Ifahamu Nanga ya Meli (Ship Anchor)

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,944
12,506
Nanga ni kifaa kilichotengenezwa Kwa ajili ya kuzuia Meli isipelekwe na upepo au mawimbi pale itapokuwa imesimama endapo imemaliza safari, marekebisho au maegesho kwenye maji. Nanga ilianza kutumika tangu karne za Zamani ambapo Wagiriki walikuwa wakitumia vikapu vya mawe kama nanga walipokuwa katika Pwani.

images.png

Nanga hutengenezwa Kwa material ya Chuma,Cast na nanga za vyombo vidogo baadhi hutumia aluminum.Nanga wengi tumezoea kuiona ikiwa Juu ya Meli au ikining'inia pembeni ya Boti au Meli na wengine utengeneza urembo wenye kufanana na nanga ambao huvaliwa kama pambo.

Nanga zimewekwa makundi mawili nanga za kudumu (Permanent Anchor) na Nanga za Musa(Temporary Anchor). Nanga za kudumu hutumika kuzuia meli zinaposhusha Hizi nanga Huwa zimetengenezwa Kwa tofali kubwa za Zege ambalo limewekwa kwenye sakafu ya maji. Nanga za Muda (Temporary Anchor) Hizi ndio nanga ambazo meli hutembea nazo Kwa ajili ya kuweka wafikapo eneo la nangani au kwenye tahadhari.

images (4).jpeg

Nanga inajumuisha kamba/mnyororo ambao hushikilia nanga, nanga yenyewe na kwenye Meli Kuna sehemu ya mnyororo kupita (Hawse pipe),mashine ya kushusha na kupandishia, sehemu ya kutunzia nyororo(chain rocker). Mnyororo wa nanga Huwa na kipimo Cha urefu wa 1(Shackle) Shekeli Moja ambayo sawa na 15fathom kipimo cha waingereza ambacho ni 90feet (27.4mita).
Meli hupewa urefu wa Shackle kulingana na ukubwa ilionao na nanga Huwa mbili na sheria inataka kuwepo nanga Moja ya ziada endapo nanga Moja itapotea au kupata tatizo hii utiliwa mkazo kwenye maeneo Kabla ya kuvuka mifereji mikubwa mfano(Suez Canal,Panama Canal).

Nanga ya Vyombo vidogo
Nanga kwenye vyombo vidogo au Boti uwekwa kulingana na wastani wa nguvu na uzito wa Boti ambapo vyombo kuanzia mita 5 nanga inatakiwa ianzie 3.1 kg na Kwa mita 6 mpaka 10 iwe 4.5kg. Kwenye Boti Ndogo nyororo au Kamba hutumika kushikilia nanga.

Aina za Nanga
1.Stock Anchor

Ni nanga ambayo Juu Huwa na chuma Cha kuzuia baada ya eneo la maungio ya nanga na mnyororo Hizi zilikuwa nanga zilizotumika zamani kwenye vyombo vingi
Stock-anchor-462x478.jpg

2.Stockless Anchor
Hii ni nanga isiyokuwa na chuma Cha kuzuia baada ya sehemu ya maungio ya nanga na nyororo. Kwa Sasa hii utumika kwenye vyombo vingi sababu ya urahisi kwenye kufanya kazi.

Stockless-anchor-462x288.jpg

Sehemu sahihi za kushusha nanga
Nanga ushauriwa kuwekwa sehemu Yenye udongo laini au tope katika sakafu ya maji au Bahari Ili iweze kushika vizuri. Sehemu zenye miamba au mawe nanga haiwezi kushika vizuri na kusababisha Chombo kusogea baada ya kusukumwa na wimbi au upepo.
Kwa maeneo ambayo ni karibu na Bandari hutengwa eneo maalum la meli kuweka Nanga, ambapo eneo hilo huonyeshwa kwenye ramani ya eneo husika (Anchorage Area).Hii husaidia watumiaji vyombo vya majini kujua sehemu salama ya kuangusha nanga na urahisi wa kuinua, pia kusaidia meli kutoweka nanga sehemu ambazo chini kumepita cable za umeme,mikongo ya mtandao au Bomba.
Nanga ni sawa na handbrake kwenye gari.

Namna ya kuangusha nanga
Nanga huwekwa sehemu ambayo inafaa Yenye asili ya sakafu ya tope au udongo laini. Nanga itaangushwa chini taratibu Mpaka itapogota kwenye sakafu Kisha Boti itasogea uelekeo upepo uvumapo Ili nanga ishike vizuri katika sakafu.

images (7).jpeg

Kwa ushauri/utengenezaji na marekebisho ya vifaa vya majini karibuni Spabiton Civil and General Construction Ltd.
Tupo Kigamboni-Vijibweni na Tanga-Mkwaja

images (5).jpeg
 
asante mkuu darasa zuri utotoni tulikuwa tunajisemea tu ooh meli ilitia nanga (tukimaanisha ilipiga kasi nyingi)😄😄
 
mkuu je meli ikiwa inataka kuondoka na na nanga imenasia kwenye tope je huwa inatumika mbinu ipi kuitoa wakati Imeeng'ng'ania chini
kuna mtu maalum wa kupiga mbizi kwenda kuitoa kwenye TOPE au inakuajekuaje
tupe ELIMU
Nanga kwenye meli au boti kubwa inashushwa Kwa Mashine (Anchor Windlass) hii inatumia hydraulic winch motor. Pia mkono (arm) na masikio(flukes) ya nanga hayana nafasi kubwa sana kuzama chini zaidi. Nanga kama kama ina uzito wa Tani 10 basi winch inaweza ikatumika ya uwezo wa Tani 15.Hivyo meli ikiangusha nanga Mfano wa picha hapo chini.
images.png

images (7).jpeg

Inapotoa itabidi irudi kinyume Kisha inyanyue nanga Kwa Mashine na kwenye tope ndani ya maji mnyororo ulala chini umbali wa mita kadhaa hivyo Kwa nguvu ya mashine nanga lazima itoke, changamoto ni kwenye miamba au cable zilizopita chini ya maji.
 
Jeshini 'nanga' ni 'mbumbumbu' hahaha!!

Urefu wa Chain / kamba ya nanga unatosha kukabiriana na variation ya kina cha maji?
Itakuwa wameangalia nanga ilivyo inashushwa na chain na kupandishia na ikikaa sehemu Moja haiwezi kufanya lolote mpaka iamuliwe maamuzi.

Urefu wa chain/Kamba ya nanga ndio unatosha kukabiriana na kina Cha maji Kwenye eneo husika la kuwekea nanga. Kwa Meli kubwa shackle (Shekeli) Moja Sawa na Mita 27.4 nyingi Zina shackle kuanzia 11 hivyo sehemu za karibu na Pwani au Bandari Kwenye eneo la nangani(Anchorage area) itakabiriana vizuri. Deep sea Haiwezekani kutia nanga na ikafanya Kazi Kwa ufanisi Kule utamtumia Kwa dharura kama engine zote hazifanyi Kazi hivyo chombo Ili kisipelekwe ovyo bila uelekeo ukiangusha nanga ule uzito wa nanga utafanya upepo usikutoe eneo la mbali
 
Asante mkuu, kumbe deep sea nanga inaweza kuwa hanged tu bila kufika chini na bado ikazuia meli kusukumwa mbali?
 
Nje ya mada, hivi inakuaje meli kubwa za kubebea magari au ma container mengi hata elfu 8 wakati mwingn hupigwa na mawimbi makubwa sana ILA hayazami kuna utaalam gani hapo?
 
Nje ya mada, hivi inakuaje meli kubwa za kubebea magari au ma container mengi hata elfu 8 wakati mwingn hupigwa na mawimbi makubwa sana ILA hayazami kuna utaalam gani hapo?
Physics ndogo tu hio mkuu ya form 2B. Jinsi ilivotengenezwa ndani mule, a ship is hollow therefore ensures much water displacement. Na vile vile being hollow ina maanisha uzito wa meli unakua mdogo zaidi. Vile vile hewa ndani ya meli ni nyepesi zaidi kuliko ilivo ya bahari
 
Jibu swali kama lilivo ulizwa..🤣
 
Back
Top Bottom