Ijue tafsiri ya neno mnyonge

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,533
Mnyonge / mɲɔngɛ / nomino

Wanyonge (plural)

Ngeli za nomino: a-, wa-

MAANA YA NENO:
1. mtu dhaifu; mtu asiyekuwa na nguvu Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni (ms) Synonyms: mnyela
2. mtu mwenye tabia ya upole na ya kunyenyekea
3. mtu wa hali ya chini Mnyonge kupata haki ni mwenye nguvu kupenda (methali)

Synonyms (Neno mfanano) : kabwela

MY TAKE:
Hapo kwenye neno mfanano ndiyo pamenichosha kabisa KABWELA? Kwa hiyo mtu akituita sie Wanyonge katuita nyie MAKABWELA?!!

Wanasiasa tuache kutumia neno hili halipendezi na linatweza utu wa Mtanzania.

Nyadikwa
 
Wadau habari zenu,

Naomba kujua maana halisi ya neno mnyonge, vyovyote litakavyotafsiriwa binafsi silipendi kabisa naona linaanza kushika kasi na kuota mizizi, tunaitwa sana wanyonge na wana siasa, nashauri tuitwe tu WATANZANIA.
 
Nakushukuru sana mdau, nimepost muda si mrefu nimeposit mada kama hii sikujua! kama umeelezea vizuri sana, anyway binafsi silipendi hili neno, tupaze sauti sauti wana siasa wasituite sisi wanyonge, watumie neno wananchi au Watanzania, waache kutusanifu .
 
Nakushukuru sana mdau, nimepost muda si mrefu nimeposit mada kama hii sikujua! kma umeelezea vizuri sana, anyway binafsi silipendi hili neno, tupaze sauti sauti wana siasa wasituite sisi wanyonge, watumie neno wananchi au watanzania, waache kutusanifu .
Kabisa aisee. Ni neno dhalili sana kulitumia kwa binadamu. Huo unyonge ni subjective term na mhusika ndiye anaweza kujipambanua badala ya mtu kumwita jina hilo.
 
Mnyonge, Kabwela, Kapuku, Sakala
😆😅😄😃😂😁😀😉😗😘😍😋
 
Ni neno linaweza kutafsiriwa kama mtu 'incompetent ' nikisikia mtu anahisi kachaguliwa kisa mnyonge inafikirisha sana.
 
Na viongozi wetu wanaona ufahari ku enslave wanaowaongoza kwa kutumia neno mnyonge
 
Wanyonge ni kundi kubwa la wajinga na wasiojitambua ambao ni bendera fuata upepo.

Wao hata wakienda mahakamani wakapata haki zao watajiona wamependelewa sana utafikiri hawakusitahili kupata haki yao walitakiwa wanyongwe tu.
 
Huyu hapa

FB_IMG_1575390806699.jpg


FB_IMG_1575390800494.jpg


FB_IMG_1575390792397.jpg
 
Rais wa Wanyonge na serikali ya wanyonge kumbe hao ndio watu wake? Na CCM kila siku inazungumzia wanachama wake kubwa ni watu wanyonge wa nchi hiyo, kumbe ni wale dhaifu, hohehahe na masikini wa kutupwa?

Sasa kwa nini inawataka kwa fahari kama vile jambo hilo ni la kujivunia?

Kukubali kuitwa "Wanyonge" ni aibu hivyo bora wawaite haohao wanachama wao wa CCM ambao hata waitwe mazwazwa kwao sio jambo la aibu.


IMG-20210331-WA0006.jpg
 
Mnyonge ni mtu asiyekuwa na furaha mnyonge haina uhusiano na kipato cha mtu. Mgonjwa anaweza kuwa mnyonge, unaweza ukahisi njaa ukawa myonge, unaweza kufiwa ukasikitika ukawa myonge. Ukimchapa mtoto wako anakosa raha anakuwa myonge.

Kwa kingereza mnyonge ni wretched. (of a person) in a very unhappy or unfortunate state.

"I felt so wretched because I thought I might never see you again"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom