I Hate Swahili Because It Is Purely Arabic

Status
Not open for further replies.
Wewe Jerusalem una kichwa ngumu sana sijui huelewi au ni nini?? Kwa nini post zako nyingi ni za UDINI?? Ndugu yangu chuki uliyonayo haitakupeleka pahala. Leo umekuja na mpya eti hukipendi Kiswahili kwa sababu kina arabs words sasa kweli utaishi dunia ya nani kwa mtindo huu. Mimi najivunia sana lugha yangu kwani hata hao waarabu hawaifahamu lugha yetu wanabahatisha maneno mawili matatu. Acha kutumia chuki yako ya kidini kuikashifu nchi yetu kwa kupitia lugha yetu ya Taifa. Jina lako na maneno yako ni tofauti. 'dhambi hii itakufuata nyuma.' Sisi sote ni wamoja machoni pa mungu.
 
Sasa mpwa, mbona kichwa cha habari na maudhui ni tofauti? mie nina ka shahada ka kwanza ka kiswahili tena kale ka miaka minne migumu, sijawahi ona mahali ambapo kuna lugha imekua peke yake hata hicho kidhungu kimechukua sana toka kwa walatini na lg nyingine, kwani ulisoma mambo ya lugha au umeandika hisia zako tu, haya tukikutana unikumbushe nikufundishe juu ya nadharia za kukua na kuenea kwa kiswahili!
 
Kiswahili si kiarabu.
Kiswahili ni kiswahili na kiarabu ni kiarabu. Kiswahili si kiislam wala kiarabu si kiislam. Ni lugha. Uislam ni dini. Kuna waarabu kwa mfano wapalestina, asilimia 7 ni wakristo na wanasali kwa kiarabu. Kuna waarabu ndani ya Syria karibu asilimia 9 ni wakristo na wanasali kwa kiarabu, kuna waarabu wapo Irak, asilimia 7 ni wakristo na wanasali kwa kiarabu. Hata Lebanon na Misri kuna waarabu ambao ni wakristo na wanasali kwa kiarabu. Kwa hiyo kiarabu si uislam.

Kiswahili kina maneno yenye ASILI YA KIARABU. Hapo zamani, maneno hayo YENYE ASILI YA KIARABU yalikuwa karibu 40%. Asilimia hii inaweza kuwa imepungua kutokana na kukua kwa kiswahilli kwa kuingiza maneno mengine hasa ya kibantu na kizungu, ambayo hayatokani na kiarabu.
Tusichanganye mamboz.
 
Bwana J. hana ana tatizo na mantiki na pia elimu ya lugha.
a) Kiswahili ina maneno asilimia 30-40 za Kiarabu katika msamiati wake. Huu ni athira muhimu sana lakini asilimia 60-70 SI asili ya Kiarabu.
b) Mantiki: Kama Kiswahili kingekuwa "Purely Arabic" angejua Kiarabu tayari akijua Kiswahli. Lakini hajui Kiarabu. Ukifika nchi ya Kiarabu Kiswahili kinasaidia kidogo usijisikie umepotea kabisa lakini huwezi hata kuuliza ni saa ngapi (adeesh es-sa`?) hata kama neno saa ina asili katika Kiarabu sa`.

Menginevyo akitaka kukimbilia Kiingereza Kiarabu kinamsubiri tayari. Kiarabu kilikuwa lugha muhimu ya utaalamu miaka 1000 - 500 iliyopita hivyo maneno mengi ya kitaalamu yana asili ya Kiarabu hata katika Kiingereza.

Lakini asipopenda - basi aache.
 
I hate it not because its arabic but because it makes most of us be myopic and narrow minded above all local!
 
Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao.
Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi.


Sadaq Allaahul-'Adtheem
 


Umenikumbusha kitu kimoja -- iliishia wapi ile kampeni ya kutaka kubadilisha jina la Jiji la Dar na badala yake uitwe Mzizima?

Dar es salaam - sikia vile jina la mji lilivyo tamu kutamka na lenye maana bora. Dar es salaam. Dar = mji au bandari , Salaam = Salama. nini zaidi unataka ?

Utake usitake waafrika na waarabu wana historian ndefu ya pamoja na wametajirisha utamaduni wao kwa kukopa na kubadilishana maneno, mila na tamaduni na pia sote tunaishi katika bara la Afrika. Mungu tuepushe na wabaguzi.
 
I hate it not because its arabic but because it makes most of us be myopic and narrow minded above all local!
Wengi wa nani? Namna gani?
Mimi naona hapa JF zaidi watu wakitaka kuanza kusambaza fujo, uwongo au mambo yasiyo na maana wanakimbilia Kiingereza
a) kwa sababu akiba ya k/p ni kubwa zaidi kwa Kiingereza ni wawivu kutafakari wenyewe
b) kama fikra ni dhaifu chaguo kubwa ya msamiati wa Kiingereza kinawapa nguo za kung'aa zinazoficha ukweli ya kwamba chini hawana chupi na hawakuoga (kwa kawaida nguo hizi zina mashimo kwa hiyo uuchi unaonekana)
c) kwa Kiingereza wana njia pana zaidi ya kuwa na maneno mengi bila ya kusema kitu

Mimi sioni matata kujadili swali lolote lililopo duniani na mbinguni kwa Kiswahili. Pole na allerjia yako!
 
Dar es salaam - sikia vile jina la mji lilivyo tamu kutamka na lenye maana bora. Dar es salaam. Dar = mji au bandari , Salaam = Salama. nini zaidi unataka ?.
Nunga mkono kabisa unachosema juu ya ubaguzi.
Ila tu Daressalaam nisipokosei unasambaza kosa la kawaida juu ya maana ya neno; دار ‎ dār si mji wala bandari . ni "nyumba". Kwa hiyo; Nyumba ya amani.
 
And Arabic is the language of Islamic doctrines.

And am not a muslim, neither i will be.

i will chose death between death, living and being islamised.

what do you think ma pipo?

dah kuna wayu ni wagonjwa wa akili!! sijui tutafika wapi nchi hii,watu kama hawa hawana faida hapa duniani zaidi ya kuoneza chuki zisizo na maana
 
Hilo jina unalotumia ni la kiarabu, Jerusalem = Dar Es Salaam.

Tofauti ni namna lilivyoandikwa tu, lakini ni hilohilo.

Sasa anza kwa kubadili jina lako!
 
Kiswahili ni kiislamu. Ukienda nchi kama Rwanda, Burundi, Uganda, Sudan ya kusini, Malawi ya kaskazini; kiswahili ni lugha inayozungumzwa na waislamu. Na hata hapa nyumbani kilipozaliwa kiswahili, waislamu ndiyo watu wa kwanza kuzungumza kiswahili. Mombasa, Tanga, Unguja na Pemba, Dar-es-salaam, Kilwa, Lindi mpaka Mtwara.; Kigoma na kuvuka mipaka kuingia nchi jirani. Kikaendelea kukomaa na kuusambaza Uislamu na na mpaka leo hii kinazungumzwa na watu wasiojua kilipotokea.
Na hiyo ndiyo historia yetu.

Ningelikuomba urejee tena kwa historia ya Kiswahili. Wajerumani walipokuja Tanganyika, walipambana na makabila mbalimbali wakiwemo waarabu, je walikuwa na nia gani ya kuhamasha watu kujifunza kiswahili? Mwaka 1924 (kama sikosei), kwa nini Kenya na Uganda walishiriki kukubali kuwe na Kiswahili sanifu kwa Afrika Mashariki. Nyerere alipoamua kuwaunganisha Watanganyika (wakati huo hata Wazanzibari walikuwa hawamo) alikuwa anataka kueneza uislamu? Unataka kusema waislamu wote wanazungumza kiarabu au Kiswahili?
Baada ya Jerusalem kuona kuwa hakupata wafuasi kwenye mada ya Sofia Simba na vimini kaona akimbilia hapa na kakupata wewe. Mada nyengine bana...we wacha tu!
 
AWAU'ZA WASWAHILI

1

Risala enuka hima, sikae 'kataghafali
N'na jambo 'takutuma, ubalegheshe suali
Nipate jawabu njema, yenye amani na kweli
Nauliza Kiswahili, ni lugha ya watu gani?


2
Lugha nyingi duniyani, zatamkwa mbalimbali
Na zote ulimwenguni, zina wenyewe mahali
Si Hindi Si Uzunguni, mewaumbia Jalali
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?


3
Wakamba wana kikwao, lugha yao ya asili
Na Wazungu piya nao, wana zao mbalimbali
Na Wameru wana yao, wengine ni Wasomali
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?


4
Wahindi wana Kihindi, kwa kabila mbalimbali
Na Wanandi ni Kinandi, ndizo zao akuwali
Wengine ni Wakilindi, wana yao ya asili
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?


5
Kuuliza Si ujinga, musinifanye jahili
Nautafuta niuwanga, tuzinduwane akili
Ndipo shairi hatunga, kubaleghesha suali
Nielezwe Kiswahili, ni lugha ya watu gani?


6
Mara nyingi husikiya, kuwa hichi Kiswahili
Hakina mtu mmoya, ambaye ni chake kweli
Na wengine huteteya, kina wenyewe asili
Ndipo ha'mba Kiswahili, ni lugha ya watu gani?



7
Masai ana kikwao, lugha ya tangu azali
Na Mahara wana yao, wengine Mashelisheli
Na Waluo lugha zao, Si sawa na Maragoli
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

8
Na jamii wengineo, wana lugha mbalimbali
Na kujuwa ya wenzao, ni kujifunza ya pili
Lakini wana na zao, lugha za tangu asili
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

9
Sasa ambalo nataka, kwa wenye kujuwa hili
Wa Kenya na Tanganyika, na walo kulla mahali
Nipani ilo hakika, tubalegheshe ukweli
Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

10
Miye mefikiri mno, kuamuwa jambo hili
Na huona lugha hino, lazima ina asili
Kwa sababu kulla neno, lina mwanzo wa usuli
Ndipo ha'mba Kiswahili, hi lugha ya watu gani?

11
Na iwapo hivi sivyo, niliyyoamuwa hili
Nionyeshani viliyyo, mubainishe ukweli
Nijuwe ambavyo ndivyo, tutowane mushkili
Kifunuke Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

12
Na iwapo atakuja, wa kunijibu suali
Namuomba jambo moja, twambiyane kiakili
Tusionyane miuja, jambo nisilo kubali
N'anambiye Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

13
Tamati ndio akhiri, na jina langu ni hili
Ahmadi wa Nasiri, na Bhalo ndilo Ia pili
Mtungaji mashuhuri, mpenda penye ukweli
Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

By Ahmad Nassir from Malenga wa Mvita

Kichina = Uchina = Mchina
Kihindi = Uhindini = Mhindi
Kitaliana = Italia = Mtaliana
Kifaransa = Ufaransa = Mfaransa
Kiswahili = Wapi? = Mswahili?
 
Kichina = Uchina = Mchina
Kihindi = Uhindini = Mhindi
Kitaliana = Italia = Mtaliana
Kifaransa = Ufaransa = Mfaransa
Kiswahili = Wapi? = Mswahili?
Hapa Mkuu kidogo kuna kasoro, sio lazima ulichoandika ni sahihi, wakati mwengine tunatumia lugha kimkato-mkato kurahisisha mambo ili ueleweke haraka. Ni sawa kusema Kihindi ni lugha lakini kumbuka India kama nchi kuna lugha kibao ambazo sio kihindi, mara nyingi ikitokea lugha kuzungumzwa sehemu/nchi moja pekee basi tunaweza kutumia jina la nchi kama ulivyoandika hapo juu; mfano wako kifaransa/Ufaransa/mfaransa, jee wajua kua kifaransa hakizungumzwi Ufaransa pekee? Ubelgiji na na nchi za jirani zinazungumza hiyo lugha pia. Mfano mwengine utasikia aah huyu anazumgumza ki-Tanga, ukweli hakuna lugha ki-tanga lakini huwa unamaanisha ana lafdhi (accent) ya watu wanaotokea eneo la Tanga. Kiswahili ni lugha inayozungumzwa na watu wa Afrika ya mashariki; kilugha si kosa kuwaita wazungumzaji kiswahili-Waswahili, lakini kwa vile tulivyoisanifu lugha hii ukmwita mwenzio mswahili humaanishi tena kua huyo ana kimanya kiswahili. Kadhalika nauliza nchi gani "Uarabuni"? najua wazi ni wapi wanazungumza kiarabu. Namalizia kwa kukumbusha Australia, Canada na USA wanazungumza kiingereza na si Waingereza?
 
And Arabic is the language of Islamic doctrines.

And am not a muslim, neither i will be.

i will chose death between death, living and being islamised.

what do you think ma pipo?

All you said is TRUE.

Please tell us about Islamic doctrines and how said doctrines influence Swahili and underdevelope Africa.
 
And Arabic is the language of Islamic doctrines.

And am not a muslim, neither i will be.

i will chose death between death, living and being islamised.

what do you think ma pipo?


Katika thread za kijuha hii inaongoza hapa JF. Oh well' kama walivyosema men. Toka lini watu wa deen wakawa na akili?

Sasa unataka kusema wote wanaozungumza kiswahili ni waislamu?
Wewe mwenyewe unazungumza Kiswahili, kwahio ni mujahhedeena?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom