Iache nyumba yako ipumue

Iache nyumba yako ipumue

Asante Mkuu, nimeelewa!

Watanitambua huko home leo... maana hata makopo, mandoo yasiyotumika, masufuria na mamifuko yamelundikwa tu bila sababu.......
[emoji3]halafu hivyo vyote ni pesa ujue..vinauzika bila shaka
 
Kuna wakati huwa tunaugua magonjwa yanayosababishwa na sisi wenyewe. Kuna wakati yale tunayoyabeba vichwani mwetu na kushindwa kuyaachilia hivyo hivyo hufanya hivyo kwenye majumba yetu.

Nyumba safi, yenye vitu vichache huchangamsha mwili na kuleta afya ya akili. Si lazima iwe kubwa, hata hiyo ndogo katika udogo wake yaweza kukupa nuru, hewa safi na mwanga mpaka rohoni kama hutaigeuza kuwa ghala.

Hewa safi, nafasi na mwanga wa kutosha ndani ya nyumba/ chumba huufanya mwili kuchangamka na kuwa na siha njema hata kama kula yako ni ya shida.

Nyumba safi iliyopangiliwa vizuri huvutia mahusiano mazuri yenye furaha. Nyumba nayo ina roho hebu ipe nafasi ipumue.

Natambua kuna baadhi yetu kiasili ni wabinafsi na wenye roho ya kukusanya kila kitu lakini kama wakielimishwa wanaweza kubadilika.. Unajua hata hawa wadudu kama kunguni, papasi, chawa mende nk huletwa na nyumba isiyopangiliwa na iliyojazana vitu visivyo na faida tena.

Kuna nyumba makabati ya nguo yamejaa nguo zisizovaliwa tena
Kuna nyumba vyumba na shoes rack vimejaa viatu visivyovaliwa tena
Kuna nyumba chumba cha ghala kimejaa vitu vibovu visivyotumika tena pasi, feni, sufuria viti nknk
Kuna nyumba karibia kila chumba kimejazwa vitu visivyo na faida chini mpaka juu, makawa ya chakula, mapichapicha kutani, vimitomito, vizulia, vipambopambo nknk

Kumbuka kila kimoja kati ya hivyo kimetengenezwa na malighafi tofauti tofauti, kitendo cha kuvirundika vyote sehemu moja husababisha futuko, hewa nzito na harufu za ajabu.

Fanya mambo haya muhimu
Kuwa na tabia ya kugawa vitu usivyotumia tena hasa nguo vyombo na viatu

Vitu vibovu tengeneza, gawa au uza. Kitu kisipotumika muda mrefu huwa mazalia ya wadudu na makao pia
Kuwa na utaratibu wa kuwa na vitu vichache lakini vizuri hata kama thamani yake sio kubwa sana
Fanya kila kitu ndani ya nyumba/chumba chako kiwe na nafasi yake ya kutosha

Usibabanishe vitu, usivipandanishe, usivisokomeze mahali pamoja vitashindwa kupumua

Jaribu kufanya hayo machache utaona hata stress zitakavyokupungua...kuipa nyumba nafasi ya kupumua ni kuupa mwili pia nafasi ya kulerax

Si kila wenye mapepo wametupiwa wengine wameyakaribisha wenyewe kutokana na lifestyle ndani ya sehemu wanazoishi
Asante mkuu,sema vingine tunavitunza kwa ajili ya kumbukumbu kwa vizazi vya baadaye kwamba tulishawahi kumiliki mali hapo nyuma.sasa watajuaje kama babu yao nilishawahi kumililiki panasonic
 
Asante mkuu,sema vingine tunavitunza kwa ajili ya kumbukumbu kwa vizazi vya baadaye kwamba tulishawahi kumiliki mali hapo nyuma.sasa watajuaje kama babu yao nilishawahi kumililiki panasonic
Hakuna shida kabisa kama utaviweka katika hali ya usafi na mpangilio mzuri.. Hata mimi nina vichache vya kumbukumbu lakini viko mahali pazuri, pasafi na palipopangiliwa vema
 
Sijui ni tabia sijui ni nini jamani na tumevirithi toka enzi na enzi
 
Yeah iliyojaa makorokoro yasiyotumika ni makazi ya wadudu,viumbe kama panya ,nyoka na hata mapepo wachafu.
Kwa kuongezea mkuu majoto , moja ya dalili za mtu kuwa na mapepo ni kuwa mchafu au kuishi katika mazingira machafu. Hujipendi, hujijali na mazingira yako yapo hovyo jua haupo sawa na salama, kuna viumbe umewatengenezea makazi.
 
Less is more.
Binafsi sipendi nyumba imerundikana mavitu. Living room sofa, coffee table, katelly, dinning set@Living+dinning room..jikoni kuna essential appliances na utensils..vyumbani ni kabati + mpangilio wake wa nguo, vitanda na table lamps & their stands...bafu/choo vitu muhimu tu.
Mtu unafanya usafi bila kusukumana na vitu.
Kitambo sana nimejifunza kutupa au kutonununua vitu visivyohitajika. Kimeharibika hakitengenezi, tupa kule.
 
Mkuu Mshana kuhodhi vitu hata visivyohitajika ni aina mojawapo ya ugonjwa wa akili "withholding tendecy".

Wapo wanaoamini kwamba mgonjwa wa afya ya akili ana mapepo...! Wengi wanaoanguka wakuombewa stress na ingeweza kutibiwa kitaalam.

Kama una makorokoro kibao home na huwezi kuachana nayo, tafuta huduma ya tiba ya afya ya akili.

[emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541]

Credit kwako baba Isaya
 
Ccm pia wako na matakataka mengi ndio mahana mapepo hayaweishi
[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji2839][emoji2839][emoji2839][emoji1550][emoji1550][emoji1550][emoji1550]
 
Less is more.
Binafsi sipendi nyumba imerundikana mavitu. Living room sofa, coffee table, katelly, dinning set@Living+dinning room..jikoni kuna essential appliances na utensils..vyumbani ni kabati + mpangilio wake wa nguo, vitanda na table lamps & their stands...bafu/choo vitu muhimu tu.
Mtu unafanya usafi bila kusukumana na vitu.
Kitambo sana nimejifunza kutupa au kutonununua vitu visivyohitajika. Kimeharibika hakitengenezi, tupa kule.
A very good setup[emoji1540][emoji1548][emoji1752]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom