Mbeya: Wanachama 7 wa CHADEMA walioswekwa Rumande waachiwa huru

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,696
218,215
Wanachama Saba wa Chadema wa Mkoani Songwe waliobambikiwa Makosa ya uongo wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020, yaliyotengenezwa kinafiki na watu waoga walioshindwa hoja za majukwaani, na kurundikwa Jela kwa uonevu KWA MUDA WA ZAIDI YA MIEZI 18, Leo wameachiwa huru kutoka Jela na Mahakama Kuu kanda ya Mbeya, BAADA YA SERIKALI KUTOKUWA NA NIA YA KUENDELEA NA KESI HIYO.

Unyama kama huu wa kishamba wametendewa Viongozi na Wanachama wengi wa Chadema Nchi mzima, hasa baada ya serikali ya awamu ya 5 kushindwa kabisa kujibu HOJA NZITO ZA CHADEMA kwenye Majukwaa ya kisiasa , ndipo wakaamua kutumia Jeshi la Polisi chini ya Simon Sirro kuwakomesha wanachama wa Chadema.

Bali sisi kama tulivyosema siku zote, na Tunarudia tena kusisitiza kwamba KILA UBAYA UTALIPWA TU.

Mungu ibariki Chadema
 
Wanachama Saba wa Chadema wa Mkoani Songwe waliobambikiwa Makosa ya uongo wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 , yaliyotengenezwa kinafiki na watu waoga walioshindwa hoja za majukwaani...
Watanzania tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa lile alilotufanyia tarehe 17 03 2021. Yule hayawani alikuwa anaenda kuiangamiza kabisa nchi yetu

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom