Naona wengi humu ama mmeingia JF juzi ama mmeanza kusoma makala zinazoikosoa serikali majuzi tu. Tulioanza zamani tuligundua toka awali kabisa kwamba adui wa taifa hili ni CCM na wakati huo CCM haikuwa na mtu wa kumtupia lawama kwa sababu CCM ndio ilikuwa kila kitu...bunge, polisi, jeshi, mahakama n.k. Popote pale tulipojikuta, tulifikishwa na CCM pamoja na serikali yake, hawakuwepo wa kutupiwa lawama zaidi yao.
Tulipoanza kudai mfumo wa vyama vingi, kwa shinikizo kutoka ndani na nje, CCM kwa shingo upande ililazimika kuridhia lakini kwa masharti ambayo hayakuwekwa wazi. Baada ya kuona hatari iliyoletwa na mfumo huo, wajanja ndani ya CCM walikaa kitako na kutafakari ni vipi wataendelea kuaminiwa na wananchi. Kitu kimoja walichokiridhia ni kwamba sasa angalau wamepatikana alternatives wa kuwatupia lawama mambo yakienda kombo,upinzani.
Lakini hapo napo walikwaa kisiki, kwa hayati Mwalimu Julis Kambarage Nyerere, mwanzilishi, national icon, Baba wa Taifa na mwanachama namba moja wa Chama cha Mapinduzi. Mwalimu alikuwa kama LUKU kwa CCM na wengi waliotaka kwenda nje ya mstari hakuwamezea maneno, aliwapa kavu kavu. Alichosahau Mwalimu ni kwamba he had created a monster, a monster that would stop at nothing to get what it wanted at whatever cost.
Thus Mwalimu became the first victim of a product of his own creation,
a monster out of control! Mwalimu aliwapiga stop Lowassa na Kikwete mara tu baada ya mfumo mpya wa vyama vingi...alikuwa ana sababu zake, alijua jinsi mizizi ya CCM ilivyojikita katika kila nyanja. Nia yake kubwa ilikuwa ni namna ya kukipunguzia nguvu hili zimwi kwa sababu alijua kwa nguvu ilizo nazo, CCM isingeweza kuachia madaraka hivi hivi kirahisi.
Alikuwa anatafuta namna na kulidhoofisha hili zimwi hadi kufikia hatua ya kutamani kuiona CCM ikipasuka vipande viwili angalau vijitokeze vyama viwili vyenye nguvu sawa. Baada ya kifo kilichogubikwa na utata, Mwalimu akatuacha Watanzania kama yatima na yasemekana (sina hakika) machozi yake kabla ya kukata roho yaliashiria vitu viwili...
masikitiko na huruma kwa kutuacha Watanzania mikononi mwa manyang'au yasiyo na huruma.
Nikipata muda nitarudi niendeleee na hii makala na namna inavyowahusu wanafiki waliokuja kujitokeza baadaye kama
Mzee Mwanakijiji, Mwakyembe, Shivji na wengineo...