Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,108
- 18,325
PhD aliisahau mbeya
Nadhani sasa itungwe Sheria ya kwamba hawa ' Wakubwa ' wa Serikalini wawe wanatuwekea na Majina ya Vyuo Vikuu vyao walivyosoma huko Ulaya na kupata hizo ' Doctorate Degree ' zao ili nasi tujiridhishe kwani siyo Siri Mimi GENTAMYCINE kwa hii Elimu yangu tu ya Darasa la Saba naona nawazidi Wakubwa / Viongozi wengi mno na ambao ni ' Wasomi ' katika suala zima la Ujengaji Hoja na matumizi sahihi ya Akili tulizopewa bure na Mwenyezi Mungu.
Sasa nathibitisha rasmi kuwa nina ' Mashaka ' makubwa na ' PhD ' ya Waziri Mwakyembe na za Watu wengine kama Sita ( 6 ) hivi ila leo nawaweka ' Kiporo ' kwani haiwezekani na haiingii akilini Mtu mwenye Elimu Kubwa tena ya kuwa na Doctorate Degree / PhD lakini bado anawaza Kipopoma / Kipumbavu namna hii.