Iwaay

Member
May 21, 2016
35
52
Ndugu msomaji mimi Leo nimeona nitoe pendekezo kwa Serikali kuangalia ni jinsi gani ikawasaidia vijana wanaohitimu Vyuo vikuu kutumia vyeti vyao kupata mikopo ya kuanzisha biashara mara baada ya kuhitimu.

Kama Serikali ilivyowasaidia vijana hawa kupata mikopo ya kusoma Vyuo basi ni bora pia wakasaidiwa kupata mikopo yenye riba nafuu ya kupata mitaji ya kuanzisha biashara ambayo itaunganishwa na ile ya elimu ya juu ili walipe kwa pamoja baada ya mwaka moja au miwili ya kuanzisha biashara zao hizo.

Vijana hao wanapohitimu Hawana mitaji na pia benki zetu hazitoi mikopo bila ya kuwa na Mali isiyohamishika hivyo kama Serikali itaongeza kigezo kuwa mhitimu aweze kupata mkopo kupitia cheti chake cha chuo kikuu itakuwa imewasaidia vijana wengi wenye ndoto za kuwa wafanyabiashara kupata mkopo.

Serikali pia itakusanya kodi kupitia biashara zao na kuongeza pato.
 

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
4,011
6,504
Sasa mkishindwa kulipa mikopo hivyo vyeti vyenu tutamuuzia nani ili kupata pesa zetu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom