Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Status
Not open for further replies.
kama mwanahilisi wamedanganya basi wakawashitaki, wasipofanya hivyo shame on TISS
 
Tuwapuuze waandishi ila sio ukweli,sasa tutawapuuza kwa lipi? kwa tunakiamini ni ukweli,taarifa imewaumbua kwasababu iko detailed vya kutosha !
 
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamaba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visvyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.

TISS hivi risasi ikichomoka kwenye chemba yake unaweza kuirudisha?eti umegairi laaah asha utakachofanikiwa ni kuokota ganda la hiyo risasi na madhara yake.
 
unajua bora hata wangeongelea huyo Rama alitumwa nini na aliripoti nini ofcn baada ya Uli kutekwa
 
wamekana taarifa iliyoandikwa na mwanahalisi juu ya ushiriki wa TISS ktk kumteka na hatimaye kumtesa DR. Ulimboka

source;chanel 10

watuambie rama siyo mtumishi wao? Na wengine walioandikwa humo sio watumishi wao? Kwa nini waliwasiliana na dr uli sekunde chache kabla hajatekwa? Huyu rama si ndo aliyetajwa na lema kwamba anamfuatilia? Kama kawaida ya watu wa mabwepande, maswali magumu,majibu yake mepesi. Ndo maana tunasajili na wakimbizi na wahamiaji haramu wakijiita watanzania.
 
Ole wenu mlio ingia kwenye idara hyo kwa migongo ya kujuana,nyie ndie mnaopelekeshwa na wanasiasa...

Hilo kanusho la TISS Limekuja kumsafisha nani? Na ni nani mwandishi wa hilo tamko? maelezo ya Gazeti la Mwanahalisi wameelezea mpango mzima kuanzia May..nyie mmejibu kirahisi tu kuwa ni UZUSHI..Kama ni Uzushi mko tayari kumfungulia mashitaka Mhariri wa Gazeti hilo? au Tusome tupuuze...Mimi nilijua Wangekanusha Mstari kwa Mstari.,la kwanza lingekuwa Ni kutomtambua Ramadhani Ighondu lakini tuyapuuze.
 
wameshikwa pabaya sana hawa watu....inabidi watumie nguvu kubwa sana kujisafisha......

Kweli nakubaliana kwa idara hii nyeti kadiri ya uchunguzi ulioanikwa pale kwa Mwanahalisi wamefuliwa nguo na kubaki uchi kabisa mbele ya mkwe wao (wananchi). Mbaya zaidi kudadafuliwa hata taswira kamili ya watu najina, walikozaliwa, umri na nick names, namba zao za simu zilivyokuwa zinatumika kwa kuwasiliana na watu mbalimbali, ni aibu kwani hawajakanusha uchunguzi huo ila ni jibu la juu juu tu bila kujibu kuhusu wahusikam majina na namba za simu.
 
Mhkhh, nitamshangaa yeyote atakayedhani kuwa watu hawa watakubali kuwa wanahusika!!!!!
 
Kweli nakubaliana kwa idara hii nyeti kadiri ya uchunguzi ulioanikwa pale kwa Mwanahalisi wamefuliwa nguo na kubaki uchi kabisa mbele ya mkwe wao (wananchi). Mbaya zaidi kudadafuliwa hata taswira kamili ya watu najina, walikozaliwa, umri na nick names, namba zao za simu zilivyokuwa zinatumika kwa kuwasiliana na watu mbalimbali, ni aibu kwani hawajakanusha uchunguzi huo ila ni jibu la juu juu tu bila kujibu kuhusu wahusikam majina na namba za simu.

Mkuu unaweza ukatuwekea hiyo habari nzima, kwa siye ambao hatujafanikiwa kuisoma?
 
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamaba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visvyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.

kama hizo taarifa ni za uongo mbona wao wasizidharau badala yake wanajitokeza kukanusha?.....nadhani watanzania wa sasa si wale wa 1940s... taarifa hizo wanavujisha wenyewe kwa kuwa huenda wamegawanyika halafu wanakuja kutuambia siyo sahihi? mwisho wa ubaya ni aibu!!
 
Kweli hatavunjika moyo Pembeni kulia Amiri Mkuu wenu kushoto Liwalo na liwe huku nyuma Mkuchika.
Lazima Damu imwagike ili Ndoa yenu idumu au kuvunjika hatuna jinsi
 
Je, kuna viongozi waliopo madarakani kwa sasa ambao ni wana Uzalendo wa kweli?
 
Tuwapuuze waandishi ila sio ukweli,sasa tutawapuuza kwa lipi? kwa tunakiamini ni ukweli,taarifa imewaumbua kwasababu iko detailed vya kutosha !

Mkuu,,tafadhali mie sijabahatika kuiona Mwanahalisi na hiyo habari,unfortunately siwezi pata nakala yake na mtandaoni siku hizi hawaweki wale,,weka kipande hicho hapa mkuu nifaidi
 
Je, kuna viongozi waliopo madarakani kwa sasa ambao ni wana Uzalendo wa kweli?

6.jpg

Mwakiembe, ni mzalendo kuliko TISS na kanusurika kama Dr. Ulimboka na matokeo hata nywele hana, hivyo jibu kuhusu hao TISS analo Mwakiembe.
 
nchi hii sidhani kama kuna usalama wa taifa....wanyama wanatolewa mbugani mpaka wanapandishwa ndege,wao wako kimya alafu bado tusiwaite usalama wa mafisadi.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom