Huyu single mother nasitisha mara moja kumuoa

Hapo vip!!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mimi ni mtu ambaye nilikuwa siamini katika kumuoa single mother ila baadaye nikajikuta nimekutana na single mother nikaona nitengue msimamo wangu ila kwa hili msimamo wangu narudi kuiheshimu.

Mnamo mwaka huu mwezi wa January, nimekutana na mdada mmoja ambaye tulimaliza naye chuo, na kwa bahati nzuri nilikuwa nasoma naye course moja na pia tulikuwa group moja kwenye discussion. Hivyo na mfahamu kwa kiasi alikuwa ni binti mwenye msimamo kwenye mahusiano.

Kipindi hicho sikuweza kumtongoza kwasababu nilikuwa nipo kwenye stress kubwa wakati nasoma university.

Ila ilikuwa namkubali kubali kiasi, ila wakati tukiwa mwaka wa tatu akakutana na jamaa alikuwa ni graduate na anakazi. Jamaa akafanikiwa kumuweka kwenye himaya yake. Kwangu haikuniumiza sana kwa kwasababu sikuwahi kumtongoza akanitoe nje.

Siku zikaenda jamaa akaenda kujitambulisha kwa binti, ikapangwa mpaka siku ya harusi na vitu kwa hivyo.

Jamaa akawa anahairisha harusi mara kwa mara ila kafanikiwa kuzaa naye mtoto, ila baadaye wakaingia kwenye misuguano wakavunja uhusiano na sababu mwanamke anasema jamaa alikuwa na mwanamke mwingine na mpaka sasa eti jamaa anaishi naye na amezaa naye mtoto, anyway mwanamke akamchukua yule mtoto aliyezaa na jamaa akampeleka kwa wazazi wake.

Mpaka nakutanane naye ameachana na jamaa na kwa takribani miaka mitatu. Anyway baada ya kunieleza hayo kwa uchungu nikaanza naye mahusiano baadaye nikaona kwasababu ni mwanamke ambaye namfahamu kitabia tokea nikiwa chuo acha nifumbe macho nifanye haraku za kuweka ndani kwa heshima.

Anyway baada ya kuanza naye mahusiano akapata ujauzito nikaona ili nisimkweze na aone nipo sereous naye ngoja nikamtambulishe, nikampeleka home kwa utambulisho.

Nikawa nimebakiza kibarua ya kwenda kwao ambaye mpaka sasa sijaenda bado.

Sasa leo akanipigia simu akaniambia amepata msiba, nikamuuliza nani akasema baba mkwe wake wa zamani na waenda na dada yake. Anyway sikutaka kumcrash.

Ila nimeona nipate muda wakutafsiri hiyo picture na kujiuliza maswali mengi.

1. Binafsi najiuliza kama ametoka misri na ameamua kwenda Caana kwanini anarudi nyuma

2. Na kama wameachana na hawakufunga ndoa na ameshatambulishwa katika familia nyingine anaenda kule kama nani...?na kwasababu gani hasa...?

Binafsi nikaona huyu anacheza na akili yangu kwasababu kama yupo sereous akesahau kule pa zamani na kusonga mbele na njia mpya...

Mimi ni mtu ni kazi yangu na biashara zangu, sasa naona kwasababu hana kazi labda anaona apate mahali ambapo atapunguza makali fulani ya stress za mahusiono na maisha may be.

Binafsi naona niwe naye karibu amzee yule kiumbe then niangalie ustarabu mwingine ila asilani sintoweza kumoa tena...m
Unakaribishwa kwa ushauri
Hakuna baya hapo, yumkini marehemu na mkwe Bwana zamani walikuwa wanaelewana vizuri ..... Labda kama hukumpenda kwa dhati mkuu.
 
Mbona sioni tatizo hapo, kumbuka wawili hao wameunganishwa na mtoto/watoto, it's obvious kwamba kukiwa na tatizo upande wowote lazima wahusiane, like it or not.

Muunganiko wa wawili hao upo relevant as long as mtoto/watoto wapo kwenye equation, bear it in your SKULL...

The best solution ni wewe kutembea mbele maana sioni ukiweza kuhimili hizo purukushani.
Hajitambui huyo binti.
Kwanza, Huo msiba hauna umuhimu kivile na wala hauhusiani na mtoto moja kwa moja.
Pili, kama ilikuwa lazima aende angetakiwa kuomba ruhusa au ushauri kwa mchumba wake wa sasa hivi ila alikuwa keshaamua yeye akampa taarifa tu

Tatu, mwanamke anayejitambua hawezi kubeba mimba mara mbili kwa ahadi tu ys kuolewa
 
Hapo vip!!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mimi ni mtu ambaye nilikuwa siamini katika kumuoa single mother ila baadaye nikajikuta nimekutana na single mother nikaona nitengue msimamo wangu ila kwa hili msimamo wangu narudi kuiheshimu.

Mnamo mwaka huu mwezi wa January, nimekutana na mdada mmoja ambaye tulimaliza naye chuo, na kwa bahati nzuri nilikuwa nasoma naye course moja na pia tulikuwa group moja kwenye discussion. Hivyo na mfahamu kwa kiasi alikuwa ni binti mwenye msimamo kwenye mahusiano.

Kipindi hicho sikuweza kumtongoza kwasababu nilikuwa nipo kwenye stress kubwa wakati nasoma university.

Ila ilikuwa namkubali kubali kiasi, ila wakati tukiwa mwaka wa tatu akakutana na jamaa alikuwa ni graduate na anakazi. Jamaa akafanikiwa kumuweka kwenye himaya yake. Kwangu haikuniumiza sana kwa kwasababu sikuwahi kumtongoza akanitoe nje.

Siku zikaenda jamaa akaenda kujitambulisha kwa binti, ikapangwa mpaka siku ya harusi na vitu kwa hivyo.

Jamaa akawa anahairisha harusi mara kwa mara ila kafanikiwa kuzaa naye mtoto, ila baadaye wakaingia kwenye misuguano wakavunja uhusiano na sababu mwanamke anasema jamaa alikuwa na mwanamke mwingine na mpaka sasa eti jamaa anaishi naye na amezaa naye mtoto, anyway mwanamke akamchukua yule mtoto aliyezaa na jamaa akampeleka kwa wazazi wake.

Mpaka nakutanane naye ameachana na jamaa na kwa takribani miaka mitatu. Anyway baada ya kunieleza hayo kwa uchungu nikaanza naye mahusiano baadaye nikaona kwasababu ni mwanamke ambaye namfahamu kitabia tokea nikiwa chuo acha nifumbe macho nifanye haraku za kuweka ndani kwa heshima.

Anyway baada ya kuanza naye mahusiano akapata ujauzito nikaona ili nisimkweze na aone nipo sereous naye ngoja nikamtambulishe, nikampeleka home kwa utambulisho.

Nikawa nimebakiza kibarua ya kwenda kwao ambaye mpaka sasa sijaenda bado.

Sasa leo akanipigia simu akaniambia amepata msiba, nikamuuliza nani akasema baba mkwe wake wa zamani na waenda na dada yake. Anyway sikutaka kumcrash.

Ila nimeona nipate muda wakutafsiri hiyo picture na kujiuliza maswali mengi.

1. Binafsi najiuliza kama ametoka misri na ameamua kwenda Caana kwanini anarudi nyuma

2. Na kama wameachana na hawakufunga ndoa na ameshatambulishwa katika familia nyingine anaenda kule kama nani...?na kwasababu gani hasa...?

Binafsi nikaona huyu anacheza na akili yangu kwasababu kama yupo sereous akesahau kule pa zamani na kusonga mbele na njia mpya...

Mimi ni mtu ni kazi yangu na biashara zangu, sasa naona kwasababu hana kazi labda anaona apate mahali ambapo atapunguza makali fulani ya stress za mahusiono na maisha may be.

Binafsi naona niwe naye karibu amzee yule kiumbe then niangalie ustarabu mwingine ila asilani sintoweza kumoa tena...m
Unakaribishwa kwa ushauri
Kumuacha kwa sababu hiyo sioni kama ni sahihi... Usisahau aliyefariki ni babu wa mwanae
 
Usijumuishe, wote hao wanasahaulika vizuri tu ambae hasahauliki ni aliyekupatia kunako mahala huyo ndo haswaa Ni ngumu kumsahau
[emoji23][emoji23] ongea lugha ya taifa mkuu

Inamaana baba mtoto unaweza kumsahau ila yule aliyeiva Kwenye 6×6 ndio anabaki moyoni???

Daah aisee wanawake ni viumbe wengine kabisa[emoji23][emoji23]
 
Aina yetu ya kufikiri haifanani,

Halafu kusahau nakokuzungumzia Ni ile kumkumbuka mtu ukapata msisimko wa kihisia
Isitoshe kuna ambao tuna roho ngumu ukitupa jongoo unatupa na mti wake na kusonga mbele Kama injili
 
Maisha mengine hayana tofauti na enzi za utumwa. Kumbuka huyo dada alishatengeneza uhusiano na ile familia na kama walikuwa wameshafikia hatua ya kutangaza ndoa ni hatua ambayo familia za pande zote mbili zinafahamiana. Kama ilitokea kuachana na tayari walikuwa na mtoto sio rahisi kuweka uadui wakati wameunganisha damu.. inawezekana hakuna ule upendo uliokuwepo mwanzoni kabla ya kuachana ila hakuna uadui mkubwa wa kumfanya yule dada asihudhurie hata msiba wa watu wa karibu na nwanaume aliyezaa nae.Muache kuona wanawake kama viumbe wasiojitambua . natamani kuona wanawake wakiishi maisha yao kwa kujiamini na kujipa thamani kubwa. Hao mnaowaita single mom sio kwamba walipenda japo kuna wengine naweza walaumu kama walioingilia ndoa za watu na kuzaa au waliotegesha mimba ili wapendwe..ila sio wote wana historia moja. Kikubwa mwanamke ukishaona mwanaume amekuacha na mtoto pambana na maisha mpende mwanao na kumlea vizuri na ukiwa vizuri kiuchumi hakuna mtu atayekuletea dharau hata kidogo. Kudharaulika kunakuja pale ambapo huna kipato na unakuwa tegemezi na unayemtegemea anakuona una mtoto wa mwanaume mwingine..
 
Mimi nadhani kitendo cha kushiriki msiba wa ba mkwe sio kosa sana labda awe hajakuomba ruhusa.Kama ni mwaminifu ni mwaminifu tu na kama sio ni sio.Mfano hata ungepata single mother ambae ni mjane kama wengi walivyosema kwamba ukitaka kuoa single mother uhakikishe umeona kaburi la mumewe,mbona Kuna kesi nyingi tu za watu kua na mahusiano na shemeji au baba wakwe?hao nao tutawazungumziaje?Pia unaweza kupata ambae sio single mother na mkaoana vizuri Ila badae akakuchit kwa jamaa mwingne kisiri siri.wapo wanawake wengi tu huchit waume zao ila hawakuolewa wakiwa single mother.
Mkwe wa nani?
 
Du naandika ,nafuta any way pambana mkuu .ila kuhusu kwenda msibani hapo si kwa mzazi mwenzie ?.Ila uchunge lazima watabust ,hawaachanagi hawa viumbe
Mzazi mwenzie na wakati wameachana anaenda kweny msiba wa uyo mzee kufanya nn sasa ujue mambo mengi muda mwingine wanawake wenyewe uwa wanayaharibu maisha yao arafu usingizia wanaume wabaya dah....
 
Mbona sioni tatizo hapo, kumbuka wawili hao wameunganishwa na mtoto/watoto, it's obvious kwamba kukiwa na tatizo upande wowote lazima wahusiane, like it or not.

Muunganiko wa wawili hao upo relevant as long as mtoto/watoto wapo kwenye equation, bear it in your SKULL...

The best solution ni wewe kutembea mbele maana sioni ukiweza kuhimili hizo purukushani.
Na hatoziweza kweli
 
Unajua watu wengi hasa wanawake wanashindwa kutofautisha vitu kadhaa katika mapenzi vinavyoleta taflani ,mfano ni vigumu sana kukabili pale mpenzi wako au mke anapokuwa na urafiki na mwanaume mwingine haijalishi katika stage gani undugu,ujirani,workmate n.k

Na hauitaji kuprove kwamba ana cheat au acheat ndio maana wewe unaweza kuondoka nyumbani mwaka mzima na kumuacha mkeo na wala usiwe na wasiwasi

Lakini siku moja tu ukiwa nae akawa anaongea na simu na mtu mwingine mambo ya kawaida tu roho lazima ikupasuke na inawezekana ikawa ndio mwanzo wa mgogoro wenu,hapa unasahau kama mwaka mzima ulimuacha peke yake ivyo alikuwa anaweza kuwa anafanya anachokitaka

Hapa jamaa kinachomuuma ni huyo Ke kumpa appreciation huyo mzazi mwenzie kwa kuonyesha anajali tatizo lake la msiba, Wanawake wengi jambo ili hawalijui wanahisi mambo yapo kama wanavyotaka wao kumbe sisi wanaume tunajaji katika dimesion nyingine kabisa...wanaume tuna wivu sana
 
Aina yetu ya kufikiri haifanani,

Halafu kusahau nakokuzungumzia Ni ile kumkumbuka mtu ukapata msisimko wa kihisia
Isitoshe kuna ambao tuna roho ngumu ukitupa jongoo unatupa na mti wake na kusonga mbele Kama injili
Nimekupata mkuu, hongera sana kama unamudu hilo ni wachache sana maana walio wengi ni wapasha viporo
 
Hapo vip!!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mimi ni mtu ambaye nilikuwa siamini katika kumuoa single mother ila baadaye nikajikuta nimekutana na single mother nikaona nitengue msimamo wangu ila kwa hili msimamo wangu narudi kuiheshimu.

Mnamo mwaka huu mwezi wa January, nimekutana na mdada mmoja ambaye tulimaliza naye chuo, na kwa bahati nzuri nilikuwa nasoma naye course moja na pia tulikuwa group moja kwenye discussion. Hivyo na mfahamu kwa kiasi alikuwa ni binti mwenye msimamo kwenye mahusiano.

Kipindi hicho sikuweza kumtongoza kwasababu nilikuwa nipo kwenye stress kubwa wakati nasoma university.

Ila ilikuwa namkubali kubali kiasi, ila wakati tukiwa mwaka wa tatu akakutana na jamaa alikuwa ni graduate na anakazi. Jamaa akafanikiwa kumuweka kwenye himaya yake. Kwangu haikuniumiza sana kwa kwasababu sikuwahi kumtongoza akanitoe nje.

Siku zikaenda jamaa akaenda kujitambulisha kwa binti, ikapangwa mpaka siku ya harusi na vitu kwa hivyo.

Jamaa akawa anahairisha harusi mara kwa mara ila kafanikiwa kuzaa naye mtoto, ila baadaye wakaingia kwenye misuguano wakavunja uhusiano na sababu mwanamke anasema jamaa alikuwa na mwanamke mwingine na mpaka sasa eti jamaa anaishi naye na amezaa naye mtoto, anyway mwanamke akamchukua yule mtoto aliyezaa na jamaa akampeleka kwa wazazi wake.

Mpaka nakutanane naye ameachana na jamaa na kwa takribani miaka mitatu. Anyway baada ya kunieleza hayo kwa uchungu nikaanza naye mahusiano baadaye nikaona kwasababu ni mwanamke ambaye namfahamu kitabia tokea nikiwa chuo acha nifumbe macho nifanye haraku za kuweka ndani kwa heshima.

Anyway baada ya kuanza naye mahusiano akapata ujauzito nikaona ili nisimkweze na aone nipo sereous naye ngoja nikamtambulishe, nikampeleka home kwa utambulisho.

Nikawa nimebakiza kibarua ya kwenda kwao ambaye mpaka sasa sijaenda bado.

Sasa leo akanipigia simu akaniambia amepata msiba, nikamuuliza nani akasema baba mkwe wake wa zamani na waenda na dada yake. Anyway sikutaka kumcrash.

Ila nimeona nipate muda wakutafsiri hiyo picture na kujiuliza maswali mengi.

1. Binafsi najiuliza kama ametoka misri na ameamua kwenda Caana kwanini anarudi nyuma

2. Na kama wameachana na hawakufunga ndoa na ameshatambulishwa katika familia nyingine anaenda kule kama nani...?na kwasababu gani hasa...?

Binafsi nikaona huyu anacheza na akili yangu kwasababu kama yupo sereous akesahau kule pa zamani na kusonga mbele na njia mpya...

Mimi ni mtu ni kazi yangu na biashara zangu, sasa naona kwasababu hana kazi labda anaona apate mahali ambapo atapunguza makali fulani ya stress za mahusiono na maisha may be.

Binafsi naona niwe naye karibu amzee yule kiumbe then niangalie ustarabu mwingine ila asilani sintoweza kumoa tena...m
Unakaribishwa kwa ushauri

Kama kweli unampenda huyu dada katika muda mliokaa nae na hakuwahi kukuonyesha tatizo lolote zaidi ya hili la kwenda kwenye msiba wa mkwe wa mahusiano ya zamani nakushauri yafuatayo.
Kwanza mwambie ukweli kuwa usingepeda ajihusishe kwa vyovyote na mahusiano yake ya zamani kama ameamua kuwa na wewe.
Naamini kuwa inawezekana alikuwa na urafiki na wifi zake wa zamani, na pengine wamemwambia, ki ubinadamu ameshindwa kukataa, wewe mwambie unavyotaka na usichotaka, yeye kama ana akili ataamua kuchagua.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mzazi mwenzie na wakati wameachana anaenda kweny msiba wa uyo mzee kufanya nn sasa ujue mambo mengi muda mwingine wanawake wenyewe uwa wanayaharibu maisha yao arafu usingizia wanaume wabaya dah....
True kabisaaaa Kama jamaa kaamua kulea mpaka mtoto wake kufikia huyo dada hana nidhamu kabisa.hakuna kitu kibaya Kama watu walio achana kwa vitu vidogo TU na walikuwa na mtoto wakikutana hao lazima kipigwe TU [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] zikikumbushwa zile moments na ndio zinazo haribu mambo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] ndio maana unakuta mwanamke anae jitambua humpeleka mtoto kwao au kwa huyo mwanaume Alie zaa nae ili kuondoa usumbufu usio na tija

NB: Hakuna kitu mwanamke anacho kipenda Kama ndoa na kuitwa mke wa fulani na ndio maana single mother wote walio na watoto Zaid ya mmoja wako stressed Sana na kuish nao Ni ngumu Sana wanaona Kama Wana nyanyasika

Kuishi na single mother inahtaji moyo , uvumilivu,chochote utakacho kifanya anaona unamuonea,hawapendi kukosolewa kabisa
 
Wataka kupanda mnazi ilihali unevaa msuli!

Kuna vitu kama huna amani navyo moyoni usifanye...

Sasa mleta mada wajiona kabisa moyo wako ni wa plastiki halafu wataka oa 'singo maza'...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom