PostGE2025 Ijue safari ya ufunguaji kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu (ICC) kwa muktadha wa hali ya Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Emekha Ikhe

Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
52
Reaction score
84
UFUNGUAJI WA KESI KATIKA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA UHALIFU ICC KWA MUKTADHA WA HALI YA TANZANIA

Naomba nitumie lugha rahisi kwa Ufafanuzi ambayo hata asiye mwanasheria aelewa ili kuendelea kutoa Ushirikiano wa taarifa za uhalifu wa Haki za Binadamu uliotokea Kabla, Wakati na baada ya Kilichoitwa Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29th Oktoba 2025. Kama Taifa, Tunaweza kupuuza vitu vingine lakini sio UHAI wa Watu wetu wakiwemo (GEN-Z) ambao kwa zaidi ya asilimia 90% ndio waathirika wakubwa.

Nitoa ufafanuzi kuhusu Utaratibu wa kufungua kesi ya jinai katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), kama sehemu ya kutoa elimu na vilevile kuendelea kutoa wito kwa Watanzania wote ambao huenda wameathirika wa uhalifu wa haki za binadamu bado hawatoi Ushirikiano wa taarifa kwa kuwa hawajui athari zake. Kimsingi taarifa zenye Ushahidi ndio nyenzo wezeshi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ili kuwaweka Wshukiwa hatiani na kupigania HAKI YA KUISHI ambayo ipo hatarini Tanzania.​

Ufuatao ni utaratibu wa kufungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na unahusisha hatua kadhaa kama ifuatavyo;

Mosi, Kujiridhidha Mamlaka ya Mahakama- (Court Jurisdication)

Hatua ya kwanza Kabisa, huanzwa na kujiridhisha Mamlaka ya Mahakama katika kusikiliza jinai/uhalifu husika, hapa lazima Mlalamikaji au Walalamikaji au Mahakama yenyewe ijiridhishe kwamba ina mamlaka kisheria ya kusikiliza jinai au uhalifu wa Haki za Binadamu ambao unalalaikiwa

Pamoja na ukweli kwamba, Mwendesha Mashtaka wa ICC ana mamlaka kamili Kisheria kufungua kesi mwenyewe (Suo Moto) kupitia ofisi yake, Nieleze njia kuu tatu zilizoruhusiwa na sheria za Kimataifa juu ya utaratibu za Kufungua kesi;​
Kesi-Kufunguliwa na Nchi Mshiriki, Nchi ambayo imeridhia na kuidhinisha Mkataba wa Kimataifa wa Rome (Rome-Statute) na Mkataba wa uanzilishi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), inaweza kufungua kesi ICC kwa kuelezea hali halisi ya Uhalifu wa Haki za Binadamu katika eneo lake au mahali pengine kwa Mwendesha Mashtaka wa ICCclass=y2iqfc>
Kesi-Kufunguliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN Security Council, Baraza la Kufungua kesi kwa kupeleka hali halisi ya Uhalifu wa Haki za Binadamu uliotokea katika nchi yeyote kwa Mwendesha Mashtaka wa ICC, na kutoa mamlaka ya Mahakama ya ICC hata kama uhalifu husika ulitokea katika eneo la nchi isiyo Mwanachama (Non State party)
Kesi-Kufunguliwa na Mwendesha Mashtaka wa ICC, Huu ni Mpango wa Mwendesha Mashtaka mwenyewe (Suo Moto): Mwendesha Mashtaka wa ICC anaweza kuanzisha uchunguzi kwa hiari yake mwenyewe kulingana na taarifa kutoka kwa vyanzo vya kuaminika, ikijumuisha Waathiriwa, Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), au vyanzo vingine. Katika kesi kama hizo, Mwendesha Mashtaka anahitaji idhini kutoka kwa majaji (3) wa Awali ili kufungua Jarada la uchunguzi rasmi. style='font-family:"Century Gothic",sans-serif;mso-bidi-font-family:"Times New Roman"​
Baada ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa ICC kupokea taarifa au rufaa, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka hufanya uchunguzi wa awali ili kubaini kama malalamiko ya Uhalifu wa Haki za Binadamu unakidhi vigezo vya Kufunguliwa kwa Kesi katika Mahakama ya ICC, ikiwa ni pamoja na kutathmini mamlaka yake ya kuendesha shitaka husika kwa ajili ya kutoa haki kwa Wathiriwa na adhabu kwa Waliohusika katika Uhalifu wa Haki za Binadamu
Kwa Muktadha wa Tanzania, Njia zote tatu zinatumika, Kuna Makundi mbalimbali yametumia njia mbali mbali tajwa hapo juu katika kufikisha malalamiko ya Uhalifu wa Haki za Binadamu Tanzania ili Mahakama ya ICC ichukue hatua dhidi ya wahusika wa Uhalifu. Tumeona Ripoti na documentary mbalimbali ikiwemo ile ya CNN ambayo pasi na shaka itatumika kama sehemu ya ushahidi maana ni chombo cha habari kinachoaminika.

Pili, Uchunguzi wa Tuhuma.

Hivyo, baada ya Mahakama ya ICC Kupokea malalamiko ya Uhalifu wa Haki za Binadamu kwa njia yoyote kati ya hizo tatu nilizozieleza hapo juu, kinachofuatia ni uchunguzi wa kina wa tuhuma za Uhalifu wa Haki za binadamu. Ikiwa vigezo vyote vya Uchunguzi vimetimizwa, Mwendesha Mashtaka atakusanya ushahidi, atahoji mashahidi mbalimbali wakiwemo waathiriwa wa Matukio ya Uhalifu wa Haki za Binadamu, na kutambua washukiwa wa tuhuma husika. Ikumbukwe, kwa Mujibu wa Sheria, Mwendesha Mashtaka wa ICC, ana wajibu wa kuchunguza kwa Haki bila kupendelea upande wowote, hivyo anawajibu wa kuangalia hali za pande zote mbili za kuwatia hatiani au kuwaondolea hatia kwa usawa ili kuthibitisha Haki.​
HATI YA KUKAMATWA KWA WASHUKIWA;
Kulingana na ushahidi wa Uhalifu wa Haki za Binadamu uliokusanywa, Mahakama ya ICC Kupitia Mwendesha Mashtaka wa ICC kwa hatua ya awali, atawajibika kutoa Hati ya kukamatwa kwa Washukiwa wa Uhalifu wa Haki za Binadamu. Hivyo Washukiwa wanaweza kufika Mahakamani kwa hiari yao au kwa shuruti, Ikumbukwe kuwa, ICC inategemea Mataifa kukamata na kuletwa kwa washukiwa kama washukiwa hawatatii wito kwa hiari yao.​
Hatua ya Kabla ya Kesi (Pre-Trial Stage)

Baada ya Washukiwa wa Uhalifu wa Haki za Binadamu kukamatwa au kujitokeza kwa hiari mbele ya Mahakamani ICC, kesi inaanza kwa hatua ya awali ambapo: Mshukiwa wa Uhalifu anafika mbele ya majaji watatu(3), ambao wanathibitisha utambulisho wao na kuhakikisha wanaelewa mashtaka na haki zao kama ambavyo Mahakama nyingi duniani ikiwemo nchini Tanzania hufanya.

Baada ya hapo, Uthibitisho wa Usikilizaji wa Mashtaka unafuatiwa ambapo; Mwendesha Mashtaka anawasilisha ushahidi unaounga mkono kila shtaka dhidi ya washukiwa. Ikumbukwe pia kwamba, Wawakilishi wa kisheria (Mawakili) wa waathiriwa wanaweza pia kushiriki katika Mahakama hii kuwakilisha Maslahi ya wateja wao. Kisha majaji watatu wataamua ikiwa kuna ushahidi wa kujitosheleza kupeleka kesi kwa hatua inayofuata.
KUSIKILIZWA KWA KESI YA MSINGI
Ikiwa Majaji wameamuru Ushahidi umejitosheleza na kesi kuendelea kwa hatua inayofuata, na mashtaka yamethibitishwa na Majaji kwa hatua ya awali, Kesi itaanza Kusikilizwa mbele ya majaji watatu na mbele ya washitakiwa. Ikimbukwe Mashauri ya aina hii hufanyika hadharani ili Haki ionekane inatendeka. Upande wa Mashtaka lazima uthibitishe hatia ya mshtakiwa bila shaka yoyote. Pande zote mbili, Yaani, Upande wa Mashtaka na upande wa Utetezi (Washitakiwa) unawasilisha ushahidi na kuwachunguza mashahidi kwa Mujibu wa Sheria.
HUKUMU YA MAHAKAMA YA ICC
Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Majaji hutoa hukumu au uamuzi wa kutiwa hatiani au kuachiliwa kwa Washitakiwa. Iwapo Washitakiwa watapatikana na hatia, Mahakama ya ICC inatoa hukumu kwa Mujibu wa Sheria, ambayo ni kifungo cha hadi miaka 30 jela au kifungo cha maisha. Mahakama pia inaweza kuagiza fidia kwa waathiriwa na ndio umuhimu kwa waathiriwa kuwa na Mawakili watao wasilisha maslahi yao Mbele ya Mahakama ya ICC .
RUFAA DHIDI YA MAAMUZI YA ICC
Katika Muundo wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Kuna hatua ya awali na hatua ya rufaa kama mmoja wapo hajaridhishwa na maamuzi ya awali ya Mahakama ya ICC, Washukiwa kupitia Mawakili wao na Mwendesha Mashtaka wana haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu kwenye hatua ya Rufaa ya Mahakama ya ICC. Ikumbukwe kwamba; Utekelezaji wa hukumu unategemea ushirikiano wa Nchi Wanachama, kwani ICC haina vituo vyake vya magereza.lang=SW style='font-family:"Century Gothic",sans-serif;mso-bidi-font-family:

HITIMISHO
Watanzania, tunapaswa kujua kwamba tuna deni kubwa la DAMU ZA WATU, katika kuirudisha nchi yetu teule kwenye misingi, Kutokama na Damu na Maafa ya Ndugu na Jamaa zetu, Hakika tuunawajibu wa kihistoria, ni wajibu shurutishi kwetu na ni lazima tuutekeleze ili FIMBO YA MUNGU ISITUCHAPE, bila kufunika Kombe, Mwanaharamu apite.

Tunawajibu wa kuchukua hatua kali za kihistoria kwa Mujibu wa Sheria ili Kutetea Haki za Ndugu na Jamaa zetu waliouwawa kikatili, Waliotekwa na waliopotezwa bila kosa lolote linalostahili walivyotendewa. Naamini Nchi yetu itarudi katika Misingi ya HAKI iletayo AMANI ya kudumu.

Mahakama ya ICC inafanya kazi kwa mujibu sheria Kushughulikia Uhalifu wa Haki za Binadamu unaofanywa na Serikali yoyote ile pale ambapo Mifumo ya Mahakama ya kitaifa haitaki au haiwezi kuchunguza au kushtaki uhalifu huo kwa dhati kama ilivyo nchini Tanzania.​

ALPHONCE LUSAKO

WAKILI

alusako@protonmail.com
 
Attachments

Hongera pongezi kudadavua vizurikwa maslahi ta Taifa na wapenda Haki
 
Nitoa ufafanuzi kuhusu Utaratibu wa kufungua kesi ya jinai katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), kama sehemu ya kutoa elimu na vilevile kuendelea kutoa wito kwa Watanzania wote ambao huenda wameathirika wa uhalifu wa haki za binadamu bado hawatoi Ushirikiano wa taarifa kwa kuwa hawajui athari zake. Kimsingi taarifa zenye Ushahidi ndio nyenzo wezeshi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ili kuwaweka Wshukiwa hatiani na kupigania HAKI YA KUISHI ambayo ipo hatarini Tanzania.
Shirika la Intelwatch la Afrika Kusini limewasilisha mashtaka mahakama ya ICC

, kuitaka mahakama hiyo kuchunguza madai mazito ya mauaji, utekaji na utesaji wakati wa maandamano ya tarehe 29 Oktoba 2025.

Pia imeitaka Mahakama hiyo kutoa hati za kukamatwa kwa Rais.

Shirika la Intelwatch la Afrika Kusini limewasilisha mashtaka mahakama ya ICC​

Mamlaka ya ICC​

Madai mazito katika faili nene la Samia Hassan lililofikishwa katika dawati la ICC the Hague Uholanzi, linasema ICC ina mamlaka katika kesi hii kwa sababu Tanzania ni mwanachama. ICC inaweza tu kushtaki kesi ambapo mahakama za kitaifa zimethibitisha kutokuwa tayari au haziwezi kufanya hivyo.

Jalada hilo linasema mahakama za Tanzania zimethibitisha kuwa haziko tayari au haziwezi kushtaki makosa haya yanayodaiwa kwa sababu zimeanzisha "uchunguzi sifuri" wa uhalifu wowote mkubwa ulioandikwa kwenye jalada na zimewazawadia uhuru badala ya kuwaadhibu wahusika rasmi wa uhalifu huu.

Na mashtaka yanaongeza kuwa Mkataba wa Roma wa ICC unamruhusu Samia Hassan na maafisa wake wakuu - ikiwa ni pamoja na jeshi, polisi na wakuu wa kijasusi - kushtakiwa kwa uhalifu huu dhidi ya ubinadamu chini ya kanuni ya ICC ya "wajibu wa amri" ya maafisa wakuu kwa hatua za vikosi vilivyo chini ya udhibiti wao wa moja kwa moja.

Inasema mauaji katika kipindi cha baada ya uchaguzi wa Oktoba 30 hadi 6 Novemba 2025 "yalitekelezwa kwa mujibu wa amri kutoka ngazi za juu za serikali, ikiwa ni pamoja na idhini ya Rais Samia Hassan ya 'kuchukua hatua zote na kuhusisha vyombo vyote vya usalama'". Ripoti hiyo inaongeza kuwa kiwango kikubwa cha mauaji hayo pia kilijumuisha uhalifu wa kuangamiza ICC.

"Huu haukuwa udhibiti wa msongamano ambao ulisababisha vifo kwa bahati mbaya; ilikuwa mauaji ya kukusudia." Ushahidi wa picha unaonyesha kuwa vikosi vya usalama vilifyatua risasi bila tahadhari, zikilenga vifua na vichwa na kuendelea kufyatua risasi hata waandamanaji walipokimbia

Mauaji yaliyolengwa​

Ripoti hiyo pia inamtuhumu Samia Hassan na serikali yake kwa mauaji kadhaa ya viongozi wa upinzani kabla ya uchaguzi, akiwemo mwanamkakati mwandamizi wa Chadema, Ally Kibao, aliyetekwa nyara kwenye basi jijini Dar es Salaam tarehe 6 Septemba 2024 alipokuwa anaelekea kwao Tanga . Mwili wake uligunduliwa siku iliyofuata msituni karibu na Bahari ya Hindi, uso wake ukichomwa na tindikali.

Na ripoti hiyo inamtuhumu Samia Hassan na maafisa wake wakuu kwa uhalifu wa ICC wa "kutoweka kwa nguvu", ikibainisha kuwa wataalam huru wa Umoja wa Mataifa wameandika zaidi ya kesi 200 za kutoweka kwa nguvu kati ya 2019 na Juni 2025.

Tori-Tanzania-kiongozi-wa-upinzani-akamatwa
Vikosi vya usalama vya Tanzania wakipiga doria baada ya kuzuia mkutano wa upinzani uliopigwa marufuku kufanyika Dar es Salaam tarehe 23 Septemba 2024. (Picha: EPA-EFE / Anthony Siame)

Hawa ni pamoja na: Humphrey Herson Polepole, balozi wa zamani wa Tanzania nchini Cuba na baadaye mkosoaji mkubwa wa serikali, alitekwa nyara nyumbani kwake tarehe 6 Oktoba 2025, wiki tatu tu kabla ya uchaguzi, na hajaonekana tangu wakati huo; angalau wanachama 50 wa vuguvugu la Shehe wa Uamsho walitekwa nyara mwaka 2013 na kushikiliwa kwa kulazimishwa kutoweka kwa miaka minane kabla ya mashtaka kuondolewa Juni 2021.

Soma zaidi: Ikiwa Watanzania 10,000 kweli wamekufa, kutojali kimataifa si chaguo

Ripoti hiyo inaongeza kuwa watu wengi walikamatwa na vikosi vya usalama na kisha kutoweka katika kipindi cha uchaguzi wa 2025.

Na inasema "mateso yanatumiwa kwa utaratibu na vikosi vya usalama vya Tanzania" dhidi ya wapinzani wa kisiasa.

Inataja kesi za Boniface Mwangi , mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu nchini Kenya, na Agather Atuhaire, wakili na mwandishi wa habari kutoka Uganda, waliosafiri hadi Tanzania tarehe 19 Mei 2025 kuangalia kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa CHADEMA , Tundu Lissu. Walikamatwa pamoja siku hiyo hiyo.

Wote wawili walivuliwa nguo na kupigwa kikatili. Atuhaire pia alishambuliwa kingono. Ripoti hiyo inabainisha: “Ukatili wa kijinsia umetumiwa kwa utaratibu wa kawaida wa vyombo vya usalama kama silaha ya ukandamizaji nchini Tanzania.”

Shutuma dhidi ya Samia Hassan na maafisa wake pia ni pamoja na mateso yao kwa jamii za Wamasai kaskazini mwa Tanzania, "kwa misingi ya kikabila na kitamaduni". Inasema serikali "imekiuka kwa utaratibu haki za Wamasai kwa ardhi ya mababu zao, maisha ya kitamaduni, na mila za kitamaduni kupitia kufukuzwa kwa lazima, ghasia, na kunyimwa ushiriki wa kisiasa".

Inaongeza kuwa kufukuzwa kwa Juni 2022 huko Loliondo kulikuwa na "kinyama hasa".

Kuzimwa kwa mtandao​

Katika shtaka la ICC, ripoti hii pia inataja kuzima kwa mtandao - kuanzia tarehe 29 Oktoba 2025 hadi 4 Novemba 2025 - kama uhalifu dhidi ya ubinadamu, hasa kwa sababu inasema kukatika kwa umeme "kuliwezesha kutendeka kwa uhalifu mwingine dhidi ya ubinadamu ikiwa ni pamoja na mauaji, mateso, na kutoweka kwa nguvu".

Pia ilizuia raia kutafuta matibabu kwa wale waliojeruhiwa na vikosi vya usalama. Na ilikiuka kifungu cha 7(1)(k) cha Mkataba wa Roma wa ICC, ambacho kinakataza kwa makusudi “mateso makubwa, au majeraha makubwa kwa… afya ya akili…” kwa sababu kiliwazuia Watanzania wengi kujua iwapo wapendwa wao waliuawa au kujeruhiwa katika maandamano hayo.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa kifungu cha 7(1) cha sheria hiyo kinafafanua uhalifu dhidi ya ubinadamu kama mojawapo ya vitendo 11 vilivyoorodheshwa - ikiwa ni pamoja na mauaji, ukatili, utesaji, ubakaji na utekaji nyara - "wakati unafanywa kama sehemu ya shambulio lililoenea au la kimfumo dhidi ya raia yeyote, na ujuzi wa shambulio hilo".

Inasema kuwa uhalifu inaodai ulienea kwani mashambulizi ya vikosi vya usalama yaliathiri baadhi ya mikoa ya Tanzania na maelfu ya wahanga. Hali ya utaratibu wa mashambulizi hayo ilidhihirishwa na kupelekwa kwa vikosi vya usalama kwa wakati mmoja katika maeneo kadhaa, kuunganishwa kwa mtandao kwa uratibu, mauaji ya watu wengi yaliyoratibiwa katika miji kadhaa kwa wakati mmoja, utupaji wa miili na kukamatwa kwa watu wengi na uratibu wa vikosi maalum washirika kadhaa yaliyohusika katika shambulio hilo.

Na ripoti hiyo inasema Mkataba wa Roma pia unahitaji kwamba shambulio liwe "kulingana na au kuendeleza sera ya vyombo vya dola au idara za vikosi maalum " ili kufanya shambulio hilo. "Sera hiyo haihitaji kuandikwa rasmi lakini inaweza kuzingatiwa kutoka kwa jumla ya mazingira."

Inaweza kuzingatiwa kuwa mashambulio hayo yalikuwa uamuzi wa kisera kwa sababu Samia Hassan aliidhinisha shambulio hilo waziwazi na taarifa yake kwa umma mnamo tarehe 1 Novemba 2025, kama alivyoapishwa Dodoma ndani ya kambi ya jeshi , kwamba "tutachukua hatua zote na kuhusisha vyombo vyote vya usalama" ili kukandamiza maandamano

Sera hiyo pia inaweza kuzingatiwa kutokana na upandishaji vyeo wa maafisa wanaohusika na ukatili na ugawaji wa rasilimali nyingi za serikali kwa shambulio hilo, ikijumuisha kupelekwa kwa vitengo vya jeshi na magari ya kivita katika mikoa kadhaa, kuzima kwa mtandao kwa kudumu kunahitaji uratibu na kampuni za mawasiliano, uendeshaji wa vituo vya kizuizini vya siri, shughuli za utupaji wa miili.

Ripoti hiyo pia inawafungulia mashtaka mkurugenzi wa Usalama wa taifa TISS, kamanda wa polisi wa Dar es Salaam, mkuu wa jeshi la ulinzi CDF JWTZ na inspekta jenerali wa polisi IGP kwa kuhusika na mashambulizi dhidi ya waandamanaji.

Pia inamtaja mkuu wa Tume ya Uchaguzi INEC kwa "kuwezesha udanganyifu wa uchaguzi". Inamtaja jaji kwa "kuwezesha mashtaka ya kisiasa", ikiwa ni pamoja na kuwa mhusika katika mashtaka ya uhaini ya Lissu.

Inamfungulia mashtaka waziri wa habari kwa kuzima mtandao pamoja na makamanda kadhaa wa kikosi cha usalama cha kanda maalum.

Hati hiyo, iliyoonwa na Daily Maverick DM, inamtaja Samia Hassan tu kwa jina. Kwa sababu za kisheria, majina ya maafisa wake yanarekebishwa, ingawa yanaweza kuhesabiwa kutoka kwa ofisi zao.

Waandishi wa hati hiyo wanaomba ICC kufungua uchunguzi wa awali na kufuatilia uchunguzi na mashtaka kwa haraka, kwani kucheleweshwa kutaruhusu uhalifu kuendelea, ushahidi kuharibiwa na mashahidi kunyamazishwa.

DM
 
Back
Top Bottom