Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International limeitaka Tanzania kuachana na mashtaka dhidi ya mchekeshaji maarufu nchini humo Idris Sultan
Idris anatarajiwa kufika mahakamani kesho tarehe 9 mwezi Julai, kujibu mashtaka ya ''kushindwa kusajili kadi ya simu ambayo awali ilikuwa ikilimilikiwa na mtu mwingine'' na kushindwa kuripoti umiliki wa kadi ya simu''.
Idris alikamatwa mwezi Mei baada ya video iliomuonesha akicheka huku akiitazama picha ya zamani ya rais wa Tanzania John Magufuli, kusambaa mitandaoni.
Baada ya kushikiliwa na polisi kwa zaidi ya wiki moja Sultan alifikishwa katika mahakama ya Kisutu na kusomewa shitaka la kutosajili nambari ya simu aliyokuwa anaitumia ambayo imesajiliwa kwa jina la mtu mwingine.
Anayetajwa kusajili laini hiyo, Innocent Maiga pia alishtakiwa pamoja na Bw Sultan kwa kosa la kutoarifu mabadiliko ya umiliki wa laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake.
Msanii huyo aliachiwa kwa dhamana baada ya watu wawili kusaini bondi ya Shilingi za Tanzania milioni 15 kila mmoja, wakili wake Bennedict Ishabakaki aliieleza BBC.
Wawili hao wanatuhumiwa kufanya makossa hayo kinyume cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektoniki na Posta, na endapo watakutwa na hatia watakabiliana na adhabu ya faini isiyopungua Shilingi milioni tano, ama kifungo kisichopungua miezi 12 ama vyote faini na kifungo.
Mkurugenzi wa Amnesty International wa kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Deprose Muchena alisema:
''Ni ushahidi kwamba mamlaka nchini Tanzania hazina kesi dhidi ya Idris Sultan na wako tu wanamnyanyasa kwasababu uchekeshaji wake umewakwaza. Mahakama lazima ifute mashtaka yaliyobuniwa kupata sababu dhidi yake''.
Kabla ya kufikishwa mahakamani, polisi na wakili wa msanii huyo waliiambia BBC kuwa alikuwa pia akihojiwa kwa tuhuma za kutenda makosa ya kimtandao.
Wakili Ishabakaki pia aliiambia BBC kuwa mteja wake alikamatwa na kuhojiwa na polisi juu ya mkanda wa video uliosambaa mitandaoni hivi karibuni akionekana akiicheka picha ya zamani ya rais Magufuli.
Hata hivyo, hakufunguliwa mashtaka yoyote kuhusiana na suala hilo.