Hapa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa tu!
Ila, inasikitisha na kushangaza kuona watu ambao pengine mtu ungedhani wana uelewa flani hivi, wakiunga mkono uminywaji wa civil liberties, ambao upo dhahiri kabisa.
Wengine wanaunga mkono udhalimu huo kwa sababu tu hawampendi huyo Idris, au kwa sababu eti wanaona si mchekeshaji mzuri.
Mambo ambayo ni irrelevant kabisa.
Awe mchekeshaji mzuri au mbaya, awe bishoo au msela, au awe chochote au vyovyote vile, hayo hayahusiki kabisa.
Safari ya Tanzania ni ndefu sana na nachelea kusema kuwa Watanzania wenyewe ndo kikwazo....
Nimeelezea hapo juu tatizo la kutenganisha dhana na watu.
Hili ni tatizo kubwa sana.
Kuna mtu anapenda kuona Idris ananyanyaswa hivi, lakini hapendi kuona Kipanya akinyanyaswa.
Hajui kwamba kimsingi ukishakubali Idris anyanyaswe hivi, umekubali si tu Kipanya, bali pia waandishi, cartoonists, comedians na hata wachangiaji wa JF, wanyanyaswe hivi hivi.
Kwa sababu, kama issue ni kumdhalilisha rais, basi JF itabidi ifungiwe.
Kwa sababu kuna watu kila siku tunamnanga Magufuli kwa namna ambayo inaweza kuitwa tunamdhalilisha.
Haipiti wiki hapa sijaandika "Magufuli is a country bumpkin".
Na uongozi wa JF hauwezi kudhibiti hili, kwa sababu kuna watu wengi sana wana machungu na Magufuli.
Sasa hilo maana yake nini?
JF ifungwe ili watu wasipate pahali pa kumdhalilisha rais?
Na unajua watu wanaofungwa mdomo wanafanya nini?
Inakuwa kama una pressure cook something halafu hufungui ufuniko, unaweza kutengeneza bomu likapasuka.
Nchi zilizoendelea kiuchumi si wajinga kuachia uhuru wa kujieleza. Unawasaidia wananchi na serikali.
Nchi ambayo ina some semblance ya uhuru wa kujieleza, watu wanakuwa wanajiachia. Mtu anafanya uhalifu, halafu anapiga picha na hela za uhalifu Facebook. Askari uchunguzi wao unaishia Facebook tu.
Nchi ambayo imebana uhuru, hata kazi ya askari inakuwa ngumu. Watu wamejawa woga. Wanapanga na kufanya uhalifu kwa siri sana. Next thing you know, mapinduzi ya damu!
Kwa hiyo, hawa wenzetu Wamarekani na Waingereza kuachia uhuru wa kujieleza si wajinga.
Serikali inajua hata ikibana watu, watu wana sehemu ya kwenda kutoa steam zao kwenye internet, watapiga kelele wapunguze machungu.
Sisi watu wanabanwa, wakitaka kupunguza machungu kwa kucheka wanafungwa.
Serikali inatafuta watu ubaya hapo.