Iko wapi CHADEMA ya Operesheni Sangara na M4C?

siioni kabisa, ile chadema iliyoenda kupiga kambi kanda ya pwani zaidi ya wiki moja.

Ile chadema iliyosambaa kanda zote kuelemisha wananchi kuhusu ufisadi na maovu ya ccm kwa ujumla.

Ile ya lema, mnyika, mdee, kwa upande mmoja sugu,silinde,msigwa kwa upande mwingine. Lissu, wenje na wengineo.

Ile ya viongozi wenye upeo toka makao makuu,pr.safari, pr.baregu na wengineo.

Ile ya vijana makamanda tofauti toka idara tofauti makao makuu.

Kweli leo chadema ni ya kupelekwa ikulu na akina sumaye, masha, msindayi na mahanga?

Wako wapi makamanda wa ukweli tuliowazoea wananchi, waliokipaginia chama kwenye jua na mvua usiku na mchana.?

Najua mtasema wengi wapo bize na kampeni kwenye majimbo yao.

Lakini binafsi naamini lema, lissu alieashinda asilimia tisini ya serikali za mitaa, silinde ambae wananchi wake wanaimba chadema hadi usingizini, sugu ambaye ni rahisi wa mbeya, mdee mwanamke shujaa wa siasa za upinzani tanzania na wengineo.

Hawawezi kushindwa kupoteza siku mbili kwenye majimbo yao na kumnadi lowassa kwenye mbio za urais.

Poleni makamanda najua wengi wenu mnamadukuduku mioyoni mwenu ila ni ngumu kusema kwa kuogopa kuitwa wasaliti.

Kwa hatua ilipofikia chadema, kilikuwa sio chama cha kutegemea sumaye awapeleke ikulu wala masha wala msindayi hata lowassa mwenyewe.!

Bado naililia chadema yangu ya ukweli na mtetezi halisi wa watanzania sio hawa wasaka madaraka tu.!

Tukutane october 25

mkuu mbona kampeni hata mwezi bado, subiri, silaha nzito hutumika wakati vita imepamba moto
 
Yaani pumba tupu ...hao uliowataja wote ni wagombea ubunge na wana kazi maalumu ya kuzunguka na chopa kwenye msjimbo kadhaa kumnadi mgombea urais hata ratiba ya chama hamuijui then mnaajiita chadema......hamjalazimishwa c muondokee

Najiuliza kwa kuandika humu siyo kujibu uliyoandika:

1. Ni kitu gani kinaendelea ndani ya vyama vinavyounda UKAWA kwa ujio wa viongozi waliotemwa CCM, na maneno yaliyotamkwa na kiongozi wao mmoja mkuu siku chache zilizopita?

2). Iwapo UKAWA watashinda uchaguzi itakuwaje muungano huu, ikizingatiwa kwamba kuna chama ndani ya UKAWA kisicho na usajiri lakini kina nguvu kubwa kuliko vilivyopo?

3). Iwapo UKAWA wasiposhinda uchaguzi, kutasalimika ndani ya vyama hivi, hasa viongozi!

Siku zimebaki chache tu kitendawili kiteguliwe.
 
Kwanini tunaamini Lowasa atasimamia kile tulichopigania kwa miaka mingi ...... Akiwageuka mtalia na nani ..... Hivi kama swala ni Uchadema .....Chadema ni nini .....tukiamua Leo CCM kuiita Chadema na Chadema kuwa CCM bado utaichagua Chadema ..... nini kimetuingia hadi tunamsaliti jemedari wetu aliyesimama na sisi wakati wa jua na mvua ...
Hata hivyo kwa sasa iliyokuwa CHADEMA ni ccm na iliyokuwa CCM ndio chadema
 
mkuu mbona kampeni hata mwezi bado, subiri, silaha nzito hutumika wakati vita imepamba moto
Ndio yaleyale ya kuleta zimamoto wakati nyumba imeteketea.!

Ngoja tusubiri.!
 
Hivi Chadema wanategemea dakika hii ku handle issue ya Dr Slaa na kushinda uchaguzi .....issue ya Zitto ilichukua muda mrefu na bado ikaacha majeraha ....sijui tumekumbwa na nini .....tumeacha vijanà wa M4U na watu wetu kueneza uongo dhidi ya mtu anayejua alijenga wapi na abomoe wapi tena dakika hizi ....huu ni upuuzi kufikiri mnaweza kumfanyia propaganda Dr Slaa .... Muda haupo na atawaumiza vibaya ....
Mkuu bandiko lako linaacha hisia kali za kizalendo ndani ya chama, lakini hakuna namna.

Tuvumilie maumivu, huku tukijipanga kupata chama bora cha upinzani miaka kadhaa ijayo.
 
usicheze na mbowe, yule jamaa level ingine. au umesahau alivyokuwa akimkejeli slaa juzi? kuwa treni inayoenda kanda ya magharibi ikifika mnyoni wengine wakashuka wao wanendelea na safari? au umeisahau ile ya kupwa na kujaa kwa maji hakusubiri mtu? huyo ndo mbowe a.k.a born town.

Siioni kabisa, ile Chadema iliyoenda kupiga kambi Kanda ya pwani zaidi ya wiki moja.

Ile Chadema iliyosambaa Kanda zote kuelemisha Wananchi kuhusu Ufisadi na maovu ya ccm kwa ujumla.

Ile ya Lema, Mnyika, Mdee, kwa upande mmoja Sugu,Silinde,Msigwa kwa upande mwingine. Lissu, wenje na wengineo.

Ile ya viongozi wenye upeo toka makao makuu,Pr.Safari, Pr.Baregu na wengineo.

Ile ya vijana makamanda tofauti toka idara tofauti makao makuu.

Kweli leo Chadema ni ya kupelekwa ikulu na akina Sumaye, Masha, Msindayi na Mahanga?

Wako wapi makamanda wa ukweli tuliowazoea wananchi, waliokipaginia chama kwenye jua na mvua usiku na mchana.?

Najua mtasema wengi wapo bize na kampeni kwenye majimbo yao.

Lakini binafsi naamini Lema, Lissu alieashinda asilimia tisini ya serikali Za mitaa, Silinde ambae wananchi wake wanaimba Chadema hadi usingizini, Sugu ambaye ni Rahisi wa Mbeya, Mdee mwanamke shujaa wa siasa za upinzani Tanzania na wengineo.

Hawawezi kushindwa kupoteza siku mbili kwenye majimbo yao na kumnadi Lowassa kwenye mbio za urais.

Poleni makamanda najua wengi wenu mnamadukuduku mioyoni mwenu ila ni ngumu kusema kwa kuogopa kuitwa wasaliti.

Kwa hatua ilipofikia Chadema, kilikuwa sio chama cha kutegemea Sumaye awapeleke ikulu wala Masha wala Msindayi hata Lowassa Mwenyewe.!

Bado naililia Chadema yangu ya ukweli na mtetezi halisi wa watanzania sio hawa wasaka madaraka tu.!

Tukutane October 25
 
Mbowe hii laana na kelele zetu ipo siku vitamtoa usingizini na atajikuta mtupu
 
Labda sio mbowe huyu ninayemjua.
mbowe akampigie magoti slaa? thubutu.
kwanza hana nini mpaka aende kwa slaa? kama ni pesa anayo!
au husikii anavyomkejeli siku hizi? mara ''kupwa na kujaa kwa bahari hakusubiri mtu''! hivi hamjifunzi kitu hapo?

Nakwambia tutamkumbuka dr Slaa daima.mtazungumka weeeee lakkni mwisho wa siku mtarudi kwa Dr Slaa. Na nasema Mbowe atakuwa wa kwanza kupiga magoti kwa Slaa pale Chadema itakapokuwa imepasuka na kusambaratika, na wafuasi sasa kuanza kudai haki zao
 
Mbowe hii laana na kelele zetu ipo siku vitamtoa usingizini na atajikuta mtupu
Kuna watu wanaamini wataishi kwa propaganda muda wote, ila tuwe wavumilivu ukweli utadhihirika tu.!
 
Wacheni mchezo wa kitoto, nyie magamba mnajifanya makamanda kujadili mambo ya CDM. ukilia kuliko mwenye mtoto ujue wewe ni ...
 
Kwanini tunaamini Lowasa atasimamia kile tulichopigania kwa miaka mingi ...... Akiwageuka mtalia na nani ..... Hivi kama swala ni Uchadema .....Chadema ni nini .....tukiamua Leo CCM kuiita Chadema na Chadema kuwa CCM bado utaichagua Chadema ..... nini kimetuingia hadi tunamsaliti jemedari wetu aliyesimama na sisi wakati wa jua na mvua ...

Mkuu kuna usemi watu wanasema cdm walimpenda dr slaa kwa kusema ukweli kuhusu ufisadi na leo hii wana cdm hawampendi Dr slaa kwa kusema ukweli kuhusu ufisadi
 
Mkuu kuna usemi watu wanasema cdm walimpenda dr slaa kwa kusema ukweli kuhusu ufisadi na leo hii wana cdm hawampendi Dr slaa kwa kusema ukweli kuhusu ufisadi

Na huo ndio ukweli watu wanapenda siasa nyepesi kuliko hoja.!
 
Wacheni mchezo wa kitoto, nyie magamba mnajifanya makamanda kujadili mambo ya CDM. ukilia kuliko mwenye mtoto ujue wewe ni ...
Hakuna gamba hapa watu tunapenda mabadiliko ya ukweli siyo ya maigizo na yanayodhaminiwa na akina Rostam.!
 
Back
Top Bottom