I Hate Swahili Because It Is Purely Arabic | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

I Hate Swahili Because It Is Purely Arabic

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Ng'wanangwa, Dec 10, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  And Arabic is the language of Islamic doctrines.

  And am not a muslim, neither i will be.

  i will chose death between death, living and being islamised.

  what do you think ma pipo?
   
 2. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2010
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  To me it sounds like you hate yourself. Je hiyo lugha unayotumia kujieleza ni lugha yako au...?
   
 3. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Jerusalem,
  Kuna ka-jukwaa kanaitwa D I N I embu isogeze kule tuichangie vizuri..
   
 4. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,420
  Likes Received: 3,768
  Trophy Points: 280
  Sioni sababu ya kuki-hate kiswahili. Kama ni uislamu ni wao na kiarabu ni chao...............
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Jerusalem, Umeumwa na mbu sugu na sasa una malaria sugu. Hii ilikutokea wakati mnasoma chuo kikuu cha Anopheles pamoja na Malaria sugu. soma mlilofauli vizuri lilihusu namna ya kufarakanisha ukristo na Uislamu. Hili somo wanasoma watu wenye akili ndogo zaidi duniani kwa sababu ni jepesi kueleweka hata kwa wale walio na mtindio wa ubungo. Ni somo la kukata tawi la mti huko umelikalia linahitaji wajinga ili kulielewa. werevu wengi hawajapata kufaulu somo hili.
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  thank you.

  i talk openly.

  you talk openly.

  so, we are even.
   
 7. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jerusalem kuna msemo wa "kiswahili" usemao MKATAA KWAO NI MTUMWA ni wazi wewe ni mtumwa na bado unaishi kwa fikra za kikoloni. Kiswahili hakika uhusianio wowote wa moja kwa moja na uislam, kumbuka hata Uingereza ambako hutumia lugha uliyotumia kujieleza ambayo wewe unafikiri ndio lugha bora, pia waislam wako. Na pia nikueleze ukristo ambao unajaribu kuupa uhusiano wa moja kwa moja na kiingereza unawasilishwa kwa lugha mbalimbali kutokana na eneo husika. Ningekuelewa kama ungesema tu kwa sababu zako na kwa imani yako unachukia UISLAM, na hata kama hivyo ndiyo si kuna JUKWAA lake!
   
 8. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kiswahili is a lingua franca, and it is made in Tanzania! It has arabic words, kireno, kijerumani but largely it's bantu words! I am not originally a bantu person, i am a hamite..but so what..tunakwenda na wakati na mazingira and i don't regret...maisha yanaendelea! Kiswahil kisihusishwe na dini yoyote wala waraabu, hata wao hawakijui! Hata waislamu siyo waarabu peke yao! sipendi uislamu, ila singilii dini zwatu kama nisivyotaka ya kwangu kuingiliwa! But that's has nothing to do with the Kiswahili! It's melodic jo!
   
 9. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #9
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kiswahili ni kiislamu. Ukienda nchi kama Rwanda, Burundi, Uganda, Sudan ya kusini, Malawi ya kaskazini; kiswahili ni lugha inayozungumzwa na waislamu. Na hata hapa nyumbani kilipozaliwa kiswahili, waislamu ndiyo watu wa kwanza kuzungumza kiswahili. Mombasa, Tanga, Unguja na Pemba, Dar-es-salaam, Kilwa, Lindi mpaka Mtwara.; Kigoma na kuvuka mipaka kuingia nchi jirani. Kikaendelea kukomaa na kuusambaza Uislamu na na mpaka leo hii kinazungumzwa na watu wasiojua kilipotokea.
  Na hiyo ndiyo historia yetu.
   
 10. N

  Nonda JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280


  Jerusalem,

  Shalom,

  Ninaposoma michango yako, hunifanya nitabasamu.
  Fofofo inaonekana anakufahamu vyema. Umekuwa ni mtu wa misimamo mikali.
  Why don’t you arrange a match with MS ?

  Inaonekana unapata tabu sana, una msongo wa mawazo, nimeona katika threads nyengine unatumia Kiswahili, tena Kiswahili sanifu, fasaha. Sasa kwa nini ulijifunza lugha hii?
  Unapendelea hapa Tanzania tutumie lugha gani?

  Kiswahili ni kibantu, si kiarabu wala si kiislamu. Waulize wataalamu wa lugha kama itakusaidia kupunguza au kuondoa chuki yako dhidi ya Kiswahili.

  Kiswahili kina maneno yenye asili ya kiarabu, (sio kiislamu) kwa 44% tu. Na lugha zote duniani huazima, hukopa maneno kutoka katika lugha nyengine na kuyatohowa. Yakishapita hatua hiyo huwa ni maneno ya lugha husika siyo tena ya kule yalikoopolewa.

  Ukubwa wa Tanzania ulivyo, na lugha zaidi ya 120, tumshukuru Nyerere aliyefanya juhudi kuieneza lugha hii ili kutuunganisha kama taifa.

  Kama tatizo lako ni uislamu, hilo ni jambo jengine na ni vyema uwaachie wenyewe uislamu wao ,wewe shughulika na imani uliyonayo. Waswahili husema,”pili pili usiyoila yakuwashiani?”
  Pia kama hujuwi au ndiyo misimamo mikali imekuzidi kimo, siyo waarabu wote kuwa ni waislamu.

  Katafute ushauri nasaha mapema, ndugu.

  Shalom,
   
 11. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  AWAU'ZA WASWAHILI

  1

  Risala enuka hima, sikae 'kataghafali
  N'na jambo 'takutuma, ubalegheshe suali
  Nipate jawabu njema, yenye amani na kweli
  Nauliza Kiswahili, ni lugha ya watu gani?


  2
  Lugha nyingi duniyani, zatamkwa mbalimbali
  Na zote ulimwenguni, zina wenyewe mahali
  Si Hindi Si Uzunguni, mewaumbia Jalali
  Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?


  3
  Wakamba wana kikwao, lugha yao ya asili
  Na Wazungu piya nao, wana zao mbalimbali
  Na Wameru wana yao, wengine ni Wasomali
  Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?


  4
  Wahindi wana Kihindi, kwa kabila mbalimbali
  Na Wanandi ni Kinandi, ndizo zao akuwali
  Wengine ni Wakilindi, wana yao ya asili
  Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?


  5
  Kuuliza Si ujinga, musinifanye jahili
  Nautafuta niuwanga, tuzinduwane akili
  Ndipo shairi hatunga, kubaleghesha suali
  Nielezwe Kiswahili, ni lugha ya watu gani?


  6
  Mara nyingi husikiya, kuwa hichi Kiswahili
  Hakina mtu mmoya, ambaye ni chake kweli
  Na wengine huteteya, kina wenyewe asili
  Ndipo ha'mba Kiswahili, ni lugha ya watu gani?  7
  Masai ana kikwao, lugha ya tangu azali
  Na Mahara wana yao, wengine Mashelisheli
  Na Waluo lugha zao, Si sawa na Maragoli
  Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

  8
  Na jamii wengineo, wana lugha mbalimbali
  Na kujuwa ya wenzao, ni kujifunza ya pili
  Lakini wana na zao, lugha za tangu asili
  Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

  9
  Sasa ambalo nataka, kwa wenye kujuwa hili
  Wa Kenya na Tanganyika, na walo kulla mahali
  Nipani ilo hakika, tubalegheshe ukweli
  Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

  10
  Miye mefikiri mno, kuamuwa jambo hili
  Na huona lugha hino, lazima ina asili
  Kwa sababu kulla neno, lina mwanzo wa usuli
  Ndipo ha'mba Kiswahili, hi lugha ya watu gani?

  11
  Na iwapo hivi sivyo, niliyyoamuwa hili
  Nionyeshani viliyyo, mubainishe ukweli
  Nijuwe ambavyo ndivyo, tutowane mushkili
  Kifunuke Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

  12
  Na iwapo atakuja, wa kunijibu suali
  Namuomba jambo moja, twambiyane kiakili
  Tusionyane miuja, jambo nisilo kubali
  N'anambiye Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

  13
  Tamati ndio akhiri, na jina langu ni hili
  Ahmadi wa Nasiri, na Bhalo ndilo Ia pili
  Mtungaji mashuhuri, mpenda penye ukweli
  Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

  By Ahmad Nassir from Malenga wa Mvita
   
 12. F

  Future Bishop Member

  #12
  Dec 10, 2010
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jerusalem, I strongly differ with you; I know you did not choose to be born in a christian family and a muslim child did not choose to be born in that family. In view of this reality once you get to know the truth about your faith, you need also to know about the other faith so that you can be able to differentiate and be able to help the other side. To me is not the issue of swahili, as christians we need to go beyond learn and get to know arabic language so that we can read their books and be able to help each other. It is only the truth/facts that can set someone free; so by knowing your faith as christian and knowing what others believe through their books it will help you to help them.
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Dec 10, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na kama unaishi Dar es Salaam, basi ni vyema ukahama. The name is purely Arabic.
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Dec 10, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Umenikumbusha kitu kimoja -- iliishia wapi ile kampeni ya kutaka kubadilisha jina la Jiji la Dar na badala yake uitwe Mzizima?
   
 15. N

  Newvision JF-Expert Member

  #15
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I do not subscribe to your view. Kiswahili has many roots and not purely Arabic see for example Schule for Shule -German
  picha for picture is English, Mesa for meza is portuguese and see for example Kitivo for chemichemi from Kipare and many more. So it has been enriched from so many sources and not only Arabic au siyo?
   
 16. N

  Newvision JF-Expert Member

  #16
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante kaka nimeipenda hii
   
 17. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  :redfaces:!!!!!!!!!!!!!!?????????????????:faint:
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Dec 10, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180


  Punguza hasira ndg yangu Jerusalem.
   
 19. N

  Nonda JF-Expert Member

  #19
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280

  Mkuu,

  asante, ahsante kwa beti hizi.

  Mtu wa Pwani, "Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?"

  Ni lugha ya mtu kama wewe........watu wa pwani, mwambao.
  Kiswahili ni cha waswahili. Kila lugha ina wenyewe!
   
 20. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #20
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni ishara ya kuchanganyikiwa.

  Basi shauri taifa lizungumze kiyahudi kama lugha ya taifa. Tutajifunza na yale maandishi yao
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...