Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 77,215
- 165,817
Kuomba ni kero kubwa, yani hata ukikaa zako mahali ujiagizie ka kuku, watakuja tu kukuomba!!!!!!
84 wanaenda wahenga, wazee wasiopenda fujoMkuu club84 hivi bado kuna watu wanaendaga?? Wewe utakuwa unaongelea Dodoma ya zamani. Sasa hivi Malaya wote utawakuta malaika
Dodoma mifumo ya maji imefika hadi mkonze kuelekea mbele huko kama utaenda iringa, ukielekea kwa pinda zuzu maji yapo, ukija kizota-nkuhungu maji yapo rudi huku ilazo-kisasa sasa nyie mnaosema maji ya shida au mnamaanisha vijijini huko?...
Chadulu zipo mbili kama ilivyo Makole na hata hiyo Kikuyu zimegawanyika pia!..
Nimeishi kikuyu ya juu hilo tatizo sijalipata, nikahamia maeneo ya magorofani pia sikukumbana nalo..Ni sawa kabisa.. miundo mbinu kama mabomba yapo sehemu kubwa sana, tatizo ni utokaji wa Maji. Fanya utafiti hasa wakati ambao Wakubwa wapo Dodoma utanielewa vizuri.
Watu wanaoishi maeneo kama Kisasa, Area C na D hawawezi kuona shida hii kwa sababu ni maeneo ambayo Wakubwa wanaishi na maji yapo muda wote.
mbona ni ya kutafuta tu. tanzania hii kuna sehemu sio pachafu.Mlezi nenda maeneo ya karibu na Daraja la Kigamboni na maeneo ya Mlezi katikati.
Hazina nenda upande wa pili wa Shule ya Mlezi,
Sabasaba nenda yale maeneo yenye soko na stand.
Soko Kuu kila sehemu ni chafu, pitia Eneo la Bustani ya
Mh. Mavunde na pale kwenye kituo cha Tax.
Hiyo ni mifano tu.
Mkuu Magorofani maarufu kama MAGOROFA YA CDA kuna shida ya maji tangu kitambo. Na nimefanikiwa kufika eneo hilo ambalo kwa sasa Magorofa mengi ni kama Magofu.Nimeishi kikuyu ya juu hilo tatizo sijalipata, nikahamia maeneo ya magorofani pia sikukumbana nalo..
Magorofa ya Nhcf umefikaaaMkuu Magorofani maarufu kama MAGOROFA YA CDA kuna shida ya maji tangu kitambo. Na nimefanikiwa kufika eneo hilo ambalo kwa sasa Magorofa mengi ni kama Magofu.
Eneo hilo pia lilikuwa na uchafu wa kutosha.
Kapicha tafadhali maneno matupu hayanogi
Napita
Kwa
Majonzi![]()
Ila Kwa usafi 100%Waliyarekebisha na sasa ni Masafi. Wakati nafanya utafiti wangu kuna mdau alinielekeza maeneo hayo na nilienda face to face.
Yameboreshwa sana.
Sio uchafu bomoa bomoa imepita hapo unapoongelea uchafu unakosea wakat unaelewa kabisa walichokifanya reli ni nn unazan hapo mpaka stand ihame mambo yatakaa sawaaNimefika Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoa leo. Nilipotaka kupiga picha kuna mdau akanieleza kama nahitaji simu yangu niache hiyo shughuli.
Soko Kuu la Majengo Leo tangu Asubuhi Halmashauri walikuwa wanazoa uchafu.
sawaMkuu Magorofani maarufu kama MAGOROFA YA CDA kuna shida ya maji tangu kitambo. Na nimefanikiwa kufika eneo hilo ambalo kwa sasa Magorofa mengi ni kama Magofu.
Eneo hilo pia lilikuwa na uchafu wa kutosha.
Ila Kwa usafi 100%
Sio uchafu bomoa bomoa imepita hapo unapoongelea uchafu unakosea wakat unaelewa kabisa walichokifanya reli ni nn unazan hapo mpaka stand ihame mambo yatakaa sawaa
Mkuu ulienda kwa shangazi yako au ulitumwa?vp wamekulipa sh.ngap?Habari zenu ndugu zangu,
Kwa muda wa Majuma kadhaa nipo Dodoma Mjini na nimekuwa nikifanya uchunguzi wangu binafsi.
Katika uchunguzi wangu nimegundua mambo kadha wa kadha.
Hapa nitazungumzia mambo makubwa mawili,
1. Usafi na Mazingira Dodoma Mjini
2. Maeneo hatarishi kwa Mkoa wa Dodoma hasa Dodoma Mjini.
SEHEMU HII YA 1 NITAJIKITA ZAIDI KWENYE SUALA LA USAFI.
Kwa ujumla Dodoma Mjini ni mji mchafu katika maeneo mengi japo baadhi ya maeneo ni masafi
Sababu za uchafu huu ni;
1. Mwamko mdogo wa wananchi juu ya usafi.
2. Uwajibikaji mdogo wa mamlaka zinazohusiana na usafi
MAENEO AMBAYO WANANCHI WANA MWAMKO MDOGO WA USAFI;
a. Hazina
b. Mlezi
c. Kikuyu
d. Majengo
e. Kizota
f. Chang'ombe ya chini
g. Chadulu
h. Maili mbili
j. Bahi road
k. Makulu
l. Makole
Kwa wale mnaohamia Dodoma na wapenda Usafi Epukeni sana maeneo haya.
MAENEO AMBAYO MAMLAKA HAZIWAJIBIKI SAWASAWA KATIKA UKUSANYAJI TAKA,
1. Kwenye madampo karibu yote uchafu umejaa hadi kumwagika chini.
2. Masoko yote (Mfano, Bonanza, Soko Kuu la Majengo na Sabasaba) ni machafu sana. Ukifika kwenye masoko haya utajionea mwenyewe.
3. Kituo kikuu cha Mabasi ya Mkoani na Jamatini kuna uchafu wa kutisha. Kwa wale waliopita Dodoma siku za karibuni watakuwa wameshuhudia hali hii ya Uchafu.
BINAFSI SIAMINI KAMA MAMLAKA HUSIKA ZINAJUA HALI YA USAFI KWA MKOA WA DODOMA.
NB:
SEHEMU YA 2 NITAWALETEA MAENEO MAARUFU KWA UUZAJI WA MADAWA NA VIBAKA.
Nawasilisha.
Unaweza ku - "SUBSCRIBE " Topic hii ili nitakapo andika SEHEMU YA 2 tuweze kuwa pamoja. Nitaleta taarifa hapahapa.
Ndiooooo Nimesema bomoa bomoa imeharibu mazingiraMkuu Demiss, pale ni pachafu pamoja na kwamba walibomopewa. Vyakula vinauzwa kwenye Mazingira hayo hayo machafu.