Kilimo bora cha matikiti maji by king camel

Mrkingcamel

Member
Jul 27, 2021
16
12
UTANGULIZI

Matikiti maji ni tunda kubwa la mviringo ambalo linastawi vizuri katika maeneo ambayo ardhi yake aitwamishi maji kwa mda mrefu. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao la tikitiki maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.Kuna aina mbili za matikiti maji moja tikikiti lenye mbegu na lisilo na mbegu.

Tikiti maji linahitaji vitu vitano muhimu ili uweze kuzalisha kwa wingi kama

1.mwanga wa jua wa kutosha kwa maana hiyo eneo linatakiwa lisiwe na kivuli

2.Uwepo wa nyuki kwa ajiri ya uchavishaji

3.Maji ya kutosha

4.Virutubisho

5.Nafasi ya kutosha hususani katika upandaji



Mahitaji muhimu

1.Hali ya hewa

Matikiti maji yanahitaji kipindi kirefu cha hali ya ujoto.Kukiwa na hali ya ubaridi na mvua nyingi ina madhara kwa tikitikimaji ambayo inasababisha ukuaji hafifu,kuchelewa kukomaaa,ukuaji mbovu wa tunda na pia husababisha tunda kuwa na uwazi katikati.

2.Hali ya udongo

Tikiti maji linahitaji udongo ambao hautuamish maji kwa kipindi kirefu aina ya udongo huo ni kichanga au kichanga tifitifu…Shamba likiwa na udongo ambao unatuamisha maji kwa mda mrefu(mfinyazi sana) husababisha ukuaji wa taratibu wa zao na pia husababisha kupasuka kwa tunda.Hali ya uchachu kwa udongo ni pH 6 hadi 7.

3.Mbegu

Kiasi cha mbegu ni gram 500 kwa kila eka



Uchaguaji wa mbegu

Kitu muhimu katika mkulima ni uchaguaji wa mbegu bora,Upandaji wa mbegu ambayo haina soko hupelekea kukosa faida pindi unapo fanya mauzo

Mbegu Bora za Matikiti

Mbegu maarufu ya tikiti ni Sukari F1, hata hivo madukani zinapatikana nyingi bora na tofauti tofauti kama vile:

Arashani F1 – kutoka Syngenta

Sukari F1 – Kutoka East Africa seeds

Sugar king F1 – kutoka Africasia

Juliana F1 – kutoka Kiboseed

Zebra F1 – Kutoka Balton

Pato F1 – Kutoka Agrichem



Sukari F1

Inawahi kukomaaa inachukua siku 90 na ina uwezo mzuri wa kutengeneza matunda

Inauzito wastani kilo 7 hadi 8 nyengine hufikia kilo 12

Usafirishaji na utunzaji wake ni rahisi

Ina mishirizi meupe iliyo ambatana na kijani iliyokolea


Sugar queen F1 hybrid

Inachukua siku 75 mpaka 80

Ni kijani kwa nje na nyekundu kwa ndani yenye kuvutia

Inauzito wastani kilo 8 hadi 10

ukinzani wa kinyausi/mnyauko

Inatoka kampuni ya Syngenta



Uwaandaji wa shamba

Hakikisha kuwa shamba lako limelimwa vizuri na udongo kulainika mpaka lifikie udongo wote hauna mabonge mabonge.

Upandaji wa tikiti maji

Panda mbegu 2 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa mita 1 hadi 2 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 – 3 kutoka mstari hadi mstari.

[https://3]


Zingatia: usitumie mbegu za tikiti ulilonunua (kwa ajili ya kula) kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2).



Katika kilimo cha umwagiliaji

1.umwagiliaji wa kutumia mifereji

Miferejeji inataikiwa kuwa na upana am l 30,mche moja hadi mwingine ni sm60 na kutoka mstari hadi mstari ni m 3 na nusu



[https://1]


Mfumo wa umwagiliaji kutumia mfereji



2.Umwagiliaji wa kutumia matone

Inatakiwa kuinuka kwa tuta kwa mita 1 na katika tuta moja sm 45 katikati ya mstari mmoja na mwengne na pia mita 3 katikati ya mistari katik ya bomba kweny tuta moja had lingine.



[https://1]


Mfumo wa umwagiliaji kutumia matone



Kuweka mbolea

1.kupandia

Weka samadi kiasi cha ton 8 kwa eka kabla mlimo wa mwisho…ili kuwezesha udongo na samadi vichanganyikane.

Tumia mbolea ya dukani mfano NPK,DAP na MOP katika mda wa kupanda mbegu.



2.Kukuzia

Tumia mbolea za kukuzia ili kupata mavuno mengi



Zingatia

· Ucheleweshaji au uwekaji kiasi kikubwa cha mbolea za nitrojen husababisha kuwa na uwazi katikati wa tikitiki hii utokea kwenye kipindi cha baridi

· uwekaji kiasi kikubwa cha mbolea za nitrojen husababisha idadi kubwa ya mauwa dume hupelekea matunda machache

·



KWA HILO TUNA MSHAULI MKULIMA KUPIMA UDONGO WAKE KWANZA ILI AWEZE KUWEKA KIWANGO SAHIHI CHA VIRUTUBISHO



Shughuli nyenginezo

1.Utoaji wa magugu

Hii inatakiwa kufanywa mara kwa mara ili kuruhusu shamba kuwa safi.Na pia wakati wakuondoa magugu epuka kuweka jeraha kwa mmea



2.Kupruni(pitching)

Katika tikiti maji shina kuu hukatwa kichwani endapo ifikapo mita 1 na nusu ili kuruhusu shina la pembeni kuota.Hili zoezi linafaida kubwa ambayo nikuongeza uzarishaji wa matikiti.

Katika hatua ya mwanzo ya matunda kuanza tunashauri yale matunda ambayo yamekumbwa na ugonjwa au yamearibika kwa sababu tofauti tofauti yanatakiwa kuondolewa….Ili kubwakiwa na na matunda 2 hadi 3 kwa kila shina(vine) matokea yake katika hili huongeza ukubwa wa tunda na mavuno.

Kupunguza uenezwaji wa magonjwa tunashauri usipruni shina wakati lina maji maji



3.Uchavishaji

Tikitiki maji linahitaji nyuki kwa ajiri ya uchavushaji na pia ukuaji wa tunda,utafiti unaonyesha kila ua la kike linatakiwa kufikiwa mara saba kwa ajiri ya utungaji sahihi.Uchache wa uchafushaji hupelekea tunda kuwa na shape bofu hii husababishwa na baridi,mvua nyingi na upepo mkali ambao hufanya nyuki kutofanya kazi yake kifasaha….Asubuhi kabisa Nyuki huwa na hali nzuri kwa ajri ya ufanyaji wa kazi ndo maana inashauriwa kutopiga sumu wakati huo.



4.Mavuno

Mavuno ya tikiti maji kutegemea mfumo wa ulimaji,msimu na vitu vingine.wastani wa mavuno kwa kila eka inanza tan 25 hadi 30.



Wadudu na magonjwa
Kwa kawaida zao hili halina wadudu na magonjwa mengi yanayolishambulia. Hii hutegemeana na uchaguzi sahihi wa eneo linalofaa kwa kilimo cha zao hili pamoja na hali ya hewa. Pamoja na hayo kuna baadhi ya wadudu ambao wamezoeleka katika zao hili.
Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea. Magonjwa kama Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea.Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa kuthibiti ugonjwa magonjwa hayo hapo juu.
Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda.
Dawa aina ya abernil,ninja,dudu all,actara,farmerguld itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda.
Vidukari: Wadudu hawa ni moja ya wadudu waliozoeleka kwenye matikiti, hushambulia sana zao hili na mara nyingi wasipodhibitiwa mapema Kabla ya kupanda hakikisha kuwa udongo una joto la wastani wa nyuzi joto 70°C. Unaweza kupanda kwa kutumia jembe la mkono au reki. Fukia mbegu kwenye mashimo kwa kutumia udongo laini na shimo lisiwe na kina kirefu, liwe na wastani wa inchi 1, ili kutoa urahisi kwa mbegu kuota.
Kwa kawaida tikiti hupandwa kwa mstari mmoja kwenye tuta lenye mwinuko wa inchi 6 na upana wa futi 4. Nafasi kati ya mche na mche iwe ni sentimita 120.



Ugonjwa
Zao hili hushambuliwa zaidi na ugonjwa wa Ubwiri unga. Ugonjwa huu ni hatari sana na usipodhibitiwa mapema kwa kuwa hushambulia majani ya mmea, husababisha mmea kufa baada ya muda mfupi jambo ambalo huathiri mavuno.Ni vigumu sana kuzalisha zao hili wakati wa msimu wa mvua, hivyo inashauriwa kupanda wakati wa kiangazi. Hali hii itasaidia mazao haya kustawi vizuri, ikiwa ni pamoja na kuepuka matunda kuoza kutokana na mvua kuwa matunda ya tikiti hukaa chini kwenye udongo.



Uvunaji Matikiti
Kabla ya kuvuna matunda ni vema kwanza kujua kuwa matikiti huchukua takribani miezi mitatu mpaka mitano toka inapopandwa mpaka kukomaa. Hii hutegemea na aina ya matikiti yenyewe. Tikiti lililo komaa linaatakiwa na mwonekano wake huwa kama ifuatavyo;
Rangi ya mng’ao hupotea Upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano.Pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu. Ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake unakuwa kama mlio wa ngoma.Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi





Sio ugonjwa lakini ni tabia yaki phisiolojia

1.Shingo ya chupa

Hii ni shape baya la tikiti maji ambalo linasababishwa na uwepo mdogo hali ya uchavushaji na hali ya joto kushuka



Kudhibiti

Usipige sumu wakati wa asubuhi kipindi cha mauwa husabaisha kutowakimbiza nyuki na pia mwagilia katika mda sahihi ambao umepishana sawa



2.Kunyauka kwa kitako

Hii usabishwa na upungufu wa virutubisho vya kalsiam au upungufu wa unyevu au vyote kwa pamoja na pia uwekaji wa mbolea za nitrogen kwa kiasi kikubwa.



Kudhibiti

Weka chokaa kama udongo wako una pH ndogo,zingatia umwagiliaji unafanana wa kila siku kwa kuzingatia mda,ondoa tunda liloathirika,punguza matumizi makubwa ya nitrojen katika kipindi cha utungaji wa tunda,piga mbolea ya maji ambayo inakiasi kikubwa cha kalsium au weka mbolea ya CAN au yarabela nitrobor.



3.Kupasuka kwa tunda

Hiii husababishwa na hali ya ubaridi kipindi tunda linaanz kujitunga,kiwango kikubwa cha nitrojen,umwagiliaji wa kiasi kikubwa ambao hauna mpangilio katika hatua tunda linapoanza kujitunga….Tunda lililoathiriwa linakuwa shape ya bapa na linang’aa tofaut na mwanzo



Kidhibiti

Tumia mbolea ya yarabera nitrabor kabla tunda lijaanza kutungwa au mbolea za majani kupunguza uwaribifu.punguza matumizi makubwa ya mbolea za nitrojeni na umwagiliaji sahihi wa kuzingatia mda au kuwa na unyevu usiobadirika badirika.



4.Michirizi ya rangi nyeupe

Hii utokea katikati ya tikiti maji.hii husababishwa na kiasi kikubwa cha unyevu unyevu na kiasi kikubwa cha nitogeni katika kipindi tunda linataka kukomaaa



Kudhibiti

Umwagiliaji mzuri na uwekaji wa kiasi sahihi kipindi cha ukomavu

images%20(10).jpg
 
Back
Top Bottom