Idris Sultan atimiza siku 7 Rumande

Hayati Mzee Moi alikuwa mkali sana,ila kuna lijamaa lilikuwa likimwigiza sana,alikuwa anacheka sana jamaa alivyokuwa anamuigiza...
Ina maana alikuwa easy kwa utani 😂😂😂 ila kuna watu wako serious hawatakagi mazoea. Hao ndio wa kuwa nao makini.
 
Mwache aendelee kukaa rumande mpaka akili itakapomkaa sawa. Mtu kipaji hana ana kazi ya kujifanya Mockingbird tu.

Yeye kila tukio analigeuza mzaha ili afurahishe vi slay queen vinavyo mfollow huko insta.
Huyo dogo ni zaidi ya boya. Nilivyoiona ile video aliyoifanya nilishangaa sana.
Aendelee kunyea "debe" mpaka akili imkae sawa.
 
Idadi ya watu wanaosapoti mtu kua rumande kisa picha kuchekwa is very alarming it's like kuna kikao ambacho sikuhudhuria na tulikubaliana kua hakuna kuchekana.

Sasa nashindwa kuelewa. Ni ile wivu wetu wa wabongo kua jamaa ana hao slay queen kukuzidi au ni hicho kikao ndiyo kinamhukumu huyu jamaa.
Mimi binafsi wala simuonei wivu, ila naona alichofanya ni upuuzi. Aendelee kupata malipo ya upuuzi alioufanya.
 
Ni kweli na ningesikitika iwapo ingekuwa imemkuta Masoud Kipanya but sio kwa huyo dogo anaejiona mjanja kwa kufanya upuuzi mtandaoni na kujiona ati ni msanii wa Comedy.

Magufuli sio Billnass!!!
Tauche kuangalia suala hili kwa kuangalia watu, taungalie dhana.

Moja ya matatizo makubwa ya siasa za Afrika ni kuangalia watu badala ya kuangalia dhana.

Kimsingi hapa, huna hoja ya kidhana ya kumtosa Idris na kumtetea Kipanya.

Kwa sababu, ukishaweka upenyo wa Idris kunyanyaswa kwa minajili ya kumdhalilisha rais, umeshaweka upenyo kwa Kipanya kunyanyaswa kwa minajili ile ile.

Kuna haki za msingi za kikatiba za uhuru wa watu kujieleza zinavunjwa hapa, hili si suala la Idris tu.

Ni suala la haki za kikatiba kuvunjwa.
 
Ile picha kila mtu aliyeiona alikuwa akiicheka kimyakimya, chumbani kwake. Idriss went too far ukichukulia pia alishaingia matatani kabla.

Japo anaweza asifungwe kwa kuwa watashindwa kusema wanamshtaki kwa kosa gani haswa, ila watamtesa sana na huenda wakamharibia hata deals zake nyingine
 
Ni ujinga na umasikini tu.

Comedians wa Marekani kila wiki wanamkong'ota Trump wanavyotaka.Na hakuna anayefungwa kwa ujinga wa kumdhalilisha rais.

Yani huku comedians wasipomkong'ota rais, huyo rais watu watahoji kama ni rais kweli au ni robot. Ataonekana hawezi kazi, kashindwa kutoa ajira kwa comedians.

Itaonekana comedians hawajamkubali kwamba ni rais, wamemsusia.

Tena White House ya Marekani huwa inapanga siku moja maalum inaitwa "White House Correpondents Dinner". Inakuwa bonge la party, wanaalikwa waandishi wa habari wa kila aina, wanaalikwa celebrities wa kila aina. Anakuwepo comedian mmoja anakuwa kama MC.

Anamnanga rais vibaya vibaya. Mpaka rais naye anajitupia vijembe yeye mwenyewe.Watu wanacheka, kuanzia rais mpaka waandishi wa habari.

Na nchi nzima tunaangalia kwenye TV, live. Watu wanaishi kwa uhuru wa kujua kwamba, rais naye ni mtu tu. Si Mungu mtu.

Hawa watu wanajua ku take it easy. Rais si Mungu, ni mtu tu naye.

Kitendo cha comedians kupata cha kumzodoa rais ni sifa ya rais kuweza kutengeneza ajira.

Sasa Magufuli ana sifa hii ya kuweza kutengeneza ajira kwa vijana, vijana wanajiajiri kwa mgongo wa Magufuli, wanafungwa!

Wanaonewa tu.

Uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi ya kikatiba Tanzania.
 
Mchekeshaji na mwanamitindo maarufu nchini Idris Sultan ameendelea kusota rumande kwa siku saba kutokana na makosa ya kimtandao. Idris aliitwa kuhojiwa na jeshi la Polisi toka may 19, 2020 ambapo anashikiliwa hadi leo.

Sheria zinasemaje kwa mtuhimiwa? Ana haki zake nae pamoja na kutuhumiwa.
#KatibaNiYetu

View attachment 1459884
Huyu Dogo ataitoa kimaso maso sanaa ya ucheshi Tanzania. Anachokipitia kinaweza kuchukuliwa kama chagizo la kulitizama upya swala na Sheria ya mtandaoni na au matumizi ya picha ya nambari uno.

NB
Ikumbukwe kwamba ni kosa pia kisheria kutumia kitambaa cha bendera ya Taifa Kama kitambaa cha kufutia jasho au kamasi. Sheria hizi inabidi zitizamwe upya.
 
Ni ujinga na umasikini tu.

Comedians wa Marekani kila wiki wanamkong'ota Trump wanavyotaka.Na hakuna anayefungwa kwa ujinga wa kumdhalilisha rais.

Yani huku comedians wasipomkong'ota rais, huyo rais watu watahoji kama ni rais kweli au ni robot. Ataonekana hawezi kazi, kashindwa kutoa ajira kwa comedians.

Itaonekana comedians hawajamkubali kwamba ni rais, wamemsusia.

Tena White House ya Marekani huwa inapanga siku moja maalum inaitwa "White House Correpondents Dinner". Inakuwa bonge la party, wanaalikwa waandishi wa habari wa kila aina, wanaalikwa celebrities wa kila aina. Anakuwepo comedian mmoja anakuwa kama MC.

Anamnanga rais vibaya vibaya. Mpaka rais naye anajitupia vijembe yeye mwenyewe.Watu wanacheka, kuanzia rais mpaka waandishi wa habari.

Na nchi nzima tunaangalia kwenye TV, live. Watu wanaishi kwa uhuru wa kujua kwamba, rais naye ni mtu tu. Si Mungu mtu.

Hawa watu wanajua ku take it easy. Rais si Mungu, ni mtu tu naye.

Kitendo cha comedians kupata cha kumzodoa rais ni sifa ya rais kuweza kutengeneza ajira.

Sasa Magufuli ana sifa hii ya kuweza kutengeneza ajira kwa vijana, vijana wanajiajiri kwa mgongo wa Magufuli, wanafungwa!

Wanaonewa tu.

Uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi ya kikatiba Tanzania.

Hapa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa tu!

Ila, inasikitisha na kushangaza kuona watu ambao pengine mtu ungedhani wana uelewa flani hivi, wakiunga mkono uminywaji wa civil liberties, ambao upo dhahiri kabisa.

Wengine wanaunga mkono udhalimu huo kwa sababu tu hawampendi huyo Idris, au kwa sababu eti wanaona si mchekeshaji mzuri.

Mambo ambayo ni irrelevant kabisa.

Awe mchekeshaji mzuri au mbaya, awe bishoo au msela, au awe chochote au vyovyote vile, hayo hayahusiki kabisa.

Safari ya Tanzania ni ndefu sana na nachelea kusema kuwa Watanzania wenyewe ndo kikwazo....
 
Comedians wa Marekani kila wiki wanamkong'ota Trump wanavyotaka.
Bahati mbaya sana Tanzania na Marekani kwenye issues za freedom of speech/expression na mambo mengine mengi tu hatupo sawa. Sisi sio comedians tu, hata ile mihimili mingine (Bunge na Mahakama) inapokea order kutoka kwa Jiwe. Jiwe akimwambia Waziri wa Afya vua mask, anavua haraka etc etc. Comedians wetu wakidhani wapo USA wataumia. It is sad but ndio reality kwa sasa
 
Hapa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa tu!

Ila, inasikitisha na kushangaza kuona watu ambao pengine mtu ungedhani wana uelewa flani hivi, wakiunga mkono uminywaji wa civil liberties, ambao upo dhahiri kabisa.

Wengine wanaunga mkono udhalimu huo kwa sababu tu hawampendi huyo Idris, au kwa sababu eti wanaona si mchekeshaji mzuri.

Mambo ambayo ni irrelevant kabisa.

Awe mchekeshaji mzuri au mbaya, awe bishoo au msela, au awe chochote au vyovyote vile, hayo hayahusiki kabisa.

Safari ya Tanzania ni ndefu sana na nachelea kusema kuwa Watanzania wenyewe ndo kikwazo....
Nimeelezea hapo juu tatizo la kutenganisha dhana na watu.

Hili ni tatizo kubwa sana.

Kuna mtu anapenda kuona Idris ananyanyaswa hivi, lakini hapendi kuona Kipanya akinyanyaswa.

Hajui kwamba kimsingi ukishakubali Idris anyanyaswe hivi, umekubali si tu Kipanya, bali pia waandishi, cartoonists, comedians na hata wachangiaji wa JF, wanyanyaswe hivi hivi.

Kwa sababu, kama issue ni kumdhalilisha rais, basi JF itabidi ifungiwe.

Kwa sababu kuna watu kila siku tunamnanga Magufuli kwa namna ambayo inaweza kuitwa tunamdhalilisha.

Haipiti wiki hapa sijaandika "Magufuli is a country bumpkin".

Na uongozi wa JF hauwezi kudhibiti hili, kwa sababu kuna watu wengi sana wana machungu na Magufuli.

Sasa hilo maana yake nini?

JF ifungwe ili watu wasipate pahali pa kumdhalilisha rais?

Na unajua watu wanaofungwa mdomo wanafanya nini?

Inakuwa kama una pressure cook something halafu hufungui ufuniko, unaweza kutengeneza bomu likapasuka.

Nchi zilizoendelea kiuchumi si wajinga kuachia uhuru wa kujieleza. Unawasaidia wananchi na serikali.

Nchi ambayo ina some semblance ya uhuru wa kujieleza, watu wanakuwa wanajiachia. Mtu anafanya uhalifu, halafu anapiga picha na hela za uhalifu Facebook. Askari uchunguzi wao unaishia Facebook tu.

Nchi ambayo imebana uhuru, hata kazi ya askari inakuwa ngumu. Watu wamejawa woga. Wanapanga na kufanya uhalifu kwa siri sana. Next thing you know, mapinduzi ya damu!

Kwa hiyo, hawa wenzetu Wamarekani na Waingereza kuachia uhuru wa kujieleza si wajinga.

Serikali inajua hata ikibana watu, watu wana sehemu ya kwenda kutoa steam zao kwenye internet, watapiga kelele wapunguze machungu.

Sisi watu wanabanwa, wakitaka kupunguza machungu kwa kucheka wanafungwa.

Serikali inatafuta watu ubaya hapo.
 
Bahati mbaya sana Tanzania na Marekani kwenye issues za freedom of speech/expression na mambo mengine mengi tu hatupo sawa. Sisi sio comedians tu, hata ile mihimili mingine (Bunge na Mahakama) inapokea order kutoka kwa Jiwe. Jiwe akimwambia Waziri wa Afya vua mask, anavua haraka etc etc. Comedians wetu wakidhani wapo USA wataumia. It is sad but ndio reality kwa sasa

Pascal Mayalla alimuuliza Magufuli kuhusu checks and balances, Magufuli akamjibu kwamba kuna mhimili mmoja umechimbiwa chini zaidi.

Kuna trick hua Jpm anaitumia kukwepa baadhi ya maswali kuyatolea majibu ya moja kwa moja.

Hamna kitu amejibu kutokea swali la msingi hadi swali dogo!
Umemsikiliza jpm kwa makini hapo?
Serikali inayoshikilia dola ni ile yenye mamlaka juu ya pesa.
Hio miamala mingine ni dummy tu.
 
Huyo jamaa akae tu huko hata mwaka mzima, anaonekana ana mambo ya kitoto pamoja na umaarufu wake.... Kubwa jinga hilo.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom