Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Status
Not open for further replies.
Usalama wa taifa unakuwa na majibu rojo kiasi hikii? Yaani huu ndiyo mwisho wao wa kufikiri? Yaani kweli wanategemea wananchi waamini tamko dhaifu kiasi hiki? Kama ndiyo huu tuliobaki nao basi hatunao. Maana sasa tunaona wazi sababu wanyama wanarushwa nje ya nchi bila hata woga. Ndege za kijeshi za nchi za mbali zinakuja kutua na kupakia na kuondoka! Loh!. Heilikopta tunasikia zinatua migodini na kuondoka na dhahabu wakiwa wameandikisha robo tu ya shehena iliyomo ndani, mpo tuu! Hivi hii idara inaundwaje na kwa maslahi ya nani?
 
Jamaa hawana busara kabisa usishangae kesho wakaibuka na ushauri wako hawana mshauri.wanalinda kikundi si taifa
 
jamani intelijensia!!!!.... intelijensia!!!!.... intelijensia!!!!....uhhhhhiiiiiiiiiiii, twafaaaaaaaa wako wanapanga jinsi ya kuwaua wakosoaji wa siri-kali, hawana mbinu mpaka mwanahalisi iwatafunie, hata kumeza hawawezi, wame wekana kwa kujuana tu, 2015 tutaifumua tuweke watu "inteligent"
 
Hii ni dharau kubwa sana. Yaani mnakaa kabisa kwenye mikutano yenu huko kwenye ofisi zenu na kuamua kutoa taarifa kama hiii! Shame on you ! Hamna hata mtu mwenye upeo kidorgo akawapa jicho la nje.

Kanusheni basi kama huyo "Rama" sio mfanyakazi wa idara na hizo details sio zake kama mnaweza!
 
Hata mimi nilitegemea wangekuja na taarifa za kina zenyekujieleza.

Kama wakitaka kukanusha tukawaelewa waanze kubainisha kuanzia yule Abeid/David/Rama, halafu ije Kova na yule Mkenya wa Mchungaji Gwajima,

Then ndiyo waje hizi series za simu zinazoshahabiana na tukio zima la Dr.Ulimboka. Kutuambia tupuuze tu wakati tupo njia panda haitakuwa kitu rahisi hivyo.
 
Yani hii idara kweli inanichosha, hata ukanushaji bado wa kisanii maana wangejibu ki-professional kama vile kutoa ufafanunuzi wa eneo alilopelekwa Dr kuteswa kabla ya kupelekwa msitu wa mauaji, pia wangetoa ufafanuzi wa aliyekuwa akiwasiliana na Dr mara kwa mara kama ni mtumishi wa serikali haijalishi ni idara gani, gari walilotumia kama ni la idara au la, simu zilizotumika nk, halafu wangemalizia kwa kutuambia kuwa idara ya polisi inafanyia kazi wote wanaohisiwa..
 
Tamko dhaifu sana kama dhaifu mwenyewe. Aisee.....is that all you (uwt)can say??? Shame on you and whoever is behind it.
 
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamaba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visvyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.

TISS Mmeamua kuuza utumbo kwanini mnaogopa manzii?
 
Kama hii nayo imepikwa, basi upishi ni wa hali ya juu. Kuna mwandishi mmoja ktk kitabu chake anauliza, kama siyo kuhoji uwepo wa mungu. Anasema kama mungu yupo, kwa nini anaachia 'innocents' to suffer?

Kwanini ha-intervene ktk maendeleo kama haya?

Anamalizia kwa kusema, kama kweli God yupo, he is devastatingly biased in favour of the rich and the powerful nk. Philosophically, this is a logical and powerful reasoning, kiimani je??

Tuko hapo wanajf.
 
Naamini kuna watu wenye akili sana na kushauri vyema katika usalama wa Taifa, ila hawapewi nafasi. Nina uelewa mdogo, ila nimeona udhaifu mkubwa wa TISS kwa kipindi kirefu sasa, kuanzia uchaguzi 2010.
 
Tulimteka Ulimboka,..... aaahh hatukumteka!!.......Ni sisi tulimteka........Haiwezekani, hatukumteka...,Unajua tulimteka ,....Nooo, hatukumteka, hatukumteka tunakanusha...eeehh tunahusika....hatuhusiki wananchi puuzeni,....
 
Mi wapuuzi pekee kama waliotoa tamko ambao wanaweza kupuuza uchunguzi wa mwanahalisi, binafsi kwa jinsi uchambuzi ulivyowekwa wazi ngumu kupuuza.
 
ni matamko ya kipuuzi,tanzania ipo ktk hatua kubwa katika suala upashanaji habari,tanzania ya leo ni tofauti na ya miaka 5 nyuma,kutuletea ngonjera za kijinga wakati kila mtu anaelewa nini kilifanyika hata kabla ya mwanahalisi kutoa series ya matukio sasa gazeti limekuja kumalizia yote yaliyobaki,bora wanyamaze
 
TISS Mmeamua kuuza utumbo kwanini mnaogopa manzii?

Mnakumbuka watu wakishapata nafasi nyeti hasa vyeo vya juu serikalini wana tabia ya kushindana mbio ndefu kwenda kule miti mirefu Bwagamoyo. Dhana nzima ni kujikinga na hawa jamaa yasiwapate ya akina Mwakiembe, na mnyonge zaidi usiye na ulinzi kamili ndiyo unakutana na ya Dr. Ulimboka.
 
Tulimteka Ulimboka,..... aaahh hatukumteka!!.......Ni sisi tulimteka........Haiwezekani, hatukumteka...,Unajua tulimteka ,....Nooo, hatukumteka, hatukumteka tunakanusha...eeehh tunahusika....hatuhusiki wananchi puuzeni,....

Kanusho ni la juu juu tu, hawajajibu tuhuma zilizomo kuhusu akina Rama. Hapo ndipo unapoona wanasema no no no hatukumteka, na papo wanakubali yes yes tulihusika kwa kutokanusha uchanganuzi wa Mwanahalisi.
 
It could make sense if the press release could be denying that the so called Rama is not their official. Poor public relation here because of the belief that the public is ignorant. Gone are the days when this government section was the intelligence of the leadership.
 
mods mna maslahi gani na habari ya Mwanahalisi?
Mnamlinda nani na kwa maslahi ya nani?
Kwanini mnafuta habari ya kubenea wakati gazeti lipo tayari mtaani?

Nashukuru nimeshaisoma habari nzima na nimeicopy
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom