Huyu ndiye Kinana, Je analipeleka wapi taifa letu?

Huyu ndiye Kinana, Je analipeleka wapi taifa letu?

Hivi ile adhabu ya kumcharaza mtu viboko kumi na mbili wakati akiingia gerezani na kumi na viwili wakati wa kutoka ili akamuoneshe mkewe ilikuwa kwa wala rushwa tu ama na kwa hawa wahujumu uchumi! Haiwezekani kuwa kiongozi wa umma wakati unahusika kwenye kila aina ya uchafu!
 
Usisahau bro 2015 ipo karibu hela ya TSHETS,KOFIA,KUNUNULIA UBWABWA na KHANGA ndo hizo
Zabuni ya Mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi jijini Dar ulipitia kwenye misukosuko ya urasimu wa hali ya juu baada ya wanachama na makada maarufu wa CCM kuteka mchakato mzima,

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na Katibu mkuu wa CCM ndugu Abdulahman Kinana ndie aliyeileta nchini Tanzania Kampuni ya Strabag ya Ukandarasi wa Ujenzi iliyoanzishwa na Muastria katika mji wa Villach na kuweka makao yake makuu mjini Vienna Austria ambapo kampuni hii ndiyo ilishinda zabuni hiyo

Kinana aliileta kampuni hii kutoka tawi la kampuni hiyo lililopo Ujerumani,

Kuileta kampuni hiyo nchini ni jambo jema, lakini hoja yangu ni namna Kinana anavyousababishia TRA kukosa mapato kutoka kwenye Kampuni hiyo ya uingizaji mitambo ya ujenzi nchini,

Taarifa za TRA mpaka jana zilikuwa zinaonyesha kuwa kampuni hiyo imeingiza mizigo/mitambo yenye thamani ya kodi ya shilingi za kitanzania 16 milioni tu kupitia kampuni ya Sharaf Shipping Company ambapo Taarifa zinaonyesha kuwa Kinana anamiliki hisa 7,500 kati ya 10,000 za kampuni hiyo inayoitwa Sharaf Shipping Company iliyosajiliwa Dar es Salaam tangu mwaka jana mwezi wa saba.

Kinyume chake taarifa na nyaraka za kiintelijensia kutoka ndani ya kampuni hiyo ya Strabag zinaonyesha kuwa kampuni ya Strabag imeilipa 8.56 bilioni kampuni ya wakala wa meli ya Sharaf Shipping Company kama malipo stahiki ya kodi ya uingizaji mitambo nchini tangu kampuni hiyo ilipoanza uingizaji wa mitambo ya ujenzi nchini 03-07-2012,

Kisha ikailipa tena 7.8 bilioni kama gharama za uwakala wa mitambo hiyo,

Wanabodi hayo ni machache tu lakini nitaweka hapa nyaraka za malipo ya Strabag kwa Sharaf Shipping Company na nyaraka za malipo ya Sharaf Shipping Company kwa TRA kama Mods watanipa kibali cha kuweka hapa,

Maafisa wa TRA wanasema linapofika suala la Sharaf Shipping Company hufanya kazi kwa maagizo ya katibu mkuu wa ccm,

Huyo ndie katibu mkuu wa chama tawala nchini Tanzania
 
Hapa sijakusoma, unamtetea Kinana au unamkosoa mtoa hoja? Inawezekana kuna msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Ujenzi, je ni vipi hizo bilioni kadhaa alizochulipwa kwa ajili y amalipo ya kodi?...N akodi iliyolipwa ni 16 M?

Hizi ni porojo tupu. Unazungumzia kodi kwenye mradi wenye msamaha wa kodi au lengo ni kuendeleza sera ya siasa za majitaka? Kwa kukusaidia kuna kampuni nyingine inaitwa ashref-interbeton wanajenga barabara ya Iringa-Mbeya nao hawalipi kodi, waambie TRA wakupe document zao yawezekana kampuni ya Kinana ilihusika kusafirisha vifaa vyao pia.
 
Watanzania ni waoga, hat ausimame pale Jangwani uwaambie watanzania tusimamie haki haitakaa itokee! Kinana na timu yake wataendelea kula nchii hii watakavyo! Ukiangalia safu ya Uongozi wa CCM na safu ya serikali inayoondoka madarakani 2015 ni wazi wanajenga timu ya kuendelea kulinda maslahi yao come after 2015! Ni nchi ambayo uongozi, madaraka n.k unatolewa kwa kujuana, uswahiba zaidi ya utendaji, udini zaidi ya uzalendo na uadilifu....Maslahi mbele, kuoneana aibiu kwa hali ya juu na siasa za chuki kwa wanaowajibika au kusema ukweli! JK alishaihatibu hii nchi, haitengenezeki.....


Zabuni ya Mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi jijini Dar ulipitia kwenye misukosuko ya urasimu wa hali ya juu baada ya wanachama na makada maarufu wa CCM kuteka mchakato mzima,

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na Katibu mkuu wa CCM ndugu Abdulahman Kinana ndie aliyeileta nchini Tanzania Kampuni ya Strabag ya Ukandarasi wa Ujenzi iliyoanzishwa na Muastria katika mji wa Villach na kuweka makao yake makuu mjini Vienna Austria ambapo kampuni hii ndiyo ilishinda zabuni hiyo

Kinana aliileta kampuni hii kutoka tawi la kampuni hiyo lililopo Ujerumani,

Kuileta kampuni hiyo nchini ni jambo jema, lakini hoja yangu ni namna Kinana anavyousababishia TRA kukosa mapato kutoka kwenye Kampuni hiyo ya uingizaji mitambo ya ujenzi nchini,

Taarifa za TRA mpaka jana zilikuwa zinaonyesha kuwa kampuni hiyo imeingiza mizigo/mitambo yenye thamani ya kodi ya shilingi za kitanzania 16 milioni tu kupitia kampuni ya Sharaf Shipping Company ambapo Taarifa zinaonyesha kuwa Kinana anamiliki hisa 7,500 kati ya 10,000 za kampuni hiyo inayoitwa Sharaf Shipping Company iliyosajiliwa Dar es Salaam tangu mwaka jana mwezi wa saba.

Kinyume chake taarifa na nyaraka za kiintelijensia kutoka ndani ya kampuni hiyo ya Strabag zinaonyesha kuwa kampuni ya Strabag imeilipa 8.56 bilioni kampuni ya wakala wa meli ya Sharaf Shipping Company kama malipo stahiki ya kodi ya uingizaji mitambo nchini tangu kampuni hiyo ilipoanza uingizaji wa mitambo ya ujenzi nchini 03-07-2012,

Kisha ikailipa tena 7.8 bilioni kama gharama za uwakala wa mitambo hiyo,

Wanabodi hayo ni machache tu lakini nitaweka hapa nyaraka za malipo ya Strabag kwa Sharaf Shipping Company na nyaraka za malipo ya Sharaf Shipping Company kwa TRA kama Mods watanipa kibali cha kuweka hapa,

Maafisa wa TRA wanasema linapofika suala la Sharaf Shipping Company hufanya kazi kwa maagizo ya katibu mkuu wa ccm,

Huyo ndie katibu mkuu wa chama tawala nchini Tanzania
 
Tumechaka na ufisadi wa ccm.hata kama hakuna ukweli wowote kwenye hii mada.hii ni tone dogo sana kwenye bahari.wanazindi kutunisha matumbo yao na mafisadi wezao weupe wanaowaita wawekezaji.ni wezi watupu wamejaa ndani ya ccm.kuna issue kumbwa sana.
 
Koplo V, bora unywe sumu ujiue. ona sasa unavyoaibika kutokana na kujichanganya. kwenye ,maelezo yako ya hii thread umesema kuwa kampuni imeanza kuingiza mizigo nchini 03.o7.2012. sasa unasema kuwa TRA imeanza kulipwa 03/07/2012. Utaratibu ni kuwa, mzigo hulipwa TRA kabla haujatolewa bandarini. sasa iweje mzigo uanze kuingizwa Februari 2012 na malipo yafanyike Julai 2012/ BILA SHAKA UTAKUWA UMEVURUGWA WEWE. Ninaamini kuwa maelezo yote ni yako. sasa mbona unaitafuta aibu mchana kweupeee

Pole sana
 
hv ccm wamepanga nini na wananchi wao hasa kwenye uchaguzi wa 2015,hongereni wadau kwa kuwatanua mawazo wananchi wa tz hasa kwa wale ambao elimu ze2 ni za kina kayumba.
 
Hii rubbish.....kulikua na uharaka wa kukurupuka kuja na thread bila ya kuwa na eveidence kwanza.....watu wengine ni wangese sana......majungu kwenda mbele
 
kuteleza kupo cha ajabu nini iwapo waziri alishindwa kutamka muungano wa tanzania ni kati ya wapi na wapi? Tulieni ukweli utajulikana tu. Mimi napita tu.
 
NAMUOGOPA ABDURAHMAN KINANA



Na Absalom Kibanda

Kwa mara nyingine tena, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeandika historia mpya baada ya kufanya mabadiliko mazito katika safu yake ya uongozi wa kitaifa.

Ni mabadiliko mazito si kwa sababu tu yamefanywa na CCM ambayo imekuwa na rekodi ya kubadili sura za watendaji wake kwa namna na kwa njia tofauti, bali kutokana na ukweli kwamba safari hii mabadiliko hayo yamehusisha watu wazito, wenye historia ya kipekee katika medani ya uongozi ndani na nje ya chama hicho.

Ingawa kwa mtazamo wa haraka haraka, mabadiliko hayo yanaweza yakaonekana kuwa ni ya kuyabeza au kuyapuuza kama ilivyotamkwa na baadhi ya wadadisi wa mambo wakiwamo wachambuzi wa masuala ya siasa na hata wanazuoni, ukweli unabaki pale pale kwamba kile kilichofanywa na CCM kinaweka alama ya kipekee katika mwenendo wa siasa za kitaifa za siku zijazo.

Wasifu mzito na historia za kutukuka za baadhi ya wateule wanaounda timu ‘mpya’ ya viongozi watendaji wa CCM kwa kiwango kikubwa ndicho kitu kikubwa pekee kinachosababisha mtu yeyote makini ajikute akipata shida kuyabeza yale yaliyofanywa na chama hicho tawala mwishoni mwa wiki kule Dodoma.


Msuko mpya wa safu ya wakuu wa idara za CCM uliotangazwa na Rais Jakaya Kikwete ukiwajumuisha wanasiasa wasiojua mizaha wawapo kazini kama alivyo Philip Mangula, au makada wa muda mrefu wa chama hicho wa kariba ya Muhammad Seif Khatib na Zakia Meghji una kila sababu ya kutafutiwa dawa mahususi na makamanda wa kambi ya upinzani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipambana kuing’oa CCM madarakani.

Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.


Kwa muktadha wa makala ya leo na kwa kuzingatia nafasi kuu ya utendaji aliyopewa, nitazungumzia kwa sehemu tu wasifu wa Kinana, mtu ambaye naamini anapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu na wakati mwingine kudhibitiwa ili kasi yake ya kukijenga chama alichopewa dhamana ya kukinusuru isije ikasababisha kuyumba kama si mauti ya kisiasa kwa baadhi ya vyama vya upinzani.

Ni wazi kwamba, kuteuliwa kwa Kinana kuwa Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa, akirithi mikoba iliyomshinda, Wilson Mukama, kumetutia ganzi baadhi yetu ambao kwa muda mrefu tumekuwa ‘mashabiki’ au waumini wa kuchagiza kwa njia ya kalamu na wakati mwingine katika mijadala ya wazi kwamba, taifa lilikuwa na haja ya kutafuta mabadiliko ya uongozi kutoka nje ya chama tawala.

Sitaki kuwa miongoni mwa wapenda mabadiliko ambao kwa njia za kujifariji au za kujipa matumaini hewa wameingia katika mkumbo wa jumla jumla wa kumbeza Kinana kwa namna wanayotaka kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba, mtu huyo anaweza akasukumwa kirahisi kwa namna ile ile ilivyopata kuwa kwa watangulizi wake kadhaa waliopata kushika wadhifa huo.

Hupaswi kuwa na akili nyingi kutambua kwamba, umahututi wa CCM kisiasa, kulikokifikisha chama hicho tawala kufikia hatua ya kupoteza dira na kuanza kuliona kaburi la kupoteza madaraka ya dola ndiko kulikorejesha hekima za usikivu kichwani mwa Kikwete hata akalazimika kuwarejesha akina Kinana, Mangula, Seif Khatib na Meghji katika kilinge cha siasa za ushindani mkali ndani na nje ya CCM.

Siyo siri hata kidogo kwamba, hekima hii mpya ya Kikwete ya kumrejesha Kinana ulingoni, ambaye siku chache tu zilizopita alitangaza kustaafu siasa huku akisema alikuwa akikusudia kuwaachia vijana kusukuma gurudumu la uongozi, inahusisha kichwa zaidi ya kimoja kutoka ndani na nje ya CCM.

Kama ilivyo kwa wengi wengine nilianza kulisikia jina la Kinana likihusishwa na ukatibu mkuu wa CCM miaka miwili au mitatu iliyopita hali ambayo ilipata kusababisha nifikie uamuzi hata wa kumuuliza yeye mwenyewe kuhusu taarifa hizo.

Jibu ambalo Kinana mwenyewe alipata kunipa kwamba alikuwa akipenda kuona akiendelea kupata fursa ya kukitumikia chama chake kama mshauri na kwa nyakati mahususi kama zile za kampeni na si kwa nafasi ya ukatibu mkuu lilikuwa likinipa sana faraja.

Kilichokuwa kikinipa faraja si kingine chochote bali fikra zangu (sahihi au potofu) ambazo siku zote zilikuwa zikinifanya niamini kwamba, ukatibu mkuu kwa Kinana ilikuwa ni silaha moja ya maangamizi kwa vyama vya upinzani ambavyo naamini vinapaswa kuendelea kupewa fursa ya kuaminiwa na kukomaa.

Katika mazingira ambayo CCM imeweza kuepuka zahama ya kumeguka vipande viwili kwa kuzingatia maono aliyokuwa nayo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwangu mimi Kinana wa zama hizo alikuwa na anaendelea kubakia kuwa tishio kubwa kwa ustawi wa upinzani ambao ni rutuba muhimu kwa maendeleo ya demokrasia na misingi ya utawala bora.

Hili ndilo ambalo naamini wapinzani wanapaswa kulitazama na kulitafakari nyakati hizi wanapoendesha harakati zao za kukabiliana na maguvu ya dola na haya mapya ya hoja ambazo aghalab zitaongozwa na Kinana nyakati hizi taifa linapojiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa miaka mitatu ijayo.

Haitoshi kwa kina Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Dk. Willibrod Slaa na Zitto Kabwe kumbeza Kinana na timu ya watendaji wake eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.


Wapinzani na wachambuzi wa mambo wanapaswa kujua na kutambua kwamba, Kinana ni mwanasiasa wa vitendo, msomaji mzuri wa vitabu, ripoti, taarifa, magazeti, msikilizaji na msikivu mzuri wa mambo mepesi na mazito kuliko alivyokuwa ‘utopia’ Mukama anayeamini na kuzitetea nadharia zisizotekelezeka.


Si hilo tu, wapinzani wanapaswa kutambua kwamba, historia yake ya uaskari alioutumikia miaka 20 hadi mwaka 1972 akifikia cheo halisi cha jeshi cha Kanali ikimhusisha na mafunzo mahususi ya kimkakati ni sehemu ya mambo ambayo yanatawala nidhamu ya kazi ya aina ya kipekee iliyomfanya Kinana akawa jemedari wa mapambano ya CCM tangu mwaka 1995 hadi leo.


Wachambuzi wa mambo, nikiwamo mimi mwenyewe ambao siku zote tumekuwa tukiiona CCM kuwa chama kinachokufa kwa maana ya kuchungulia kaburi, tunapaswa kuanza kutafakari upya mawazo yetu hayo, nyakati hizi Kinana alipopewa dhamana ya kuwa mtendaji wake mkuu.

Tutakuwa wendawazimu iwapo tutamlinganisha Kinana na Mukama na kusahau kwamba huyu aliye kilingeni leo ndiye aliyemuongoza Benjamin Mkapa katika mapambano makali ya kisiasa mwaka 1995, zama Augustine Mrema alipokuwa tishio la kwanza la kweli dhidi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Alikuwa ni Kinana aliyefanya kazi kubwa katika kipindi chote cha kampeni akiratibu na kuongoza kampeni zote za Mkapa zilizomjumuisha pia Mwalimu Nyerere katika mazingira ambayo wengi walikuwa wakiamini CCM ilikuwa katika mwelekeo wa anguko la kihistoria.

Kinana ambaye kabla ya mwaka 1995 alikuwa tayari amepata kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi alitumia vyema mbinu za medani na zile za kidemokrasia na kiplomasia kumjengea uhalali Mkapa ambaye wakati huo alikuwa mwanasiasa ambaye hakuwa akijulikana sana.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, siku chache tu baada ya kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza mwaka 1995, kwa sababu ama ya ulevi wa madaraka au kwa kutingwa na kazi za kimamlaka, Mkapa alisahau kazi kubwa aliyofanyiwa na Kinana.

Ni katika kipindi hicho cha kati ya mwaka 1995 na 2000 ndipo nilipokutana kwa mara ya kwanza na mara kadhaa na Kinana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam nikiwa nimeongozana na mhariri wangu, Muhingo Rweyemamu, ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni ambako nilipata fursa ya kumsikiliza na kuufahamu upeo mkubwa wa kuona mambo aliokuwa nao mwanasiasa huyo.

Tangu wakati huo hadi wakati wa kampeni za mwisho za mwaka 2010, niliendelea kukutana kwa nyakati fupi fupi na Kinana na mara kadhaa nikawa mtu wa kufuatilia na kuzisikiliza kwa makini, habari zake kutoka ama kwa marafiki au maadui zake wa kisiasa.

Sikushangazwa hata kidogo niliposikia tena kwamba, Mkapa alilazimika kumuangukia tena Kinana na kumuomba aongoze tena kampeni zake mwaka 2000 kabla ya Kikwete naye hajafanya kile alichofanya mtangulizi wake alipomuomba mwanasiasa huyo adhibiti joto la kiti cha urais mwaka 2010.

Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.


Si ajabu hata kidogo kwamba, hata kabla ya kufikia huko, ni Kinana huyo huyo ambaye alipata kuwa Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Rais wa Tanzania katika eneo la Maziwa Makuu na kabla ya hapo akiwa Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) zama akiwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1972 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

Anarithi mikoba ya Mukama akiwa mmoja wa wanasiasa wachache wa CCM wa rika ile ile la kina Kikwete ambaye alilikimbia na kulikana kundi la mtandao mwaka 2005 ambalo baadhi yetu tunaamini kuwa, ndilo lilisababisha kuzaliwa kwa siasa mpya za kupakana matope, kuzushiana na kuhujumiana ndani na nje ya CCM.

Lakini pengine kubwa katika yote hayo anaingia madarakani huku akiwa na hazina ya uzoefu mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya vyama vya upinzani na kushinda katika mazingira ambayo aghalab yamekuwa yakiacha vidonda visivyopona kwa wapinzani tangu mwaka 1995. Huyu si mtu wa kumpuuza au kumbeza hata kidogo.
 
Juliana, tulia na tafakari mambo. Hizi allegations ni serious na haifahi kudharau, suala muhimu hapa ni kumtaka mtoa allegations awasilishe ushahidi wa anachodai ili kuweza kutenganisha pumba na mahindi. Kama hana tutamwona ni hovyo na tutamdharau.
 
Hizi ni porojo tupu. Unazungumzia kodi kwenye mradi wenye msamaha wa kodi au lengo ni kuendeleza sera ya siasa za majitaka? Kwa kukusaidia kuna kampuni nyingine inaitwa ashref-interbeton wanajenga barabara ya Iringa-Mbeya nao hawalipi kodi, waambie TRA wakupe document zao yawezekana kampuni ya Kinana ilihusika kusafirisha vifaa vyao pia.

Acha Longolongo wewe gamba. Hakuna kampuni yoyote yenye jina hilo si hapa Tanzania tu bali hapa Duniani. Barabara ya Iringa-Mbeya inajengwa na AARSLEFF-BAM J.V (Joint Venture kati ya kampuni mbili za AARSLEFF na BAM).
 
Acha Longolongo wewe gamba. Hakuna kampuni yoyote yenye jina hilo si hapa Tanzania tu bali hapa Duniani. Barabara ya Iringa-Mbeya inajengwa na AARSLEFF-BAM J.V (Joint Venture kati ya kampuni mbili za AARSLEFF na BAM).

We jamaa akili zako pungufu kweli sasa gamba hapa linakujaje? Hivi nyie watu mnaugua ugonjwa wa siasa enhee? Ni joint venture ndiyo (AARSLEFF - INTERBETON JV) so tatizo lako ni nini? Je hawana misamaha ya kodi? Ni vema ukajifunza kujikita kwenye pointi kuliko kugeuka mwalimu wa imla kwa kusahihisha spelling.
 
Back
Top Bottom