Ifahamu Dodoma

Ifahamu Dodoma

b191

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
742
Reaction score
1,032
Habari zenu ndugu zangu,

Kwa muda wa Majuma kadhaa nipo Dodoma Mjini na nimekuwa nikifanya uchunguzi wangu binafsi.

Katika uchunguzi wangu nimegundua mambo kadha wa kadha.

Hapa nitazungumzia mambo makubwa mawili,

1. Usafi na Mazingira Dodoma Mjini

2. Maeneo hatarishi kwa Mkoa wa Dodoma hasa Dodoma Mjini.

SEHEMU HII YA 1 NITAJIKITA ZAIDI KWENYE SUALA LA USAFI.

Kwa ujumla Dodoma Mjini ni mji mchafu katika maeneo mengi japo baadhi ya maeneo ni masafi

Sababu za uchafu huu ni;
1. Mwamko mdogo wa wananchi juu ya usafi.

2. Uwajibikaji mdogo wa mamlaka zinazohusiana na usafi

MAENEO AMBAYO WANANCHI WANA MWAMKO MDOGO WA USAFI;
a. Hazina

b. Mlezi

c. Kikuyu

d. Majengo

e. Kizota

f. Chang'ombe ya chini

g. Chadulu

h. Maili mbili

j. Bahi road

k. Makulu

l. Makole

Kwa wale mnaohamia Dodoma na wapenda Usafi Epukeni sana maeneo haya.

MAENEO AMBAYO MAMLAKA HAZIWAJIBIKI SAWASAWA KATIKA UKUSANYAJI TAKA,

1. Kwenye madampo karibu yote uchafu umejaa hadi kumwagika chini.

2. Masoko yote (Mfano, Bonanza, Soko Kuu la Majengo na Sabasaba) ni machafu sana. Ukifika kwenye masoko haya utajionea mwenyewe.

3. Kituo kikuu cha Mabasi ya Mkoani na Jamatini kuna uchafu wa kutisha. Kwa wale waliopita Dodoma siku za karibuni watakuwa wameshuhudia hali hii ya Uchafu.


BINAFSI SIAMINI KAMA MAMLAKA HUSIKA ZINAJUA HALI YA USAFI KWA MKOA WA DODOMA.

NB:
SEHEMU YA 2 NITAWALETEA MAENEO MAARUFU KWA UUZAJI WA MADAWA NA VIBAKA.


Nawasilisha.

Unaweza ku - "SUBSCRIBE " Topic hii ili nitakapo andika SEHEMU YA 2 tuweze kuwa pamoja. Nitaleta taarifa hapahapa.

----
Updates; Sehemu ya PILI

Ninawasalimu wanajamvi wote.

Naomba nijikite moja kwa moja kwenye dhumuni husika la andishi langu la Leo;

Leo naomba niainishishe maeneo hatarishi kwa Dodoma Mjini katika vipengele vifuatavyo;

1. Maeneo yenye vibaka sana

2. Maeneo maarufu kwa uuzaji wa Dawa za Kulevya ikiwemo Bangi na Mirungi.

3. Maeneo maarufu kwa biashara ya Ngono.

NB: Mtaniwia radhi kwa kutokuwa specific kwa kumtaja mtu au biashara yake.

NAOMBA NIANZE:

1. MAENEO YENYE VIBAKA WENGI
Ukihamia Dodoma kama wewe ni Mchelewaji wa kurudi nyumbani usiishi maeneo yafuatayo;
a. KIKUYU
b. MAJENGO
c. KIZOTA
d. CHANG'OMBE YA CHINI
e. CHADULU
f. MAILI MBILI
g.BAHI ROAD
h. MAKOLE
I. MAKULU

Maeneo haya ni hatari sana kwa kutembea usiku pia kama una vitu vya dhamani ni maeneo hatarishi pia.

2. MAENEO MAARUFU KWA UUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA

a.HAZINA AIRPORT na MJI MPYA

√ Haya ni maeneo maarufu sana kwa uuzaji wa Unga "Cocaine n.k". Hazina kuna mfanyabiashata yupo karibu na ofisi nyeti akiendesha hii biashara. Vijana wengi watumia unga huenda maeneo haya kujipatia huduma.

b. MAKOLE AIRPORT NA CHAMWINO

√ Ni maeneo maarufu kwa upatikanaji wa Mirungi. Wahitaji wengi wa Mirungi huipata maeneo haya. Zipo gari binafsi na za-biashara ambazo hutumika kusafirisha Mirungi kuingia Dodoma.

c. HAZINA, MAJENGO, KIKUYU, KIZOTA, CHANG'OMBE YA CHINI, CHADULU, MAILIMBILI, BAHI ROAD, MAKOLE na MAKULU

√Haya ni maeneo ambayo BANGI inauzwa sana na watumiaji wake wapo wengi pia. Mfano, Eneo la MAJENGO kuna Kibanda maalumu cha kuvutia Bangi. Mvutaji hufika hapo na Bangi yake na kiasi kati ya 200 hadi 500 kwa ajili ya kulipia huduma ya kuvutia Bangi kwenye Banda.

√ Maeneo mengine maarufu kwa uuzaji wa Bangi ni Vituo vya Daladala ambavyo kuna wapiga debe, mfano Nkuhungu, Chang'ombe ya Chini, na Jamatini.

3. MAENEO MAARUFU KWA BIASHARA YA NGONO

Ukiwa Dodoma huduma hii inapatikana sana UHINDINI, MAKOLE na AIRPORT. Nyakati za usiku Dada poa wengi wanapatikana maeneo hayo.

Pia wapo ambao huziacha namba zao kwa wahudumu wa Nyumba za Wageni na pindi unapohitaji huduma hupigiwa simu na kuja kukupatia huduma.


Hapo ndipo mwisho wa utafiti wangu.


Nawasilisha.
 
ngoja niwahi dawati la mbele tayari kufuatilia mada
 
Nionyeshe nilipo ongopa
Kuhusu Saba saba, Hazina, Mlezi na hata Kikuyu sio yote

Dodoma barabara zote zinaeleweka na suala la usafi maeneo mengi limezingatiwa labda kama kuna tatizo la uzoaji taka

Dodoma mimi ni home away from home, nimekulia hapo na kusoma hapo na likizo huwa nipo hapo,

Tena hiyo Majengo Sokoni nimekuta na huo mtaro umesafishwa unang'aa kitu ambacho sijawahi kuona kifanye miaka mingi niliyoishi hapo.

Sasa sijui uchafu huo unaoongelea wewe ni upi na sikatai kuna baadhi ya maeneo bado si masafi sana ila asilimia kubwa ya Maeneo uliyoyataja hujawa mkweli
 
Hahaha unataka tusihamie Dodoma nini?! Sasa tuahirishe kuja?!
 
Kuhusu Saba saba, Hazina, Mlezi na hata Kikuyu sio yote

Dodoma barabara zote zinaeleweka na suala la usafi maeneo mengi limezingatiwa labda kama kuna tatizo la uzoaji taka

Dodoma mimi ni home away from home, nimekulia hapo na kusoma hapo na likizo huwa nipo hapo,

Tena hiyo Majengo Sokoni nimekuta na huo mtaro umesafishwa unang'aa kitu ambacho sijawahi kuona kifanye miaka mingi niliyoishi hapo.

Sasa sijui uchafu huo unaoongelea wewe ni upi na sikatai kuna baadhi ya maeneo bado si masafi sana ila asilimia kubwa ya Maeneo uliyoyataja hujawa mkweli

Mlezi nenda maeneo ya karibu na Daraja la Kigamboni na maeneo ya Mlezi katikati.

Hazina nenda upande wa pili wa Shule ya Mlezi,

Sabasaba nenda yale maeneo yenye soko na stand.

Soko Kuu kila sehemu ni chafu, pitia Eneo la Bustani ya
Mh. Mavunde na pale kwenye kituo cha Tax.

Hiyo ni mifano tu.
 
watanzania kila kitu mnataka mashindano ya ubishi ,changamoto haibishiwi kwahiyo nyie mnataka yatajwe mazuri tu na mabaya yenu mtayajuaje ili mlekebishe!Dodoma ni mji mzuri sana ila unanapungufu kadhaa ambayo inahitajika kurekebishwa ikiwepo wa uchafu kwa baadhi ya maeneo kama mtoa mada alivyo alezea.
 
Back
Top Bottom