuata wanachama mia mbili kila mkoa.
Jukumu ambalo walijua watalimaliza kama mzaha.
Ni hili lililomfanya ainue simu na kumpigia Dokta
Masurufu na kumpongeza kwa kazi nzuri kabla
hajamuuliza kama ana tatizo lolote. Masurufu
alipojibu hana, Christopher alimtakia kazi njema na
kumuagizia mtu mmoja zaidi kwa ajili ya ushauri
wakati wa kujaza fomu hiyo ya chama ya
kuombea kuteuliwa kuwa mgombea.
Masurufu alikubali tu, Christopher akazidi kufurahi.
* * *&&&&&&*******

Wakiwa mbioni kumaliza zoezi la kupata
wadhamini mia mbili kila mkoa katika mikoa kumi
ya Tanzania Bara na miwili ya Tanzania visiwani,
na zoezi likiwa linaenda vizuri, ndipo Frank Meneja
wake alipomfuata na kumjuza kuwa mambo si
shwari kama yanavyoonekana.
Kwamba ulikuwa umepangwa mkakati kabambe
wa kumwangusha wakati huu wa kura za maoni
kwa kumfanyia rafu. Akiwa amefundishwa na
Christopher McDonald kutopuuza lolote, Dk
Masurufu alijikuta akimkaribisha shushushu huyo
Frank John ambaye pia alikuwa Msaidizi wake
mkuu.
“Unasema mambo si shwari?” Alimuuliza.
“Ndiyo mkuu, na muda si muda yataharibika
kabisa kama hazitachukuliwa hatua madhubuti za
kulinusuru hili. John Tengeneza sio mtu mzuri hata
kidogo!”
“Huyu Tengeneza ni nani?”
“Ni mmoja wa watu waliotangaza nia ya
kugombea urais kwa mwaka huu kupitia chama
tawala na kama ulivyo wewe, naye ana nafasi
kubwa ya kufanya vizuri?”
“Mie mbona simfahamu vizuri?”
“Mara hii umesahau kuwa umeishi nje ya Tanzania
kwa takribani mwongo mmoja na ushei?
Tengeneza ni jamaa aliyeibuka siku za karibuni
akiwa ndani ya serikali ya awamu ya tatu ambapo
amefanya vingi na mengi!”
“Na kuhusu fedha je? anaweza kuwa na fedha
kama nilizonazo mie?”
“Hilo siwezi kulisemea. Lakini mpaka mtu
ameamua kugombea urais ambacho ni cheo cha
juu kabisa nchini, bila shaka atakuwa amejiandaa
vya kutosha!” Frank akatua.
Msurufu akainua kichwa na kufikiria.
Moyowe ukianza kupiga kwa hofu. Alikuwa
ameelekeza nguvu zake kwa wagombea watatu tu
ambao kwao alikuwa na hofu nao. Wagombea hao
ni Jakaya Mrisho Kikwete, Salim Ahmed Salim na
Frederick Tluway Sumaye walikuwa wamemtisha
kutokana na rekodi zao za uongozi na namna
walivyotumikia chama, serikali na wananchi.
Hawa alikuwa amewasoma na kuwatambua vya
kutosha na tayari alikuwa ameshapata namna ya
kuwashinda. Namna ambayo alikuwa na uhakika
na mafanikio yake kwa asilimia tisini na tisa kwa
moja.
Kuibuka kwa John Tengeneza, kukamfanya akune
kichwa mara mbili kufikiria namna ya kumpiku.
Kilichomuumiza ni ule ukweli kuwa sasa atakuwa
na maadui wanne badala ya watatu wa awali
ambao alitakiwa kuwafanyia faulo ili hatimaye
mwisho wa siku Halmashauri kuu na kamati kuu
ya chama viweze kumpitisha kwa kura zote kuwa
mgombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa tiketi ya CCM.
“Sawa!” Masurufu akapumua baada ya kukosa
fikra za maana. Akaendelea. “Turudi kwenye pointi
yetu. Tengeneza amefanya nini?”
“Ameandaa mpango wa kukuangusha kwa
kupandikiza wadhamini wasio na sifa katika fomu
zako za kuomba kudhamin!”
“Kitu gani?” Masurufu akashtuka.
“Ndiyo hivyo. Na tayari amefanikiwa. Robo tatu ya
watu waliojitokeza kukudhamini ni feki na yeye
anasubiri kikao cha uteuzi tu aweze kukuwekea
pingamizi!”
“Mungu wangu!” Masurufu akamudu kutamka.
Ukimya ukapita. Ukimya huo uliodumu kwa muda
ulivunjwa na Masurufu mwenyewe kwa kuomba
aelezwe kwa kina hili limetokeaje!
Frank akamueleza kinagaubaga toka alivyopewa
jukumu la kuwa Meneja wa Masurufu, na
alivyowajibika kutafuta habari za wapinzani wake
ili kupambana nao vizuri, mikakati aliyoweka na
namna alivyoweza kujipenyeza katika ngome
mbalimbali za waliotarajiwa kuwa wapinzani wa
Dk Masurufu ndani ya chama kwa kuwatumia
vijana wake ambao alikuwa amewapandikiza huku
na huko.
Ni mmoja wa vijana wake hao aliyemletea kanda
ndogo ya Cassette Tape recorder ambayo alikuwa
amepewa na kuingia nayo katika moja ya vikao
vya John Tengeneza. Ni baada ya kusikiliza ndipo
alipogundua kuwa John alikuwa amefaulu
kumtegea watu wasio na sifa wakati akitafuta
kudhaminiwa na walikuwa wamefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kwa kuwa robo tatu ya watu
waliomdhamini Dk Masurufu walikuwa watu wao.
Ni hapo alipokimbia kwa Dokta Masurufu na
kumueleza kila kitu.
“Hiyo tape recorder iko wapi?” Akauliza mwisho
wa maelezo ya Frank.
“Hii hapa!” Frank akajibu akiitoa na kumpa.
Masurufu akaipokea, Frank akaaga na kuondoka.
Alipofika mlangoni tu Masurufu akamwita tena.
“Kuna haja ya kuandaa mkutano mwingine wa
wanaumoja haraka iwezekanavyo. Tafadhali
waandae wajumbe, ndani ya muda mfupi tu, tuwe
tumekutana. Sawa?”
“Hakuna tatizo Mkuu! Nitaandaa na kukujulisha!”
Akajibu.
“Vizuri Frank, unaweza kwenda. Ahsante kwa
taarifa. Umefanya kazi nzuri sana. Ndio maana
nakupenda Frank. Endelea kupambana.
Tutakapoiweka nchi mikononi mwetu tutafidia
usumbufu wote huu!”
“Usijali Mkuu!Naielewa hali ilivyo!” Akajibu tena na
kuondoka
Alipobaki pekee, akaikabili redio yake na
kuitumbukiza ile Tape recorder. Alichokisikia
kilikaribia kuufanya moyo wake usimame kwa hofu.
Alipomaliza, akabonyeza mahala katika meza yake
na muda si muda Steve akawa mbele yake,
akamwambia bila kumwangalia,

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Masurufu akaipokea, Frank akaaga na kuondoka.
Alipofika mlangoni tu Masurufu akamwita tena.
“Kuna haja ya kuandaa mkutano mwingine wa
wanaumoja haraka iwezekanavyo. Tafadhali
waandae wajumbe, ndani ya muda mfupi tu, tuwe
tumekutana. Sawa?”
“Hakuna tatizo Mkuu! Nitaandaa na kukujulisha!”
Akajibu.
“Vizuri Frank, unaweza kwenda. Ahsante kwa
taarifa. Umefanya kazi nzuri sana. Ndio maana
nakupenda Frank. Endelea kupambana.
Tutakapoiweka nchi mikononi mwetu tutafidia
usumbufu wote huu!”
“Usijali Mkuu!Naielewa hali ilivyo!” Akajibu tena na
kuondoka
Alipobaki pekee, akaikabili redio yake na
kuitumbukiza ile Tape recorder. Alichokisikia
kilikaribia kuufanya moyo wake usimame kwa hofu.
Alipomaliza, akabonyeza mahala katika meza yake
na muda si muda Steve akawa mbele yake,
akamwambia bila kumwangalia,
“Niko hapa mkuu!”
“Hali si shwari Steve!”
“Kumezidi kitu gani tena bosi?”
Masurufu akaitwaa ile tape recorder pale mezani
na kumpa. Akamwambia, “Kaisikilize kwanza halafu
uje tuzungumze!”
Bila kuongeza neno, Steve akaipokea na kupotelea
nje kulikokuwa na makazi yenye ofisi yake. Muda
mfupi baadae akarejea na akiwa amechoka kama
alivyochoka Dk Masurufu awali.
“Nimesikia Mkuu na nimeiona hatari inayotunyemelea! Nasubiri amri yako tu nifanye
nini kuzuia hili!”
“Vizuri Steve. Hili ndilo nililokuitia. Yako mengi ya
kufanya lakini ningependa tujadiliane kwanza.
“Niko tayari! Nadhani pia kuna umuhimu wa
kumjulisha Christopher! Maana hii ni vita, na tayari
imeanza. Tunatakiwa kujibu mapigo!” Steve
akatua.
“Bado sijamuarifu Chris! Mambo mengine naona
kama vile yako ndani ya uwezo wetu. Huyu John
Tengeneza tunammudu kabisa! Ni bahati nzuri
njama hizi tumezigundua mapema!”
“Nikingali nakusikiliza bado Mkuu!” Alikuwa Steve.
“Nakuja huko. Kwanza nataka utumie uwezo wako
kujua yote yaliyo nyuma ya John Tengeneza.
Sitapenda auawe kwa kuwa kifo chake kinaweza
kufanya uchaguzi usogezwe mbele na hivyo
kutuchelewesha zaidi!”
“Una maana gani bosi?
“Nataka kujua udhaifu wake ukoje, ana madhambi
kiasi gani, ana shilingi ngapi benki, watu gani
anaowategemea kumuwezesha kiuchumi, na
kadhalika. Sawa?!”
“Sawa!”
“Jukumu hili lifanyike haraka iwezekanavyo. Yupo
Frank, Yule kampeni meneja wangu aliyewezesha
Tape record hii kurekodiwa. Yeye atakusaidia
kupita pale usipoweza kupita nimaana kukupa
taarifa. Yeye pia ana vijana wanaojua mengi
ambao wanaweza kukusaidia kwa namna moja au
nyingine! Je,” Masurufu Akauliza alipofika mwisho,
“Kuna la ziada?
“Hakuna” Steve akajibu. Mwili ukimsisimka. Sasa
alikuwa anaingia msambweni rasmi. Masurufu
alipoona hana la ziada, akamwambia
“Unaweza kwenda Steve! Nakutegemea sana!”
Steve akaondoka.
* * ***&&&&*******

Kikao kilichofuata kilikuwa nyeti na kikubwa kuliko
vingi vilivyotangulia. Hiki kilikuwa kimefanyika
Dodoma Hotel kwa siri baada ya kufanya uhakiki
wa majina ya wadhamini na kugundua kuwa ni
kweli kulikuwa na mamluki wasio na sifa
waliopandikizwa kwa Dk Masurufu, ili baadae
Masurufu awekewe pingamizi na kuondolewa.
Kingine kilichopelekea kikao hiki kuwa nyeti na
kikubwa ni ule ukweli waliokuja kuugundua wakati
wa uhakiki kuwa Dk Masurufu hakuwa anakubalika
sana kwa wanachama wa CCM kama walivyokuwa
wamefikiria awali.
Licha ya kwamba tayari walikuwa wamenunua
gazeti moja makini pamoja na watendaji wake,
kukodi Televisheni mbili na redio mbili pamoja na
kupata ahadi ya sapoti kubwa toka magazeti ya
udaku na kampuni kubwa za matangazo; Bado
Masurufu hakuwa anakubalika sana.
Hili pamoja na lile la wadhamini, yakawa sababu
ya kuwepo kama sio umuhimu wa mkutano wa
huu kufanyika, ambao kwao ulitarajiwa kuja na
mwarobaini wa matatizo yote hayo. Kichwa
kiliwauma wajumbe wa kikao hiki, bongo
zikachemka, wakaumba na kuumbua vitu
mbalimbali ili mwisho wa siku viweze kuwavusha
salama katika kikombe hiki cha Uchaguzi Mkuu.
Taarifa ya awali iliyotolewa na Steve haikuwa
tofauti sana na ile aliyopewa Frank. Kwamba John
Tengeneza alianza mikakati ya kwenda Ikulu
mapema zaidi na alikuwa amewekeza mtaji
mkubwa kwa wananchi.
Vile alikuwa Mkuu wa polisi na alifanya kazi nzuri
sana iliyomvutia kila mmoja kwa kukomesha
ujambazi na kudumisha amani na usalama, vile
alikuwa kwenye taasisi ya kuzuia rushwa na
alikuwa vilevile amefanya kazi nzuri ya kuzuia
ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma na vile
alikuwa na rekodi nzuri za kiutendaji, muadilifu
kwa maana halisi, ingemuwia vigumu sana Dr
Masurufu kutoa ushindani wa maana kwa
Tengeneza pasipo kuingiza hila.
Pamoja na kwamba Steven alikuwa anaendelea
kuhakiki uwezo wa Tengeneza kifedha, Masurufu
hakutaka kujiongopea kwamba Tengeneza
hatokuwa na uwezo huo kwa sababu kama
ameweza kumpachikia mamluki na kuwasambaza
katika baadhi ya mikoa ya Tanzania, na kama
amedhamiria kweli kuutwaa ukuu wa nchi, itakuwa
maajabu kama hana fedha za kutosha.
Ni hili lililomtisha na kumuogopesha Dr Masurufu,
kwamba anaweza kupoteza muda na fedha na
asipate hicho anachokitaka. Alipowafikiria G-8
Original na tishio lao kwake akajikuta akikosa raha
kabisa. Ni hapo alipoamua kuitisha kikao hiki cha
wanaumoja. Kikao hiki kilikuwa na kazi moja tu,
kuzipitia changamoto zilizokuwa mbele yao na
kupanga mikakati ya ushindi wa kishindo ndani ya
chama.
Wakijadili changamoto hiyo, wajumbe waliona
ugumu wa kumkabili Tengeneza. Kila walichofikiria
waliona kama hakiwasaidii kwenda mbele badala
yake kilikuwa kikiwarudisha nyuma. Wakiwa
wamekata tamaa kabisa, ndipo mjumbe mmoja
alipokuja na wazo la kumchafua Tengeneza kwa
kumpachikia kashfa na kuiandalia ushahidi wa
kubuni ambao ungekuwa radhi kuung’ang’ania
ukweli huo hata mbele ya vyombo vya habari na
mahakama.
Kashfa gani, hilo likaachwa mikononi mwa timu ya
propaganda.
Kumalizika kwa hili kukafanya waijadili mikakati ya
ushindi baada ya chama kumpitisha Dr Masurufu
kuwa mgombea wake. Suala la kujiuza lilipewa
umuhimu wa kwanza.
Baada ya majadiliano ya kina walikubaliana
kuendelea kutafuta vyombo vya habari
vinavyoukubalika na kuwanunua watendaji wake,
kutengeneza tovuti zitakazokuwa zikiendeleza
utafiti wa nani anakubalika zaidi na matokeo
yalenge kumpendelea Dr Masurufu.
Mkakati wa kutengeneza fulana za kutosha, kanga,
vilemba, vitenge, miamvuli, vishikio vya funguo,
mifuniko ya matairi ya magari na vingineyo nayo
haikusahaulika. Uandaaji wa vitu kama mchele,
chumvi, sukari na mafuta bila kusahau pombe kwa
ajili ya kuwarubuni wapiga kura wa vijijini na mjini
nao ukapangwa.
Takwimu ya wanaotarajiwa kupiga kura ikafanywa
kwa kutumia takwimu za Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kufuatia orodha ya watu waliojiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura. Kila
mwananchi alitengewa Shilingi elfu ishirini ambazo
angepewa kwa awamu tatu.
Awamu mbili za mwanzo, wangepata shilingi elfu
tano tano pamoja na kilo za mchele sukari, unga
na nusu lita ya pombe za kienyeji. Awamu moja ya
mwisho kila mmoja angepata shilingi elfu kumi
pamoja na kitenge, mwamvuli au kilemba kwa
akina mama. Kofia, vizibao, mabazee ya chama na
vuvuzela kwa wanaume.
Wakifanya tathmini ya mwisho wa kikao, Masurufu
na wenzie waliona kuwa mkakati huu, na ule wa
kuwanunua wajumbe watakaoshiriki kikao cha
uteuzi kwa kuwatengea milioni kumi kila mjumbe
mmoja ikiwa ni pamoja na kucheza rafu kidogo
hapa na pale bila kusahau ule mpango mama wa
kuwanunua wagombea wenzake wenye uchumi
uliokonda, kwa pamoja utawasaidia kwenda Ikulu
kiulaini kabisa.
Walihitimisha kwa kugawana majukumu na fedha
na kutakiwa kuwasilisha taarifa za maendeleo ya
majukumu yao mara kwa mara kwa Frank John
ambaye alikuwa mkuu wao wa kazi na Kampeni
Meneja wa Dk Masurufu Hussein Masurufu.

SURA YA SITA
SAMSON KIDUDE

Kutoka kuongea na Inspekta Kimaro, Kamishna wa
jeshi la polisi kukawa kama kumeiamsha akili ya
Samson Kidude mithili ya betri iliyotolewa chaji.
Akiendesha gari yake taratibu aina ya Toyota RAV
4 kutokea hapo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi;
Samsoni alijikuta akiwa na mawazo mengi kupita
kiasi.
Mawazo yaliyomfanya naye aanze kuutazama
uchaguzi huu kwa macho mawili, ule ushabiki wa
kawaida akauweka pembeni. Huu ukiwa ni
uchaguzi wa tatu wa mfumo wa vyama vingi vya
siasa baada ya ule wa kwanza wa mwaka 1995
ambao haukuwa shwari hata kidogo.
Ukafuatiwa na ule wa mwaka 2000 ambapo
Benjamin Mkapa alikuwa anamaliza awamu ya pili
ya ngwe yake, ambapo akiwa ni rais bado na
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi aliweza
kusimamia vyema hata ukamalizika salama
salimini.
Huu wa mwaka 2005 ulikuwa mgumu kwa kila hali.
Mgumu kwa maana kwamba chama kilikuwa
kinaingia katika kura za maoni na baadae uchaguzi
mkuu bila yule kinara wake maridhawa, Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere!
Huu ukiwa na ziada ya kitu kimoja zaidi. Watu
wakiwa wameelevuka kupita kiasi. Hawana uoga
hata chembe wakikisoa chama, Rais na serikali
yake bila hofu. Mafisadi wakiwa wametamalaki kila
kona hali kila mwananchi akigeuka na kutaka kuwa
mjasiriamali wa kutaka kupata faida tu bila kujali
wananchi wenzake, bila kujali kama amepewa
dhamana na umma au hajepewa, bila kujali kama
ni kiongozi au lah.
Hili pamoja na lile la minong’ono ya fulani kafanya
hiki au huyu anatarajia kufanya kile, kwa pamoja
vikamfanya Samson Kidude aone kwamba hastahili
kukaa na kuamini kuwa hali ni shwari pasipo
kuchukua hatua.
Mpaka anafika ofisini kwake Upanga bado alikuwa
hajaamua aanze na lipi kati ya mengi ambayo
alifikiria kuyafanya. Akaingia na kujitupa nyuma ya
meza yake juu ya kiti cha kuzunguka. Muda si
mrefu mlango ukagongwa akaingia katibu muhtasi
wake na nakala za magazeti. Akayatua juu ya
meza ya Samson na kumwambia,
“Magazeti yako hayo hapo. Bila shaka yametimia!”
“Ahsante,” Samson akajibu na kuyaangalia tu kama
hayaoni.
“Je?” Assia, Katibu Muhtasi wake akauliza
“Ungependa kunywa nini?”
“Mara hii umesahau kinywaji changu? Nikuambie
mara ngapi kuwa…!”
“Kumradhi bosi!” Assia akawahi. “Nakuletea!”
Akatoka.
Kutoka kwa Assia kukamfanya arejee kuyaangalia
magazeti. Kama Rais anashindwa kufanya
maamuzi magumu ajiuzulu! Kilinadi kichwa cha
habari cha gazeti moja mashuhuri. Kichwa hiki
kikamkumbusha Samsoni sakata la kongamano la
Mwalimu Nyerere Forum. Wanaosema Rais hawezi
kufanya maamuzi magumu ni wehu! liliandika
gazeti jingine.
Ukafuatia mlolongo wa majibizano uliochusha na
kuudhi. Akaanza kufikiria chanzo cha wazee hawa
kutoheshimiana na kutoleana majibu ya hovyo.
Alikuwa amemuomba Katibu wake amkusanyie
magazeti yote yenye taarifa hizo kwa imani
kwamba kulikuwa na chokochoko zilikuwa
zikiandaliwa na huu ulikuwa mwanzo tu .
Na alikuwa amefuatilia kwa kiasi na kutogundua
lolote la maana zaidi ya hisia tu kuwa baadhi ya
maswahiba wa Rais walikuwa wameamua
kumzunguka baada ya yeye kutoonyesha msaada
wa aina yoyote kwao wakati wa matatizo yao.
Zaidi ya hii sababu nyingine iliyotajwa ilikuwa ni
ya watu hao kutoingizwa katika madaraka.
Samson hakuona kama hili linaweza kuwa sababu
ya amani kutoweka katika kipindi hiki tete cha
kuelekea uchaguzi mkuu. Hata hivyo aliamua
kuyaitisha tena magazeti haya baada ya yale
mazungumzo yake na Inpekta Kimaro ambaye
alikuwa na wasiwasi na uchaguzi mkuu.
Muda si muda katibu muhtasi wake Assia akaingia
na kumtengea kahawa. Alipoondoka Samsoni
akaendelea kuyaperuzi magazeti kwa umakini wa
hali ya juu kwa matumaini ya kukutana na kitu
kipya. Hakukutana nacho.
Akaanza kuona kama anajipa mzigo wa bure
usiokuwa na tija wala mafao!
* * *

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO

Na alikuwa amefuatilia kwa kiasi na kutogundua
lolote la maana zaidi ya hisia tu kuwa baadhi ya
maswahiba wa Rais walikuwa wameamua
kumzunguka baada ya yeye kutoonyesha msaada
wa aina yoyote kwao wakati wa matatizo yao.
Zaidi ya hii sababu nyingine iliyotajwa ilikuwa ni
ya watu hao kutoingizwa katika madaraka.
Samson hakuona kama hili linaweza kuwa sababu
ya amani kutoweka katika kipindi hiki tete cha
kuelekea uchaguzi mkuu. Hata hivyo aliamua
kuyaitisha tena magazeti haya baada ya yale
mazungumzo yake na Inpekta Kimaro ambaye
alikuwa na wasiwasi na uchaguzi mkuu.
Muda si muda katibu muhtasi wake Assia akaingia
na kumtengea kahawa. Alipoondoka Samsoni
akaendelea kuyaperuzi magazeti kwa umakini wa
hali ya juu kwa matumaini ya kukutana na kitu
kipya. Hakukutana nacho.
Akaanza kuona kama anajipa mzigo wa bure
usiokuwa na tija wala mafao!
* * *&&&&&*******

Ilikuwa ni saa kumi na mbili na dakika ishirini na
mbili jioni wakati Dk Masurufu alipopaki gari lake
nje ya nyumba ya Profesa Zonga wa Zonga kule
Kimara Baruti. Akashuka na kupokelewa kwa
bashasha zote baada ya kupiga honi
iliyomtambulisha.
“Nimekuja tena Maalim!” Akamwambia mara
alipoingia katika ofisi ya Profesa Zonga iliyokuwa
juu ya Bangaluu hilo alilomjengea miaka ile ya
kisogoni!”
“Karibu Mkuu! Kumezidi kitu gani tena?”
“Nafasi Mkuu. Toka nitangaze nia maadui
wameniandaa na kuitishia kabisa nafasi yangu.
Naomba unisaidie, wewe ni tegemeo na kimbilio
langu pekee. Nakuomba Profesa!”
Profesa Zonga akachukua karatasi kadhaa, kidau
cha wino mwekundu wa zafarani na kipande cha
mti. Wakati huo huo akamwita msaidizi wake na
kumtaka aandae chetezo na ubani. Msaidizi yule
Mwilenga wa Mwile akaandaa vitu upesi upesi.
“Fatiha!” Alikuwa Masurufu baadae akinyunyiza
ubani katika chetezo. Moshi ulipoanza kufuka naye
akaanza kuandika, huku akitamka maneno
aliyoyajua mwenyewe kwa kushirikiana na Mwile.
Zoezi hilo lilidumu kwa takribani dakika kumi na
tano hivi. Alipomaliza akamwambia.
“Masurufu!”
“Tawire Profesa!”
“Hakuna tatizo!”
“Eti?”
“Umesikia sahihi. Sioni tatizo lolote. Nyota yako
ingali inang’aa sana. Bado una nguvu za kutosha
kuingia Ikulu bila wasiwasi wowote. Hakuna cha
nani wala nani wote nawaona hapa wanakufukuzia
kwa mbali kabisa. Na nakuhakikishia
hawatakushika.
Uso wa Masurufu ukakunjuka, tabasamu la
wastani likatokeza usoni mwake. Akasema.
“Yaweza kuwa kweli. Ila kuna huyu John
Tengeneza yaelekea ameshanitengeneza, maana
kila ninapokanyaga nakuta ameishapita na kuacha
madhara mbele yangu, ndiyo maana nimekimbilia
kwako.
Profesa akamtumbulia macho asimuelewe. “Una
maana gani Dokta?”
Hapo tena Dokta Masurufu akaeleza yote
yaliyofikia baina yake na Tengeneza na namna
alivyotaka kumuingiza mkenge wa wadhamini.
“Na wewe umechukua hatua gani?” Profesa Zonga
akauliza na kujibiwa. Halafu akafanya tafakari ya
kina, kabla hajaliandika tena jina la Tengeneza
katika mitambo yake na kuanza kulitengeneza
upya!”
“Hana lolote!”Akasema baadae na kuongeza
“Waungwana wamethibitisha hivyo!”
“Kweli?”
“Kabisa kabisa. Ila …” Profesa akatua na kupiga
funda la kahawa chungu. Masurufu akasimamisha
masikio. Profesa akaendelea.“Inatubidi tufanye vitu
kadhaa. Kwanza ni tambiko. Hili inabidi likafanyike
kwenye milima ya uluguru na Pwani usiku wa
kesho na inabidi liambatane na sadaka ya kondoo
kumi na tano na mbuzi watano. Lengo la hili
itakuwa kupata baraka ya mizimu ya uluguru na
pwani na kama unavyojua Ikulu iko Dar es salaam
mahala ilipo mizimu hiyo.
Pili inabidi tuififize nyota ya Jonh Tengeneza na
wenzake. Hapa tunahitaji ng’ombe fahali mweusi,
nazi sabini na moja, vyungu saba , nyembe saba,
sindano saba, ndimu saba, chumvi ya mawe na
madawa ya kufifiza nyota ambayo yanapatikana
Mombasa na bonde la mto Rufiji. Baada ya hapo
utakuwa huru kufanya lolote na chochote mpaka
utakapokikalia kile kiti cha enzi. Kiti cha nchi!”
“Kuhusu gharama?” Maana sifikirii kama vitu hivyo
naweza kuvipata kwa kuwa nina mambo mengi ya
kufanya na muda hautoshi kabisa.
“Gharama ya kazi na vifaa haitazidi milioni kumi!”
“Haina shida!” Masurufu akaifungua briefcase yake
na kutoa vitabu viwili vya hundi, akaandika hundi
mbili kila moja ya milioni tano na kumkabidhi
Profesa Zonga.
“Hili tumelimaliza! Je” Akauliza Masurufu, “Kuna
jingine?”
“Lipo! Tena hili ni muhimu kupindukia!”
“Lipi tena?”
“Yaelekea mipango yako mingi inaratibiwa na mkeo
Glady, siyo?”
“Uko sawa kabisa!”
“Hilo ni kosa. Waungwana hawataki kabisa mambo
ya wanawake!” Moyo wa Masurufu ukafanya pah!
Hakujua ni vipi anaweza kumweka mbali mkewe
katika kipindi hiki ambacho wamekuwa bega kwa
bega kuhakikisha kwamba wanaingia Ikulu. Asili ya
safari hiyo hata uwezo wa kipesa alionao ukiwa ni
juhudi za mkewe kipenzi anayempenda sana!
“Kwanini Profesa?”
“Swali zuri Dokta! Umeuliza vizuri sana.
Waungwana wasichopenda kutoka kwa wanawake
ni zile damu zao za kila mwezi ambazo sio siri
huwa zinawasumbua sana katika kutekeleza
mambo yao. Mfano hapa tunatengeneza tambiko
kuweka sawa mambo yetu, mkeo akipata hedhi tu
kazi yote tuliyofanya inakuwa ni bure. Vivyo hivyo
katika kumfunga nyota John Tengeneza!
Masurufu akachoka. Alimjua vizuri sana mkewe,
uchakalikaji wake na jinsi alivyo mjenga hoja mzuri
na asiyejubali kushindwa kirahisi. Kumwambia tu
akae pembeni eti kwa kuwa Profesa Zonga
amesema, ingekuwa sawa na kuchokoza mzinga
wa nyuki.
“ Kwa… kwa… kwani hakuna njia nyingine
Profesa?”
“Haya sio matakwa yangu, Dokta. Mie ni tarishi tu.
Wenyewe wapo na wanatoa amri ya kila
kinachofanyika!”
“Lakini… lakini…?”
“Unautaka urais au huutaki?”
“Nautaka!”
“Basi kafanye yanayotakiwa kufanywa. Kwa heri!”
Dr. Masurufu akaondoka kinyonge.
* * ***&&&&&*****

“Kuna simu yako toka Ikulu!”Assia alimwambia
Samsoni mara tu alipopokea simu yake. Usingizi
ulikuwa umeanza kumnyemelea baada ya mawazo
kupigana vikumbo katika kichwa kutafuta jambo
ambalo hata yeye hakulijua sawa sawa.
Akamuuliza Assia!
“Atakuwa mzee Chilo bila shaka!”
“Ndiyo!”
“Okay, niunganishe!”
“Vipi Samson?” Sauti ya Mzee Chilo ikasikika.
“Salama mkuu, Shikamoo!”
“Marahaba. Ni hivi punde tu nimetoka kuongea na
rais na bado ningali katika viunga vya Ikulu.
Naomba tuonane katika ofisi ya yangu ya siri
iliyopo pale Ubungo Plaza. Yaelekea kukawa na
dharura!”
“Sawa mkuu!” Samsoni akajibu.
“Okay!” Kwaheri!” Mzee Chilo akaaga na kukata
simu.
Naam! Kumekucha sasa! Samson akawaza
akitabasamu baada ya kuutua mkonga wa simu
chini. Dharura kwake ilimaanisha kazi. Na kazi
mpaka unapoona ameingilia mzee Chilo baada ya
kufanya kikao baina yake na Rais, haiwezi kuwa
kazi ndogo hata kidogo.
Mzee Chilo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi wa
usalama wa taifa, ambaye alikuwa akiongoza Idara
ya ulinzi na usalama wa taifa. Samson kidude
ambaye awali alikuwa mwajiriwa wa jeshi la polisi
idara ya upelelezi wa makosa ya jinai akiwa na
cheo cha Sub Inspekta; hakuwa akimjua kabisa
mzee Chilonga Anderson Chilonga almaarufu kama
Chilo.
Kumjua kwake kulikuja kama nasibu tu, wakati
alipojikuta ameingia katika mkasa mmoja
uliohusisha ubadhirifu mkubwa wa mali za umma
kupitia kampeni ya kitapeli ya kufua umeme
bandia, mkasa ambao uliratibiwa na vigogo
wakubwa wakiwemo wa jeshi la polisi ambao
kimsingi walikuwa mabosi wake.
Samsoni angali anakumbuka vizuri sana kuwa
ufuatiliaji wa mkasa ule ambao mwanafasihi
Hussein ameuandikia kitabu na kukiita Nipe Roho
Yako ulimfanya aponee chupuchupu baada ya
kugundua uozo mkubwa uliokuwa ukilipeleka taifa
katika hujuma nzito ambayo ingeiingiza taifa katika
machafuko.
Hujuma hizo ambazo zilipelekea Rais kuwatimua
kazi wakuu wa usalama, maafisa wa jeshi la polisi
na wasaidizi wao, pia zilipelekea Rais kuvunja
Baraza la wasaidizi wake baada ya kumfuta kazi
waziri wa umeme na madini.
Ni baada ya matokeo hayo ndipo alipoanza
kuwindwa auwawe, na suluhisho likawa ni yeye
kuacha kazi ya upolisi na kuanza kuishi kwa
kujificha. Mambo yalipotulia akajitokeza akiwa
mfanyabiashara. Biashara ambazo ziliwafanya
viongozi waliosalia katika kadhia hiyo kuacha
kumuwinda baada ya kumpa onyo zito wakiamini
hatokuwa tishio tena kwao.
Akiwa katika hali hii, Samsoni Kidude alijikuta
akiachama pale alipokuja kuchukuliwa na
kupelekwa ikulu, ambapo Rais na Mkurugenzi wa
usalama wa taifa walikuwa wakimsubiri. Huko
alitakiwa kueleza sababu ya kuacha kazi hali taifa
likihitaji mchango wake.
Ikiwa nafasi aliyoililia muda mrefu, Samson
alimueleza Rais kinagaubaga wa yale aliyogundua
na ulafi uliomo miongoni mwa watu
wanaolisimamia jeshi la polisi. Akamuhakikishia
kwamba hatoweza kurudi kazini asilani labda kwa
mtindo mwingine.
Baada ya majadiliano ya kina ndipo ilipokubaliwa
Samson arejee kazini kwa siri machoni pia wengine
akiwa Mfanyabiashara na raia wa kawaida. Afanye
kazi zake kwa uhuru na mtindo atakaoona unafaa
na akiwa na tatizo amuone mzee Chilonga ambaye
atakuwa mshauri na kiongozi wake, Nao wanaweza
kuripoti moja kwa ima kwa Mkuu wa usalama wa
Taifa au Rais mwenyewe. Hatua hii ilifuatiwa na
vigogo wachache waliosalia katika kadhia ile
ambao walikuwa wamempa onyo Samson, nao
kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Katika hili Samson aliruhusiwa pia kuwatumia watu
alioona wanafaa ili kufanikisha mipango yake,
kitengo chake ambacho kiliitwa maalum
kikitengewa bajeti ya kutosha toka Usalama wa
Taifa.
Ridhaa ya haya toka Ikulu ndiyo iliyomfanya
afungue ofisi yake pale Upanga na akamuajiri
mrembo Assia Khalifa mwenye ziada ya akili na
maarifa kuwa sio tu katibu Mhutasi wake, bali pia
mlinzi na msiri wake. Kabla ya Ofisi kuanza kazi,
alipelekwa nje ya nchi alikojifunza zaidi ya ujasusi
na ukomandoo.
Naam! Alikuwa na haki ya kusema kumekucha.
Chilonga huwa hamwiti bure. Hii itakuwa mara ya
pili baada ya ile ya mwanzo ambapo mwito wake
ulimuingiza katika sakata jingine zito lililoitwa EPA,
Eleza Pesa Alipozificha! Sakata ambalo mbali ya
kumfanya ayaweke rehani maisha yake mara
kadhaa na kunusurika katika dakika za lala
salama; pia sakata hilo lilikuwa limemuachia mke
mzuri sana, Shuwena Mhasibu Jamaldin!
Mazungumzo yake na Chilo yalikuwa mafupi tu.
Kwamba nchi ilikuwa inaingia katika jaribio lingine
la kihistoria.
Jaribio la Uchaguzi pasipo baba wa Taifa. Wenye
hila na chokocho tayari wamekaa macho juu
wakisubiria kuona litakalotokea. Wengine
wakitamani kuona amani na utulivu tuliodumu nao
kwa takribani miaka arobaini na tano sasa
inatoweka na kuwa kinyume chake.
Manyang’au, mafisadi na waroho wa mali za
umma wameanza kutupa karata zao kuhakikisha
wanavuna. Haya pamoja na ile hofu ya Inspekta
Kimaro ambayo aliifikisha kwa Mnadhimu Mkuu,
nae akaitupa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi aliyeitua
kwa Rais na Rais kuirudisha kwa Chilonga, kwa
pamoja viliwajulisha kuwa hawapaswi kulala tena.
“Rais ameruhusu kutumia kila rasilimali
tunayoitaka!” Chilo akahitimisha.
“Hakuna shida, mwambie asiwe na wasiwasi,
Tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu na mambo
yatakuwa shwari tu, midhali haya yamefika
mapema sioni kama kuna shida tena!” Samson
akajibu.
Likaondokea kuwa jibu lililompa faraja Mzee
Chilonga Anderson.
* * *

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA
“Hakuna shida, mwambie asiwe na wasiwasi,
Tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu na mambo
yatakuwa shwari tu, midhali haya yamefika
mapema sioni kama kuna shida tena!” Samson
akajibu.
Likaondokea kuwa jibu lililompa faraja Mzee
Chilonga Anderson.
* * *

Masurufu aliingia kwake akiwa na unyonge ule ule.
Juhudi za kuuondosha na kujivika uchangamfu
bandia zilikuwa zimekwama mithili ya jitihada za
mlevi chakari anayejitahidi asipepesuke mbele za
watu anaowaheshimu.
Mkewe alimgundua mapema tu na kuanza kuhoji
sababu!
“Hakuna kitu!” Masurufu alikuwa amemjibu hivi
mara kadhaa huku akijivika uchangamfu ambao
nao haukukawia kumtoroka. Mara kadhaa alijikuta
amemsahau mkewe na kuzama katika dimbwi la
mawazo akivuta fikara.
“Masurufu!” Mkewe alimwita tena.
“Naam!”
“Unajua unanishangaza unapoendelea
kung’ang’ania hakuna kitu hali mwili, akili na roho
yako vikikusaliti!” Akamtazama vizuri “Una nini
wewe? Enhe? Hebu niambie Sweetie wangu!”
Hatia zikamuelemea Masurufu. Akashindwa
kumuangalia Glady usoni.
“Unajua kama mficha maradhi kifo humuumbua?”
Lilikuwa swali linguine la mkewe.
“ Najua!” Akajibu kwa moyo mzito.
“Na unajua kama mchuma janga hula na wa
kwao?”
“Sikiliza mama Rose!” Masurufu akashindwa
kuvumilia. “Huna haja ya kunihimiza kwa misemo
na methali kama mtoto wa shule ya msingi. Mie ni
mtu mzima. Najua hicho unachokihofia zaidi ya
unavyotaka kufikiria. Nimekwambia mara zote
hakuna kitu mpenzi wangu. Sijawahi kukudanganya
na sitakaa nije nikudanganye!”
“Lakinii!” Mkewe akapoa. “Body Language
inakusaliti mume wangu. Kama kuna tatizo
niambie, kumbuka mimi ni kila kitu kwako!”
“Sio nikumbuke tu. Bali najua fika. Kwamba wewe
ni kila kitu kwangu. Hebu niamini basi kuwa
mabadiliko yangu haya ni hali ya kawaida tu!”
“Mh! Sawa dia!” Mkewe akakubali
“Aksante kwa kunielewa.”
Ukapita ukimya mfupi.
“Baba Rose!” Mkewe akaita tena na kuuvunja
ukimya
“Rebeka Laaziz!”
“Leo uliniaga kwamba unakwenda kwa Profesa
Zonga!”
Moyo wa Masurufu ukapiga kite kwa nguvu. Kite
kilichoambatana na mshituko mdogo ambao Glady
aliuona sawia. Akajifanya kama hajaona kitu na
kuendelea. “Ila hujaniambia kilichojiri, tafadhali
naomba uniambie basi!”
“Profesa kasema hakuna tatizo kabisa, Tengeneza
sio tishio na ametutaka tuendelee na mipango yetu
kama tulivyoipanga!”
Kitu fulani kikamfanya Glady au mama Rose ahisi
kuwepo kwa walakini katika sentensi hii. Hata
hivyo kwa kuwa alishamuona mumewe na
kugundua kuwa kuna kitu anachokificha, Glady
hakuendelea na maswali zaidi.
Hata changamoto alizokutana nazo katika jukumu
la kuanzisha asasi ya kuwasaida wanawake kama
wake wengine wa marasi waliotangulia, yakiwa ni
maandalizi ya kuwa First Lady, akawa amesahau
kumueleza mumewe huyu Dokta Masurufu.
Badala yake alijikuta akishika majukumu halisi
kama mama nyumbani na mwisho wa yote
akajikuta ameanguka kitandani chini ya mumewe.
Hata baada ya kufanya mapenzi ya kina, bado Dr
Masurufu hakuwa tayari kumueleza mkewe chanzo
cha kupotea kwa furaha yake na kuingiwa na
unyonge.
Siku ya pili usiku kwa kutumia kwa kutumia ndege
ya kukodi walikuwa katika Chinole katika milima
ya Uluguru wakifanya tambiko. Mizimu
iliwahakikishia tena baada ya kunywa damu ya
kutosha kuwa hakuna kitachomzuia Dr Masurufu
kuingia Ikulu.
Maelezo ya mizimu, mazingira ya maeneo yenyewe
pamoja na mtikisiko aliokuwa nao Profesa Zonga
kwa pamoja vilimhakikisha kuwa nchi ilikuwa yake
kwa kila hali.
Masikini laiti angelijua kuwa kuna mtu
alitangulizwa kule msituni kisha mti mkubwa
ukapasuliwa na yeye kuingizwa ndani yake ili
aongee kama mzimu…!
Kumalizika kwa zoezi hilo kulifuatiwa na zoezi
jingine zito la kufifiza nyota ya John Tengeneza na
wenzake siku ya pili yake. Hili lilifanyikia Kerege
Bagamoyo. lilikuwa zoezi fupi lililochukua wastani
wa masaa matatu hivi ambapo Dr Masurufu
aliogeshwa, kisomo kikasomwa, ngo’mbe mweusi
akachinjwa Masurufu akaruka damu yake na
kichwa kikazikwa chini, ndani ya kinywa cha
kichwa hicho kukiwa na majina ya wabaya wote
wa Dokta Masurufu.
Zoezi hili lilifuatiwa na uvunjaji wa nazi sabini na
moja uliofanywa na Masurufu mwenyewe!
Ukaangaji wa nyembe, sindano, na chumvi ya
mawe na vingine vingi. Mpaka shughuli inakwisha,
moyo wa Masurufu ulikuwa kwaatu kabisa,
aliamini kuwa safari ya Ikulu sasa imeiva
barabara!.
Ambacho hakukijua ni kwamba miongoni mwa
wapambe wake aliowaamini na kuambatana nao
kila mahali, mmoja alikuwa akimpelekea habari
zote mkewe Glady Stevenson Ombwe!
* * *&&&******

Siku hii Profesa Zonga akawaita waandishi wa
habari na kuwaeleza mambo kadha wa kadha
kubwa likiwa utabiri wa nani atakuwa Rais wa nchi
hii baada ya Rais anayemaliza awamu yake
kung’atuka.
Katika utabiri wake ingawa hakutaja jina, alitaja
alama zote alizonazo Dr Masurufu na kutoa onyo
kuwa atakayejaribu kushindana nae atapata laana
na uchizi. Kwamba nyota yake ilikuwa inang’aa
sana na alikuwa chaguo la Mungu pamoja na
viumbe vyote.
Kwamba kumpinga ni kwenda kinyume na adhabu
ya hilo ni laana, uchizi na pengine kifo. Hivyo yeye
kama Profesa Zonga wa Zonga, mnajimu na
mtabiri maarufu alikuwa anawaonya wote
wanaotarajia kusimama kujihadhari zaidi
vinginevyo hawatapa zaidi ya hasara.
Siku iliyofuata magazeti yalibeba habari hizi kwa
uzito ule ule uzito uliozidi mipaka. Profesa Zonga
amtabiria Masurufu kuukwaa Uraisi! Gazeti moja
lilidai na kuongeza Nambari za kinajimu zimempa
alama zote za ndiyo. Tayari amechukua fomu
CCM. Wapinzani wake matumbo joto!
Dokta Masurufu safari ya Ikulu yaiva Lilikuwa
gazeti jingine. Utabiri wathibitisha hivyo.
Atakayepambana nae kuambulia laana, Uchizi!
Likahitimisha
Hayakuwa haya pekee, kila moja liliibeba habari hii
na kuipa umuhimu wa pekee. Hata hivyo hazikuwa
habari zilizodumu sana. Kwani wanaharakati wa
mashirika yasiyo ya kiserikali walimshukia Profesa
Zonga na baadhi wa wahariri na wamiliki wa
vyombo vya habari huku wakisaidiwa na watu
walioonyesha na kutangaza nia ya kugombea
urais.
“Profesa Zonga sio Mungu!” mmoja wa viongozi
wa vyama vya Siasa alisema kwa jazba. “kamwe,
hatuwezi kumsikiliza! Nasi tutasimamisha
mgombea ili tuone kama atapata laana kweli!”
Akahitimisha huku wafuasi wake wakimshangilia.
Hii sio nchi ya kishirikiana! Profesa Zonga aache
unafiki na umbea wake! Walikuwa wanaharakati
wengine. Yalisemwa mengi, lakini ni machache
sana yaliyopewa nafasi katika vyombo vya habari
na hayakupewa uzito ule le kama aliopewa Profesa
Zonga. Naam! Bahasha zake kwa waandishi wa
habari zilikuwa zimefanya kazi kweli.
Kule vijijini ambako walipelekewa magazeti kwa
gharama za Dr Masurufu, habari zikaendelea
kushika kasi, Masurufu alikuwa chaguo la Mungu
pamoja na viumbe vyake. Wanakijiji wakamsubiri
kwa hamu ili wasikie atakuja na kitu gani kipya
cha kuwakomboa toka katika umaskini wao
unaochusha na kuudhi.
Nchini Uingereza Chritopher MacDonald aliendelea
kuchekelea kadiri upepo ulivyokuwa ukimuangazia
Dr Masurufu. Hili la mnajimu likiwa limemfanya
afurahi zaidi, hata akainua simu kumuuliza
Masurufu walikolipata wazo hili.
“Ni utaratibu wake kutabiri na kuzungumza na
waandishi wa habari kila baada ya muda fulani!”
Akamjibu.
“Kwa hiyo ni wewe uliyemuuzia wazo hili? Maana
naona limekuwa na mwitikio mzuri kweli kwa
jamii!”
“Hapana! Ni mawazo yake tu. Lakini Profesa
Zonga ni mtu wangu kwa kila hali. Ni yeye
aliyenifanya ning’ae ughaibuni na hata Safari
yangu ya Ikulu anaisimamia yeye kwa mlango wa
nyuma kwa kiasi kikubwa sana tu!”
“Una maana gani Dokta?”
“Sie waafrika Chris! Mambo yetu hayaendi bila
nguvu za mababu na mizimu!”
Christopher akaelewa. Alishapata habari toka Steve
kuwa Masurufu ameamua kuingiza masuala ya
ushirikiana katika harakati zake. Na yeye kwa
kuwa hakuona athari yoyote akawa amemtaka
Steve amuache tu ila ahakikishe lengo lao
haliathiriki.
Labda kilichomtia wasiwasi ni ile hujuma ya
wadhamini bandia ambayo Masurufu alikuwa
ametoa ushauri maridhawa wa kulitatua baada ya
kufanya kikao ambacho Christopher pia alihudhuria
kwa kutumia njia za kielectronic za mnazi wake
Steve.
Hofu yake ilikuwa kama Profesa Zonga angehitaji
amali ya hisa kwa kile anachokifanya baada ya
Masurufu kuwa Rais.
Alipohakikishiwa kwamba Zonga hatohitaji hisa
kwa kuwa alikuwa akilipwa kwa kila hatua,
Christopher MacDonald akaishia kufurahi tu
akiomba waendelee na harakati kama
walivyopanga.

ITAENDELEA....
 
SEHEMU YA KUMI NA SABA

Alipohakikishiwa kwamba Zonga hatohitaji hisa
kwa kuwa alikuwa akilipwa kwa kila hatua,
Christopher MacDonald akaishia kufurahi tu
akiomba waendelee na harakati kama
walivyopanga.
KASHFA
“Nimemaliza kazi Mkuu!” Steve alimwambia Dr
Masurufu mara tu walipoingia katika chumba chao
cha siri pale nyumbani kwa Dr Masurufu. “Hii ni CD
yenye picha chafu za John Tengeneza ambazo
amekuwa akipiga na watoto wa shule
anaowarubuni na kuwaharibia maisha, John ni
fataki. Hili ni faili la watu walio na wanaomdhamini
kifedha ili agombee Urais.” Akatua
Masurufu akafanya pupa kuangalia watu
wanaomfadhili John Tengeneza. Wengi
aliwafahamu, walikuwa katika ule mtandao
alioutengeneza wakati ule akiwa Waziri wa fedha.
Hili likamfanya autilie shaka uadilifu anaodaiwa
kuwa nao John.
“Faili hili pia…” Steve akaendelea “Lina orodha ya
akaunti zake na baadhi ya mikataba aliyoingia na
matajiri wa nchi ili akiwa Rais ashirikiane nao.
Kwa ujumla ni faili lenye kila kitu. Na
limenigharimu kuua watu wawili kulipata. Naamini
hili likifika mbele ya watanzania John atabaki
mtupu kabisa. Itamlazimu kuwa na moyo wa jiwe
na roho ya chuma kuendelea kung’anga’nia Urais
wa Tanzania sio tu kupitia CCM, bali hata nje ya
hapo!” Steve akahitimisha.
“Wow!” Masurufu akashangilia akimkumbatia na
kumpongeza Steve kwa kazi kubwa, ngumu na
nzuri. Machozi ya furaha yakamtoka pale
alipofikiria kuwa zana za kumuua kabisa kisiasa
John Tengeneza zilikuwa mbele ya meza yake,
zikisubiri kauli yake tu!
Christopher alifikiria nini kuniletea mtu kama Steve!
Akajiuliza akijitoa kifuani kwa Steve baada ya
kumpongeza tena kwa mara nyingine na nyingine!
Akaipigia simu kamati yake ya wanaumoja na
kuwataka wakutane nyumbani kwake haraka.
Wakati anawasubiri wajumbe wafike, akainua simu
tena kumpigia Christopher kumjuza kinachoendelea
na hatua waliyofikia katika kumsambaratisha John
Tengeneza.
“Good Job!” Christopher akamwambia. “Ukiweza
kupata taarifa za wapinzani wako wengine pia,
wengine fanya hivyo. Hiyo ndiyo siasa. Siasa sio
mchezo mchafu pekee bali pia ni mchezo wa
kuviziana na kanuni zake ni kama zile za michezo
ya mieleka unanielewa?
“Nakuelewa vizuri sana!”
“Eeh! Katika mieleka ukizubaa kidogo tu
umekwisha. Ndio maana wanasema usijaribu
mchezo ule. Wakati ukitafuta taarifa za hao
wengine, make sure nawe huachi mianya ya taarifa
zako kuvuja maana hilo likitokea hakutakuwa na
maana ya tunachokifanya sasa. Okay?”
“Haina Shida! Maadamu niko na Steve, hakuna
kitakachoharibika!”
“Na katika hili, mwambie Steve asiwe na huruma
hata chembe!”
“Nitamwambia. Always Steve hana mzaha.
Amekwishaua wawili na na kuokoa milioni mia
mbili wakati akiniletea siri hii!”
Alipomaliza kuongea na Christopher, baadhi ya
wajumbe walikuwa wamefika akiwemo Frank John
Mariki Kampeni Meneja wake. Wote kwa pamoja
wakazizunguka picha zile na kuziangalia, kabla
hawajaligeukia faili na kuliperuzi.
Waliyoyakuta na kuyaona yakawafanya wajiulize
kama Tengeneza aliyetajwa kuwa muadilifu na
kuifanyia nchi kazi nzuri, ndiye ambaye faili lake la
siri lilikuwa na zaidi ya Uvundo, je kuna muadilifu
kweli nchini?
Hata hivyo wao wakiwa chui ndani ya ngozi ya
kondoo, hili halikuwa shughulisha sana, badala
yake walikenua kwa kupata njia ya kumuadhibu
adui yao. Wakajipangia mikakati ya kummaliza
John kabisa kabisa na kugawana majukumu, tayari
kwa utekelezaji.
* * *
Mikakati ilitekelezwa vizuri, gazeti la Dr. Masurufu
likawa la kwanza kuibuka na habari za kashfa za
John Tengeneza. Kwamba alikuwa fataki na
kamwe hakufaa kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano, kitendo chake cha kutembea na watoto
wa shule na kuwaharibia maisha viongozi wa
Tanzania ya kesho, hakikufaa kuungwa mkono.
Kwamba alikuwa kinyume kabisa na ajenda ya
watoto.
Picha kadhaa za aibu za John Tengeneza
zikatolewa ukurasa wa mbele huku gazeti likidai
kumiliki CD yenye kila uozo wa John. Magazeti ya
udaku yakaipa uzito habari hii na kuigeza ajenda
ya kibiashara ambapo kwa kuwa na habari hizo,
magazeti yao yaligombewa kama njugu sokoni.
Majina ya matajiri waliomdhamini kwa
makubaliano ya kuwapa vyeo yakatolewa pamoja
na idadi ya fedha, mahala zilikowekwa pamoja na
nambari za akaunti. Watu wakabaki midomo wazi
wasiamini kama Tengeneza alikuwa hivyo
anavyodaiwa.
Haya yakawa yamechokoza nyuki
Mara moja siasa zikabili uelekeo. Familia ya John
Tengeneza na watu wake wakaanza kuhaha
kutafuta nani aliyevujisha siri hizi hatari, ambazo
zilikuwa zimehifadhiwa mbali na watu wake wawili
aliwaamini vyema Mathew na Mathias, ambapo
alipofuatilia zaidi aligundua kuwa watu wake hao
walikuwa marehemu. Ndipo akaelewa kuwa
tuhuma zile ambazo yeye zilimbomoa sana, kwa
vijana wake ziliwagharimu maisha.
Ghadhabu zikampanda pale vijana wake
walipomletea taarifa kwamba Dr Masurufu ndiye
aliyekuwa nyuma ya njama hizi chafu. Akaanza
kuwaza na kuwazua namna atakavyoweza kulipa
kisasi.
Mara akaanza kupokea waandishi wa habari
waliotaka kujua anasemaje kuhusu tuhuma hizo na
kama anatarajia kujiengua katika kinyang’anyiro
cha kuwania kuteuliwa na chama kuwa kiongozi.
Kama ambavyo huwa kwa wanasiasa wengi, naye
alikanusha kwa nguvu zake zote kuwa huo ulikuwa
uzushi na uongo mtupu. Aliwataja waliotoa
tuhuma hizo bila hata kumpa nafasi ya kujitetea
kuwa ni wanafiki na wazandiki wakubwa na
kwamba kama wanafikiria atajitoa katika
inyang’anyiro hicho walie tu, kwani sasa
ataongeza nguvu zaidi ili hatimaye aweze kushinda
na kuteuliwa na chama.
Hata hivyo aliwahakikishia waandishi kwamba
anawasiliana na wakili wake ili aandae taratibu za
kumfikisha mahakamani kila aliyemkashifu na
kumchafua ambapo atawadai mabilioni kwa
mabilioni ya shilingi.
Habari hizi zilipotoka zikazusha mjadala mitaani.
Kama ilivyo ada zikawachulia watanzania muda
mwingi kuzijadili baadhi wakiafiki na baadhi
kutoafiki huku wingi wao wakisubiria kwa hamu
John Tengeneza afungue kesi.
Kesi haikufunguliwa! Badala yake walishuhudia
siku kadhaa mbele magazeti megine tofauti na yale
ya mwanzo, Redio na Televisheni ambavyo vilikuwa
vikimuunga mkono John Tengeneza vikaibuka na
habari mbaya na chafu kwa Dr Masurufu.
Kwamba licha ya kulelewa na Baba wa Taifa
Masurufu alikuwa fisadi nambari moja nchini, Papa
la Rushwa, Mkwepaji mkubwa wa kodi na jambazi
wa kalamu. Mifano hai ya kutosha ikatolewa
kulithibitisha hili, mali zake alizozipata wakati ule
zikiwekwa hadharani na kutakiwa akanushe
uthibitisho wa vielelezo hivyo kama anadhani
anaonewa.
Sio hivyo tu, alielezwa pia namna alivyolitumia
vibaya jina la Baba wa Taifa kujinufaisha,
alivyolitumia Azimio la Arusha na Kampeni za
uhujumu Uchumi kujilimbikizia mali pamoja na vita
vya Uganda ya mwaka sabini na nane vyote kwa
pamoja viliudhihirisha umma kuwa ni kweli Dr
Masurufu alikuwa fisadi nambari moja nchini.
Habari hizi ambazo wengi ziliwaacha midomo wazi,
baadhi wakishika vichwa kutoamini wakisikiacho,
kwa Masurufu zilikaribia kuondoka na roho yake
kwa kuwa alijikuta akishikwa Shinikizo la damu
baadae kizunguzungu kikali kabla hajaanguka chini
na kuzirai ambapo alikimbizwa hospitali ya Ocean
Road zilikoanza juhudi za kuokoa maisha yake.
Habari za ugonjwa wake zikatakiwa kuwa siri
kubwa hata watumishi wake ofisini hawakujua
yupo wapi!
***Mfyuuu! Ikulu mchezo!

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom