I got it! Mheshimiwa Spika mnataka kutuloga!!?

I got it! Mheshimiwa Spika mnataka kutuloga!!?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,240
Reaction score
44,487
42470281_bbc72ccff5_o.jpg


Vikao vya wachawi hufanyika kwa siri. Sasa sijui kama uchawi upo na una nguvu au ni imani tu lakini ukweli ni kuwa wapo watu wanaamini katika nguvu za uchawi. Vikao vya wachawi hawaalikwi waandishi wa habari. Sababu kubwa ni kuwa vikao hivyo vinahusiana na mambo ya kudhuru zaidi kuliko kitu kingine chochote. Wachawi basi hupenda mambo yao yawe ya siri sana.

Mtu anapoamua kwenda kutafuta msaada wa wachawi (ni wale waganga wa kienyeji wenye uwezo wa kudhuru) ni kwa sababu ameshindwa kukabiliana na kile alichokiona kuwa ni tishio. Mara zote watu wanapoamua kutafuta msaada huo ni kwa sababu wanaamini mbinu za kawaida za kukabiliana na mtu zimeshindikana. HIli ni kweli siyo katika Afrika tu bali hata katika mataifa mengine ambayo imani hizi za kishirikina zipo.

Kwa vile vikao vya wachawi ni vya siri basi ndio maana havirushwi 'live' ila nina uhakika kama tukiwapa nafasi warekodi vikao vyao makaburini watatupatia 'edited versions' ya vikao hivyo. Unafikiria watakapoleta hayo matoleo yaliyohaririwa wataonesha nani wanapanga kumla nyama? Wachawi hawaachi hadi wakamatwe! Sasa kama ni kweli upo uchawi mimi sijui; ila kwamba wapo watu wanaoamini nguvu zake hilo halina shaka. Na kwa wale wenye kuamini nguvu zake, uchawi ni tishio kubwa sana kwani mambo yanayofanywa na wachawi yanavunja kanuni zote zinazojulikana za Fizikia.

Uamuzi wa Bunge kuamua kuleta pendekezo kwenye kikao kijacho kuwa Bunge lisioneshwe moja kwa moja kwa mamilioni ya wananchi wa Tanzania ndani na nje ni uamuzi unaofanana na kikao cha wachawi. Sijui ni nani aliyekuja na wazo hili sasa hivi baada ya wazo hilo kutupwa miezi michache huko nyuma. Lakini kwamba sasa umekuwa ni uamuzi rasmi na kwamba wapo watu wenye akili timamu bungeni wamefikia uamuzi huu ni lazima niulize kama hawa ndugu zetu si vigagula!

Wanachoogopa hawa watu wa Bunge kwa wananchi kuona moja kwa moja vikao vya Bunge ni nini? Kwamba wananchi watawaona wabunge wenye kutoa hoja zisizo na mashiko na hivyo wabunge hao wataanza kupunguza ujiko waliodhania kuwa wanao? Ama wanaogopa kuwa kwa kadiri wananchi wanavyozidi kuwaona wabunge wao wanavyobishana na kulumbana basi kule kulegalega kwa Bunge kutazidi kuwa dhahiri? Au wanaogopa kuona kuwa wananchi watazidi kuona kupwaya kwa serikali yao? Au wanaogopa zaidi kibinafsi kuwa waliodhaniwa kuwa ni viongozi kumbe si lolote na si chochote? Au wanaogopa watu kuona jinsi sera za CCM zisivyoweza kutetewa na jinsi ambavyo kwenye kila kikao sera hizo zikioneshwa kuwa hazitekelezeki huku majibu ya "serikali ina nia" na "serikali iko njiani" yakiendelea kutolewa kwa miaka hamsini sasa?

Lakini mimi nafikiria kuna sababu nyingine ya kutisha zaidi - wanataka kuturoga. Nadhani jaribio lao lile la "unga unga Bungeni" lilikuwa ni jaribio la kwanza kutaka kuliroga taifa zima tuwe mazezeta tusiofikiri, tusiouliza maswali na wenye kuamini kila tunaloambiwa na watawala. Kwa vile ndumba zile nusura zinaswe kwenye luninga jaribio lao la kuturoga lilishindikana. Matokeo yake ni kuwa wananchi wamefunguka zaidi na kuwaelewa wabunge wao; wameilewa serikali yao na kwa kweli wananchi hawakumwogopa kabisa mchawi wao. Aliyedhaniwa ni mchawi mkuu wa taifa aligundulika kuwa ni kilaza tu tena tapeli.

Sasa inaonekana wanataka kujaribu tena. Lakini katika kujaribu huku wameficha nyuma yake dharau. Wametudharau Watanzania na dharau ambayo kwa kweli inapita kwa mbali matusi ambayo Spika na Naibu wake wanadaiwa kutumiwa kwa sms. Maana kudharau taifa zima kwa kweli inataka moyo! Wanaweza vipi kuamua tu kuwa "hatutaki Watanzania watuone tunavyozungumzia mambo yao hadi tuamue tuwaoneshe nini". Sasa kama hii siyo dharau ya taifa (contempt of the nation) tuiite nini? Kwanini wasiamue tu kuvunja Bunge au wafanyie vikao kwenye jumba la spika lile jipya? Au waende kwenye nyumba ya Waziri Mkuu? au wakitaka wakafanyie vichakani baada ya kulishana yamini kwanza!?

Binafsi napinga, nalaani, na ninakataa kudharauliwa hivi. NInakataa kuonekana mjinga na kuwa sisathili kujua wale ambao wamechaguliwa na wananch na waliopita kuomba kura wengine kwa kupiga magoti na kulamba watu miguu leo wana ujasiri wa kusema 'tuwafiche wananchi waliotuchagua". Mtanisamehe - huu ni miongoni mwa maamuzi ya kipumbavu. Mtu mwenye akili akikushauri jambo la kijing akijua wewe nawe una akili halafu ukakubali atakudharau - alisema Baba wa Taifa. Wametuambia jambo la kijinga swali ni je tunajitambua na sisi tuna akili?

Nina pendekezo - kama kweli uamuzi huu utachukuliwa naomba uchukuliwe hadharani angalau mara hiyo moja kabla hawajaacha kurusha matangazo wapigiwe kura ya kuitwa majina (roll call) ili tujue wabunge wetu ambao wanataka kutuficha wanachofanya Bungeni ni kina nani? Na kama kuna wabunge wa upinzani wanaofikiri hili ni jambo jema wasimame na waseme sasa; kama wapo wabunge wa CCM wanaamini kuwa hili ni jambo jema wasimame na wajitaje kwa majina yao Bungeni kuwa wanaunga mkono kuwaficha wananchi waliowaajiri kujua nini wanafanya.

Angalau tutawajua wachawi wetu kwa majina yao!

Na. M. M. Mwanakijiji
 
Mkuu Mwanakijiji, naona Madame Spika anataka kulivunja Bunge kabisaaaa. Ameshaanza na Kamati, kinachofuata ni kulivunja lote. Sasa uamuzi kama huu nadhani haoni sababu ya kuupeleka hewani moja kwa moja (live), badala yake ameona kiporo ndio kinatufaa sisi Watz. Na amini usiamini watakaosema Ndiyooooooooo watashinda kwa kishindo.
 
Hii hoja ikifika bungeni itapita maana CCM ni wengi. Lakini ili kutumhukumu mtu kimakosa, naunga mkono wazo la kutaka kila mbunge aitwe (mmoja mmoja) wakati wa kupiga kura, ili wananchi wajue pasi na shaka kuwa nani anataka vikao vya bunge viwe siri, na nani anataka bunge liendeshwe kwa uwazi.

Kila mtu ahukumiwe kwa matendo yake.
 
Udikteta wa Hitler haukuanza siku mmoja, alianza taratibu kama tunavyoyaona sasa, mwisho ukawa dikteta halisi. Hata kauli ya Rais kwamba Polisi wasiogope Lawama imenisononesha sana. Lazima tuilaani hatua hii ya kuipeleka nchi kwenye udikteta. Nadhani hata baba zao wanaowafadhili (wahisani) hawatakaa kimya ktk hili. Let us see.
 
Tanzania Jumbe ni kweli inaongoza kwa imani za kichawi, hata wanasiasa mnaamini kuwa mnaweza kulogwa! Mmeshaloga wangapi hadi mpate hofu hiyo?
 
Hii hoja ikifika bungeni itapita maana CCM ni wengi. Lakini ili kutumhukumu mtu kimakosa, naunga mkono wazo la kutaka kila mbunge aitwe (mmoja mmoja) wakati wa kupiga kura, ili wananchi wajue pasi na shaka kuwa nani anataka vikao vya bunge viwe siri, na nani anataka bunge liendeshwe kwa uwazi.
Kila mtu ahukumiwe kwa matendo yake.
FJM,
Hawatakubali kufanya hivyo kwa sababu nao wanataka warudishwe bungeni 2015. Kwa hiyo, utaratibu ule ule wa siku zote; Ndiyooooooo!!!
Napendekeza wabunge wa Chadema watoe sauti kubwa ya kupinga jambo hili kwa nguvu zote, kama siyo kutoka nje basi iwe staili yo yote inayofaa ya kupambana humo humo ndani.
 
Yaani sijui nisemeje,inachosha kwakweli.

Watanzania wenzangu kweli tunaweza kuendeshwa namna hii kama mataahira? Watu wanapata wapi huu ujasiri wa hata kujaribu kutamka haya hadharani alafu tukawaacha?

Hiki ni kiburi na ni dhahiri wapinzani wasipojiandaa sasa CCM hawako tayari kuachia madaraka kwa amani! Tujiandae Watanzania,Maana hii si siasa tena bali uhaini! Bunge kuonyeshwa live imekuwa hisani tena!!!

Nafikiri imetosha sasa!!!!
 
Nikwamba bunge kua live sio matakwa yawabunge,duniani kote nilazima bunge liwe hewani,ambae ataki ajiuzuru ubunge na usgika.hii haihitaji mjadala wakiamua watakua wanatafuta makubwa maana tutakwenda dodoma kwa mguu na wataisoma namba,hua inafikia mahali punda anagoma kwenda wajaribu na ndio maana tbc ilikua inavunga kukatakata sasa tutajua nani nikibarua kwa mwenzie
 
Kama bunge linataka kufanya mapenzi basi ni sawa wanaweza kujifungia na kufanya mapenzi yao na nashauri ikiwezekana lifanyike usiku ili mapenzi yao yanoge zaidi...

Lakini kama bunge linataka kujadili mustakabali wa nchi hii basi hapa hakuna hisani tena ... wananchi ambao ndio tumewapeleka bungeni tunayo haki ya kujuwa ni nini kinajadiliwa kwa mustakabali wa nchi yetu.

kama wabunge wataongea pumba - tutajua, watakaosigina demokrsia-tutajua .. mwisho wa siku tutaamua mbivu na mbichi...

spika na naibu wake wasikimbie vivuli vyao....
 
MMM, safi sana kwa mada yako na pendekezo lako pia. Wabunge wanao unga mkono hoja ya kufuta utaratibu wa kurusha hewani (LIVE) vikao vya bunge waamue kwa kusaini. Utaratibu wa Spika kuwahoji na kujibu kwa pamoja Ndiyoooooo au Hapaaana usitumike hapa. Ikiwezekana Wabunge wapeleke Bungeni Hoja ya kutaka kubadilisha mfumo huu wa spika kuhoji wabunge kwa hapana na ndiyo ili kuuunga mkono hoja ama la. Mfumo wa sasa si sahihi. Sisi Wananchi waajili wao tunataka kila mbunge aseme hayo kwa mkono wake.
 
Basi tena kama hili watalipitisha hakuna haja ya uchaguzi.Laana hii haitawacha kamwe.
Chonde Chonde Chadema jambo hili mulifikishe kwenye Mahakama ya wananchi hata kabla hawaja leta hoja hii Bungeni .

Lakini kwa vile Mch.Mtikila anamauzoefu na kesi hizi za Kikatiba Chadema na Vyama vingine wanaweza kumshawishi na kumsapoti Mchungaji Kufungua Kesi ,maana Kikatiba kila moja anahaki ya kupata habari na hasa inayohusu uendeshaji wa Serikali.
 
Huyu Mama hashauriki, chochote mtakachomshauri ataenda kuuliza kwa mzee wa LIWALO NA LIWE na yeye ataenda kuuliza kwa FASTJET na mwisho wa siku maamuzi ya fastjet ndio yanaongoza bunge. Hakuna bunge hii miaka mi5. I miss u Samwel Sitta, you are Legend
 
Yaani sijui nisemeje,inachosha kwakweli.

Watanzania wenzangu kweli tunaweza kuendeshwa namna hii kama mataahira? Watu wanapata wapi huu ujasiri wa hata kujaribu kutamka haya hadharani alafu tukawaacha?

Hiki ni kiburi na ni dhahiri wapinzani wasipojiandaa sasa CCM hawako tayari kuachia madaraka kwa amani! Tujiandae Watanzania,Maana hii si siasa tena bali uhaini! Bunge kuonyeshwa live imekuwa hisani tena!!!

Nafikiri imetosha sasa!!!!

.........

Yes,uko sahihi mkuu serikali ya ccm na bunge lao wanataka kutupeleka mahali ambapo siyo na
inaonyesha kweli wamedhamiria kutoachia madaraka hata kwa kumwaga damu.

Ina maana matumizi ya kodi zetu inaonekana ni hisani sisi kuona kweli jamaa wanatufanya ni maboga"
 
Kiukweli watanzania katika hili tunatakiwa tusimame na kutaka kuwa kila mbunge asiyetaka bunge lirushwe
Live asaini na ijulikane nani na nani ambao hawataki tuwaone wanachokifanya bungeni"
 

....Au wanaogopa watu kuona jinsi sera za CCM zisivyoweza kutetewa na jinsi ambavyo kwenye kila kikao sera hizo zikioneshwa kuwa hazitekelezeki huku majibu ya "serikali ina nia" na "serikali iko njiani" yakiendelea kutolewa kwa miaka hamsini sasa?....

Asante Mzee Mwanakijiji
 
Waondoe kabisa na vikao vya Bunge, ikibidi wawe wanafanya vikao facebook, au wafungue mtandao wawe wanafanya online conference (itakupunguza na gharama) au kama vipi waendeshe vikao kwa sms, ukizingatia Bunge ni rubber stamp ya yale yote wanayotaka kufanya na hakuna jipya....
 
Back
Top Bottom