Msajili afuta Kampuni 440 katika Sekta mbalimbali nchini

Msajili afuta Kampuni 440 katika Sekta mbalimbali nchini

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
430
Reaction score
88
Msajili wa Kampuni nchini Kenya amefuta kampuni 440 kutoka kwenye rejista rasmi ya kampuni, hatua iliyogusa biashara katika sekta mbalimbali za uchumi.

Kwa mujibu wa Gazette Notice ya Oktoba 4, 2026, kampuni hizo zilivunjwa rasmi na majina yao kuondolewa kwenye Register of Companies chini ya Section 894(5) ya Companies Act.

Sekta ya ujenzi na real estate imeathirika zaidi, huku zaidi ya kampuni 80 zikiondolewa kwenye rejista.

Zaidi ya kampuni 60 katika sekta ya transport na logistics pia zimeathirika, huku agribusiness na manufacturing zikiwa na zaidi ya kampuni 50 kila moja.

Sekta ya hospitality na tourism pia imeguswa, ikiwa na zaidi ya kampuni 40, wakiwemo waendeshaji wa hoteli, lodges na kampuni za utalii.

Financial services, retail, wholesale trade, technology na professional services pia zimeorodheshwa miongoni mwa sekta zilizoathirika.

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya kampuni 2,200 zimefutwa kwenye rejista mwaka 2026 pekee kupitia hatua kadhaa za Msajili wa Kampuni.

Hatua hiyo inakuja wakati Kenya ikiendelea kukabiliana na changamoto za ajira na mazingira magumu kwa baadhi ya biashara.

Je, hii ni kawaida ya kusafisha rejista ya kampuni zilizokufa kimya kimya, au idadi hii inaonyesha mazingira magumu zaidi ya kufanya biashara nchini?

jobseekers.jpg.webp
 
Back
Top Bottom