Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,754
Kuna wakati huwa tunaugua magonjwa yanayosababishwa na sisi wenyewe. Kuna wakati yale tunayoyabeba vichwani mwetu na kushindwa kuyaachilia hivyo hivyo hufanya hivyo kwenye majumba yetu.
Nyumba safi, yenye vitu vichache huchangamsha mwili na kuleta afya ya akili. Si lazima iwe kubwa, hata hiyo ndogo katika udogo wake yaweza kukupa nuru, hewa safi na mwanga mpaka rohoni kama hutaigeuza kuwa ghala.
Hewa safi, nafasi na mwanga wa kutosha ndani ya nyumba/ chumba huufanya mwili kuchangamka na kuwa na siha njema hata kama kula yako ni ya shida.
Nyumba safi iliyopangiliwa vizuri huvutia mahusiano mazuri yenye furaha. Nyumba nayo ina roho hebu ipe nafasi ipumue.
Natambua kuna baadhi yetu kiasili ni wabinafsi na wenye roho ya kukusanya kila kitu lakini kama wakielimishwa wanaweza kubadilika.. Unajua hata hawa wadudu kama kunguni, papasi, chawa mende nk huletwa na nyumba isiyopangiliwa na iliyojazana vitu visivyo na faida tena.
Kuna nyumba makabati ya nguo yamejaa nguo zisizovaliwa tena
Kuna nyumba vyumba na shoes rack vimejaa viatu visivyovaliwa tena
Kuna nyumba chumba cha ghala kimejaa vitu vibovu visivyotumika tena pasi, feni, sufuria viti nknk
Kuna nyumba karibia kila chumba kimejazwa vitu visivyo na faida chini mpaka juu, makawa ya chakula, mapichapicha kutani, vimitomito, vizulia, vipambopambo nknk
Kumbuka kila kimoja kati ya hivyo kimetengenezwa na malighafi tofauti tofauti, kitendo cha kuvirundika vyote sehemu moja husababisha futuko, hewa nzito na harufu za ajabu.
Fanya mambo haya muhimu
Kuwa na tabia ya kugawa vitu usivyotumia tena hasa nguo vyombo na viatu
Vitu vibovu tengeneza, gawa au uza. Kitu kisipotumika muda mrefu huwa mazalia ya wadudu na makao pia
Kuwa na utaratibu wa kuwa na vitu vichache lakini vizuri hata kama thamani yake sio kubwa sana
Fanya kila kitu ndani ya nyumba/chumba chako kiwe na nafasi yake ya kutosha
Usibabanishe vitu, usivipandanishe, usivisokomeze mahali pamoja vitashindwa kupumua
Jaribu kufanya hayo machache utaona hata stress zitakavyokupungua...kuipa nyumba nafasi ya kupumua ni kuupa mwili pia nafasi ya kulerax
Si kila wenye mapepo wametupiwa wengine wameyakaribisha wenyewe kutokana na lifestyle ndani ya sehemu wanazoishi