I got it! Mheshimiwa Spika mnataka kutuloga!!?

Maneno yangu yanasimama kama yalivyo; uzuri wa watu kuona Bunge rejea nilichosema wakati ule Nape alivyotoa hili pendekezo; bado niliamini Bunge ndio lina wajibu huo. Siamini na hakuna mtu amenishawishi hadi hivi sasa kuwa kuna haki ya kuona Bunge "live" kwa vile ni haki fulani. Sasa hapa gumu ni lipi hasa?
Hii coment yangu naamini umeiona japo unairuka.
"Hapana mkuu. Unajaribu kucheza tuu na maneno, lakini kitu ambacho kiko wazi kabisa ni kuwa umepiga u turn kubwa sana.
Kwamba mwaka 2013 ulijaribu hata kukiri kuwa "tukiwakubalia hili (la kutoonyesha bunge live) basi tuwe tayari kubong'oa mbele yao" mpaka leo unaandika makala ndeeeeefu kuwa "bunge kuonyeshwa live sio haki ya Mtanzania". Mtu yeyote mwenye akili ya kawaida tuu hawezi kuona kuwa hii ni sawa!! Ni mabadiliko makubwa sana;Ni mbingu na ardhi. Na kwa mtu mwenye uwezo wa kiuchambuzi na kiakili kama wako mabadiliko haya si ya bahati mbaya hata kidogo!!"
Mzee Mwanakijiji
 
Ni kazi sana kuitetea CCM ukitumia ajili yako ya kuzaliwa. Inawezekana tu kwa akili ya kushikiwa na ndo kazi inayompata MMK hapa.
 
Maneno yangu yanasimama kama yalivyo; uzuri wa watu kuona Bunge rejea nilichosema wakati ule Nape alivyotoa hili pendekezo; bado niliamini Bunge ndio lina wajibu huo. Siamini na hakuna mtu amenishawishi hadi hivi sasa kuwa kuna haki ya kuona Bunge "live" kwa vile ni haki fulani. Sasa hapa gumu ni lipi hasa?
Naona MM ameomalia "haki ya kuona bunge live". hatari moja ya msimamo wako ni kuonekana unatafuta "refuge" kwenye "semantics", unacheza na maneno, wakati zamani ulikuwa unaangalia "spirit". kuna ripoti ya Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, TLS, inayopatikana hapa : http://tls.or.tz/wp-content/uploads/2015/07/FOI-Research-Report_Final-Version1.pdf
"Kwa hali halisi kama ambavyo itafafanuliwa kwa kina katika tafiti hii, haki ya kupata taarifa Tanzania imekuwa si rahisi kupatikana kutokana na vikwazo kadha wa kadha ikiwemo kutokuwepo kwa mazingira wezeshi ya mfumo wa kisheria na urasimu katika taratibu za kiutawala ambazo huwa kisiki katika kupata haki ya taarifa. Kwa nyongeza, historia ya haki ya taarifa Tanzania inaeleza kwamba haki ya kupata taarifa imekuwa ikitafsiriwa mara kwa mara kama uwepo wa vyombo vya habari bila kutilia mkazo mantiki ya taarifa zinazosambazwa kwa umma.

Haki ya kupata taarifa ni moja ya msingi muhimu sana katika maendeleo. Haki hii imetafsiriwa na kujumuishwa katika mikataba ya kimataifa ya (kisheria na isiyo ya kisheria) ambayo Tanzania imetia saini. Pia ni moja wapo ya haki za binadamu ambazo zinalindwa kupitia kanuni za kimataifa na sheria za desturi za kimataifa (Mendel, 2007, Uk.1). Haki hii ipo katika mikataba mbali mbali ya kimataifa na kikanda kama vile:

i. Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu1948, Ibara ya 19;

ii. Mkataba wa kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa8 (ICCPR) chini ya Ibara ya 19 (2);

iii. Mkataba wa Aarhus (Mkataba wa haki ya kupata taarifa, ushiriki wa umma katika

kufanya maamuzi na ufikiaji wa haki katika mambo ya mazingira), Tume ya Uchumi

ya Umoja wa Mataifa wa Uchumi kwa ajili ya Ulaya, 25 Juni 1998;

iv. Mkataba wa Kupambana na Rushwa, Mkutano Mkuu-Azimio Na. 58/4 la Oktoba

31, 2003;

v. Maoni Na. 34, Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Septemba 12,

2011 ambayo inatafsiri Ibara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Kiraia na Kisiasa

(ICCPR) wa mwaka 1966 juu ya uhuru wa maoni na kujieleza;

vi. Mkataba wa Afrika wa Watu na Haki za Binadamu, 1981 Ibara ya 9;

vii. Azimio la Uhuru wa Kujieleza Afrika, 2002, inayothibitisha Haki ya taarifa Afrika;

viii. Azimio la Afrika juu ya Demokrasia, Chaguzi na Utawala Bora, Januari 30, 2007;

ix. Azimio la Afrika juu ya Maadili na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala, 2011

Ibara ya 6.

3.0.2 Mifumo ya Kisheria za Kitaifa

3.0.2.1 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Ibara ya 18 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2005) inatoa haki ya kutafuta, kupokea na kusambaza habari bila kufungwa/kuzuiliwa na mipaka ya kitaifa (Katiba ya JMT, 1977).

Katiba inakataza kuingiliwa kwa mawasiliano binafsi na wakati huo huo ina vifungu vyenye kutoa haki ya kupewa taarifa kwa wakati wote katika matukio mbalimbali ya nchi na duniani kwa ujumla ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na jamii. (HakiElimu et al, 2005).

Ibara ya 189 inaeleza kuwa, kila mtu:

(a) Ana uhuru wa kutoa maoni na kueleza mawazo yake;

(b) Ana haki ya kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa bila kujali mipaka ya kitaifa;

(c) Ana uhuru wa kuwasiliana na kupata ulinzi bila ya kuingiliwa mawasiliano yake;

na

(d) Ana haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu ya

maisha na shughuli za watu na pia masuala muhimu kwa jamii.

Hata hivyo, Katiba ya sasa haikutaja kwa vipengele kwamba haki na uhuru huo unaweza kutekelezwa kupitia vyombo vya habari kama ilivyoelezwa wazi katika ibara ya 18 (1)10 iliyopo katika toleo la awali. Kuondolewa huku katika katiba ya sasa imepelekea wadau wa vyombo vya habari kusema kuwa hakuna uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania (MCT, 2008).

Pamoja na hayo, ibara ya 30 (2) ya Katiba imeweka mipaka ya haki ya mtu mmoja kupata taarifa endapo inahatarisha haki za watu wengine au maslahi ya umma. Pia, katiba haitoi utaratibu wa kuhakikisha kwamba umma kwa ujumla na hasa watu walio katika mazingira ya vijijini na wasiojiweza kijamii na kiuchumi kuweza kupata taarifa muhimu, pia haitoi agizo la uwazi wa taarifa na adhabu dhidi ya mamlaka ambazo zitaficha taarifa au kukataa kutoa habari kwa umma".

Tuache kumung'unya maneno: watawala hawapendi mambo yao yajadiliwe waziwazi, hasa unapokuwa na vijana machachari ambao wanao uwezo wa kuyaweka wazi, na pia unao watu ambao wapo tayari kuwapa "data" hizo nyeti. inaaminika kwamba matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2015, ambayo yametoa ushindi mnono kwa wapinzani kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na huko nyuma, yamechangiwa na mambo kama haya ya kuonesha bunge live. lakini kwa data tu za utumbuaji majipu, inaonesha kweli hali ni mbaya sana. kwa hiyo serikali inataka kudhibiti "uozo" usianikwe mno, ili kupisha jitihada za Rais Magufuli kurudisha imani ya watu kwa serikali yao. Lakini mimi sidhani kama Serikali ina sababu ya kuogopa "kuvuliwa nguo". kama JK hakuogopa hayo yote, na hali ilikuwa namna ile, kwa nini Magufuli ahofie "uwazi", wakati anachapa kazi vizuri tu?
 
yaani solution na way foward hamna hapa, watu wana rely kwenye post ya mwanakijiji! baaasi! si wabunge si rai hakuna aliyeonyesha njia gani ifuatwe na nini kifanyike

tunaishia kulalama na kutafuta wachawi

Wewe kwani vipi? Hii post ni kuhusu kubongo'a kwa MM, wewe mkuu fungua post inayohusu "solution na way forward" tutakuja huko ku-discuss...
 
Tushalogwa tayari huenda hata mganga wa kutibua uchawi huu keshakufa kafara!
 
Mnapata shida sana..ugomvi uko kwenye kudai kama haki...na pe lendekezo langu lina simama. Badala ya kususa i gepigwa kuwa wabunge waamue. Lakini huwezi kudai kuwa ni haki. Na inawezekana kweli wanataka kutuloga! ..suala ni suala la haki...Ni vizuri. Kuona mijadala lakini huwezi kudai kuona kama suala la haki. Mnaofikiri nimejigeuka ni kwa sababu hamnisomi. Sijasema mahali popote sasa hivi kuwa si nambo jema au haifai bunge kuoneshwa "live" napo wengine kutokana na kufikiri nimesema nini wanashindwa kuelewa nilichosema.

Umenukuliwa ukisema hivi:

"Binafsi napinga, nalaani, na ninakataa kudharauliwa hivi. NInakataa kuonekana mjinga na kuwa sisathili kujua wale ambao wamechaguliwa na wananch na waliopita kuomba kura wengine kwa kupiga magoti na kulamba watu miguu leo wana ujasiri wa kusema 'tuwafiche wananchi waliotuchagua". Mtanisamehe - huu ni miongoni mwa maamuzi ya kipumbavu. Mtu mwenye akili akikushauri jambo la kijing akijua wewe nawe una akili halafu ukakubali atakudharau - alisema Baba wa Taifa. Wametuambia jambo la kijinga swali ni je tunajitambua na sisi tuna akili?"

Ndugu MM, uliwauliza watu wajiulize kama wanajitambua wana akili, sasa watu wenye akili zao wamekataa hayo maamuzi, wewe mwenzetu umebadilika unataka watu waende wakapigie kura "maamuzi ya kipumbavu"!!

Hiviii, na wewe mwenzetu unajitambua kama una akili?
 
Naona MM ameomalia "haki ya kuona bunge live". hatari moja ya msimamo wako ni kuonekana unatafuta "refuge" kwenye "semantics", unacheza na maneno, wakati zamani ulikuwa unaangalia "spirit". kuna ripoti ya Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, TLS, inayopatikana hapa : http://tls.or.tz/wp-content/uploads/2015/07/FOI-Research-Report_Final-Version1.pdf
"Kwa hali halisi kama ambavyo itafafanuliwa kwa kina katika tafiti hii, haki ya kupata taarifa Tanzania imekuwa si rahisi kupatikana kutokana na vikwazo kadha wa kadha ikiwemo kutokuwepo kwa mazingira wezeshi ya mfumo wa kisheria na urasimu katika taratibu za kiutawala ambazo huwa kisiki katika kupata haki ya taarifa. Kwa nyongeza, historia ya haki ya taarifa Tanzania inaeleza kwamba haki ya kupata taarifa imekuwa ikitafsiriwa mara kwa mara kama uwepo wa vyombo vya habari bila kutilia mkazo mantiki ya taarifa zinazosambazwa kwa umma.

Haki ya kupata taarifa ni moja ya msingi muhimu sana katika maendeleo. Haki hii imetafsiriwa na kujumuishwa katika mikataba ya kimataifa ya (kisheria na isiyo ya kisheria) ambayo Tanzania imetia saini. Pia ni moja wapo ya haki za binadamu ambazo zinalindwa kupitia kanuni za kimataifa na sheria za desturi za kimataifa (Mendel, 2007, Uk.1). Haki hii ipo katika mikataba mbali mbali ya kimataifa na kikanda kama vile:

i. Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu1948, Ibara ya 19;

ii. Mkataba wa kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa8 (ICCPR) chini ya Ibara ya 19 (2);

iii. Mkataba wa Aarhus (Mkataba wa haki ya kupata taarifa, ushiriki wa umma katika

kufanya maamuzi na ufikiaji wa haki katika mambo ya mazingira), Tume ya Uchumi

ya Umoja wa Mataifa wa Uchumi kwa ajili ya Ulaya, 25 Juni 1998;

iv. Mkataba wa Kupambana na Rushwa, Mkutano Mkuu-Azimio Na. 58/4 la Oktoba

31, 2003;

v. Maoni Na. 34, Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Septemba 12,

2011 ambayo inatafsiri Ibara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Kiraia na Kisiasa

(ICCPR) wa mwaka 1966 juu ya uhuru wa maoni na kujieleza;

vi. Mkataba wa Afrika wa Watu na Haki za Binadamu, 1981 Ibara ya 9;

vii. Azimio la Uhuru wa Kujieleza Afrika, 2002, inayothibitisha Haki ya taarifa Afrika;

viii. Azimio la Afrika juu ya Demokrasia, Chaguzi na Utawala Bora, Januari 30, 2007;

ix. Azimio la Afrika juu ya Maadili na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala, 2011

Ibara ya 6.

3.0.2 Mifumo ya Kisheria za Kitaifa

3.0.2.1 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Ibara ya 18 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2005) inatoa haki ya kutafuta, kupokea na kusambaza habari bila kufungwa/kuzuiliwa na mipaka ya kitaifa (Katiba ya JMT, 1977).

Katiba inakataza kuingiliwa kwa mawasiliano binafsi na wakati huo huo ina vifungu vyenye kutoa haki ya kupewa taarifa kwa wakati wote katika matukio mbalimbali ya nchi na duniani kwa ujumla ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na jamii. (HakiElimu et al, 2005).

Ibara ya 189 inaeleza kuwa, kila mtu:

(a) Ana uhuru wa kutoa maoni na kueleza mawazo yake;

(b) Ana haki ya kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa bila kujali mipaka ya kitaifa;

(c) Ana uhuru wa kuwasiliana na kupata ulinzi bila ya kuingiliwa mawasiliano yake;

na

(d) Ana haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu ya

maisha na shughuli za watu na pia masuala muhimu kwa jamii.

Hata hivyo, Katiba ya sasa haikutaja kwa vipengele kwamba haki na uhuru huo unaweza kutekelezwa kupitia vyombo vya habari kama ilivyoelezwa wazi katika ibara ya 18 (1)10 iliyopo katika toleo la awali. Kuondolewa huku katika katiba ya sasa imepelekea wadau wa vyombo vya habari kusema kuwa hakuna uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania (MCT, 2008).

Pamoja na hayo, ibara ya 30 (2) ya Katiba imeweka mipaka ya haki ya mtu mmoja kupata taarifa endapo inahatarisha haki za watu wengine au maslahi ya umma. Pia, katiba haitoi utaratibu wa kuhakikisha kwamba umma kwa ujumla na hasa watu walio katika mazingira ya vijijini na wasiojiweza kijamii na kiuchumi kuweza kupata taarifa muhimu, pia haitoi agizo la uwazi wa taarifa na adhabu dhidi ya mamlaka ambazo zitaficha taarifa au kukataa kutoa habari kwa umma".

Tuache kumung'unya maneno: watawala hawapendi mambo yao yajadiliwe waziwazi, hasa unapokuwa na vijana machachari ambao wanao uwezo wa kuyaweka wazi, na pia unao watu ambao wapo tayari kuwapa "data" hizo nyeti. inaaminika kwamba matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2015, ambayo yametoa ushindi mnono kwa wapinzani kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na huko nyuma, yamechangiwa na mambo kama haya ya kuonesha bunge live. lakini kwa data tu za utumbuaji majipu, inaonesha kweli hali ni mbaya sana. kwa hiyo serikali inataka kudhibiti "uozo" usianikwe mno, ili kupisha jitihada za Rais Magufuli kurudisha imani ya watu kwa serikali yao. Lakini mimi sidhani kama Serikali ina sababu ya kuogopa "kuvuliwa nguo". kama JK hakuogopa hayo yote, na hali ilikuwa namna ile, kwa nini Magufuli ahofie "uwazi", wakati anachapa kazi vizuri tu?
Mimi Mwanakijiji hebu pitia hapa mkuu. Upinge na hii mikataba [emoji125] [emoji124] [emoji125] [emoji124]
 
Ni bahati mbaya sana wasomi wetu wsmekuwa wachumia tumbo. Anatetea kinachoshibishs tumbo lake tu!
 
Hii coment yangu naamini umeiona japo unairuka.
"Hapana mkuu. Unajaribu kucheza tuu na maneno, lakini kitu ambacho kiko wazi kabisa ni kuwa umepiga u turn kubwa sana.
Kwamba mwaka 2013 ulijaribu hata kukiri kuwa "tukiwakubalia hili (la kutoonyesha bunge live) basi tuwe tayari kubong'oa mbele yao" mpaka leo unaandika makala ndeeeeefu kuwa "bunge kuonyeshwa live sio haki ya Mtanzania". Mtu yeyote mwenye akili ya kawaida tuu hawezi kuona kuwa hii ni sawa!! Ni mabadiliko makubwa sana;Ni mbingu na ardhi. Na kwa mtu mwenye uwezo wa kiuchambuzi na kiakili kama wako mabadiliko haya si ya bahati mbaya hata kidogo!!"
Mzee Mwanakijiji

Hata mechi za Yanga na Simba huwa sio 'live' kwa amri ya kamati zao za ufundi na tamaa ya pesa.
 
Uamuzi wa Bunge kuamua kuleta pendekezo kwenye kikao kijacho kuwa Bunge lisioneshwe moja kwa moja kwa mamilioni ya wananchi wa Tanzania ndani na nje ni uamuzi unaofanana na kikao cha wachawi. Sijui ni nani aliyekuja na wazo hili sasa hivi baada ya wazo hilo kutupwa miezi michache huko nyuma. Lakini kwamba sasa umekuwa ni uamuzi rasmi na kwamba wapo watu wenye akili timamu bungeni wamefikia uamuzi huu ni lazima niulize kama hawa ndugu zetu si vigagula!

Wanachoogopa hawa watu wa Bunge kwa wananchi kuona moja kwa moja vikao vya Bunge ni nini? Kwamba wananchi watawaona wabunge wenye kutoa hoja zisizo na mashiko na hivyo wabunge hao wataanza kupunguza ujiko waliodhania kuwa wanao? Ama wanaogopa kuwa kwa kadiri wananchi wanavyozidi kuwaona wabunge wao wanavyobishana na kulumbana basi kule kulegalega kwa Bunge kutazidi kuwa dhahiri? Au wanaogopa kuona kuwa wananchi watazidi kuona kupwaya kwa serikali yao? Au wanaogopa zaidi kibinafsi kuwa waliodhaniwa kuwa ni viongozi kumbe si lolote na si chochote? Au wanaogopa watu kuona jinsi sera za CCM zisivyoweza kutetewa na jinsi ambavyo kwenye kila kikao sera hizo zikioneshwa kuwa hazitekelezeki huku majibu ya "serikali ina nia" na "serikali iko njiani" yakiendelea kutolewa kwa miaka hamsini sasa?
Siongezi neno.
 
aisee! haujajibu kitu

naomba writeup ya mbunge yeyote wa upinzani au ccm aliyplekea mahali popote pale humu ndani ili TBC ionyeshe matangazo! just that

yaani usikite Alinda mimi na wewe tuko pamoja haunielewi tu, ila hao wawakilishi wetu ndio hawafanyi wajibu wao

halafu at the end, mwanakijiji ndio anakuwa kama ndio Mbowe mwenyewe
Hoja binafsi ngapi zimekataliwa kwa kusema hawana muda wa kuzipokea?

Na sio kila kitu mbunge au rais kuna mambo mengine wananchi tunatakiwa kusimama pamoja imara
 
Back
Top Bottom