IGP Sirro: Nitachukua hatua ndani ya siku tatu kutekwa kwa MO Dewji

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro amesema ndani ya siku tatu atachukua hatua kuhusiana na tukio la kutekwa kwa Mo Dewji, ametoa kauli baada ya Rais Magufuli kusema tukio hilo limeacha maswali mengi kwa wananchi yanayohitaji majibu.


======

Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema atachukua hatua ndani ya siku tatu au nne kuhusu kilichosemwa na Rais John Magufuli juu ya jeshi hilo.

Sirro ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku tatu tangu Rais Magufuli alipohoji ukimya wa jeshi hilo katika baadhi ya matukio yanayopaswa kushughulikiwa na jeshi hilo likiwamo la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji.

Katika hotuba yake fupi baada ya kuwaapisha mawaziri wawili waliobadilishana wizara, Rais alitoa mfano wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kukaa kimya kuhusu sakata la kutekwa kwa mfanyabiashara huyo na matukio mengine.

Rais Magufuli alisema tukio hilo limeacha maswali mengi kwa wananchi yanayohitaji majibu akisisitiza kuwa Watanzania si wajinga.

Katika mahojiano na Mwananchi juzi, ambalo lilitaka kujua hatua gani atakazichukua baada ya kauli ya Rais, Sirro alisema ndani ya siku tatu au nne zijazo ataweka hadharani hatua zitakazochukuliwa kuhusu suala hilo.

Alipoulizwa ni hatua gani zitachukuliwa, mkuu huyo wa polisi alisema: “Siwezi kuzitaja kwa sasa kwa sababu bado tupo kwenye uchunguzi, tutazieleza baada ya siku hizo nilizokuambia.”

Jumatatu wiki hii, Rais Magufuli akiwaapisha Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Dk Augustine Mahiga kuongoza Wizara ya Katiba na Sheria, alihoji ukimya wa polisi unavyoacha maswali katika baadhi ya matukio.

Rais Magufuli alilizungumzia tukio la Mo ambaye alitekwa saa 11 asubuhi ya Oktoba 11, mwaka jana katika Hotel ya Collesum iliyopo Barabara ya Haile Selassie, Oysterbay jijini Dar es Salaam ambako bilionea huyo kijana Afrika alikwenda kufanya mazoezi.

Dewji, ambaye pia ni mwekezaji wa klabu ya Simba alipatikana Oktoba 20 baada ya kutelekezwa kando ya eneo la Gymkhana jijini hapa.

“Mtu aliyetekwa alikutwa Gymkhana usiku, lakini watu wanajiuliza mmh aliendaje pale. Lakini alipowekwa pale na bunduki zikaachwa pale, unajiuliza huyu mtekaji aliamua kuziacha je angekutana na polisi wanaomtafuta njiani?” alihoji Rais Magufuli.

Alisema baada ya Mo kupatikana, siku hiyo asubuhi Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alionekana “akinywa chai” na mfanyabiashara huyo.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro amesema ndani ya siku tatu atachukua hatua kuhusiana na tukio la kutekwa kwa Mo Dewji, ametoa kauli baada ya Rais Magufuli kusema tukio hilo limeacha maswali mengi kwa wananchi yanayohitaji majibu.

Mpaka maagizo kutoka juu yatoke ndiyo achukue hatua, siku tatu zinaagukia jumapili kwa hiyo wataanza kuwakamata makanisani kama yule mkurugenzi wa manyoni
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro amesema ndani ya siku tatu atachukua hatua kuhusiana na tukio la kutekwa kwa Mo Dewji, ametoa kauli baada ya Rais Magufuli kusema tukio hilo limeacha maswali mengi kwa wananchi yanayohitaji majibu.
kwa hyo alikua anasubiri mpaka ambiwe na jiwe
 
Bado amepwaya siku tatu zote za nini hizo hatua zilipaswa kuchukuliwa toka kauli ya kutowafanya wajinga watanzania ilipotolewa
 
Back
Top Bottom