Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,331
- 8,254
Vijana wanapenda kujiajiri ila wengi hawana mitaji anzisheni mikopo ya graduates ila kuipata mwaangalie vyeti tu na vitambulisho vyao ili wajiajiri wenyewe na kodi zitaongezeka.
Wazazi wamejinyima wamewasomesha watoto ili wapate ajira. Wazazi wengine hata nguo nzuri hawakununua, wala nyama na wali hawakula.
Walifanya kazi ngumu za kilimo cha jembe la mkono ili wapate fedha za ada. Lakini fedha zilizopatikana baada ya kuuza mazao yote hata laki 2 hazikufika. Wazazi wengine waliuza kila kitu nyumbani ili watoto wao waende shule.
Wazazi wengine walifanya kazi za hatari hata za kuuza gongo na pombe ili watoto wao waende shule.
Kiukweli mpaka mtoto anamaliza shule mzazi anakua amechoka haswa kiuchumi, kiafya na kiakili.
Sasa kama hali ndio hiyo mzazi anapata wapi nguvu ya kumsaidia mtoto wake kujiajiri.
Mngejitahidi kuwakopesha graduates mikopo, ukopaji uwe wa tofauti usiangalie kwamba mtu ana asset mwaangalie vyeti tu na vitambulisho vyao ili wajiajiri wenyewe na kodi zitaongezeka. Uzuri watafanya biashara na watalipa kodi.
Inakuaje bodaboda anakopeshwa alafu msomi hawezi kopeshwa? Inakuwaje mama ntilie anakopeshwa alafu msomi hawezi kopeshwa.
Kama kweli tunawapenda wasomi wenzetu na tunaumia kwasababu hawana ajira tutengeneze program ya kuwakopesha hao wasomi wote wanaohitimu vyuo wenye mawazo ya kufanya biashara.
Na mkopo huo utamke wazi mtu anayekopeshwa asiwe ameajiriwa.