Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

muhongo, prof fake wa miamba at his best... kwani Mengi ndo kamtuma akaibe pesa za escrow. ... kama walikuwa na bifu, nae kaiba sasa mengi afanyeje? Amsafishe?... hope mengi atakuwa anachekelea na za mwizi muhongo zinahesabika.... atang'oka tu hata kama mkulu atamtetea.....

Tatizo ni kwamba Mengi kamkomalia Mhongo Wakati na yeye ni Mwizi na mkwepaji kodi, iweje Mengi awanyooshe wengine vidole wakati yeye si msaafi.

Sakata la Escrow linawahusu Majaji,Gavana, Wizara ya biashara, wizara ya feza na Wizara ya Nishati , iweje Mengi amkomalie Mhongo peke yake? Kwani ndiye alizitoa pesa BOT ? Vitalu vya Gesi vimemfanya Mengi amchukie Mhongo hakuna mfano.
 
Katika Beti Zako Zote Ondoa (m) Kisha Kibwagizo....
"Akataka Kuufanya Ugomvi Wa Nchi Nzima.." Kiendeleee,,,, Lol!
 
Historia inaonesha kuwa wote walioshindana na mengi hasa wanasiasa wote chali kuanzia akina Masilingi, Masha, Khan, hata huyu Muhongo atang'oka tuu
 
mengi ana uraia pacha uingereza na tanzania alipofanyaufisadi east africa alikimbilia uingereza akachukua urai wa uingereza ili asikamatwe na nyerere utawala wa mwinyi akarudi na kuwa raia wa tz

Huyo babu baba wa mapacha kama lilivyo jina lake huwa ana Madhambi Mengi hakuna mfano cha Ajabu etu kuna watu wamekariri kuwa Mengi ni MUNGU kila analosema limetoka Mbinguni.
 
Tatizo ni kwamba Mengi kamkomalia Mhongo Wakati na yeye ni Mwizi na mkwepaji kodi, iweje Mengi awanyooshe wengine vidole wakati yeye si msaafi. Sakata la Escrow linawahusu Majaji,Gavana, Wizara ya biashara, wizara ya feza na Wizara ya Nishati , iweje Mengi amkomalie Mhongo peke yake? Kwani ndiye alizitoa pesa BOT ? Vitalu vya Gesi vimemfanya Mengi amchukie Mhongo hakuna mfano.
so what kwani kwa Rais kuna azimio la Kumuondoa Mengi au fake oooh sor f...u.
 
Huko ni kutapatapa tu kwa serikali ya kikwete maji yameshakuwa ya shingo...busara angeachia tu ngazi ili tuitishe uchaguzi wa mapema hiyo ingemjengea heshima yeye na chama chake....sasa kama mnajua mengi alifisadi kupitia NBC mbona hamjampandisha mahakamani kama kweli kuna ushahidi?

Ushahidi wa escrow uko wazi tunasubiri atoke madarakani ili zile fedha zilichokuliwa kwenye viroba zimtafune maana ripoti ya hosea anajaribu kuikalia...
 
Historia inaonesha kuwa wote walioshindana na mengi hasa wanasiasa wote chali kuanzia akina Masilingi, Masha, Khan, hata huyu Muhongo atang'oka tuu

Kumbuka Huko nyuma hakuwa akitumia Mabilioni kama alizompa Sendeka ili wamung'oe Mhongo, na kila kitu alikuwa akimaliza kule kule Dodoma, safari hii kakumbana na kisiki yaani hata kama itatokea Mhongo akang'oka Mengi atakuwa ametumia mapesa kibao, kwa kifupi Muhongo kamtoa jasho Mengi na sasa wajanja wanaenda kwa Mengi kuchukua pesa kila siku kwa kazi moja tu ya kumng'oa Muhongo.
 
so what kwani kwa Rais kuna azimio la Kumuondoa Mengi au fake oooh sor f...u.

Azimio lipi? Hilo Azimio si ni la Shinikizo la Mengi baada ya kutembeza mkwanja kupitia kwa Sendeka.
 
FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:
Kwa miaka mingi kumukuwepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wenyewe.

Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali na baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali. Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania. Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo kwani siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho. Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi.
Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Historia inaonyesha amewahi kuanzisha ugomvi na watu wafuatao kwa sababu anazozijua yeye.
a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.

c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.

l) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.

m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.

n) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba.
Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Laiti kama ungejua kiini cha mgogoro kati ya Manji na Mengi. Haihusiani kabisa na mambo ya biashara kwani biashara za Manji ni za kurithi na za Mengi haziingiliani kabisa kiushindani.

Fanya utafiti ili ujue hasa kiini cha mgogoro wao usikurupuke kwa kuwa umeambiwa au umetumwa.
 
mleta mada umekuja kumtetea fisadi Muongo
 
Ukabila ndiyo umekutawala mpaka unashindwa kusimama kwenye ukweli nani hajui kuwa mengi anahusika na kuchomwa kwa benki mbona kila kitu kipo wazi mengi ni mwizi na fisadi namba moja katika ukanda huu wa SECAFA.

Wapi nimegusia ukabila wewe ndio utakua na visa kwa ukabila. Weka hapa hyo ripoti inayoonyesha uhusika wa Mengi hapa sio porojo tu.
 
Watanzania tunapenda sana kutumika, sasa hii thread sioni mashiko yake kabisa....na kwanini huyu aliyeileta ametumia muda wake mwingi kuandika mambo ambayo hayana faida zozote.

Hao wote uliowataja kuwa na visa na Mengi walifanya maovu mengi kuliko hayo ya kutofautiana na Mengi.
 
huko kwingine sijui ila kwa bongo nenda vijijini ikifika taarifa ya habari usiku utaona watu wanajazana vibandani kuangalia ITV,ITV imekuwa kama tv ya taifa hamna mwenye mda na tbc

Kwa kanda ya kaskazini hiyo, lakini kwa kanda ya Magharibi na Maziwa Makuu ni Star TV inaangaliwa sana na hasa Habar za kitaifa na Kimataifa na BBC Swahil ndio imevunja rekodi ya kutazamwa
 
Mtoa mada nikuulize swali moja, kama watu wawili wanagombea vitalu vya gas na kwa ufisadi wa nchi hii zaidi ya asilimia 70 ya faida inaenda kwa mwekezaji, katika hili ni bora mwekezaji gani apate wa nje atakayechukua faida asilimia 70 kupeleka huko kwao au mzawa ambaye atawekeza nchini na kunufaisha watanzania wenzake hata kama ni ndugu zake tu?

Simtetei Mengi na sina ukaribu naye ya ukabila, dini, urafiki au undugu wa aina yoyote ile.

Baadhi ya hao viongozi uliowataja kama wangekuwa ni wasafi ningefikiria mara mbili hoja yako nakini kwa uzalendo wa nchi yangu ni bora mtanzania apate kuliko kubakishiwa mashimo tu kama hali ilivyo Geita na Kahama
 
FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:
Kwa miaka mingi kumukuwepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wenyewe. Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali na baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali. Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania. Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo kwani siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho. Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi.
Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Historia inaonyesha amewahi kuanzisha ugomvi na watu wafuatao kwa sababu anazozijua yeye.
a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.

c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.

l) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.

m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.

n) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba.
Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Huu usenge rudisha Lumumba mbwa wewe
 
mbona tatizo la wizi wa EScrow ni mkubwa kuliko hizi blaaahhh blaaaah mazoweka hapa shame on you
 
Back
Top Bottom