Ikulu, Dodoma: Rais Magufuli apokea ripoti ya TAKUKURU na CAG. Asema Corona haitazuia Uchaguzi Mkuu 2020

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,875
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anakabidhiwa Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2018/2019 inayowasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Seriakali (CAG) Charles Kichere.

Aidha Mhe. Rais atapokea Ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2018/2019 itakayowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Taasisi hiyo Brigedia Jenerali John Mbungo.

Hafla inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu Chamwino Jijini Dodoma Machi 26, 2020.




=========
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu hautaahirishwa licha ya kuwepo kwa mlipuko wa virusi vya corona.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Machi 26 Ikulu ya Chamwino, Dodoma wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na ripoti ya Takukuru.

Amesema baadhi ya watu wamekuwa wakifikiri kwamba kazi hazifanyiki na hakuna kukutana kwa sababu ya corona. Amesema hata nchi zilizoathirika zaidi na virusi hivyo, bado mabunge yao yanakutana kama kawaida.

"Sisi tunaendelea kukutana, ndiyo maana hata Bunge linaendelea na vikao vyake, hata huko kwenye nchi zilizoathirika kabisa, mamilioni ya watu wamekufa kwa corona, bado mabunge yao yanakutana. Kazi lazima ziendelee...

"Na uchaguzi tutafanya, wapo wanaofikiri kwamba tutaahirisha, nani anataka kukaa kwenye maofisi haya muda wote huo," amesema Rais Magufuli wakati akizungumza kwenye hafla ya kupokea ripoti hizo.

Rais Magufuli ameeleza kushangazwa na mwandishi mmoja kuandika habari kwamba "Baraza la madiwani lafanya mkutano licha ya corona" na kuhoji kama mikutano ya aina hiyo imezuiwa.

Amesisitiza kwamba kazi lazima ziendelee kufanyika licha ya uwepo wa virusi hivyo na mikutano ya baraza la madiwani, Bunge na hata ile anayoifanya yeye itaendelea kufanyika kwa sababu ni sehemu ya kazi zao.


=================

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amesema katika ukaguzi wao wamebaini malipo ya jeshi la polisi kiasi cha sh Milioni 193.13 kwa watumishi 11 ambao wamefariki,kufukuzwa na kustaafu.

Kichere ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa ya ripoti ya CAG ya mwaka 2018/19 kwa Rais John Magufuli.

Alisema katika ukaguzi wao wamebaini fedha hizo kutolewa kinyume cha matakwa ya kanuni ya fedha ya mwaka 2001.

Aidha, amesema kuna taasisi tano za serikali zimefanya manunuzi ya Sh bilioni 5.2 bila kuwepo kwa nyaraka za mikataba.
 
Report ya CAG nadhani kwanza itakuwa imereview nini kilikuwa revealed kwenye ukaguzi wa mwaka jana, recommendations zilikuwa zipi na kwa kiasi gani hizo recommendations zilikuwa acted upon by Rais mwenyewe na watendaji wote.

It doesn't make a lot of sense kufanya huo ukaguzi na kuibuka na madudu yaleyale huku recommendations zikiwa ignored na kila mtu.

Bila shaka this time around CAG hakuzuiwa kupita maeneo yote.
 
Back
Top Bottom