Iache nyumba yako ipumue

Iache nyumba yako ipumue

Kuna wakati huwa tunaugua magonjwa yanayosababishwa na sisi wenyewe. Kuna wakati yale tunayoyabeba vichwani mwetu na kushindwa kuyaachilia hivyo hivyo hufanya hivyo kwenye majumba yetu.

Nyumba safi, yenye vitu vichache huchangamsha mwili na kuleta afya ya akili. Si lazima iwe kubwa, hata hiyo ndogo katika udogo wake yaweza kukupa nuru, hewa safi na mwanga mpaka rohoni kama hutaigeuza kuwa ghala.

Hewa safi, nafasi na mwanga wa kutosha ndani ya nyumba/ chumba huufanya mwili kuchangamka na kuwa na siha njema hata kama kula yako ni ya shida.

Nyumba safi iliyopangiliwa vizuri huvutia mahusiano mazuri yenye furaha. Nyumba nayo ina roho hebu ipe nafasi ipumue.

Natambua kuna baadhi yetu kiasili ni wabinafsi na wenye roho ya kukusanya kila kitu lakini kama wakielimishwa wanaweza kubadilika.. Unajua hata hawa wadudu kama kunguni, papasi, chawa mende nk huletwa na nyumba isiyopangiliwa na iliyojazana vitu visivyo na faida tena.

Kuna nyumba makabati ya nguo yamejaa nguo zisizovaliwa tena
Kuna nyumba vyumba na shoes rack vimejaa viatu visivyovaliwa tena
Kuna nyumba chumba cha ghala kimejaa vitu vibovu visivyotumika tena pasi, feni, sufuria viti nknk
Kuna nyumba karibia kila chumba kimejazwa vitu visivyo na faida chini mpaka juu, makawa ya chakula, mapichapicha kutani, vimitomito, vizulia, vipambopambo nknk

Kumbuka kila kimoja kati ya hivyo kimetengenezwa na malighafi tofauti tofauti, kitendo cha kuvirundika vyote sehemu moja husababisha futuko, hewa nzito na harufu za ajabu.

Fanya mambo haya muhimu
Kuwa na tabia ya kugawa vitu usivyotumia tena hasa nguo vyombo na viatu

Vitu vibovu tengeneza, gawa au uza. Kitu kisipotumika muda mrefu huwa mazalia ya wadudu na makao pia
Kuwa na utaratibu wa kuwa na vitu vichache lakini vizuri hata kama thamani yake sio kubwa sana
Fanya kila kitu ndani ya nyumba/chumba chako kiwe na nafasi yake ya kutosha

Usibabanishe vitu, usivipandanishe, usivisokomeze mahali pamoja vitashindwa kupumua

Jaribu kufanya hayo machache utaona hata stress zitakavyokupungua...kuipa nyumba nafasi ya kupumua ni kuupa mwili pia nafasi ya kulerax

Si kila wenye mapepo wametupiwa wengine wameyakaribisha wenyewe kutokana na lifestyle ndani ya sehemu wanazoishi
Umenena vema ila naomba uwatoe kunguni kwenye hiyo list. Kunguni huletwa kutoka guest house za kuleee..
 
Mimi nina utoto ni kweli. Je wewe mwenye ukubwa tuambie cha maana ?
Cha maana ninachoweza kukuambia ni acha utoto,au kama kuacha uwezi punguza utoto kwenye Mambo ya Msingi!!
 
Ushauri mzuri sana huu, binafsi napenda mabambo ya aina moja tu.... PICHA TU. 📷

nikicheki huku wazee wangu, kule familia yangu nk...
 
Umeongea vyema my.

Katika mtu asopenda makorokoro mmoja mie. Siishi kutupa na kugawa mpk wanangu wananambia mama wewe too much.

Nawaambia kukaa na makorokoro ndani unaweka makaazi ya mashetani.

Hapa nisichoweza kutupa au kugawa ni mabuku na vitabu vyao tu ila navyo vinanitia wazim.
Tupo wengi.Nachoma sana nguo ambazo naona zimepauka au kuchakaa kiasi siwezi mpa mtu.Sipendi makorokoro.Wasichana wangu washanijua kuna vitu nakuta washavitupa kabla hata sijasema.
 
Umenena vema ila naomba uwatoe kunguni kwenye hiyo list. Kunguni huletwa kutoka guest house za kuleee..
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]lakini kunguni hakai mahali pasafi, ukileta hiyo mbegu ntumbani kama nyumba ni chafu itamea lakini kama nyumba ni safi hiyo mbegu itakufa
 
Hiki chumba cha dereva taxi kilikuwa zaidi ya haya tunayojadiliana hapa.. Huu unaweza kuwa ni ugonjwa
MJUMBE+WA+ENEO+HILO%2CBADILI+MAKOYE+%28KATIKATI%29+AKIWA+NA+MWENYE+NYUMBA+NA+BAADHI+YA+WANANCHI..jpg
View attachment 1767218
 
Kule kwetu kuna msemo"ekyai ky'omunju tikiburwa kya kukoma" ni msemo wa zamani ila faida yake ni ndogo sana ukilinganisha na usumbufu alioandika MUSHANA. Ata ofisini kuna vitu sio vya lazima unaweza kuvipunguza pa.
 
Kuna wakati huwa tunaugua magonjwa yanayosababishwa na sisi wenyewe. Kuna wakati yale tunayoyabeba vichwani mwetu na kushindwa kuyaachilia hivyo hivyo hufanya hivyo kwenye majumba yetu.

Nyumba safi, yenye vitu vichache huchangamsha mwili na kuleta afya ya akili. Si lazima iwe kubwa, hata hiyo ndogo katika udogo wake yaweza kukupa nuru, hewa safi na mwanga mpaka rohoni kama hutaigeuza kuwa ghala.

Hewa safi, nafasi na mwanga wa kutosha ndani ya nyumba/ chumba huufanya mwili kuchangamka na kuwa na siha njema hata kama kula yako ni ya shida.

Nyumba safi iliyopangiliwa vizuri huvutia mahusiano mazuri yenye furaha. Nyumba nayo ina roho hebu ipe nafasi ipumue.

Natambua kuna baadhi yetu kiasili ni wabinafsi na wenye roho ya kukusanya kila kitu lakini kama wakielimishwa wanaweza kubadilika.. Unajua hata hawa wadudu kama kunguni, papasi, chawa mende nk huletwa na nyumba isiyopangiliwa na iliyojazana vitu visivyo na faida tena.

Kuna nyumba makabati ya nguo yamejaa nguo zisizovaliwa tena
Kuna nyumba vyumba na shoes rack vimejaa viatu visivyovaliwa tena
Kuna nyumba chumba cha ghala kimejaa vitu vibovu visivyotumika tena pasi, feni, sufuria viti nknk
Kuna nyumba karibia kila chumba kimejazwa vitu visivyo na faida chini mpaka juu, makawa ya chakula, mapichapicha kutani, vimitomito, vizulia, vipambopambo nknk

Kumbuka kila kimoja kati ya hivyo kimetengenezwa na malighafi tofauti tofauti, kitendo cha kuvirundika vyote sehemu moja husababisha futuko, hewa nzito na harufu za ajabu.

Fanya mambo haya muhimu
Kuwa na tabia ya kugawa vitu usivyotumia tena hasa nguo vyombo na viatu

Vitu vibovu tengeneza, gawa au uza. Kitu kisipotumika muda mrefu huwa mazalia ya wadudu na makao pia
Kuwa na utaratibu wa kuwa na vitu vichache lakini vizuri hata kama thamani yake sio kubwa sana
Fanya kila kitu ndani ya nyumba/chumba chako kiwe na nafasi yake ya kutosha

Usibabanishe vitu, usivipandanishe, usivisokomeze mahali pamoja vitashindwa kupumua

Jaribu kufanya hayo machache utaona hata stress zitakavyokupungua...kuipa nyumba nafasi ya kupumua ni kuupa mwili pia nafasi ya kulerax

Si kila wenye mapepo wametupiwa wengine wameyakaribisha wenyewe kutokana na lifestyle ndani ya sehemu wanazoishi
You're the best Mshana Jr. Ahsante kwa elimu nzuri mtu mzito.
 
'Feng shui' rule...

Bahati mbaya wabongo huwa tunajenga na kuishi tu
 
[emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Kuna aina ya mavazi
Aina ya mapambo.

Aina ya mziki humtambulisha mtu hata anapoishi...! Unakuta mdada ana furushi la nywele kichwani tena bandia, ana hereni mbili mbili masikio yote, ana Kishaufu puani, ana mapete vidoleni mikono yote, ana mabangili, ana cheni shingoni, shanga kiunoni, vikuku miguuni.

Ana nyusi bandia kabandika, ana makeup mpaka hazitoshani usoni...huyu ukimkuta miziki yake anayopenda.... Ukikikuta chumba chake au nyumba yake.

Ukiikuta dressing table yake ni full vurumai
Hahahahahahha kaka nimecheka hadi machozi
 
'Feng shui' rule...

Bahati mbaya wabongo huwa tunajenga na kuishi tu
Nimejiongeza
Read on for five feng shui rules that should never be broken!
Be organized and tidy. This is first on the list for a reason! ...
Keep your bed away from the window. Feng shui is very strict about this rule! ...
Separate work and rest areas. ...
Use the Bagua Map properly. ...
Know your colors
downloadfile.jpg
 
Kumbuka kila kimoja kati ya hivyo kimetengenezwa na malighafi tofauti tofauti, kitendo cha kuvirundika vyote sehemu moja husababisha futuko, hewa nzito na harufu za ajabu.
Hi ni kweli haina ubishi nililiona baada ya kuhama kutoka nyumba ya kupanga kwenda kwenye nyumba ya bure na yenye nafasi ya kutosha, nililala usingizi wa ajabu wa zaidi ya masaa 12
 
[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Umenena vyema mkuu,

Chumba safi na kilichopangliwa kinaleta pumzko la mwili na akili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom