Huyu ndiye Kinana, Je analipeleka wapi taifa letu?

Huyu ndiye Kinana, Je analipeleka wapi taifa letu?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,026
Reaction score
20,511
Zabuni ya Mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi jijini Dar ulipitia kwenye misukosuko ya urasimu wa hali ya juu baada ya wanachama na makada maarufu wa CCM kuteka mchakato mzima,

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na Katibu mkuu wa CCM ndugu Abdulahman Kinana ndie aliyeileta nchini Tanzania Kampuni ya Strabag ya Ukandarasi wa Ujenzi iliyoanzishwa na Muastria katika mji wa Villach na kuweka makao yake makuu mjini Vienna Austria ambapo kampuni hii ndiyo ilishinda zabuni hiyo

Kinana aliileta kampuni hii kutoka tawi la kampuni hiyo lililopo Ujerumani,

Kuileta kampuni hiyo nchini ni jambo jema, lakini hoja yangu ni namna Kinana anavyousababishia TRA kukosa mapato kutoka kwenye Kampuni hiyo ya uingizaji mitambo ya ujenzi nchini,

Taarifa za TRA mpaka jana zilikuwa zinaonyesha kuwa kampuni hiyo imeingiza mizigo/mitambo yenye thamani ya kodi ya shilingi za kitanzania 16 milioni tu kupitia kampuni ya Sharaf Shipping Company ambapo Taarifa zinaonyesha kuwa Kinana anamiliki hisa 7,500 kati ya 10,000 za kampuni hiyo inayoitwa Sharaf Shipping Company iliyosajiliwa Dar es Salaam tangu mwaka jana mwezi wa saba.

Kinyume chake taarifa na nyaraka za kiintelijensia kutoka ndani ya kampuni hiyo ya Strabag zinaonyesha kuwa kampuni ya Strabag imeilipa 8.56 bilioni kampuni ya wakala wa meli ya Sharaf Shipping Company kama malipo stahiki ya kodi ya uingizaji mitambo nchini tangu kampuni hiyo ilipoanza uingizaji wa mitambo ya ujenzi nchini 03-07-2012,

Kisha ikailipa tena 7.8 bilioni kama gharama za uwakala wa mitambo hiyo,

Wanabodi hayo ni machache tu lakini nitaweka hapa nyaraka za malipo ya Strabag kwa Sharaf Shipping Company na nyaraka za malipo ya Sharaf Shipping Company kwa TRA kama Mods watanipa kibali cha kuweka hapa,

Maafisa wa TRA wanasema linapofika suala la Sharaf Shipping Company hufanya kazi kwa maagizo ya katibu mkuu wa ccm,

Huyo ndie katibu mkuu wa chama tawala nchini Tanzania
 
Koplo V Je uliwahi kusikia kuwa Ari, Nguvu na Kasi Mpya?(ANGUKA) Je ulishasaghau kwamba huyu ndo aliyekuwa Campaign Manager wa chaguzi karibu zote za awamu ya tatu na ya Nne? Sasa tulia kama anayenyolewa vile Anaipeleka Tanzania kwenye dunia iitwayo ANGUKA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Hopeless!Thibitisha hoja yako sio kulia lia kama mtoto ambae hajanywa uji
.
Rubbish

masalia umepanic???
yani sasa hivi tunawachoresha tu, ngoja documents zote za huu uchafu wa kinana zikamilike tuwamulike kwenye magazeti na midahalo mbalimbali washenzi nyie.
 
Koplo V Ukoo wa panya CCM Babu, Bibi, Baba, Mama, mtoto, mjukuu yote haya ni majizi hakuna kushangaa!! Sembuse Adultembo KINDOVU!!?????? Mnaendelea kumuonea EL mbona hili ni sawa na sakata la Richmond tuu!??
 
Last edited by a moderator:
CCM wamechokwa hadi idara muhumimu zimeamua kuvujisha siri za uovu uanofanywa na watendaji wake.

cc to Nape Nnauye
 
Last edited by a moderator:
Hili kwa CCM linawezekana tu,

Mkuu lete tu hizo nyaraka, JF ndio kisima cha habari
 
Koplo V Hizo taarifa za TRA umezitoa wapi, na hizo nyaraka za Kampuni hiyo ziko wapi? weka hapa , otherwise unatupotezea muda.
 
Last edited by a moderator:
huu mnyukano ni hatari. hebu ngoja nikanywe maji kwanza nipoze injini.
 
Koplo V Hapo ndo ulipoharibu kabisa. kumbe ni taarifa za umbea tu. pole sana kwa kupoteza muda wako kutuletea udaku
 
Last edited by a moderator:
CCM wamechokwa hadi idara muhumimu zimeamua kuvujisha siri za uovu uanofanywa na watendaji wake.

cc to Nape Nnauye

Hivi mtu akija na uzushi wake humu anakuwa na nyaraka toka idara nyeti, si ajabu huyu ni mwandishi wa Tanzania daima, naye utasema ana habari.
 
Hopeless!Thibitisha hoja yako sio kulia lia kama mtoto ambae hajanywa uji
.
Rubbish
...Tulikwambia utafute kazi kam vijana wenzako......uweze kulipa kodi na kuisadia nchi...ukawa unatutukana sasa unaona hasira ulizo kuwa nazo zinakufanya upanic.....na wewe unahesabika kati ya wasaliti wa kuu wa harakati za pili za ukombozi wa taifa hili.....time will come ...na utaona mwisho wa usaliti wako
 
Back
Top Bottom