Tiss haina tatizo katika hili, bali tatizo ni uchakavu wa nyaya au kuna nati zilizolegea ndani ya vichwa vya viongozi wao. Hivyo siyo vyema kuilaumu idara nzima kwa upuuzi wa viongozi chakavu, wenye mawazo mgando na wasioenda na wakati. Upuuzi kama huu ndiyo ulipelekeaga KGB ikavunjwa.
Upuuzi wa Tiss
1. Mbali na jaribio la kitoto la kutaka kupata information kutoka kwa ulimboka kwa kum'tocha, hali ya kuwa kuna teknolojia nyepesi ipo mitaani, ya kukamata mawasiliano ya simu, email n.k, inaonyesha udhaifu uliopitiliza wa idara, ama aliyeongoza hiyo operation.
2. Kashfa ya pili ya aibu na fedheha, ni kwa Tiss kuwa exposed dhahiri shahiri kwa ushiriki katika kumteka na kumtesa Ulimboka, tena kwa njia zinazokinzana na haki za binaadamu duniani.
3. Agent wa intelijensia huwa ni vigumu kutambuliwa, hivyo basi, nia aibu kubwa sana kwa Tiss kwa agents wake kutambuliwa na kuanikwa wazi kiasi hiki kwa jamii. Nchi zilizoendelea, mkurugenzi wa intelijensia angekuwa ameshapigwa chini. Hali ambayo ina hatarisha usalama wa familia zao kitaani.....!
4. Kuonnyesha Ukilaza, na hali ya kupeana kazi ndani ya Tiss kwa watu wasio na uwezo wala sifa, inakuwaje agents watumie simu zao binafsi katika operation za idara?!!
5. Ukanushaji wa kitoto usio na mashiko, ukizingatia kauli nyingi za Zoka (Human Resouce) wa TISS za kukimbila mahakamani kila idara inapotajwa, lakini kwa hili zito, idara imetoa SMS tu.....what a shame...?!
6. Na hata andiko lenu linasema tu kuwa MwanaHALISI imeunganisha tu baadhi ya mambo, lakini idara haijatoa kasoro wapi KUBENEA amedanganya kwa majina ya wahusika, ama namba zao za simu, ama mida ya simu hizo zilipoyumika, wala hata kukanusha kuwa hao waliotajwa ni waajiriwa wa Tiss.
Kwa hali hii, tutaibiwa Twiga wote.......!
Kibanga Msese