Habari zenu ndugu zangu,
Kwa muda wa Majuma kadhaa nipo Dodoma Mjini na nimekuwa nikifanya uchunguzi wangu binafsi.
Katika uchunguzi wangu nimegundua mambo kadha wa kadha.
Hapa nitazungumzia mambo makubwa mawili,
1. Usafi na Mazingira Dodoma Mjini
2. Maeneo hatarishi kwa Mkoa wa Dodoma hasa Dodoma Mjini.
SEHEMU HII YA 1 NITAJIKITA ZAIDI KWENYE SUALA LA USAFI.
Kwa ujumla Dodoma Mjini ni mji mchafu katika maeneo mengi japo baadhi ya maeneo ni masafi
Sababu za uchafu huu ni;
1. Mwamko mdogo wa wananchi juu ya usafi.
2. Uwajibikaji mdogo wa mamlaka zinazohusiana na usafi
MAENEO AMBAYO WANANCHI WANA MWAMKO MDOGO WA USAFI;
a. Hazina
b. Mlezi
c. Kikuyu
d. Majengo
e. Kizota
f. Chang'ombe ya chini
g. Chadulu
h. Maili mbili
j. Bahi road
k. Makulu
l. Makole
Kwa wale mnaohamia Dodoma na wapenda Usafi Epukeni sana maeneo haya.
MAENEO AMBAYO MAMLAKA HAZIWAJIBIKI SAWASAWA KATIKA UKUSANYAJI TAKA,
1. Kwenye madampo karibu yote uchafu umejaa hadi kumwagika chini.
2. Masoko yote (Mfano, Bonanza, Soko Kuu la Majengo na Sabasaba) ni machafu sana. Ukifika kwenye masoko haya utajionea mwenyewe.
3. Kituo kikuu cha Mabasi ya Mkoani na Jamatini kuna uchafu wa kutisha. Kwa wale waliopita Dodoma siku za karibuni watakuwa wameshuhudia hali hii ya Uchafu.
BINAFSI SIAMINI KAMA MAMLAKA HUSIKA ZINAJUA HALI YA USAFI KWA MKOA WA DODOMA.
NB:
SEHEMU YA 2 NITAWALETEA MAENEO MAARUFU KWA UUZAJI WA MADAWA NA VIBAKA.
Nawasilisha.
Unaweza ku - "SUBSCRIBE " Topic hii ili nitakapo andika SEHEMU YA 2 tuweze kuwa pamoja. Nitaleta taarifa hapahapa.
----
Updates; Sehemu ya PILI
Ninawasalimu wanajamvi wote.
Naomba nijikite moja kwa moja kwenye dhumuni husika la andishi langu la Leo;
Leo naomba niainishishe maeneo hatarishi kwa Dodoma Mjini katika vipengele vifuatavyo;
1. Maeneo yenye vibaka sana
2. Maeneo maarufu kwa uuzaji wa Dawa za Kulevya ikiwemo Bangi na Mirungi.
3. Maeneo maarufu kwa biashara ya Ngono.
NB: Mtaniwia radhi kwa kutokuwa specific kwa kumtaja mtu au biashara yake.
NAOMBA NIANZE:
1. MAENEO YENYE VIBAKA WENGI
Ukihamia Dodoma kama wewe ni Mchelewaji wa kurudi nyumbani usiishi maeneo yafuatayo;
a. KIKUYU
b. MAJENGO
c. KIZOTA
d. CHANG'OMBE YA CHINI
e. CHADULU
f. MAILI MBILI
g.BAHI ROAD
h. MAKOLE
I. MAKULU
Maeneo haya ni hatari sana kwa kutembea usiku pia kama una vitu vya dhamani ni maeneo hatarishi pia.
2. MAENEO MAARUFU KWA UUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA
a.HAZINA AIRPORT na MJI MPYA
√ Haya ni maeneo maarufu sana kwa uuzaji wa Unga "Cocaine n.k". Hazina kuna mfanyabiashata yupo karibu na ofisi nyeti akiendesha hii biashara. Vijana wengi watumia unga huenda maeneo haya kujipatia huduma.
b. MAKOLE AIRPORT NA CHAMWINO
√ Ni maeneo maarufu kwa upatikanaji wa Mirungi. Wahitaji wengi wa Mirungi huipata maeneo haya. Zipo gari binafsi na za-biashara ambazo hutumika kusafirisha Mirungi kuingia Dodoma.
c. HAZINA, MAJENGO, KIKUYU, KIZOTA, CHANG'OMBE YA CHINI, CHADULU, MAILIMBILI, BAHI ROAD, MAKOLE na MAKULU
√Haya ni maeneo ambayo BANGI inauzwa sana na watumiaji wake wapo wengi pia. Mfano, Eneo la MAJENGO kuna Kibanda maalumu cha kuvutia Bangi. Mvutaji hufika hapo na Bangi yake na kiasi kati ya 200 hadi 500 kwa ajili ya kulipia huduma ya kuvutia Bangi kwenye Banda.
√ Maeneo mengine maarufu kwa uuzaji wa Bangi ni Vituo vya Daladala ambavyo kuna wapiga debe, mfano Nkuhungu, Chang'ombe ya Chini, na Jamatini.
3. MAENEO MAARUFU KWA BIASHARA YA NGONO
Ukiwa Dodoma huduma hii inapatikana sana UHINDINI, MAKOLE na AIRPORT. Nyakati za usiku Dada poa wengi wanapatikana maeneo hayo.
Pia wapo ambao huziacha namba zao kwa wahudumu wa Nyumba za Wageni na pindi unapohitaji huduma hupigiwa simu na kuja kukupatia huduma.
Hapo ndipo mwisho wa utafiti wangu.
Nawasilisha.