Ukae ukijua wakimalizana na huyo wanakuja kukushukia wewe.
Mpaka upige magoti na kukiri Magufuli ni Bwana!
Sent from my typewriter using Tapatalk
Mkuu Kiranga, unaeleweka sana hoja yako.
Na pia umetoa mifano mbalimbali kutanabaisha hoja yako.
Lakini Idris amechukua picha ya mheshimiwa halafu akaifanyia editing (maana original yamwonyesha akiwa na watu wengine wawili).
Lengo ni kuonyesha jinsi mheshimiwa alivyokuwa hafahamu namna ya kushona au kuchagua aina ya suti za kuvaa.
Na hiyo kwenye nedia itasambaa kwa kasi kubwa na imefanya hivyo.
Sasa hiyo ni dhihaka na kejeli kwa raisi na kama binadamu akaiona hiyo picha na kuambiwa imesambaa nchi nzima na nje ya mipaka, wewe wadhani angefanyaje aipuuze tu kwa kuzingatia alikwishapuuzia mzaha mwingine ulofanywa na Idriss?
Raisi Magufuli ameachia media ifanye kila inachotaka na ndo maana hata wewe waweza kusomwa maoni yako Tanzania.
Ila kwa mazingira ya sasa ya nchi hayaruhusu aina hiyo ya dihaka kwa kiongozi wa nchi, maana shida zilizopo halafu ukachanganya na mizaha isiyotarajiwa, matokeo yake ni hayo tunayoyaona.
Hao ulowaona huko Ikulu ya White House wakidine pamoja na Donald Trump wengine ni rafiki zake, jamaa na watu ambao ni Circle ya utawala wa Marekani hivyo wanaweza kutaniana na kusemeana kejeli watakavyo.
Mwisho, hao wote uwasemao wameshiba na wana kipato wana kila kitu, hivyo kwa Tanzania tungoje watu washibe na kisha wawe na uwezo wa kufanya shows kwenye runinga na watu wacheke.
Hata simba akishiba si waweza kumpita tu uende zako?
Kinachotakiwa ni hao watu kwa Tanzania kuanza kumzoesha raisi na viongozi juu ya maazimio yao ya kuweka vipndi vya namna hivyo au hata kutoa angalizo in advance kwa Mr Msigwa ili kuona kwamba hakutakuwa na problem endapo picha itakuwa edited halafu kuwekwa ili ifanyiwe dhihaka.