Iko wapi CHADEMA ya Operesheni Sangara na M4C?

Iko wapi CHADEMA ya Operesheni Sangara na M4C?

Ndo mana ccm wanakula nchi na kupiga madili ya kila aina mana washajua watanzania manyumbu wasiojitambua ni wengi hasa upande wa upinzani....inakuwaje mtu kama lowasa na kashfa zote zile awanunue chadema na ukawa nzima bila ata ya kujitambua kaja cdm kufanya nini????....Mtu mgonjwa kama yule atapiga madili na kuondoka nyuma atatuchia madeni....atadaiwa na nani mana maiti uondoka na kila kilichochake.
 
Huyo ananilea nkya asitulazimishe fikra zake ziwe ndiyo fikra zetu,tunataka lowasa ajibu hoja siyo wanakuja kujibu hoja wasiohusika
 
Iko wapi ccm ya mwl nyerere¿????????????¿
Mwalimu wakati wake ulishapita na ulikuwa ni wakati wa chama kimoja.

Tunaongelea Tanzania ya leo na ya wajukuu zako.
 
Naona uzi huu umejaa wale wale mnaoongozwa na siasa za jumfuata mtu, chadema inachanja mbuga
 
Tumewaachia team Lowassa, ninyi ndio kila kitu.

Haya safari njema Timu Slaa, hovyo kabisa So ingetokea leo Huyo Slaa kafa means tungefuta CDM, hopeless kabisa. Hiyo kura nasi pia tunayo tukutane Oct
 
Nilitokea kuipenda sana Chadema kama chama cha upinzani kilichokuwa mstari wa mbele kupiga vita RUSHWA na UFISADI.
Kilijipambanua vizuri sana ktk harakati zake.
Leo hii sisikii tena kwenye kampeni za Urais za Lowasa namna gani watapambana kudhibiti RUSHWA na UFISADI, kwenye vipaumbele vya lowasa hakuna!!

Tunaenda kutengeneza serikali isiokula rushwa now mpango wetu ni kuingia ikulu sio kua chama cha upinzani tu chama chochote cha siasa ambacho hakifikirii kushika madaraka ni bora kabisa kikafutwa
 
Hivi Chadema wanategemea dakika hii ku handle issue ya Dr Slaa na kushinda uchaguzi .....issue ya Zitto ilichukua muda mrefu na bado ikaacha majeraha ....sijui tumekumbwa na nini .....tumeacha vijanà wa M4U na watu wetu kueneza uongo dhidi ya mtu anayejua alijenga wapi na abomoe wapi tena dakika hizi ....huu ni upuuzi kufikiri mnaweza kumfanyia propaganda Dr Slaa .... Muda haupo na atawaumiza vibaya ....

Hapo tu ndio Dr namwona wa ajabu kumbe lengo lake ni kuharibu , kweli Lipumba ni prof sio hawa wapenda concabine
 
Huyo ananilea nkya asitulazimishe fikra zake ziwe ndiyo fikra zetu,tunataka lowasa ajibu hoja siyo wanakuja kujibu hoja wasiohusika

Hana mda mchafu wa kujibizana na watu wanaotumika na ccm
 
Siioni kabisa, ile Chadema iliyoenda kupiga kambi Kanda ya pwani zaidi ya wiki moja.

Ile Chadema iliyosambaa Kanda zote kuelemisha Wananchi kuhusu Ufisadi na maovu ya ccm kwa ujumla.

Ile ya Lema, Mnyika, Mdee, kwa upande mmoja Sugu,Silinde,Msigwa kwa upande mwingine. Lissu, wenje na wengineo.

Ile ya viongozi wenye upeo toka makao makuu,Pr.Safari, Pr.Baregu na wengineo.

Ile ya vijana makamanda tofauti toka idara tofauti makao makuu.

Kweli leo Chadema ni ya kupelekwa ikulu na akina Sumaye, Masha, Msindayi na Mahanga?

Wako wapi makamanda wa ukweli tuliowazoea wananchi, waliokipaginia chama kwenye jua na mvua usiku na mchana.?

Najua mtasema wengi wapo bize na kampeni kwenye majimbo yao.

Lakini binafsi naamini Lema, Lissu alieashinda asilimia tisini ya serikali Za mitaa, Silinde ambae wananchi wake wanaimba Chadema hadi usingizini, Sugu ambaye ni Rahisi wa Mbeya, Mdee mwanamke shujaa wa siasa za upinzani Tanzania na wengineo.

Hawawezi kushindwa kupoteza siku mbili kwenye majimbo yao na kumnadi Lowassa kwenye mbio za urais.

Poleni makamanda najua wengi wenu mnamadukuduku mioyoni mwenu ila ni ngumu kusema kwa kuogopa kuitwa wasaliti.

Kwa hatua ilipofikia Chadema, kilikuwa sio chama cha kutegemea Sumaye awapeleke ikulu wala Masha wala Msindayi hata Lowassa Mwenyewe.!

Bado naililia Chadema yangu ya ukweli na mtetezi halisi wa watanzania sio hawa wasaka madaraka tu.!


Tukutane October 25

Zitto vip hakuwemo kwenye kikosi hicho au unachuki uliopandikizwa
 
Kesho Lowasa akimteua Makongoro Mahanga na wana CCM kuwapa ubunge viti maalum na kisha kuwateua kuwa mawaziri ndio watu wa aina hii tuliwataka ..... Hivi kuna mtu hapa anaweza kunijibu nini kinamfanya aamini Lowasa atasimamia kile tulichoamini muda mrefu?

Usitoke ugambani
 
Kwanini tunaamini Lowasa atasimamia kile tulichopigania kwa miaka mingi ...... Akiwageuka mtalia na nani ..... Hivi kama swala ni Uchadema .....Chadema ni nini .....tukiamua Leo CCM kuiita Chadema na Chadema kuwa CCM bado utaichagua Chadema ..... nini kimetuingia hadi tunamsaliti jemedari wetu aliyesimama na sisi wakati wa jua na mvua ...

Mkuu inaskitisha
 
Haya safari njema Timu Slaa, hovyo kabisa So ingetokea leo Huyo Slaa kafa means tungefuta CDM, hopeless kabisa. Hiyo kura nasi pia tunayo tukutane Oct

Hatusimamii mtu bali msingi ya chama, mimi na wewe tutapita lakini chama kitabaki palepale.
 
Back
Top Bottom