Huyu Ndiye Mohamed O. Mchengerwa

Huyu Ndiye Mohamed O. Mchengerwa

Wateule wafanye kazi kwa bidii. Pia wasisahau kuwaomba msamaha Watanzania na Mungu pia, maana wengi wao ni zao la uchaguzi uliokosa sifa ya kuitwa uchaguzi huru na wa haki, wa 2020. Japo ni kweli pia kuwa wapo ambao hata bila uharibifu wa uchaguzi, wangeweza kuchaguliwa na wananchi.

Siku zote tulitakie mema Taifa letu. Na njia ya kulitakia mema Taifa na namna bora ya kuwa wazalendo kwa Taifa letu ni kupenda kutenda haki na kupigania haki za kwetu na za wengine.
 
Huyu mchengelwa ukweni ni wapi?
Maana kuoa na kuolewa ni mmoja yapo ya Cv's
Nimesikiliza clip ya DW YouTube ambako Shangazi Fatma Karume ametamka kuwa Ally Mchengelwa ni Mkwe wa Rais SSH, lakini ana elimu na uzoefu stahiki kwa kazi aliyopewa.

Namuunga mkono Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kumuweka karibu Mkwe wake.
 
Amepata nafasi nyeti sana lakini anahitahi kubadilika ili aweke integrity kwenye hiyo nafasi, na kutunza heshima ya aliyemteua.

Akiwa Msaidizi wa Jaji Mkuu alikuwa na element za UTAPELI. Kuna maamuzi ya kuhamisha Mahakimu ambayo alikuwa anafanya bila idhini ya CJ. Pengine alikuwa anapata chochote.

Nimeliweka hili kumjenga na siyo kumbomoa kwa hiyo halihitaji ubishi.
Basi ni tapeli tu huyo.
 
Wateule wafanye kazi kwa bidii. Pia wasisahau kuwaomba msamaha Watanzania na Mungu pia, maana wengi wao ni zao la uchaguzi uliokosa sifa ya kuitwa uchaguzi huru na wa haki, wa 2020. Japo ni kweli pia kuwa wapo ambao hata bila uharibifu wa uchaguzi, wangeweza kuchaguliwa na wananchi.

Siku zote tulitakie mema Taifa letu. Na njia ya kulitakia mema Taifa na namna bora ya kuwa wazalendo kwa Taifa letu ni kupenda kutenda haki na kupigania haki za kwetu na za wengine.
kweli mkuu
 
Nimesikiliza clip ya DW YouTube ambako Shangazi Fatma Karume ametamka kuwa Ally Mchengelwa ni Mkwe wa Rais SSH, lakini ana elimu na uzoefu stahiki kwa kazi aliyopewa.
Namuunga mkono Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kumuweka karibu Mkwe wake.
🙏🙏🙏
 
Legacy aliyowaachia Magufuli maCCM wenzake ni "Praise or Perish", Msukuma huyu wa Chato anamsifia mtu wa Rufiji aliyeteuliwa juzi tu eti ni mzalendo na mchapa kazi sana atamsaidia Rais kuijenga Tanzania tuitakayo.

Rais aepukane na sifa za kijinga hizi, awatathimini aliowateua baada ya kukamilisha majukumu aliyowapa na aachane na nadharia za Magufuli ajikite kwenye matokeo yanayopimika.

Mradi wa Umeme wa Rufiji ni wa Nyerere lakini hakutekeleza, siyo kwa kushindwa bali kuheshimu Mikataba ya Kimataifa na badala yake alijenga Mtera.
 
Legacy aliyowaachia Magufuli maCCM wenzake ni "Praise or Perish", Msukuma huyu wa Chato anamsifia mtu wa Rufiji aliyeteuliwa juzi tu eti ni mchapa kazi sana atamsaidia Rais kuijenga Tanzania tuitakayo. Rais aepukane na sifa za kijinga hizi, awatathimini aliowateua baada ya kukamilisha majukumu aliyowapa.
Dah imekuwa hayo tena
 
Mmmmh huyu aliyeandika nadhani anampigia chepuo.

Lakini niamini mimi hayo mengi uliosema hayana ukweli kuanzia michango yake bungeni, hadi jimboni.

Hata kurud kwake awamu ya pili kulikumbwa na sintofahamu nyingi sana.

Sisi wakazi wa rufuji ndio tuojua ukweli.

Ila mengi uliyoandika ni sifa ambazo sio zake.

Mfano miradi gani ya maji kafanya?? Unaijua barabara ya nyamwage utete? Ina hali gani?? Vipi barabara ya utete ngarambe, ??

Mirad ya maendeleo aliyafanya ambayo sio ile ya kitaifa??

Unajua shule za jimboni kwake zilivyo??

Anyways jamaa ana shule nzuri sana. Ila swala la ubunifu hana.
Angetutumia wasomi wa jimboni mwake kutatua baadhi ya changamoto, sio kusikiliza majungu toka kwa waganga njaa .
 
Mbona Walioteuliwa ni wengi tu na hujawafanyia hii Profile kama huyu? Kwani kuna nini kimetokea hadi Nguvu Kubwa hivi ya Kimaelekezo na Kiufafanuzi inalazimishwa Kujulikana Kwetu Wanyonge?

Halafu nimetafuta mahala ambapo kama umeweka Marital Status yake kama ana Mke au nae labda ni ' Mgongesha Mibesela ' tu hovyo kama akina siye Generalist na Wengineo pia.

Ila kupitia hiki ulichokiandika hapa kuna Kitu Muhimu sana nimegundua kuwa ukiwa Sokoni Kariakoo Utaoa tu mwana Sokoni Karikakoo Maenzako ila ukiwa ' Posh and VIP areas ' basi hata na Wewe pia utaoa ( utapata ) Wanawake wa huko huko tu.

Generalist 24/7 navua zangu tu Samaki hapa Kisiwani Pemba kwahiyo sijui ndiyo inamaanisha na Mimi nioe hawa hawa Wanawake ninaopara nao Samaki au hapana.

Ila tuacheni Utani hii Njemba imesoma!!
 
Mmmmh huyu aliyeandika nadhani anampigia chepuo.

Lakini niamini mimi hayo mengi uliosema hayana ukweli kuanzia michango yake bungeni, hadi jimboni...
Mimi nawajuza si kwamba nampromote
 
Mbona Walioteuliwa ni wengi tu na hujawafanyia hii Profile kama huyu? Kwani kuna nini kimetokea hadi Nguvu Kubwa hivi ya Kimaelekezo na Kiufafanuzi inalazimishwa Kujulikana Kwetu Wanyonge?...
🙏🙏🙏 shukurani mkuu.
Na wengine nitawaleta
 
Back
Top Bottom