saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,173
- 6,156
Mh. Rais wangu Dr. Samia Suluhu Hassan barabara tajwa hapo juu ni muhimu sana. Imarisha bandari ya Tanga, mikoa ya kanda za Kaskazini, kanda ya ziwa na nchi jirani za Burundi Rwanda na Uganda watachukulia mafuta bandari ya Tanga, Dsm ni mbali na kuna msongamano mkubwa. Pili barabara ya njia 4 ifike angalau KIA kutoka Tengeru(Arusha). Rais wangu utaona mabadiliko makubwa sana. Jengeni hata kwa utaratibu wa EPC plus Finance, hiyo barabara ni ya kiuchumi italipa sana.