If Chadema change position it mustt apologize, unconditionally!

If Chadema change position it mustt apologize, unconditionally!

Mhhhh! I am simply out of words! Hivi Ni Chadema walio imply kuna udhalimu au watanzania wenyewe walijionea? Kazi kweli kweli kwenye hili jukwaa la siasa! Nachoka sana na hizi siasa za Bongo especially humu ndani! God bless us all with Knowledge!
Umejibu vema. Ni wananchi ndio tulijionea wenyewe jinsi tulivyoibiwa/chakachuliwa kura zetu hata kama chadema hawakuona. kwanza waliopiga kura kuikataa ccm si wote wana chadema wala wana chadema. So, hakuna division hapo au vipi?
 
Hapo kwenye bold ndio hamueleweki. Ukisema hautambui mfumo ulimuweka mtu madarakani halafu ghafla mnamtambua mtu aliyewekwa madarakani, ni tatizo. Hizi kauli za kijanjajanja si muafaka wakati wa sasa. Kama mmeamua kumtambua fanyeni hivyo kwa haraka na ila kugeuka nyuma na kusonga mbele na kama hamumtambui semeni tu wazi hatumtambui bila kuzungukazunguka, mara mfumo mara oh....
Kwenye suala la katiba mnastahili hongera maana mko very clear na ninaamini wananchi wengi wanaopenda maendeleo ya nchi yetu wanaliona hivyo.

Hiyo hata wao wenyewe hawaelewi. Wanachokifanya nii kureplay maamuzi ya kamati kuu tu.
Hata hiyo ya kusema umma wa watanzania unahitaji katiba mpya ni upuuzi mtupu. Wao wamefanya upembuzi gani ambao summary yake inaweza kuwa umma wa watanzania unahitaji katiba mpya au JF ndio umma wa watanzania.
Umma wa watanzania hata haujui katiba ni nini. Kama kuna kitu umma wa watanzania unahitaji ni kufundishwa maana na umuhimu wa katiba.
 
Mwanakijiji,

Nashukuru kwa mwito wako. Naelewa kwamba habari za tarehe 13 Disemba za baadhi ya magazeti zilizoandika habari yenye mwelekeo wa kuashiria kuwa "CHADEMA imebwaga manyanga' katika suala la kumpinga Kikwete. Na habari za tarehe 14 Disemba zikimnukuu Dr Slaa akielezea maamuzi ya kamati kuu zinaweza kuwa zimeleta hisia tofauti kuhusu mwelekeo wa ajenda husika.

Naomba ieleweke kwamba CHADEMA haijabadili msimamo wake katika kuuelezea mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu kwamba haukuwa huru na wa haki na hivyo kutoyatambua matokeo yaliyotangazwa na NEC yaliyompa ushindi Kikwete. Hata hivyo, jambo jipya lililojitokeza kwenye maelezo ya maamuzi ya kamati kuu ni kuipanua ajenda ya katiba mpya kutoka katika kuzungumza zaidi kuhusu tume huru ya uchaguzi na kuingiza masuala ya msingi ya kikatiba kama mamlaka ya Rais, mifumo ya uwajibikaji wa viongozi, haki za binadamu nk. Hii inafanya ajenda ya katiba isiwe ya kiuchaguzi pekee bali ya mfumo mzima wa maisha ya watanzania na kustahili kuungwa mkono sio na vyama vya siasa bali umma wa watanzania kwa ujumla wao.

Sintofahamu hii inaweza kuwa imechangiwa na kauli ya kuanza kushiriki shughuli za kiserikali baada ya kususia hotuba ya Rais pale Dodoma; ni muhimu ikafahamika hali hii haitabadili mwelekeo wa msimamo.

Ajenda ya katiba mpya naamini itaendelea kudaiwa kwa juhudi zote za kibunge na za kuunganisha nguvu ya umma nje ya vyombo vya maamuzi. Binafsi naamini kwamba katiba haipaswi kudaiwa bungeni pekee, inapaswa kudaiwa mitaani kupitia mijadala, maandamano na njia nyingine za nguvu ya umma. Hii ni kwa sababu watawala wa Tanzania wanaelekea kutokuwa tayari kukubaliana na ridhaa ya umma katika suala hili. Hivyo, hakuna kurudi nyuma!

Ni changomoto tu kwamba maamuzi ya kamati kuu kuhusu suala hili kwa maana ya habari yamefunikwa na habari ya hatua ambazo wabunge wa CHADEMA tumechukua dhidi ya wabunge wenzetu wawili katika vikao vililivyopita. Naamini baada ya siku chache mjadala utarudi katika mstari wake kwa sababu mijadala ya masuala hudumu kuliko mijadala ya watu. Nawatakia mjadala mwema!

JJ

JJ
Haya mazagazaga mnayofanya, mtamalizwa nayo kwenye chaguzi zijazo. Hakuna msimamo, hamuelewi mnataka nini halafu kila mtu anajiropokea. Fikirieni impact ya mnayofanya kabla hamjachelewa. People are watching your steps closely.
 
Nakubaliana na Mh Mnyika kuwa CDM haijabadili msimamo, it was the interpretation of the statement that was misleading by the media and pundits.
The major criticism of CDM in this case is that they did not counter the spin well and let the repeated falacy become fact. But CDM has nothing to apologize for, however there are valuable lessons to be learnt.
 
I wonder if there's any purely democratic country under the sun.
 
Hapo kwenye bold ndio hamueleweki. Ukisema hautambui mfumo ulimuweka mtu madarakani halafu ghafla mnamtambua mtu aliyewekwa madarakani, ni tatizo. Hizi kauli za kijanjajanja si muafaka wakati wa sasa. Kama mmeamua kumtambua fanyeni hivyo kwa haraka na ila kugeuka nyuma na kusonga mbele na kama hamumtambui semeni tu wazi hatumtambui bila kuzungukazunguka, mara mfumo mara oh....
Kwenye suala la katiba mnastahili hongera maana mko very clear na ninaamini wananchi wengi wanaopenda maendeleo ya nchi yetu wanaliona hivyo.

Hatujasema tunamtambua, tumesema kwamba ametambuliwa na Tume na Katiba ambayo inakataza matokeo yake yasipingwe mahakamani; akitangazwa ametangazwa. For us Kikwete is legal but illegitimate president!

Suala la kutambua ama kutomtambua sio letu, kwa kuwa limeshapatiwa majibu na mfumo uliopo; logically, ukiyakataa matokeo umemkataa na aliyetokana na matokeo hayo! Tulimsusia kwenye hotuba ya kuzindua bunge ili kufikisha ujumbe kuwa tunataka tume ya uchunguzi na kuanza kwa mchakato wa katiba mpya ambayo pamoja na mambo mengine italeta tume huru ya uchaguzi. Msimamo huu uko pale pale na tunapaswa kuunganisha nguvu ya umma kuudai!

JJ
 
I will tell you what I have been honestly thinking, Tatizo la Chadema ni kukosa uongozi makini. Wanatakiwa wareshuffle haraka sana system yao ya uongozi na kuna watu inabidi frankly waachie ngazi wao wenyewe otherwise they will lead this party to hell. Na next uchaguzi kama hawatafanya la maana hivi viti vingi vya ubunge watavipoteza sana. Nachelemea kuamini kuwa kuna tatizo kuwa la kimadaraka humo ndani na kuna watu wanadhani kuwa wanahodhi chama.
 
Hizi siasa za Afrika hovyo kabisa. Watu hawana misimamo...wanapelekeshwa na upepo tu. Mara huku mara kule yaani ili mradi tu....

Ndio wanasiasa wetu Africa wababaishaji na wasanii na njaa zinawasumbua. Ndio maana mie nikiona mwanasiasa mzalendo nitamuunga but vyama vya siasa siviungi maana baadhi yao havina natija wala nia dhati ya kumkomboa mtanzania zaidi ya kutafuta pa kuonja asali tu.
 
Well it seems like everybody had something on this CHADEMA thing but no one dared to say until someone triggered it all. We love you CHADEMA but you need to do something and you need to do it very fast and accurately at the same time to help your fate in a foreseeable future.
 
Mh Mnyika, unafanya kazi nzuri kufafanua masuala haya na ukumbuke kuwa kazi ni kubwa kwani spin hii imekuwa ikiendelea kwa zaidi ya mwezi. Ila nakusihi usichoke wewe binafsi na uongozi usichoke kufafanua masuala haya.
 
Hatujasema tunamtambua, tumesema kwamba ametambuliwa na Tume na Katiba ambayo inakataza matokeo yake yasipingwe mahakamani; akitangazwa ametangazwa. For us Kikwete is legal but illegitimate president!

Suala la kutambua ama kutomtambua sio letu, kwa kuwa limeshapatiwa majibu na mfumo uliopo; logically, ukiyakataa matokeo umemkataa na aliyetokana na matokeo hayo! Tulimsusia kwenye hotuba ya kuzindua bunge ili kufikisha ujumbe kuwa tunataka tume ya uchunguzi na kuanza kwa mchakato wa katiba mpya ambayo pamoja na mambo mengine italeta tume huru ya uchaguzi. Msimamo huu uko pale pale na tunapaswa kuunganisha nguvu ya umma kuudai!

JJ

Huu mtazamo ni wako au wa Chadema?
Na Dr. SLaa aliposema hamumtambui Kikwete alikuwa anatoa uamuzi wake au wa Chadema.

Kama mmeona kosa msione ugumu kuapologise, huo ndio uungwana.
 
Kwangu mimi the issue is not apologising the issue is CHADEMA are not acting seriously at the moment. Kwanza ni kina nani wamo katika CC na huwa wanapatikana vipi?
 
Kwangu mimi the issue is not apologising the issue is CHADEMA are not acting seriously at the moment. Kwanza ni kina nani wamo katika CC na huwa wanapatikana vipi?
Mheshimiwa Mnyika nakupongeza, at last it happend. Naomba umfikishie kijana mwenzetu Zitto kwamba haraka sana ajirekebishe, wengu tunaumia sana kwa mienendo yake. Tunatambua kwamba kuna mengi hakubaliani nayo lakini si kwa kuhatarisha mafanikio ya chama kwa sasa. He can simply do it silently and with great tactics. Nimesononeka sana but in you I still have trust. I will also convey my message to Kitila, Mzee Baregu namheshimu lakini sina uhakika tena na convincing power and if at all he can turn the game around.Otherwise, nawatikia kila la kheri katika muda huu wa mageuzi. Swala mmoja la kutia maanani ni kwamba ulimwengu wote unawaona ninyi na si CCM. Kwa hawa hakuna kipya but kwenu kuna matumaini, chezeeni karata zenu vizuri and inshalah, we shall succeed.
 
Gotcha! Mwanakijiji is Neither wrong nor right! i read him as a neutral thinker in relations to CDM or CCM! he is playing with human minds just like the great job of Gilbert Ryle in his philosophical studies of the Concept of Minds in the Cartesian metaphysics. Where you can learn a lot about the Category mistakes!
 
Niliposoma magazeti ya leo, nilipatwa na butwaa sana kuona kuwa "CHADEMA wameamua kumtambua Kikwete kama Raisi halali." Ni jambo lililoniuma sana kwa vile bado nina imani kuwa Kikwete siyo Rais halali. Sasa kwa vile imani yangu ilikuwa inaendana na msimamo wa CHADEMA, basi nilikuwa ninajua kuwa nina wabunge wanaoniwakilisha huko bungeni. Sasa baada ya wao kunigeuka, ni kweli huenda kuna haja ya wao kutuomba radhi sisi wote tuliokuwa wafuasi wake. Ni afadhakli wangesema kuwa hatutambui ushindi wa Kikwete ila kuanzia sasa tutafanya naye kazi kwa vile ndiye aliyesimikwa na vyombo husika kuwa raisi wa nchi hii huku tukiamini kuwa hakuchaguliwa kihalali na wananchi.
 
Nikikonnect hoja nyingi humu ndani naanza kupata hisia ya kupotea kwa historia ya nchi yetu!!!! As if the establishments of TANU, ASP and later CCM was just a smooth ride........

Tukija kwenye hoja za Mkjj especially a,b,c ni kweli CHADEMA needs to come out or stay silent foreva. The way CHADEMA played their political game ni kwamba walituaminisha kwamba wako chimbo wakiandaa dossier yenye vithibitisho visivyopingika kuhusu ni namna gani uchaguzi ulivyoibiwa na kumpa JK ushindi. As such the masses have been in the waiting mode for just too long! Patience is running out and CHADEMA is not updating anyhow on the proceedings ya maandalizi ya dossier yao. Kuna ombwe flani na linakuwa fulfilled na uzushi (Unofficial statements from media). Hivyo basi CDM should possibly do the following, tofauti kidogo na hoja ya mkjj (tough love).

1. Waje na uthibitisho wa kisayansi kuhusu ni namna gani kura ziliibiwa na kupelekea JK kuwa mshindi though illegitimately.

2. Wakae kimya, kimya tena kimya.

3. Steal the show and change the tune from the media na wabaya wao ambao wako busy kupotray chadema kuna bonge la mgogoro unaoweza kukipasua CHAMA. Jus do something else inayoattract attention naturally.

4. Only a spokesperson kama yupo (kama hayupo ateuliwe/achaguliwe mara moja) should be in contact with the media.

5. CDM leadership should now be more strongly united than eva and find a way of making the wananchi undesrstand they are. Ikiwezekana at this particular moment badala ya kumuadhibu say Zitto promote him. Politically they can easily get away of mgogoro hata kama upo kweli kwamba ni mbinu ya CCM. Wananchi have seen that before and can alwayz understand and believe.
 
Labda hayo ndiyo matokeo ya taarifa hii ya Kubenea


Usalama wa Taifa wavamia CHADEMA

By Saed Kubenea
Created 08/12/2010 - 00:00
218


Headline


zoka_218.jpg



VIGOGO kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wametajwa "kuingilia" Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), MwanaHALISI limegundua.
Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya idara hiyo zinaeleza kuwa vigogo hao wana mahusiano ya karibu na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe.
Anayetajwa rasmi kuwa na mahusiano na Zitto ni Naibu Mkurugenzi wa TISS, Jack Zoka.
Kufichuka kwa taarifa za kuwapo "uswahiba" kati ya Zoka na Zitto kumekuja katika kipindi ambacho CHADEMA kimekuwa kikituhumu maofisa wa juu wa usalama wa taifa kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita.
Aidha, kuibuka kwa tuhuma hizi kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa mbalimbali za mawasiliano kati ya Zitto na Rais Jakaya Kikwete.
Baadhi ya mawasiliano hayo, ambayo Zitto ameyapeleka kwa rais, aliyapeleka pia kwa baadhi ya watuhumiwa ufisadi nchini.
Kwa mujibu wa mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete; viongozi wa TISS walihusika, kwa kiasi kikubwa, katika kile alichoita, "Kuchakachua matokeo ya uchaguzi."
MwanaHALISI limefanikiwa kupata rekodi ya mshororo wa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka.
Kuna mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini na TISS, hasa Zoka.

Nyaraka za mawasiliano zinaonyesha kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana na naibu mtendaji mkuu wa TISS huyo zaidi ya mara tatu kwa siku.
Kwa mfano, Zitto na Zoka walifanya mawasiliano ya simu mara tisa hapo tarehe 8 Agosti. Simu iliyotumika katika mawasilino hayo, ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754787550 ambayo hutumiwa na Zoka.
Wakati mawasiliano hayo yanafanyika, Zitto alikuwa katika maeneo tofauti.
Mawasiliano ya kwanza kati ya Zitto na Zoka yalipokuwa yanafanyika, simu ya Zitto ilisomeka kuwa alikuwa katika maeneo mbalimbali.
Mathalani, wakati mwingine simu ilikuwa ikisomeka kuwa yuko Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, Kigoma Urban (Mjini), Kigoma Rural (Vijijini), Mtwara, Uwanja wa ndege-Ilala, Oyster Bay, Ukonga, Upanga na katikati ya mji.
Gazeti hili halikuweza kugundua mara moja undani wa mawasiliano ya Zitto na Zoka.
Kinachofanya baadhi ya wachunguzi wa mambo kujenga shaka ni kwamba mmoja ni mwanasiasa, tena kutoka chama kilichopo nje ya utawala; na mwingine ni mtumishi wa idara ya usalama inayolalamikiwa kukandamiza upinzani nchini.
Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka yalianza kupamba moto kuanzia tarehe 6 Agosti 2010, siku moja baada ya CHADEMA kuzindua kampeni zake za urais.
Kulingana na uchunguzi, siku hiyo, tarehe 6 Agosti, simu ya Zitto ilisomeka kuwa yuko Kigoma Urban.
Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni, CHADEMA kupitia kada wake mashuhuri, Mabere Marando, iliibuka na lundo la tuhuma dhidi ya vigogo kadhaa wa serikali, CCM na idara ya usalama wa taifa.
Akizungumza na maelfu ya wananchi katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, Marando alisema wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT), ulifanywa na serikali na washirika wake.
Miongoni mwa vigogo aliodai kuwa walihusika kufanikisha wizi huo, ni rais wa sasa, Jakaya Kikwete, rais mstaafu Benjamin Mkapa, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Edward Lowassa.
Akiongea kwa kujiamini, Marando alisema, "fedha za EPA ni wizi uliotiwa baraka na serikali ya CCM na ndio uliomsaidia rais Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005."
Kuanzia hapo hadi sasa, Zitto na Zoka wamekuwa na mawasilino ya mara kwa mara, na karibu kila siku huzungumza kwa simu.
Mawasiliano mengine ya mara kwa mara yalifanyika tarehe 7 Agosti 2010, siku mbili tangu hotuba kali ya Jangwani. Yalianza saa 10:17 na kuendelea tena saa 10:50, saa 10:51:31, saa 11:46:13, saa 12: 14:46, saa 12:26:48 na saa 13:50: 21.
Lakini Zitto alipoulizwa kuhusu sababu ya yeye kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na vigogo wa TISS, alisema hajui na hakumbuki lolote kuhusu kuwapo mawasiliano hayo na Zoka au mkuu yeyote wa idara hiyo.

Zitto amesema yeye, akiwa mwanasiasa na kiongozi, anazungumza na watu wengi kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali ndani na nje ya nchi, lakini hajui kitu kuhusu usalama wa taifa.

Alipobanwa kuhusu mazungumzo yake na Zoka, hasa yale ya 3 Novemba 2010, saa nne na dakika 56 asubuhi, siku mbili baada ya uchaguzi kumalizika, Zitto alisema, "Siku hiyo nilizungumza na watu wengi sana. Siwakumbuki ni akina nani hasa."
Alisema, "Hicho ndicho kipindi ambacho matokeo ya uchaguzi nchini kote yalikuwa yakizuiwa ikiwamo kwetu Kigoma. Na ukumbuke mimi nilipigwa mabomu na polisi na usalama wa taifa. Nakumbuka viongozi wengi wa vyombo vya ulinzi na usalama walinipigia simu kunijulia hali na kupata taarifa ya kilichotokea," anaeleza.

"Sasa kama Zoka naye alinipigia siku hiyo sikumbuki; lakini nilipigiwa na wengi…Naomba uniambie kitu, hivi mnachokitafuta hasa ni nini?" aliuliza.
Katika njia ya kujitetea, Zitto aliuliza, "Mwanasiasa kuongea na wakuu wa vyombo vya usalama ni kosa? Maana, hata kama ningekuwa nimezungumza naye, kosa langu liko wapi?" alieleza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini.

Alipoelezwa kuwa haoni hiyo ni hujuma dhidi ya chama chake kwa kuzungumza na viongozi wa TISS na kile ambacho amekuwa akikizungumza kikiwa hakifahamiki kwa viongozi wake, Zitto alisema, "Sijawahi kukihujumu chama changu mahali popote, siku yoyote."

Jitihada za gazeti hili kuzungumza na Zoka hazikufanikiwa katika kipindi chote
cha mwishoni mwa wiki, kwa vile kila alipopigiwa, simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi.

Hata ujumbe mfupi wa maneno uliotumwa kwenye simu yake saa 2:53 asubuhi ya Jumapili; ukieleza sababu za gazeti kuzungumza naye, haukujibiwa.

Aidha, tarehe 2 Novemba, siku moja baada ya kuzungumza na Zitto, Zoka alinukuliwa akikana madai ya Dk. Slaa, kuwa TISS imesaidia kuvuruga uchaguzi.
Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Zoka alisema, "Dk. Slaa amekuwa akidanganywa na watu wanaojiita maofisa wa usalama wa taifa."
Hata hivyo, kuna meseji mbalimbali kuhusu udini na uamuzi wa CHADEMA kususia hotuba ya rais Kikwete ambazo zilitumwa na Zitto kwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA ambazo zinadaiwa kuandaliwa na idara ya usalama wataifa.
Ujumbe huo unadaiwa kuandaliwa kwa ustadi mkubwa katika kukuza suala la udini na kuleta mtafaruki katika chama.
 
We have lost the "free and fair" argument. Period.

mkuu i know you are so desperate right now, but plse ebu kaa chini kidogo, kidogo tu tuongee, Remove all doughts you have, why?? ujue mafisadi
wanajipenyeza saaana kuivuruga CDM, sasa tukianza diversions we will be weak, when things get tough & the tough get going, CDM we are tough, at the end tutashinda
plse i beg you mkuu, mafisadi hii ndio njama zao, but CDM leaders wanajua sana, hata ww shahidi the way they use their media to popularize lies against CDM na pesa na nk, don't go. don't go,hold on, tutapata Katiba mpya, NEC huru, although wamemtambua JK hata mm imeniuma, come down mkuu, najua unahasira leo, just relax buddy, we are going ahead usijali bana, relax MMM
 
I wonder if there's any purely democratic country under the sun.

U r right, no one, watu wakijua hili hawata kata tamaa, CDM twende mbele, na uzuri zaidi Mnyika yupo hapa he answers our questions, rumors or doughts directly, magazeti mengi ni ya mafisadi, so JJ anajibu hapa wazi which is best, MMM calm down, kanyaga twende mkuu
 
Issue kwa chadema sio kuomba radhi bali kujitathimini na kujipanga vizuri kwa hatua itakayofuatia. Ukizingatia ndani ya wabunge wa chadema kulikuwa na mgawanyiko katika kufikia maamuzi ya pamoja, maana kuna waliokuwa wanaunga mkono kutomtambua jk na wengine hawaungi mkono ijapokuwa suala lenyewe. la kumsusia jk lilifikiwa kwa mfumo wa demokrasia ya wengi wape hata hivyo ilianyiwa vurugu na ubinafsi wa baadhi yao. Hivyo cc ya chadema inastahili kupongezwa kwa maamuzi iliyofikia ya kutoka na azimio la kumtambua jk kwani waligundua vita inayowakabili ktk msimamo wao haipo tu kwa ccm bali pia kwa baazi ya askari wao wenyewe. Hivyo walichokifanya ni kurudisha majeshi nyuma kwa ajili ya kujipanga upya na kuwanoa askari wake(wabunge) kwamba vita ikiisha amuliwa kupiganwa askari atakaeonyesha dalili za kurudi nyuma dawa yake ni risasi. Chadema wasingekuwa watu wa mikakati na uwezo wa kungamua, katika hili wangeshindwa vibaya sana maana ccm ilikuwa tayari ishajipatia mamluki ndani ya chadema kuweza kupiga ndani na nje. Chadema tupo pamoja na raha yenu ni yetu na shida yenu ni yetu pia. Sababu ya kuomba radhi haipo maana ss raia tuliona hujuma ya wazi jinsi ilivyokuwa ikifanywa na nec hasa kwenye yale majimbo ambayo wapinzani walionekana kushinda.
 
Back
Top Bottom