IGP Sirro tafakari sana maneno ya mtu aliewaua Polisi aliposikika akisema "Nawatafuta Polisi"

Nitakuwa wa mwisho kuamini huyo dogo ni gaidi.
Kuna kitu walimfanyia. Na ninahisi walimu_underestimate kutokana na muonekano wake, hawaukujua kama atakuwa ni imara kiasi hicho.
RIEP

mtu yeyote mwenye silaha ni imara.
 
Umesikia Polisi walimnyanganya dhahabu waliyomkuta nayo katika harakati za kuuza, na jamaa ni mchimba dhahabu huko Chunya? Sasa hao ni walinzi wa mali zetu kweli? Unakumbuka wale jamaa waliuwawa Sizna na wakiwa na madini na kusingiziwa walikuwa majambazi? Polisi walimuua hata taxi driver ambae wala hakujua kinachoemdelea wao kupoteza ushahidi

Kama hawa Polisi wangejua ugumu wa kupata dhahabu kwenye machimbo Chunya, wasingethubutu kumnyanganya. Najua jamaa alikuwa anauza dhahabu kimagendo, lakini hiyo sio excuse kwa Polisi kumnyanganya ili iwanufaishe wao. Kwa hiyo kama hilo ndilo walilofanya ni good riddance kwa Polisi waovu walioko katika jeshi. Na kama kuna Polisi kjauwawa hakuhusika, basi wenzake ndio wa kulaumiwa, sio huyu mtu aliewaua

Chief, umeshasema jamaa alikuwa anauza dhahabu kimagendo kifupi sio raia mwema, kama ilivyo kwa raia wapo wema na wapo wasio wema...hata polisi wapo wema na wasio wema....yeye hakuwa raia mwema kakutana na polisi ambao nao sio polisi wema kwenye dili zao chafu huko mitaani wamedhurumiana....

ndio maana huko juu nikakwambia hii ni shida ya duniani kote, polisi wa namna hii wapo ambao kazi yao ni kupiga deal za magendo na wauza magendo hii ni duniani kote sio Tanzania tu...
tukiongea kiuhalisia, dhahabu ina taratibu zake za kuuza na kusafirisha ukienda tofauti na hizo maana yake uko tayari kupambana na risk zote huko kwenye black market....

haya sasa wameshadhurumiana na wapiga dili wenzie, katoka huko na chuki zake na hasirs zake kavamia askari lindo kawashoot kachukua silaha anataka kushambulia askari walio kazini na kuleta taharuki 'UNATAKA AACHWE ASICHUKULIWE HATUA?.....kama issue ni kulipa kisasi angemalizana na hao waliomdhurumu kwenye dili zao huko...

TUITHAMINI NA KUSHUKURU HATA HIKI KIDOGO AMBACHO POLISI WETU WANAKIFANYA KUTULINDA NA KUILINDA NCHI..
 
Nimesema mara nyingi sana humu JF, kwamba namna ya utendaji wa Polisi wa Tanzania ni ile ambayo inazalisha chuki na wananchi badala ya kukuza uhusiano mzuri. Watu wengi sana wana chuki na Polisi kutokana na vitendo vyao, iwe suala la rushwa, kubambikiwa kesi, matumizi ya nguvi isivyostahili, upendeleo kwa chama tawala nk.

Je umewahi kushuhudia ndugu yako, mtu wa karibu, akipigwa, akikamatwa bila kosa, akinyanyaswa na Polisi? Ulipata hisia gani dhidi ya Polisi? Polisi wametengeneza tabaka la Watanzania ambao hata kama huyu jamaa angesikika akisema kesho naenda kuua Polisi, wasingetoa taarifa kwa Polisi!

Polisi wanajisahau sana na kuwa na utendaji unaowatukuza watawala na kuwakandamiza au kuwapuuza raia, na hili linasababisha watu wengi kuwachukia Polisi. Kuna nchi ambazo raia huwaona Polisi kama rafiki lakini sio Tanzania. Polisi mngejenga uhusiano mzuri na raia, msingehitaji kuahidi zawadi kwa atakaetoa taarifa juu ya huyu mtu, watu wangejitokeza bila hata ahadi ya zawadi.

Kuna wakati hata niliuliza kwamba, hivi kuna mtu yeyote alie upande wa vyama vya upinzani ambae anawaona Polisi kama marafiki? Na nikasema, Polisi hawaoni kwamba ni tatizo kubwa kuwa na idadi kama hiyo inayowachukia?

Naamini kwa dhati kabisa tukio lililotokea la mauaji ya Polisi limetokana na hasira na chuki dhidi ya Polisi kwa mambo fulani waliyomfanyia huyu mtu (inasemekana walimdhurumu dhahabu waliyomkuta nayo) au hata ndugu yake. Ikafikia mahali huyu mtu ali "snap", akapata uenda wazimu wa ghafla (temporary insanity) na kuamua kutafuta Polisi ili awaue.

Sasa hili ni jambo Polisi hawapaswi kulichukulia upande mmoja, kwamba Polisi wenzao wameuwawa, bali wajiulize kwa makini sana kwa nini wameuwawa, na kama linaweza kujirudia. Sintashangaa kama huko nje kuna watu wenye hasira pia dhidi ya Polisi ambao wanaona huyu mtu kafanya kitendo cha ujasiri, na wao pia kwa hasira waliyonayo dhidi ya Polisi wakaona hata wao wanaweza!
Well said, na polisi imefika muda muafaka kubadilika, narudia, wale wanaolichafuwa jeshi la polisi tafadhali mbadilike..
 
Well said, na polisi imefika muda muafaka kubadilika, narudia, wale wanaolichafuwa jeshi la polisi tafadhali mbadilike..
Huu ndio mchezo wao
IMG-20210826-WA0005.jpg


Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Yupo Selander.

Anawatafuta polisi.

Badala ya kugeuka kuwafuata Oysterbay ambapo wapo wengi.

Anaenda kituo cha Selander?
 
Polisi ni walinzi wa Raia na Mali zao. Mengine ni changamoto ndogo ndogo kwenye maeneo yao ya utendaji.
Changamoto ndogo ndogo unazizungumzia vitu gani wewe!?

Yani mtu ambaye anakulazimisha umpe rushwa kwa kukusingizia kosa sababu tu ana kimashine cha kufyatulia invoice unaita hio changamoto ndogo ndogo? Hivi unaujua uchungu wa kusingiziwa kitu kisicho haki wewe?
 
tusipende sana kila jambo tunashutumu Polisi, hebu tujaribu kuwa na shukrani hata kwa kile kidogo wanachofanya...hivi hamuoni wanavyotulinda mitaani huku na kutatua changamoto za kila siku mtaani huku, hivi hatuoni hawa traffic police wanavyotusaidia huku mabarabarani pamoja na ujira mdogo wanaolipwa?... hakuna kazi isiyo na changamoto duniani hapa na hakuna police walio perfect dunia pote hapa tuache lawama....

Hivi hatujaona ile effort ya wale askari waliojitolea kuzikwepa risasi na kuleta amani pahala pale?.....kwa hiyo wangemuacha tu yule jamaa na bunduki zake anapiga marisasi na kuleta taharuki huku kazi zimesimama nk..
Polisi kulinda ni jukumu lao wala hatuna haja ya kushukuru sababu wanatekeleza kile ambacho wanalipwa kukifanya! Kulisha familia yako ni jukumu lako wala hustahili pongezi kwa hilo its your duty!

Ila inapotokea unahujumu wananchi thats a sin regardless unafanya majukumu yako pia ila ni dhambi kubambikia watu makosa ama kuwaweka watu ndani kwa interest zako! Upuuzi mkubwa sana!
 
wapi duniani kuna uhusiano mzuri wa jeshi la polisi na raia?
Idi amini tulimpiga kwa kuwa alikuwa na mahusiano mabaya na raia wake,so tulipata ushirikiano mkubwa toka kwa wananchi wake wenyewe,mahusiano mazuri ndo mpango mzima,
 
Ninaamini kwa dhati kabisa, kwamba kama huyu mtuhumiwa wa mauaji ya Polisi angekuwa hapa amevaa nguo ya Chadema na sio ya CCM, IGP Siro saa hizi angekuwa anafanya sherehe na kusahau kwamba kuna Polisi wake watatu wameuwawa, na hata angekuwa anafikiria kuipeleka hiyo picha mahakamani ikatumike kama ushahidi katika kesi ya ugaidi dhidi ya Mbowe

View attachment 1908213
Kwa kuongezea afande zirro ageenda na hiyo picha mahakamani na kudai gaidi kabla ya kuzidiwa nguvu na kuuawa na jeshi la polisi alikuwa akitamka maneno kuwa ametumwa na mbowe
 
kwahiyo Tanzania polisi wanabifu na raia huku mitaani.....mbona mara nyingi tu napishana nao usiku wakiwa kwenye doria zao barabarani sioni wakifyatulia raia risasi, mbona huko kwenye mabaa usiku watu wanakula ulabu sioni wakifyatua risasi....mbona hapo posta na kariakoo mchana sioni wakikamata watu hovyo?...

Bro naomba nikwambie, dunia kote polisi hawapendwi maana raia duniani kote tunapenda kuvunja sheria tuachwe tu.... duniani kote pia kuna polisi wabaya na wazuri pia..
Acha uonge hapa zambia tunawapenda sana polisi!!! Hawspendelei chama tawala!!
 
Copy and Paste

[8/25, 7:31 PM] First Born: Alikua anaenda kumuhuzia mtu dhahabu maeneo ya masaki police wakamkamata so wakat wanaenda kituo salander
[8/25, 7:31 PM] First Born: Polisi ndio chanzo aise walitaka kumzulumu
[8/25, 7:31 PM] First Born: Wakaingia chobingo hili wamalizane police wakaleta tamaa yenye akawawahi na sirahara yake ndogo
[8/25, 7:31 PM] First Born: Huyo dogo anamigodi ya dhahabu kule chunya aliachiwa na baba yake
[8/25, 7:31 PM] First Born: Huyu dogo nakaa nae mtaa mmoja police ndio wamemzungua madini yake
[8/25, 7:31 PM] First Born: Jana usiku tulikua nae mtaa I aise police ndio wameleta tamaa zao tu
[8/25, 7:31 PM] First Born: No dogo mmoja cool sana
[8/25, 7:31 PM] First Born: Baada ya hapo akachukua hizo 47 ndio kuuza kupiga hivyo huku akisema anataka police
[8/25, 7:31 PM] First Born: Ata cc tunashangaa sana kutokea hivyo
[8/25, 7:31 PM] First Born: Huyo dogo sio jambazi kabisa yani
[8/25, 7:31 PM] First Born: Inasikitisha sana... Kumbe polisi ndio walisababisha hii shida yote... Uchunguzi wa kina na wauwazi utaitajika...
...Dah! Inafikirisha na kuumiza sana!
 
Naomba kuuliza,hivi uwiano wa polisi na raia uko vp,yaan polisi anauwezo wa kudhibiti raia wangapi
 
Back
Top Bottom