Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

wake wa mengi mmeshikwa pabaya eheee, tulieni 'dawa iingie'
 
Mpaka Muhongo ana team hii kali.
Mnahangaika na Mengi wakati serikali inamtegemea
 
Mimi naomba dua kila leo kina Mengi wawe wengi nchini hapa!
 
Wewe mleta mada ningependa kukuliza swali moja tu na ukilijibu sidhani kama utaendelea kuyaandika haya
- Naomba unitajie mambo muhimu ambayo yamefanywa na Ndg. Regnald Mengi katika nchi katika kusaidia jamii na Serikali na ukimaliza unitajie na aliyofanya Muhongo katika kusaidia jamii na Serikali

Baada ya hapo linganisha je ni nani aliyebora kati ya Ndg. Mengi na Muhongo.

Mhongo ni Juzi tu kawa Waziri hukuwa mfanyabiashara hizo pesa za kusaidia jamii huko nyuma angezitoa wapi? Mengi pesa anazojidai kusaidia ni zile zile pesa za wizi kukwepa kodi, kuifirisi NBC bank, akiwafanyia pati Vilema hupeleka copy ya video kwa waziri wa fedha kusaka misamaha ya kodi, mengi hana cha bure kila Msaada kwake ni Dili na Sasa kamsaidia Rostam kukwepa Kodi baada ya kuuza hisa za voda kwa dola million 300 kisha akamugawia Mengi kwa Ajili ya kumnyamazisha na kumtaka akae kiimya hadi amalize kuha hamisha pesa zake zote pasipo kulipa kodi.
 
Kuhusu utetezi wa Wanyonge kawaulize mayatima, walemavu na maalbino watakupa jibu! Wangekuwa humu JF ungekoma Chiz wahead!!

Kwa taarifa yako Mengi huwa si Mtetezi wa chochote kile yeye hutumia fursa tu, shida za masikini kwake ni Dili, Mengi akiwasaidia masikini hupeleka copy ya video Serikalini kwenda kuomba misamaha ya kodi, Tambua kuwa Mengi hana cha bure kila kitu kwake lazima apige tu.
 
Sasa mto mada hii huoni kama una iaibisha serikali yako kushindwa na mtu binafsi!!????
Ni jinsi gani serikali ilivyo dhaifu.
 
Mengi amezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi. Utajiri wake kaukuza kilaghai i.e kwa kichoma makampuni na kulipwa bima ndefu. Mbulula wengi wanamuona mtetezi wa wanyonge. Waapi bwana

mengi ni mpuuzi sana, aligoma kuhonga tai auziwe kilimanjaro hotel, wajanja wakahonga suti wakapewa hotel
 
Anatabia ya kujihami. Hajiamini.

Huyo Babu wa ipp ni Msanii sana huwa anapenda Kudeka sana dili zake binafsi anazilazimisha ziwe dili za wananchi ambao hawanufaiki na chochote pindi akifanikiwa.
 
SERGIO
kuna vijana walipewa Laptop na kujaziwa bundle kumtetea Muhongo,
je huko si kumuangusha, kwanza aende akagombee Ubunge, maana huu wa kuteuliwa ndio umechukuliwa na ESCROW

attachment.php

mmmmh kumbe ndio maana yuko mweupe mweupe hivi
 
Muhongo propagandas hazitusaidii
Hebu atupishe maana KIPORO kimechacha!
 
mengi ni mpuuzi sana, aligoma kuhonga tai auziwe kilimanjaro hotel, wajanja wakahonga suti wakapewa hotel

Hahahaha rais dhaifu mpenda dezo.. Alipokea suti akatoa hotel, majuzi kapokea saa sijui atatoa nini... Nisingekubali kuwa na baba wa namna hii
 
Team muhongo sikilizeni tena huu ushauri wa bureee..
Huyu jamaa mnaemtetea mwisho wake ushafika tafuteni sehem nyingine mapema msije kufa njaa.
 
mengi ni mpuuzi sana, aligoma kuhonga tai auziwe kilimanjaro hotel, wajanja wakahonga suti wakapewa hotel

Huwa ana Kinyongo kibaya sana hadi leo huwa hataki kukanyaga hapo kilimanjaro hotel, kuna siku ITV walikuwa na Pat wakalipa Ukumbi huko alipoambiwa kuwa ni kilimanjaro Hotel akaamuru pat ihamishiwe Hotel ingine.
 
FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:
Kwa miaka mingi kumukuwepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wenyewe. Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali na baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali. Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania. Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo kwani siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho. Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi.
Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Historia inaonyesha amewahi kuanzisha ugomvi na watu wafuatao kwa sababu anazozijua yeye.
a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.

c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.

l) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.

m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.

n) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba.
Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Kitalu cha gesi naweza kufikiria kwamba inawezekana lakini kitalu cha gesi bure hapo sina uhakika na unachotaka tuamini. Pease naomba unijuze ni kweli Mengi anataka vitalu vya gesi bure????!!!!!!!

The Listener
Ex Detective
 
m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.

Hapa tu ndio umekuja kuharibu hoja zako zote, unataka kusema mafisadi wote wakiongozwa na Change wanamapenzi na nchi hii Kuliko Watanzania walio wengi wakiongozwa na Warioba, UKAWA na hata Mengi.?
 
Team muhongo sikilizeni tena huu ushauri wa bureee..
Huyu jamaa mnaemtetea mwisho wake ushafika tafuteni sehem nyingine mapema msije kufa njaa.

Muhongo hatetewi hapa isipokuwa kuwa Watu wameamua kuzianika Kasoro za Mengi ambaye amekuwa kinara wa kuwanyooshea wengine vidole, wakati yeye mwenyewe amejaa mapungufu lukuki, Mengi amesahau kuwa watanzania sasa wameamka wanajua kubalance pande zote, Vitalu vya Gesi vimemfanya Mengi kapagawa na kugeuzwa mladi na wajanja wa town.
 
Mimi nitakubaliana na haya mawazo yako iwapo tu utanipatia sifa za Lawrence Masha, Shamimu Khan, Basili Mramba, Masilingi, Lowasa, manji, Adam Malima, Mhongo (in relation to escrow account) na UKAWA vs CCM (kuhusu mitazamo yao juu ya katiba mpya). Ukinieleza tu nitalinganisha na mtazamo wako kisha nitakuja hoja zangu nyingine juu ya mtazamo wako

The Listener
Ex Detective
 
Tatizo ni kwamba Mengi kamkomalia Mhongo Wakati na yeye ni Mwizi na mkwepaji kodi, iweje Mengi awanyooshe wengine vidole wakati yeye si msaafi. Sakata la Escrow linawahusu Majaji,Gavana, Wizara ya biashara, wizara ya feza na Wizara ya Nishati , iweje Mengi amkomalie Mhongo peke yake? Kwani ndiye alizitoa pesa BOT ? Vitalu vya Gesi vimemfanya Mengi amchukie Mhongo hakuna mfano.


Muhongo ni mpu..uzi kauli zake zakijinga kabisa, hata mkuu wa nchi nae anashida kwenye uongozi.
Wajenga nchi ni wananchi iweje waziri aongee ujinga kama ule watu wenye akili zao timamu wakae kimya!!!? Wewe unatagemea Mbeki and ndio akujengee uchumi wako!!?
Nahili ndilo litakalo mtoa mkuu wetu kwa aibu kwa kutegemea tegemea kila kitu unaomba omba...
 
Back
Top Bottom