Nadhani watu mnapata shida; kwa sababu labda kusoma ni kugumu au kuelewa ni kugumu. Hakuna ubaya wowote wa TV kuoneshwa "live". Sijawahi kusema "ni vibaya kuonesha TV" au ni "haipaswi watu kuona kinachoendelea Bungeni". Sababu iliyotolewa wakati ule ilikuwa ni sababu ya kipuuzi kutaka kuzuia kurusha TV "live", sababu iliyotolewa sasa hivi siyo ya wakati ule - sidhani kama watu wanaona tofauti. Lakini zaidi labda inabidi niendeleee kuwaelimisha wengine. Wanaodai hadi kususa waonekane kwenye TV wanazungumzia suala la haki yao kuonwa au kurusha matangazo live. Hii haki haipo.
Nadhani ipo haja ya kuchukua hatua ya lazima ya kuufunga huu mjadala tena.