Ifaham Kitulo Ranch Makete (CANADA IN TANZANIA)

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Kitulo ni ranch ya taifa iliyo anzishwa mwaka 1963 , Rank hii ipo Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe ambao hali ya hewa ni ya baridi sana na mvua kwa wingi.

Huko kuna ng'ombe wa kisasa walio chukuliwa marekeni na nchi za ulaya ambapo hali ya hewa inaendana sana na nchi hizo.

Huko kitulo kukiwa na joto ni 19c na kukiwa na baridi hufikia 0c.
ng'ombe hao hutoa lita 15 hadi 20.

shamba lina ng'ombe 700 kwa sasa japo shamba lina uwezo wa kuchukua ng'ombe 4000.

Mheshimiwa Mwigulu amefarijika kufika na kuona shamba hilo ambalo kwa muda mrefu lilikua limetelekezwa na serikali.

chini ni baadhi ya picha.

usiniulize maswali zaidi kuhusu kitulo, sina majibu.
 

Attachments

  • 1457297039302.jpg
    1457297039302.jpg
    48.3 KB · Views: 438
  • 1457297058786.jpg
    1457297058786.jpg
    38.7 KB · Views: 499
  • 1457297078871.jpg
    1457297078871.jpg
    47.1 KB · Views: 443
  • 1457297094919.jpg
    1457297094919.jpg
    34.9 KB · Views: 385
  • 1457297112989.jpg
    1457297112989.jpg
    38.2 KB · Views: 361
  • 1457297128231.jpg
    1457297128231.jpg
    37.4 KB · Views: 318
  • 1457297154166.jpg
    1457297154166.jpg
    38.7 KB · Views: 327
  • 1457297180682.jpg
    1457297180682.jpg
    32 KB · Views: 408
Da nakumbuka sehemu wanaita Matamba! Anyway naomba kupata maelezo kama bado wanauza ng'ombe wa mbegu kwa wakulima na pia ikiwezekana mawasiliano ya wahusika.
 
Hakuna eneo dunia ambalo binadamu anaweza ishi lenye nyuzi joto 0,acha uongo


Mambo mengine uwe unawaachia wanaoyajua tu. Hiyo 0°C nayo kaipunja Kitulo, baridi ya pale hufika negative huko na kutengeneza barafu. Hilo ni eneo la KITULO kwenyewe na KIKONDO. Baridi hupungua kidogo maeneo ya Ujuni- Nkenja-Ndulamo na Makete yenyewe. Niendelee?
 
Hao ng'ombe wazalishwe wengi halafu wawauzie wananchi.

Wizara ya kilimo na mifugo iboreshe mashamba yao ya mifugo sehemu mbalimbali ili wananchi wawe wanajifunza ufugaji bora na wa kisasa kwenye hayo mashamba,ufugaji wa kuhama hama na mifugo umepitwa na wakati vile vile ni chanzo cha ugomvi kati ya wafugaji na wakulima.
 
Serikali ilitelekeza ule mradi wa ng'ombe. Nikikumbuka miaka ya 1980 hadi 1995 palikuwa na ng'ombe wengi sana. Ila kuanzia miaka ya 1997-2000 ng'ombe wengi waliibiwa kupelekwa mikoa ya kaskazini.
 
Back
Top Bottom