Ifahamu Dodoma

Ifahamu Dodoma

Kwakweli nina kirusi na sijui kiliingiaje akilini na sijui nitakitoaje. Ukinitajia tu dodoma kinachokuja kichwani kwangu kama alama ni Wakoma, Mungu nisamehe.
 
Mkuu Magorofani maarufu kama MAGOROFA YA CDA kuna shida ya maji tangu kitambo. Na nimefanikiwa kufika eneo hilo ambalo kwa sasa Magorofa mengi ni kama Magofu.

Eneo hilo pia lilikuwa na uchafu wa kutosha.
Taarifa hii ni ya muda mrefu. Lini mara ya mwisho ulikuwa Dodoma?
 
Mkuu ulienda kwa shangazi yako au ulitumwa?vp wamekulipa sh.ngap?

Nilikuwa na majukumu mengine tu, ila nilitumia muda wa ziada kufanya uchunguzi wangu binafsi.

As a part of my leasure and pleasure.
 
Naona kama mengine umezidisha chumvi ili uzi unoge...!!
 
Habari zenu ndugu zangu,

Kwa muda wa Majuma kadhaa nipo Dodoma Mjini na nimekuwa nikifanya uchunguzi wangu binafsi.

Katika uchunguzi wangu nimegundua mambo kadha wa kadha.

Hapa nitazungumzia mambo makubwa mawili,

1. Usafi na Mazingira Dodoma Mjini

2. Maeneo hatarishi kwa Mkoa wa Dodoma hasa Dodoma Mjini.

SEHEMU HII YA 1 NITAJIKITA ZAIDI KWENYE SUALA LA USAFI.

Kwa ujumla Dodoma Mjini ni mji mchafu katika maeneo mengi japo baadhi ya maeneo ni masafi

Sababu za uchafu huu ni;
1. Mwamko mdogo wa wananchi juu ya usafi.

2. Uwajibikaji mdogo wa mamlaka zinazohusiana na usafi

MAENEO AMBAYO WANANCHI WANA MWAMKO MDOGO WA USAFI;
a. Hazina

b. Mlezi

c. Kikuyu

d. Majengo

e. Kizota

f. Chang'ombe ya chini

g. Chadulu

h. Maili mbili

j. Bahi road

k. Makulu

l. Makole

Kwa wale mnaohamia Dodoma na wapenda Usafi Epukeni sana maeneo haya.

MAENEO AMBAYO MAMLAKA HAZIWAJIBIKI SAWASAWA KATIKA UKUSANYAJI TAKA,

1. Kwenye madampo karibu yote uchafu umejaa hadi kumwagika chini.

2. Masoko yote (Mfano, Bonanza, Soko Kuu la Majengo na Sabasaba) ni machafu sana. Ukifika kwenye masoko haya utajionea mwenyewe.

3. Kituo kikuu cha Mabasi ya Mkoani na Jamatini kuna uchafu wa kutisha. Kwa wale waliopita Dodoma siku za karibuni watakuwa wameshuhudia hali hii ya Uchafu.

BINAFSI SIAMINI KAMA MAMLAKA HUSIKA ZINAJUA HALI YA USAFI KWA MKOA WA DODOMA.

NB:
SEHEMU YA 2 NITAWALETEA MAENEO MAARUFU KWA UUZAJI WA MADAWA NA VIBAKA.

Nawasilisha.

Unaweza ku - "SUBSCRIBE " Topic hii ili nitakapo andika SEHEMU YA 2 tuweze kuwa pamoja. Nitaleta taarifa hapahapa.
Kwa bahati mbaya zaidi maeneo uliyotaja ni uswahilini sana tena kwenye idadi kubwa ya watu.

Kwa mfano chang,ombe ni mji mkongwe ambao hauna tofauti na kwa mtogole na maeneo mengi ya Temeke n.k

Unaonesha ww ni mgeni sana tu,dodoma ya jana ni tofauti sana na leo yaani sehemu kubwa ya mji ni safi kuliko hizo sehemu chache ambazo hazifiki 10.
Chukulia mfano:
Area A
Area D
Area C
Chamwino
Mipango
Kisasa
Uzunguni
Kikuyu usalama
Kisasa na maeneo yote kuelekea chuo kikuu
Chinangali.
Ila ninachokushangaa umetaja maeneo ya masoko tu ambapo kwa kawaida maeneo hayo huwa na usafi wa kawaida ama hafifu kabisa.
Ila nikupongeze kwa kuleta changamoto kwa watendaji wa mji wa Dodoma huenda watarekebisha na hizo kasoro chache ulizoziona mwisho wa siku utafurahia maisha.
 
Pamoja na hayo bado Dodoma itakuwa jiji na kuiacha Moshi ikiitwa manispaa
Kwenye hilo,serikali ikiamua hata Njombe,Iringa na mji wowote uendelezwe kitaifa,unakua jiji. Kwa hiyo sioni cha kulaumu. Ni kwa sababu Dodoma inawekezwa mambo mengi ili kukidhi takwa la kuwa makao makuu,na siyo fursa za kibiashara ndizo zinazoikuza Dodoma.
 
Kwa bahati mbaya zaidi maeneo uliyotaja ni uswahilini sana tena kwenye idadi kubwa ya watu.

Kwa mfano chang,ombe ni mji mkongwe ambao hauna tofauti na kwa mtogole na maeneo mengi ya Temeke n.k

Unaonesha ww ni mgeni sana tu,dodoma ya jana ni tofauti sana na leo yaani sehemu kubwa ya mji ni safi kuliko hizo sehemu chache ambazo hazifiki 10.
Chukulia mfano:
Area A
Area D
Area C
Chamwino
Mipango
Kisasa
Uzunguni
Kikuyu usalama
Kisasa na maeneo yote kuelekea chuo kikuu
Chinangali.
Ila ninachokushangaa umetaja maeneo ya masoko tu ambapo kwa kawaida maeneo hayo huwa na usafi wa kawaida ama hafifu kabisa.
Ila nikupongeze kwa kuleta changamoto kwa watendaji wa mji wa Dodoma huenda watarekebisha na hizo kasoro chache ulizoziona mwisho wa siku utafurahia maisha.
Mleta mada anatembelea masoko anaakuja kuhitimisha Dom chafu

Eti saba saba chafu kisa kapita stand kule nyuma kwa mtu ambaye hajafika Dom anaweza akaamini Saba saba yote chafu

Na hata huko alipopataja ukiachwa uswazi wa 'nyumba' ambazo ni za kawaida, mazingira bado wanajitahidi sana Viongozi wa Serikali za Mitaa Dodoma wako makini sana na suala la usafi...

Nina wasi wasi huyu mleta mada hajakaa Dom au ana tatizo flani na Dom
 
Nimeondoka Leo Jioni. Nilikuwepo kwa muda kama wiki 2 hivi.
Wiki mbili unahitimisha Dom chafu?!

Hauko serious ndio maana nikakushangaa eti Njia ya kwenda Kigamboni pachafu bila kujua pale huwa uchafu unakusanywa baada ya muda unazolewa...

Labda ungeniambia suala la kuchelewa kuzoa taka hizo hapo sawa na ni jambo la kufanyiwa kazi likawa sawa.
 
Mleta mada anatembelea masoko anaakuja kuhitimisha Dom chafu

Eti saba saba chafu kisa kapita stand kule nyuma kwa mtu ambaye hajafika Dom anaweza akaamini Saba saba yote chafu

Na hata huko alipopataja ukiachwa uswazi wa 'nyumba' ambazo ni za kawaida, mazingira bado wanajitahidi sana Viongozi wa Serikali za Mitaa Dodoma wako makini sana na suala la usafi...

Nina wasi wasi huyu mleta mada hajakaa Dom au ana tatizo flani na Dom
Haswaaaaa!!......mimi si mwenyeji wala mkazi wa mkoa huo lakini nimeishi dom zaidi ya miaka 20 hapo kabla ya kuondoka na nimeshangaa baada ya kuja hapo na kuona jinsi pamoja na ujenzi wa mitaro barabara mji ulivyopangwa vizuri na usafi wa hali ya juu.

Sijui angesema nini angekuja miaka ile stand ya mkoa ni ya vumbi kabla hapajajengwa au pale jamatini enzi zile za usiku kweusi.
 
Mleta mada kakaa wiki mbili tu haijui Dodoma..

Mimi pia nimeshi Dodoma miaka hiyo hiyo na Mzee wangu kajenga hapo Dom japo sio nyumbani ila huwa ninarudi mara kwa mara likizo.

Dom ya sahivi sio ya kipindi kile, hakika sasa hivi kwenye suala la usaf wanajitahidi sana.
 
Huu mji siuelewagi, mchanga umejaa kwenye lami, yani lami inaonekana maeneo ambayo tairi zinapita tu, na viongozi wapo tu hawalioni hilo.
 
sawasawa. mamlaka husika ziwajibike kuhakikisha Makao Makuu ya Nchi yanakuwa pasafi. Uchafu wa Dodoma huwezi kilinganishwa na huu wa jiji letu Kongwe la Dar Salama.
 
Back
Top Bottom