Ifike muda habari za vibustani vikomeshwe...

Ifike muda habari za vibustani vikomeshwe...

Hivi karibuni kwa aliyepima, kituo chochote, aliambiwa kupima ni mara moja kwa mwaka sahizi?si tena ile kila baada ya miezi mitatu @?

Haya turudi penyewe leo,Habari mabibi na mabwana na wadogo zangu nawe miss neddy na Excel mzee mapicha ndhani leo utanisaidia kunibandikia pics.

Nashangazwa sana na wanawake wantembea na waume za watu, Hivi hujawahi kufikiria future yako itakuwaje mbeleni?

Unaenda kwa mume wa mtu tena anandoa yake ya kanisani hapo, unajiaminisha"Ananipenda kweli habari za mke wake zte ananiambia,nimemshikaa unyayo kwangu hatoki" Shame on you,kwako hatoki mbona kwa Mkewe anarudi kwenda kulala wewe unakaa unajipa matumaini eti ananitunza,mjinga wewe unapoteaaa,utabaki kuwa gumegume hivyohivyo,ukikaa sawa unajidai nataka mume,mume wa mtu kakutumia hadi umekwisha habari yako,

Wananishangaza wale ambao anakuwa na mtu na yule mwanaume anamchumba labda,mpaka anaa mwingine we upo tu,Hivi kama kweli huyo mwanaume anakupenda sana kwanini asikuoe wewe hujawahi kujiuliza?

Na nyie wanaume, Yaani unaterekeza familia kisa mwanamke wa nje,hivi hamjuagi kitendo cha kuwa na mwanamke nje ni mwanzo wa matatizo?

Most of vibustani are MONSTERS utaendewa kwa waganga na kulishwa visivyolishwa na umalaya wako,mtu unakuta anamke mzuri ndani linaenda kubeba gubegube limepaka mishedo kama punda wa india,Jamani unachokosa kwa mkeo si uongezee ili upate vyote..

Ngoja niwape stori moja ya kweli kabisaa........Kulikuwa na mwanamke 1 alikuwa anakazi ya kutembea na wanaume za watu,ikafika hatua akapata tajiri mmoja wa maana,akaamua kwenda kwa mganga wa kienyeji,mganga akampa "shanga" na kikopo kidogo cha dawa,Ile shanga ilikuwa inakazi ya kuvutia wanaume,kwamba atakaye kuwa anamwona tu akamtamani basi amsogelee mwenyewe,na ukilala nae umekisha hadi familia utasahau kabisa,kwahiyo akawa anadate na vibopa hatari,akimwambia anataka nyumba watu wanaachia majumba,nk,Alikuwa akifika Period(mwezini) alikuwa anakinga damu kwenye kichupa anaiweka kwenye frij,siku mpendwa wangu@Excel ukiwa unahitajika uachie sheli unayomiliki atakupikia msosi akichanganya na ile damu ya hedhi,( MPO HAPO MAPAPA?)

Yule dada akaja kuwa Tajiri wa ajabu sanaaa ila ndoa kibaaooo zilivunjika,.......Ni habari ndefu,atakayetaka atanitafuta.

Sasa hebu jiulizeni nyie wanandoa mipapa umelishwa vingapi?

Na nyie wadada wa sahizi kutwa kwa waganga kisa watoto wa wenzenu kama mali ni rahisi kwanini msitafute vyenu,Mungu naye anaona huruma kwa viumbe wake ndo maana mnakuta yanabuma....

Nimekuja tu kutoa somo leo wala si ugomvi tena, Mwanangu Trina anawasalimu maankoz na antiz,babuz na babaz




Mimi huwa sili msosi kwa mchepuko naogopa kulishwa damu za hedhi
 
watu wanabadili majina tu,nyumba ndogo,mpango wa kando,kibustani,kidumu,na sasa tuko na mchepuko..hii ni hatari..tabia mbaya zinaanza na tukiwazacho..mawazo yako yasipouona ubaya wa michepuko taratibu matendo yako yatakamilisha..hata ambao tulidhani ni mfano kwetu nao wanaanguka kila siku


msingi wa imani ndo njia pekee iliyobaki..Mungu atusaidie sana
 
Nilichogundua kuna watu wanashabikia uzinzi na michepuko

Hofu ya Mungu haipo
Kwann uendekeze michepuko badala ya kulinda ndoa yako?
Mlipokosea mrekebishane?
Mnajidanganya hela na mda mnaopoteza kwa micheuko ungewasaidia kwenye maendeleo
Na wadada kutegemea mume wa mtu ni kutokujitambua hujui mwenzio kafight vipi had hapo walipo
Ukiona vyaelea jua vimeundwa
Urahisi ndo unatuletea laana kwa vizazi vyetu.

İnfidelity is inevitable. Period!!
 
kizazi kijacho sijui kitakuaje..kama mabadiliko hayatoanza na sisi
Inasikitisha sana..!!
..maadili yameporomoka, si kwa vijana na watoto tu hata watu wazima na kaya zao hawana maadili tena..!!
..mwisho wa siku lazima jamii ikumbushwe, tumepoteza yake tuliyofundishwa, hivyo hata watoto wetu hawajui kitu tena..!!
 
Jesus Christ...!!! Sielewi kinachoendelea baada ya hapa.....NIMEZIMIA..

ukizinduka ujiunge nami kumsaka anayehack account yangu kila tunapokuwa tunajiandaa kupata mtoto.
 
Back
Top Bottom