Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 16,952
- 62,847
Huyo CV yake iko vizuri, anafaa
Aendelee kuchapa kazi
Aendelee kuchapa kazi
Kweli, some of the details zilizowekwa ni yeye tu ndiyo anaweza kujuaNaona mh mchengelwa kaamua kuja kujipigia debe mwenyewe huku jf
Ndiyo Yeye namjuaHilo bado sijalipata
Huyu Ndiye Mohamed O. Mchengelwa
Teuzi Mpya za Baraza la la Mawaziri zimemuibua kijana Mzalendo na Mchapakazi.
Mohamed Omar Mchengelwa.
Mh.Mchengelwa ni Mbunge wa Rufiji toka 2015 akichukua nafasi ya
ya aliyekuwa Waziri wa Afya wakati wa Mzee JK Dr Seif Rashid.
Mh.Mchengelwa ni Mwanasheria msomi na bobezi katika eneo la Mahakama alikofanya kazi kabla ya kuwa Mbunge.
Mchengelwa Ni Mwanafunzi wa Shahada ya Tatu (PhD) katika Siasa na Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu Cha "Girne America University" nchini Cyprus.
Ukiacha hayo amekuwa Msaidizi wa Jaji Mkuu wa Tanzania kwa miaka sita(2009-2015).
Bungeni kwa muda mrefu amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria mpaka wakati huu Mh.Raisi anamteuwa kuwa Waziri.
Mh.Mchengelwa ni miongoni mwa Wabunge wenye kujenga hoja zenye maslahi makubwa kwa wananchi ya Jimbo la Rufiji na Tanzania kwa Ujumla.
Mfano hoja yake kwa nini tozo ya huduma inayopaswa kulipwa na Kampuni za kigeni zinazojenga Mradi wa Umeme wa Mwl Nyerere ilipwe halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni badala ya Rufiji kwenye Mradi imepelekea wilaya Rufiji kupokea mabilioni ya pesa kutoka kwenye makampuni hayo na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendelo ya wilaya hiyo kongwe, (Rufiji ni Wilaya toka Mkoloni).
Michango yake Bungeni imechangia kiasi kikubwa kuanza kwa Mradi wa Umeme wa Mwalimu Nyerere uliokwama kwa zaidi ya miaka 60(Rejea Ansad Bungeni)
Wakati fulani aliamshra fulaha Bungeni alipokumbusha ahadi ya Mwalimu Nyerere ya kujenga Barabara Tarafa ya Mkongo wilayani Rufiji aliyoitoa 1955 wakati wa Kikao Cha Halmashauri kuu ya Tanu kikichofanyika Tarafa ya Mkongo Rufiji.
Kwa Jitihada zake Mh Mchengelwa, halmashauri sasa wanajenga Shule ya Upili Tarafa ya Mkongo yenye jina la Muaaisi na Mpigani Uhuru wa Nchi hii Bibi Titi Mohamed.
Kwa Jimbo lake hakika ni Mwanasisa wa kupigiwa Mfano na kwa wanaojua siasa za Rufiji huwa ni ngumu Sana kwa Mbunge kupenya awamu ya pili lakini kwake haikuwa kazi ngumu sana kutokana na aliyoyafanya ndani ya awamu yake ya kwanza.
Kuanzia katika Utatuzi wa migogoro ya wakulima na wafugaji,Changamoto za maji,Barabara na Umeme.
Hatma ya hekari elfu hamsini zilizotengwa kando ya Mto Rufiji baada ya kukamilika ujenzi wa mradi Mwalimu Nyerere.
Kutowajibika ipasavyo kwa Mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto Rufiji/Rubada(Kwa mujibu wa tafiti kilimo Cha mpunga katika bonde hili kinaweza kulisha nchi mzima ya Tanzania)
Mara Kadhaa akijenga hoja bungeni kuwa ufumbuzi wa tatizo la sukari Tanzania utapatikana katika Bonde la Mto Rufiji(Kuna wawekezaji zaidi ya watatu wa viwanda vya Sukari Rufiji)
Ndio kusema
Mh.Mchengelwa ni Mbunge wa kuwasemea Watanzania.
Hakusita kuwa Mkali na Kusimamia alichokiamini wakati fulani alihoji Bungeni kwa lugha Kali kidogo ni Kwa nini Kampuni ya Sukari ya Kagera kukopa mabilioni ya Pesa na Kwenda kuwekeza DRC wakati nchi inashida kubwa ya Sukari,hayo na mengine mengi yenye Maslahi ya Tanzania yamekuwa ndio Kilio chake.
Jimboni kwake amefanya mengi huwezi kuweka yote hapa ila mawili yatakayomfanya akumbukwe na wana Rufiji ni Kuhakikisha kila Tarafa inakuwa na Shule ya A level(Mkongo,Ikwiriri na Shule pekee ya mabinti Mohoro)
Kutekeleza kwa asilimia 100% agizo la Serikali kuu kujenga madarasa mapya kuchukua wanafunzi waliokwama kuingia kidato cha kwanza(Madarsa 13 ya kisasa ndani ya Mwezi mmoja) na kufanya kuwa miongoni mwa halmashauri zilizofanya vyema katika zoezi hilo nchini.
Michango yake bungeni pia imepelekea Rufiji kutengewa fungu na Tamisemi kujenga jengo jipya halmashauri ili kuondokana na Boma wanalolitumia sasa lililorithiwa toka kwa Mjerumani.
Bila kusahau hoja yake Bungeni kwa nini Mradi wa Umeme wa Mwl Nyerere Rufiji utakaotoa ajira ya zaidi 6000 na serikali kuwekeza zaidi ya trilioni 6.5 unafanyika katika wilaya ambayo haina benki ya Serikali na hata binafsi imepelekea serikali kupeleka benki katika wilaya hio Kongwe.
Ndio kusema Mh.Mchengelwa anawasemea watu wake na taifa kwa Ujumla.
Ushauri wetu kwake aendelee kusemea wananchi wake na taifa bila kusahau Kilio chake cha muda mrefu juu ya ujenzi wa Barabara ya Kibiti Mloka kiwango cha lami
Kwani asilimia kubwa Malighafi za mradi ya Mradi wa Umeme Mwl Nyerere hupita kwenye barabar hii ambayo haiko kwenye hali nzuri hasa kipindi Cha Mvua.
Pia asimamie ahadi na Ilani ya Chama Cha mapinduzi ujenzi wa barabara Nyamwage Utete ambapo wabunge kabla yake hawakufanikiwa kufanya hivyo.
Kwa uzalendo wako na uchapakazi tunaamini utatumikia taifa ipasavyo katika jukumu lako jipya la Waziri ofisi ya Raisi utumishi na Utawala Bora na Kumsaidia Mh. Rais katika kazi yake ya kuijenga Tanzania Tuitakayo.
Shukurani mkuu 🙏🙏🙏Amepata nafasi nyeti sana lakini anahitahi kubadilika ili aweke integrity kwenye hiyo nafasi, na kutunza heshima ya aliyemteua.
Akiwa Msaidizi wa Jaji Mkuu alikuwa na element za UTAPELI. Kuna maamuzi ya kuhamisha Mahakimu ambayo alikuwa anafanya bila idhini ya CJ. Pengine alikuwa anapata chochote.
Nimeliweka hili kumjenga na siyo kumbomoa kwa hiyo halihitaji ubishi.
Shukurani mkuu kwa kushare kitu hiki 🙏🙏🙏Fujo zake tuna zielewa... Hawa ndio walipata fursa baada ya urafiki wao na watu msoga... Hakuna alilolufanya kushadihisha maendeleo ya wana rufiji... Kipo, muhoro, siasa, kingupira, mkongo, ngorongo, nyambunju, mbwala shida tupu... Rufiji afadhari unaipata utete na ikwiriri sio zaidi ya hapo...
Wabunge wengi tu wamewahi kuwa mawaziri na kuongoza zaidi ya kipindi kimoja ktk jimbo la rufiji... MF. Mbunge mbonde (mbonde mbunge) huyu aliwahi kuwa katibu mkuu ktk moja wizara kipindi hicho na alikuja kuhuwa mbunge na waziri katika wizara kazaa ikiwamo ya maji kama sikosei
Kuna Marehemu Prof. Mtulia aliyewahi kuwa Daktari wa Rais sijajua ni rais nani (mwinyi au mkapa sina kumbukumbu sawa), alikuja kuwa na Hosp yake Tumaini Hosp.
Kuna Dr. Seif (mwarabu wa kilimani mkongo) aliwahi kuwa mtumishi wa umma pia na amewahi fanya kazi Hosp ya wilaya ya rufiji kabla aja jiendeleza zaidi na zaidi na aliwahi kuwa pia waziri/naib waziri ktk wizara ya taaluma yake akiwa pamoja na Steven kebwe kama sikosei
Hivyo Dr. Mchengerwa ambaye baada ya kupata ubunge Muda mwingi alitumia kujiendeleza kitaaluma kuliko kufanya shughuli za kibunge...
Miaka yake mitano ya mwanzo alisoma masters na akaendelea na PhD yake, hivyo aliwatumia wana rufiji na hakuwatumikia ipasavyo...
Labda ktk huu muhula mwingine wa kibunge tuna weza sema jambo... Kuna lami ina jengwa ya tarura Km moja au moja na nusu ni Mara ya kwanza makao makuu ya halmashauri kuwa na lami na ni baada ya kuanzishwa kwa tarura na kupewa jukumu la kujenga Barbara zake za ndani...
Wamebakisha barabara ya nyamwage utete ambayo ni ahadi ya muda mrefu pamoja na mh rais wa awamu ya tano alihahidi kuitekeleza kwa kiwango cha lami...
Kuna veta ina jengwa katika pori katikati ya utete na nyamwage, hii ni sehemu ya ilani ya chama na mikakati ya serikali kuongeza vyuo hivi vya ufundi... Kuna mabonde ya kilimo cha sukari chini ya rubada hakuna kinacho fanyika...
Ushindi wake haukuwa mwepesi uligubikwa na sintofahamu nyingi na walichelewa kutangaza... Madam kuluthumu wa Cuf kipindi hicho kabla hajatimkia ACT ni mwanamke mwenye ushawishi ktk hilo jimbo, mengine kwann alishindwa ni story ndefu ambayo Madam kuluthumu mchuchuli anaweza lisemea...
Kama walivyo wana siasa walio wengi nae Mh. Dr. Mchengelwa huwa ana rejea rufiji kukiwa na jambo muhimu au jambo la kichama au kipindi cha uchaguzi wa ubunge... Alianzisha mashindano akatengeneza timu ya rufiji united kama kawaida ya wanasiasa na vijana wasio kuwa na malengo na wazee waliojikatia tamaa basi hatima zao huwa zipo ktk mifuko ya watu...
Kila la kheri Mh. Dr. Mchengelwa ktk kulitumikia taifa na watu wa jimbo la rufiji
Visca el CCM
Umeandika vizuri hongera. Ila, siku zote ukiandika kuhusu mtu, basi hakikisha jina unaliandika vile linavyotakiwa kuwa, siyo unavyotaka liwe. Mwanzo nilifikiri ni makosa ya kuandika lakini inaonekana ndiyo ulivyoamua kuandika jina lake. Ni Mchengerwa na siyo Mchengelwa, kuna uwezekano kwa kosa hilo ukawa umemwandika mtu mwingine au kama jina lake ni neno lenye maana fulani kwa lugha yoyote basi unaweza kuzua tafarani ya kuandika jina au neno lenye maana tofauti na makusudio yake.Huyu Ndiye Mohamed O. Mchengelwa
Teuzi Mpya za Baraza la la Mawaziri zimemuibua kijana Mzalendo na Mchapakazi.
Mohamed Omar Mchengelwa.
Mh.Mchengelwa ni Mbunge wa Rufiji toka 2015 akichukua nafasi ya
ya aliyekuwa Waziri wa Afya wakati wa Mzee JK Dr Seif Rashid.
Mh.Mchengelwa ni Mwanasheria msomi na bobezi katika eneo la Mahakama alikofanya kazi kabla ya kuwa Mbunge.
Mchengelwa Ni Mwanafunzi wa Shahada ya Tatu (PhD) katika Siasa na Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu Cha "Girne America University" nchini Cyprus.
Ukiacha hayo amekuwa Msaidizi wa Jaji Mkuu wa Tanzania kwa miaka sita(2009-2015).
Bungeni kwa muda mrefu amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria mpaka wakati huu Mh.Raisi anamteuwa kuwa Waziri.
Mh.Mchengelwa ni miongoni mwa Wabunge wenye kujenga hoja zenye maslahi makubwa kwa wananchi ya Jimbo la Rufiji na Tanzania kwa Ujumla.
Mfano hoja yake kwa nini tozo ya huduma inayopaswa kulipwa na Kampuni za kigeni zinazojenga Mradi wa Umeme wa Mwl Nyerere ilipwe halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni badala ya Rufiji kwenye Mradi imepelekea wilaya Rufiji kupokea mabilioni ya pesa kutoka kwenye makampuni hayo na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendelo ya wilaya hiyo kongwe, (Rufiji ni Wilaya toka Mkoloni).
Michango yake Bungeni imechangia kiasi kikubwa kuanza kwa Mradi wa Umeme wa Mwalimu Nyerere uliokwama kwa zaidi ya miaka 60(Rejea Ansad Bungeni)
Wakati fulani aliamshra fulaha Bungeni alipokumbusha ahadi ya Mwalimu Nyerere ya kujenga Barabara Tarafa ya Mkongo wilayani Rufiji aliyoitoa 1955 wakati wa Kikao Cha Halmashauri kuu ya Tanu kikichofanyika Tarafa ya Mkongo Rufiji.
Kwa Jitihada zake Mh Mchengelwa, halmashauri sasa wanajenga Shule ya Upili Tarafa ya Mkongo yenye jina la Muaaisi na Mpigani Uhuru wa Nchi hii Bibi Titi Mohamed.
Kwa Jimbo lake hakika ni Mwanasisa wa kupigiwa Mfano na kwa wanaojua siasa za Rufiji huwa ni ngumu Sana kwa Mbunge kupenya awamu ya pili lakini kwake haikuwa kazi ngumu sana kutokana na aliyoyafanya ndani ya awamu yake ya kwanza.
Kuanzia katika Utatuzi wa migogoro ya wakulima na wafugaji,Changamoto za maji,Barabara na Umeme.
Hatma ya hekari elfu hamsini zilizotengwa kando ya Mto Rufiji baada ya kukamilika ujenzi wa mradi Mwalimu Nyerere.
Kutowajibika ipasavyo kwa Mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto Rufiji/Rubada(Kwa mujibu wa tafiti kilimo Cha mpunga katika bonde hili kinaweza kulisha nchi mzima ya Tanzania)
Mara Kadhaa akijenga hoja bungeni kuwa ufumbuzi wa tatizo la sukari Tanzania utapatikana katika Bonde la Mto Rufiji(Kuna wawekezaji zaidi ya watatu wa viwanda vya Sukari Rufiji)
Ndio kusema
Mh.Mchengelwa ni Mbunge wa kuwasemea Watanzania.
Hakusita kuwa Mkali na Kusimamia alichokiamini wakati fulani alihoji Bungeni kwa lugha Kali kidogo ni Kwa nini Kampuni ya Sukari ya Kagera kukopa mabilioni ya Pesa na Kwenda kuwekeza DRC wakati nchi inashida kubwa ya Sukari,hayo na mengine mengi yenye Maslahi ya Tanzania yamekuwa ndio Kilio chake.
Jimboni kwake amefanya mengi huwezi kuweka yote hapa ila mawili yatakayomfanya akumbukwe na wana Rufiji ni Kuhakikisha kila Tarafa inakuwa na Shule ya A level(Mkongo,Ikwiriri na Shule pekee ya mabinti Mohoro)
Kutekeleza kwa asilimia 100% agizo la Serikali kuu kujenga madarasa mapya kuchukua wanafunzi waliokwama kuingia kidato cha kwanza(Madarsa 13 ya kisasa ndani ya Mwezi mmoja) na kufanya kuwa miongoni mwa halmashauri zilizofanya vyema katika zoezi hilo nchini.
Michango yake bungeni pia imepelekea Rufiji kutengewa fungu na Tamisemi kujenga jengo jipya halmashauri ili kuondokana na Boma wanalolitumia sasa lililorithiwa toka kwa Mjerumani.
Bila kusahau hoja yake Bungeni kwa nini Mradi wa Umeme wa Mwl Nyerere Rufiji utakaotoa ajira ya zaidi 6000 na serikali kuwekeza zaidi ya trilioni 6.5 unafanyika katika wilaya ambayo haina benki ya Serikali na hata binafsi imepelekea serikali kupeleka benki katika wilaya hio Kongwe.
Ndio kusema Mh.Mchengelwa anawasemea watu wake na taifa kwa Ujumla.
Ushauri wetu kwake aendelee kusemea wananchi wake na taifa bila kusahau Kilio chake cha muda mrefu juu ya ujenzi wa Barabara ya Kibiti Mloka kiwango cha lami
Kwani asilimia kubwa Malighafi za mradi ya Mradi wa Umeme Mwl Nyerere hupita kwenye barabar hii ambayo haiko kwenye hali nzuri hasa kipindi Cha Mvua.
Pia asimamie ahadi na Ilani ya Chama Cha mapinduzi ujenzi wa barabara Nyamwage Utete ambapo wabunge kabla yake hawakufanikiwa kufanya hivyo.
Kwa uzalendo wako na uchapakazi tunaamini utatumikia taifa ipasavyo katika jukumu lako jipya la Waziri ofisi ya Raisi utumishi na Utawala Bora na Kumsaidia Mh. Rais katika kazi yake ya kuijenga Tanzania Tuitakayo.
Shukurani mkuu kwa masahihisho🙏🙏🙏Umeandika vizuri hongera. Ila, siku zote ukiandika kuhusu mtu, basi hakikisha jina unaliandika vile linavyotakiwa kuwa, siyo unavyotaka liwe. Mwanzo nilifikiri ni makosa ya kuandika lakini inaonekana ndiyo ulivyoamua kuandika jina lake. Ni Mchengerwa na siyo Mchengelwa, kuna uwezekano kwa kosa hilo ukawa umemwandika mtu mwingine au kama jina lake ni neno lenye maana fulani kwa lugha yoyote basi unaweza kuzua tafarani ya kuandika jina au neno lenye maana tofauti na makusudio yake.