Sheikh23
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 1,202
- 2,002
A.alleikhum
Kwanza tupate tafsiri ya neno "Mnyonge" ( plural wanyonge)
* Mtu dhaifu; mtu asiyekuwa na nguvu.
* Mtu mwenye tabia ya upole na ya kunyenyekea.
* Mtu wa hali ya chini.
Ok,sasa twende kwenye hoja ya msingi,haya mahubiri ya kwamba hii ni serikali ya wanyonge yana maana gani? A. Kuondoa unyonge B. Kuendeleza unyonge..Je, ni nani ameuleta huo unyonge kwa wananchi?
Mategemeo ya raia wengi ni kutoendelea kuitwa wanyonge kwa kujengewa misingi ya kimaendeleo na serikali yao,hili limeferi kwani mwananchi huyu anayeitwa mnyonge ndio amekata tamaa kabisa kwani mifumo iliyowekwa imeshindwa kumkomboa kifikra,kisiasa,kijamii na kiuchumi.
Haya yanadhihirishwa na hali halisi iliyopo mtaani,kwani hakuna mnyonge aliyeguswa na serikali
> Mvuvi analia
>Mfanyabiashara analia
>Mkulima analia
>Mtumishi wa Umma,huyu analia na kusaga meno
>Mwanasiasa (Oppositions) analia
> Vijana haswa Graduates wanalia tena kilio cha kupaliwa na pilipili.
Vilio hivi vya hali ngumu vya mwananchi mnyonge sio maigizo,makada wa chama ukiwaambia haya watakwambia "hao walizoea upigaji", Upigaji kwa tafsiri ya mtaani ni wizi/kuiba/kujipatia mali kwa njia zisizo halali,sasa unajiuliza mathalani,mama lishe anampiga nani?
Mwalimu anampiga nani,maana elimu bure siku hizi hakuna michango,machinga anampiga nani? Mpiga debe anampiga nani? Mkulima anampiga nani?
Sio kila mtu kwa nafasi aliyopo ana access ya kupiga (kuiba),hivyo Akili hizi za kuambiwa makada wachanganye na za kwao,kuuza uhuru wa fikra kwa malipo ya ushabiki maandazi ni uchizi wa kiwango cha Phd...
Mwisho kabisa nategemea kabla ya uchaguzi next year tutapewa takwimu from 2015 wanyonge tulikuwa wangapi? Na kama tumepungua tupo wangapi? Pia kama idadi yetu imeongezeka takwimu ikoje?
Ndugu zangu tuendelee kuisoma namba huku tukipambana kuukataa Unyonge wa kulazimishwa.
°
°
Sheikh 23View attachment 1131560